Gangstar noma
By: benchrys
5
..kisha mnisubiri na mimi ntakuja na nataka mnipe maelezo ya kutosha ni upuuzi gani ambao nyie kabisa mnaruhusa ya kuongea ndani ya kipindi changu tena kwa. Msiniletee zogo hata kidogo maana mtakuwa mnaniongezea tu hasira hapa we ben unataka kusema nini. Madam alifoka baada ya mimi kutaka kujitetea hapo nikajisemea kuwa daha siku yangu ishaanza kuwa mbaya ni bora nisinge kuja hapa shuleni hii leo mbona naanza kukutana na majanga asubuhisubuhi tuu aah,,,nilikuwa tayari nishapata hasira licha ya kuwa nilishamsamehe m baya wangu ambae ni jane nilijihisi kama hasira zangu juu yake kama zinaanza kurudi tena
Tukiwa tumeshakaa kule ofisini zaidi ya dakika kumi na tano hivi mara mlango ukafunguliwa tena kwa nguvu kumbe alikuwa ni madam alishindwa kuuhimili ule mlango aufungue taratibu kwasababu alikuwa kachukua vitabu na madaftari mengi mimi kwa akiliyangu ya kipuuzi nilitaka kusahau kama nipo kwenye majanga nikataka niangue bonge la kicheko maana nshazoeaga joke/ matani kwa lugha ya weneyewe wanasema ila nshukuru nilishtuka nikajibanza kimya wakati huo jane alikuw ameenda kwa madam na kumpokea baadhi ya madaftari mana madam alikuwa katika wakati mgumu angeshindwa kuyatua yale madaftari na matokeo yake angeyaangusha na baadhi yange anguka.
Jane nakushukuru hata kama tabia yako sijaipenda hata mara moja kumbe kwenye ukarimu upo vyema nadhani haya madaftari nitayasahihisha badae saizi naomba kwanza kaeni hapo kwenye kiti,,alisema hayo maneno madam Linda, Linda ni jina ambalo wanafunzi wote walikuwa wakilifahamu tangu madam huyo alipojitambulisha kwa wanafunzi wote licha ya kuwa kuna baadhi ya wanafunzi walishampa jina la maneno mengi mana alikuwa akiamua hiyo siku yeye ni kuongea mambo hata mengine huyataki basi itabidi uvunge tuu na yeye kumtuliza mtu mwenye maneno mengi hakuwa anaona shida sijui katokea mkoa gani huyu mana ni mwongeaji mno
****huko nyumbani nako walikuwa wakijadili naomi - huyu beni leo atakuwa kapokea kichapo nini mana kwa jinsi alivo chelewa na nasikia kuna mwalimu wao ni mgeni na mpenda sifa kweli akiamua kukupakazia kosa hata kama huna nilazima utakubali tuu labda wewe uwe ni m bishi sana sijui kama leo kweli atapona aliongea maneno hayo naomi alikuwa kakaa na mama akimsaidia kuosha vyombo mana hadi mda huo alikuwa hajarudi kwao,, mama akema kama alichelewa alitegemea nini itabidi akubaliane tuu na hiyo adhabu. Naomi alimtazama mama kisha akaendelea na kuosha vyombo huku akisema kama ni kuchelewa kuamka ni bahati mbaya tuu
****beni na jane wakiwa darasani sijui wamemalizeje hiyo kesi yao huko ofisini
Oya huyo madam wenu mbona mnoko sana. Aliuliza joel mi sikujibu neno lolote akiwa anataka aendelee kuongea mara god nae akaingia joel na ben mnaitwa na madam.joel akauliza madam nani huyo, madam linda alijibu god tukiwa tunataka kumfuata jane akasema ben usiende huko huu mda bora uonekane mkaidi tuu.. hapo mimi nikajiuliza nisiende kwa nini au kuna jambo anajua roho ya kumsikiliza ikaanza kujileta pengine anaweza kuwa msaada.. oya joel ee mi saivi huko siendi wewe nenda ukamsikilize tuu akikwambia uniite mwambie sipo vizuri nilipomwambia hivo nikainamiana kwenye meza yangu ili nijisingizie kichwa kinanigonga,,Joel akaondoka kwenda kwa madam sio mda kidogo akarudi kakunja uso mimi sikutaka kunyanyuka nimwone licha ya kuwa nilimwona kupitia upenyo wa sweta nililolivaa..niliinamiana hadi unafika mda wa kurudi nyumbani, ulipofika ma wa kurudi nyumbani jane akanifwata tena kwa spidi na kusema leo tunaenda wote hadi kwenu nikamuone dada angu mana nishammisi ghafla mimi nikicheki yule madam yupo mbele yetu anatucheki kwa wizi wizi sikujali nikajisemea bora majanga yaishe tuu nisije maliza hili wiki vibaya nikamwambia jane mi ndio naondoka hivi kama vipi twende mana najua lazima atakuwa bado yupo home tuu. Aa ningoje kwanza nikachukue mkoba wangu pale darasani nilisahau. Powa fanya fasta ukichelewa mm hunikuti,. Jane akaondka alipoondoka tuu nikaoana madam akija tena kwangu nikajisemea hapa nishaharibu kabisa
Ben nidhamu yako ipo chini sana ivi wazazi wako hawajawahi kukufunza kuwa inabidi kuheshimu wakubwa zako unapoitwa nao kwanini umeniagizia mtu mwingine aitike wakati mimi nilimtuma god akuite wewe na sio huyo joel ambae umemtuma? Nakuuliza mwenyewe!!!
Sikujibu maana sikuelewa jambo analoongea,,,,, ok naomba tuongozane hadi kwenu sawa ben. Nilipoona kasema hivo ndipo nikatoa sauti ya kwamba madam hilo swala litakuwa gumu sana kama ni kuhusu nidham nitajirekebisha tuu,, jane alipoona nipo na madam alipita njia nyingine na kuondoka.
****nikiwa nyumbani nishakula tayari najiaandaa kuondoka kwenye misele yangu kama kawiada simu inaita.. oya ben uko wap, npo home jee, powa basi nakuwaitia hapa home au vipi, powa.. alikuwa ni joel
Nikiwa njiani kuelekea kwa akina joel mbele nikamuona yule madam yupo kimtaani zaidi kama siyo ticha vile. Shikamoo madam, powa ben mzima alipojibu salam ile niliduwaa kama sekunde nikajibu mm mzima sijui wewe, kama unavoniona hivi ndio hivi mzima wapi safari aliuliza madam, nikajibu naenda dukani pale. Ahaa ningoje hapohapo..itaendelea
Benchrys1996@gmail.com
&
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni