Ijumaa, 23 Septemba 2016

De 35

GANGSTAR NOMA
By: benchrys
35

nilielekea nje huku nilkiwa na mwendo wangu wa kunyata ambapo katika wale waliokuwapo nje hata mmoja wao hakuweza kuniona lakini mimi kila mmoja niliweza kuhisi alipo hapo ndipo nilidank na kutua katikati ya uwanja bila kishindo chochote kile kwakuwa nilishafahamu ni watu gani hata kaikunipa shida sana nikautoa upanga wangu na kuburuza chini kwenye uwanja wetu lengo langu ilikuwa zitoke cheche ili wote washituke warudi nyuma kisha pambano lianze.
      Oya huko nyuma mmesikia nini mimi nimeona kama mwanga fulani hivi au twendeni turudi wote,,,,ilikuwa ni sauti ya mmoja wa wale ambao walivamia nyumbani usiku ule baada ya kuhisi kuna kitu ambacho kipo ndani mule sio cha kawaida, basi wote waliachana safari yao ya kutaka waingie ndani nakurudi nyuma iliwaweze kukizuia kile ambacho mwenzao kakihisi,,,,,,,,

Baada ya mda mda mfupi zilikuwa ni sauti za watu wakilalamika kwa maumivu makali ambapo baba na mama na Naomi ambao walikuwa sebuleni walitaka kutoka nje ili wajionee ni nini kinaendelea lakini Naomi akawaambia kuwa wanaweza kudakwa na kutekwa lakini mama akawa mbishi zaidi kwanza ndio aliwasha taa kubwa ya nje ndipo akashuhudia ninja akipigana na watu kama kumi na tano mama alibaki ametoa tuu macho asimini anachokiona kisha akazijiba mdomo maana alitamani apige kelele kwa jinsi alivoona yule ninja akichakaza watu kama ameagizwa akakate mianzi kwa dakika chachelakini nikiwa napambana na hawa wapuuzi niligeuka nyuma nikaweza kuona mmoja wao akielekea sebuleni sikuzubaa nilitoa nyota(star) moja na kuirusha kuelekea kule kisha nikaendelea kuwapa adabu hawa wachache waliopo hapa. Kilisikika tu kishindo cha mtu kuanguka chini puuuu! Alikuwa ni yule ambae alikuwa akielekea kwenye nyumba baada ya kukutwa na ile nyota upande wa mgongo sijui alizima au ndio RIP tutajua,,,,, baada ya dakika chache lile kundi lote tayari wakawa wapo chini huku baadhi yao wakiwa na majeraha makali sana, kufumba na kufumbua tayari nilikuwa nishapotelea gizani hata asijue mtu nilikoelekea

*****ilipita mda kidogo geti lilikuwa likigongwa sana kwa fujo ambapo kila aliyekuwapo ndani aliogopa kufungua kisha zikasikika sauti hodiiiiiiiiiiiiiiiiii jaman kunauzima humu ndani, ilikuwa ni sauti ya jirani mmoja ambae yupo jirani na nyumba yetu ile,,,, lakini kutoka huku ndani hakuna sauti yeyote ambayo ilitoka kuwaitikia wale ambao walikuwa wakibisha hodi kule nje
Majirani walijitajidi kupiga hodi kama nusu saa na lisaa hivi lakini hawakufanikiwa baada ya hapo wakaamua kuyapanga mawe makubwa ili waweze kupitia juu wakafungue mlango ili waingie ndani, kwakuwa njee kulikuwa na baadhi ya mawe hawakupata shida sana waliyakusanya na kuyasogeza kisha walimchagua mmoja wao ambae ni mrefu ili aweze kupanda na kuingia ndani akafungue mlango jitihada zao zilifanikiwa vizuri kabisa mda mfupi akawa tayari ashaingia ndani akaweza kuiona miili ya watu wakiwa hoi sana hata wasiweze kuongea lakini kwakuwa alikuwa jasiri nae kinamna fulani akafuata ambacho kimemfanya aingie mle ndani,, aliwaangalia sekunde tuu kisha akafungua lile geti nakuwaachia na wengine waingie ili nao wajionee bila kusimuliwa na mtu mwingine baada ya kuwatazama wale watu kwa dakika chache baadhi yao wakaingia ndani iliwakajue kama kuna wenyejji au laa alifika baba mmoja na kugonga mlango wa sebuleni ndipo akakutana na sura ya beni ikitoka kumkaribisha huku nikijifanya ninawoga waajabu sana,,,,,,utajiuliza ndani nimefikaje kumbuka kuwa ninja ana njia nyingi za kuweza kupita sehem,,,,,,,,,yule baba akaanza kwa kuniuliza mbona mlikuwa hamuitiki tunapoita,,,
Tulikuwa tunaogopa wasije wakawa ni wenzao ndo mana hatukuitika. Nilimjibu hivo kisha akaingia ndani lakini alipokuwa anaingia tuu ndani waliweza kuonekana na polisi kama wanne hivi wakiingia ndani mle huku wameshika vitambulisho vyao, kisha mmoja akaanza kwa kujitambulisha naitwa afande kindu nimepata taarifa kwamba hapa kuna habari mbaya kwahiyo nilkuwa nahitaji wanafamilia watatu kwaajili ya ushaidi kwahiyo baba, mama na mtoto mmoja inatakiwa tuondoke..kabla hajamaliza kuongea baba akamwambia hivi nyie maafande sometime mnaona kama wananchi ni watu mbumbumbu sana hivi kirahisi kabisa saihizi ni giza kama mda unavoonyesha ni saa tatu na nusu nani anaeweza kushuhudia au kusimulia mapigano ya ninja hasa mda kama huu wa gizawale maafande baada ya kusikia ni ninja walistuka na kutazamana maana walikumbuka kuwa wamewahi kutumwa sehem wakachunguze kisha walipewa kichapona ninja halafu na hapa inaonekana ni ninja ndio kaja kuharibu tena;;;;;;wakiwa wanaendelea kushangaa mimi nilipita na kutaka kutoka nje afande mmoja akanidaka, dogo sasa unaenda wapi usiku huu na kama unavoona nje kuna majeruhi kibao tuu usije ukadakwa huko bure mana ninja sio watu wazuri hata kidogo ila baada ya kuongea aliniachia chansi yakujitetea ndipo nikamjibu nilitoka kulala ilikuwa saa mbili nilipotaka kutoka haja nikaona geti lilmefunguliwa niliogopa nikarudi tena kulala kwahiyo saiz nataka niende tuu haja niachieni bhaana huku nikionyesha kama kweli nimezidiwa nikampokonyoka nakutoka nje baada ya mda mfupi nilirudi tena ndani lakini nilishangaa kuona pale nje hakuna mtu hata mmoja na ndani hakuna polisi wala wazazi niliduwaa ghafla kisha nikaingia ndani nikachukua simu yangu na kuitrack namba ya Naomi kupitia google map nikaweza kugundua kuwa yupo njian kuelekea mjini sikuweza kujua ni safari ya wapi,

Nilienda hadi katika chumba ambacho kinakaa na pikipiki za baba ndipo nikachukua pikipiki aina ya boxer na kungoa kibanko cha namba kisha nikaanza safari kufuata uelekeo ule baaada ya kitambo furani nikaweza kuona gari fulani aina ya tenga huku likiwa na watu kama saba ndani yake ndipo nikaongeza mwendo wa pikipiki ile na kulipita kama upepo vile kishanikapotelea huku nikijua lazima wafuate tuu hii njia hii nilishuka na kipaki ile pikipik katikati ya barabara ili kumzuia anaepita kisha nikaondoka,,

Polisi walipofika pale walisimama na gari lao kisha waangaza huku na huko lakini hawakuwezza kumwona mtu yeyote walichokifanya ni kupakia pikipiki na kuoiweka kwenye gari kisha wakawasha kuendelea nasafari yao ndani ya dakika kama kama mbili usiku ule waliweza kuona mtu kasimama mbele huku akiwa na suti nyeus yaan vazi la kininja wakajadiliana yupo katikati ya barabara tumgonge tuu kama ni kesi sijui iwe tuu dereva nae akaongeza mwendo wa gari lakini akashangaa huyo ninja hata hana wazo la kuikwepa ile gari, akili ikamruka kabisa hivi huyu ni mtu au jini alipokaribia kwa huyo ninja akakwepesha kidogo lile gari ili apite pembeni lakini yule ninja nae akageukia ule upande polisi yule aliyekuwa akiendesha akaona hana namna akafunga brek ya haraka miguuni mwa yule ninja yule ninja akasogea na kuwaambia wote tokeni nje hakuna liyeweza kubisha hata kidogo wote walitoka kisha akamwita dereva na kumwambia geuza gari dereva nae hakuleta ubishi akapanda na kuligeuza kisha akaambiwa ashuke

ok sasa nazani kutuoni ni jirani safari njema nyinyi pandeni huku vidole vikiwaelekea wazazi pamoja na Naomi na nyie nyie safari njema nitawasogezea tuu gari lenu ndio msaada wangu kwaheri niliingia kwenye gari na kuondoka na baba na mama safari nzima hadi nafika nyumbani ilikuwa ni kimya hakuna anaweza kuongea chochote maana hawajui huyo ninja ni nani ambae karibia kila mda anatokea kama msaada kwao nilipofika nje ya geti niliwaambia kuwa mie nashuka kisha nikafungua mlango wangu na kupotelea,,, niliruka ukuta wa nyumba na kupitia dirishani kisha nikazama ndani nikabadili nguo na kujifanya kama ndio natoka kuangalia gari ni la nani huku baba, mama na Naomi wakishuka nao kila mtu alishuka kivyake kisha wakafunga geti wote tukaingia kulala ilipofika usiku mda wa saa..itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 34

Gangstar noma
By: benchrys
34

..siku iliyofuata niliamka na kuanza rasmi safari yangu nilitembea hadi maeneo Fulani ambako palikuwa na mti mkubwa sana nikiwa sina hili wala lile gafla nikashangaa mtu kashanivaa na baiskel nilianguka chini ambapo na yeye alianguka chini alisimama na kuniambia dogo kama siku nyingine kuwa makini sana unapokuwa katika barabara za watu kama hizi duh nilimwangalia nikajisemea halafu sometime watu sijui wanakuwa na visa na watu kwa kila eneo, nae baada ya kuona nimemwangalia akanifuata tena na kusimama mbele yangu,,,,,dogo mbona unanitumbulia macho inamaana kukwambia kwa mdomo umeniona mimi zoba au. Baada ya kuuliza vile akanipiga bonge la kofi kidogo nianguke hadi chini lakini kwakuwa tayari nilijengwa kwa kuwa na stamina sikuweza kuanguka hadi chini,,,,, baada ya pale akanifuata na kutaka anirushie ngumi niliudaka mkono na kuubana kasha nikamwambia samahani sana usijione kama unajua sana sawa mzee,,, kasha nikamwachilia ule mkono huku nikiondoka ili niendelee na safari zangu lakini bado akajifanya kidume ambapo hatua hii alinifuata ili anipige na teke mgongoni lakini nilipogundua nilidank na kumfumua huku akiwa bado kule juu. Hapo ndipo nikazipanga kwa maana nilijua lazima ataamka na hasira zake za kutosha tu, na ndivo ambavo ilikuwa
Alinyanyuka toka pale chini na kuanza kurusha ngumi za ugomvi lakini hata moja haikuweza kunipata baada ya hapo nilidank juu na kutua katika kifua chache alianguka chini na kukohoa kwa shida sana,,,,, nilicheka kidogo kasha nikamwambia kama siku nyingine hiyo nifundisho acha kujitia kidume siyo kila tu ni boya hivo sasa kwakuwa umenichelewesha naondoka na hii baiskel utafuata mtaa wa ishirini sawa. Niliokota baiskel yake na kuanza kuondoka nayo alipiga kelele za kuita lakini hata sikutaka kusikia chochote mana nilishamwambia mtaa upi afuate
           Nikiwa kama kilometa mbili hivi nishapita kutoka pale niliweza kuona kama kuna magari ambayo yalikuwa msururu sikuweza kujua yanaenda wapi,,,,na mimi nikaongeza mwendo ili niwahi kufika ambako nafika lakini cha ajabu nikiwa naweza kuendelea na safari yangu kuna mtu alijitokeza mbele yangu na kuniambia et anaomba nimwazimishe baiskel yangu hafiki mbali nimsubiri hapohapo sikukubali nikakataa baada ya mimi kukataa akasema lazima nimpe tuu nikamwambia mkubwa hizo ndoto hapa huchukui baiskel kasha nikashuka katika baiskel ile,,,,, alirudi nyuma kidogo na kutoa kisu fulani kidogo hapo ndio nikagundua kumbe sio mtu mwema nae. dah hii dunia kweli hakuna wa kumwamini,,nilijisemea maneno yale huku nikiwa nailaza baiskel yangu pale chini ili nijiandae na kitakacho tokea
     Kwanza aliokota jiwe na kunitishia nalo kisha akarusha lakini nililidaka na kumrudishia ambapo liliweza kukita katika mkono wake uliokuwa umeshika kila kisu. Kisu kilianguka chini kisha nikakiokota na kuchukua baiskel ili niondoke nikiwa nataka kuondoka na ule msururu wa magari tayari ulikuwa umeshafika jirani na sisi,,, kilichonishitua ni baada ya kuona wakipunguza mwendo wa magari yao, basi sikulaza damu niligeuza baiskel yangu na kurudi nilipotoka ili nikatafute njia mbele kama ipo itakayo niwezesha kufika hadi mahali husika ambako ni nyumbani kwetu..
..wale wenye gari waliposimama walienda moja kwa moja hadi kwa yule ambae aliniomba baiskel kibabe na kumfunga pingu kisha wakampakia kwenye gari na kuondoka nae huku mmoja wao akisema kwa jazba sana
ndugu kazi itakamilika tuu hata kama unafanya hutaki haya huyo jamaa yako ulikuwa nae ni nani naihitaji kumfahamu nae pengine anaweza kuwa msaada
Hapana huyu mimi hata sifahamiani nae kwa namna yeyote ile alijibu hivo kwa woga lakini alipiga kofila uso na kuulizwa tena ni nani huyo usituletee uboya hapa kama unavonifahamu huwaga sioni kama ni hasara kutumia hasara nyingi sana kutumia pesa iliniweze kumpata mbaya wangu wewe nishakupata lakini kuwa huyu ben ni miezi mingi sasa namtafuta lakini hakuna mafanikio ila nna mpango mwingine kabambe subirini, hapo aliongea huku amewageulia walle wenzake
..kwa bahati nzuri niliweza kupata njia nyingine ambayo inaelekea kule ambako mimi naenda basi niliifuata kwa haraka na baadaya muda tayari nikawa barabara kuu nilitembea hadi karibia nafika mtaa wetu kufika hapo simu yangu ilianza kuita nilisimama kisha nikaitoa mfukoni ili nijue ni nani kapiga hiyo simu lakini niliona ni namba ngeni sikujali nikapokea huku nikiwana tahadhali kubwa sana
ya ben uko wapi mchizi wangu mana adimu kinyama
acha uboya namba ngeni halafu eti mchizi uko wap
we sema uko wapi ilituonane,, baada kuona vile kama anataka kulazimisha nikamwambia nipo nyumbani. Baada mimi kumjibu vile tuu akakata simu na mimi nilipalaza pedeli za baiskel haraka ili niwahi pale yumbani baada ya nusu saa tayari nikawa nimeshaingia nyumbani
;waoooh jamani ben dah tulikumisije bro wetu njoo ndani basi ukapate kwanza hatamsosi wa nguvu halafu mambo mengine yaendelee,,alikuwa ni Naomi ambae alionyesha kuwa na furaha sana alinipokea begi langu kisha tukaelekea ndani. Kiukwei njaa ilkuwa ikiniuma sana nilkaa kisha ukaletwa msosi..

Hivi ben sijui atakuwa kafika salama kweli huko(alikuwa ni merry huku akiongea na Anna)
Wewe hata usijali yule kamanda hakuna cha kumtisha ila mapema bado atakuwa njiani kwanza kwao ni jirai sana. Aliongea vile Anna,,, hata sijui sana
Hawakuendelea na wakaishia pale

******nilipokuwa tayari nimesha kula nilitoka nje na kuchungulia hali ya nje vizuri baadaya kuona hakuna jipya nilirudi ndani na kulala kidogo niliamka saa mbili jioni.. kisha nikaenda nje ili nipunge angalau hata upepo lakini nilipotoka nje niliona hali tofauti maana geti lilikuwa wazi, nilirudi ndani ilinijue kama wanaacha wazi vile ila nilipofika ndani nikasikia sauti yalile geti kubamizwa ushara ya kuwa linafungwa sikutaka kutoka nje niliingia ndani huku nikiwa na imani alienipigia ndio mda wake wa kuja hapa.baada ya mda nilitoka chumbani kwangu huku nikiwa ninja mwenye nguo zake nyeusi nilpita sebuleni huku nikielekea njeitaendeleaaaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 33

Gangstar noma
By: benchrys
33

..........hallow ben nakuomba utoke nje hapa ninamazungumzo na wewe mara moja wala hatatotumia mda sana done quick ee nakungoja ben...ilisikika sauti ya kike ambayo niliisikia vyema kwenye simu ile iliyopigwa ambapo namba ilikuwa ngeni..katika ile simu kwenye yale maongezi nilimsikiliza lakini sikuweza kijibu chochote mana nilijua wazi mitego haitoi taarifa hata siku moja nilimsikiliza kisha nilikata simu, baada ya hapo niliingia chumban na kutoka huku nikiwa nimevalia zile nguo za kung fu nilizotoka nazo kwa babu kule nilifika sebuleni nilimkabidhi merry simu yangu huku nikimwambia msifungue mlango hadi niwape ruhusa mana hawa watu wanatafuta maisha ya watu
    Nilitoka nje huku nikiwa makini kama watakuwa wamejificha sehem wakinivizia wasiweze kabisa, nilifungua mlango na kutoka nje merry nae akaufunga kwa ndani....
....ivi dada huyu ni nani yako halafu mbona inaonekana hii nyumba kama inachunguzwa sana pana nini hapa..lilikuwa ni swali la anna kwa merry ambapo merry alimwambia tu anna mdogo wangu ni stori ndefu sana mda ukifika nitakusimulia usijali.....huko nje.....
Baada ya mimi kutoka nje sikuweza kumwona mtu yeyote lakini nilishajua kwamba hawa wamejificha ili wanivizie ni kweli baada ya mda kidogo nilihisi mtu akija nyuma yangu kwa spidi sana nadhani lengo lake anivae tuanguke wote chini iliwenzie waje kunishika lakini ilikuwa tofauti sana.  Baada ya kugundua vile nilimkadiria akiwa jirani nilidanki na kutulia nyuma yake huku yeye akiwa mbele na mimi nyuma yake alipogeuka tu alikutana na teke la shavu lililo mfanya abaki ameshika mdomo wake huku damu zikivuja mdomoni mwake, kujiokoa aliamua atoke nduki akikimbia kama kuku aliekatwa shingo hapo hapo na wale wenzie ndipo wakajitokeza wakanishika wakiwa kama watu saba huku kati nikiwa mtu mmoja. Nilikusanya nguvu za kutosha kisha niliinama kidogo niliponyanyuka idadi yao kubwa walipepesukia huko huku baadhi yao wakikanyagana vibaya kabisa mimi sikujali niliruka juu na kumuachia kila mmoja wao zawadi ya mateke ya uso huku nikitulia pembeni kidogo hapo ndipo niliwafanya kama mpira kila aliyekuwa akinisogelea nilipo ilikuwa ni mteke wenye afya lazima aupokee ili akakae pembeni na kupumzika nao baada ya kuona shughuli imekuwa nzito kwao wakajikwamua na kukimbilia walikotoka mimi nikajisemea watu mdebwedo halafu mnajitia kujua shit mbwa nyie.nilirudi zangu ndani lakini kabla sijaingia niufunge mlango vizuri niliangaza macho yangu nje niliona kundi jingine la watu wakija pale niliingia ndani na kufunga mlango haraka nao kwa kimbelembele chao waliufikia ule mlango na kuanza kugonga kwa fujo sana nikamwambia merry anipe ile remot akasema kama ni hivo tuu ngoja niwape shoo watajua tuu aliichukua ile remot kilichofuata huko nje ni sauti za vilio ndio zilizosikika kwa wale watu mlangoni pale lakini akili yangu ilishatambua kuwa wale walikuwa ni baadhi yao tuu niliingia chumbani kwangu na kubadili yale mavazi sikutaka kutokea mlangoni pale nilipita katika emergency door ambayo ilikuwa katika dari kisha unavuta kidogo bati kisha unatokea nje kabisa, kwa kutumia ile njia ndio nilitoka hadi nje nilifika katika bati niliruka kavu mbili dabo na kutua moja kwa moja njee huku nikiwa na nguo za kininja na kila silaha ambayo ni ya muhimu kwa ninja zikiwemo nyota,golori,cheni,upanga n.k nikiwa na staili ya goti moja chini huku nikiwa nimeinama nikawaza hawa leo lazima wanijue tuu nilinyanyuka pale na kuruka ukuta ili wanifuate nje kule nao bila kukosea wakazungukia nje kwa haraka huku wakiwa na hamu ya kunikamata et wamkamate ninja kweli wanandoto za mchana hawa.
...wakiwa na visu,mapanga, na silaha nyingine walitoka nje huku wakijadiliana leo hata kumuua tumuue tuu hakuna namna ya kusimamisha huu usumbufu wa hapa kitaa.....walinifuata huku baadhi wakinionyeshea mapanga na visu, wengi walivirusha visy vyao lakini vyote nilivipangua kwa mateke na mikono yangu baada ya hapo nilichomoa upanga wangu ambao mda wote niliuhifadhi tuu ila nao wale hawakuonyesha woga wowote walinifuata kwa moyo mmoja, waliponifikia nilianza kuuchezea upanga wangu sasa baadhi yao niliwafyeka kwa kuwajeruhi ila akili yangu ikanambia kuua si vyema hata kama ni ninja basi nikaruka na kuwasukuma kwa mateke watu watatu kisha nikasogea pembeni na kuurudisha upanga wangu tena mgongoni hapo waliobaki walijipa moyo wa kunifuata hapo na mimi sikuzubaa nikatoka na kuanza kucheza nayo huku nikidank kwa stail mbalimbali huku nikiwa wasogelea hapo ndipo nilianza kutoa kichapo kitakatifu kwa kila mmoja mana cheni ilikuwa haiui ila inakuacha na maumivu ambayo ni lazima ukae chini kuugulia baada ya dakika chache watu tayari walikuwa wameshakaa zao chini kwa maumivu makali kwenye miili yao. Niliwaambia hku nikiwa nikiwa nimebadilisha sauti kama sio mimi vile """"ondokeni hapa fasta kabla sijatumia njia ambayo ni mBaya zaidi kwao"""" waliogopa kisha wakasimama na kuondoka zao bila hata kuangalia uelekeo wao ni wapi maana baadhi yao waliangukiana waliokuwa nyuma niliwasindikiza kwa mateke mazito ili wakome wasijejaribu huu mziki.

******baada ya hapo nilijivuta tena na kuruka kavu yenye ujazo wa namna yake na kurudi tena ndani kisha nikatoa kamba niliirusha kwenye paa na kukwea kuingia ndani,, nilibadilisha nguo na kutoka tena sebuleni kusha tukaendelea na story kama kawaida macho yangu yalikuwa yakimwangalia anna mda mwingi hii yote kwa sababu nilikuwa simfahamu na kibaya sijatambulishwa ni nani ila kwakuwa mimi mwenyewe nadandia tuu kukaa pale hata sikuhitaji kumjaji kiuwazi..tukiwa tumetulia cm yangu iliita nilipoangalia alikuwa ni baba akinipigia nilipokea na kumwamkia:_
,,,,ok marhaba ben hujambo mwanangu
..baba mimi ni mzima kabisa mungu anasaidia sijui hali yenu jee
,,,huku tupo salama hofu ilikuwa kwako
..ni kweli sijawapigia mda mrefu kwakeli tatizo salio
,,,,haya sa si ungesema tu tujue cha kufanya
..nilisahau tuu
,,,,ok kesho unaweza kuja au ngumu
..ah sio ngumu nitajitahidi tuu mana nimewamisi huko
,,,,sawa basi toa taarifa unapoondoka.....alimaliza baba kwa kusema vile.
     Nililala na siku iliyofuata nikiwa kwa usafiri wa miguu niliianza safari yangu nilitembea hadi......itaendeleaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 32

Gangstar noma
By: benchrys
32

.........kwa haraka nilifunga mlango huku anna akiwa mle ndani kisha nilitoka huku nikiwa pekeyangu wale polisi na watu wa kawaida walishangaa kisha mmoja wao ambae alionekana kuwa ndio kiongozi wa wote akasema hapa tumepoteza tuu mda wetu kuja hapa hicho kiboya ndio hiki au akanyanyua simu yake na kupiga sehemu
""""hallow boss mambo gan haya sasa kutuleta katika ujinga huu ujue tumepoteza mda bure tuu hapa......ok huyo uliyemkuta mkamate kisha njoo nae hadi hapa kituoni""""
Kwakuwa alitumia cm ya ile isiyo na siri niliweza kusikia kila kitu walichokiongea. Yule mkuu wao pale akaita polisi watatu huku akiwaamrisha hebu shikeni kinyago hicho kikatoe maelezo kule.....kabla hata mmoja hajatoka kunifata nikasema hapa hamuondoki na mtu safarj njema..baada ya mimi kusema hivo yule akacheka kwa sauti kubwa hahahahahahaha niliweza kugundua kuwa hizi ni dharau nilimkazia macho hadi alitulia kucheka kisha akawaambia tena ivi nyie sinimesema mkamateni huyo,, aliongea vile kwa kufoka sana hadi waliogopa na kuanza kunifata. Walijichagua polisi watatu kisha wakawa wananisogelea lakini walichoshangaa ni kuona nimeganda tuu kama siwaoni, polisi mmoja akasogea zaidi ili anikamate lakini akiwa hata hajatulia alipata teke lenye heshima kwenye kifua chake hadi aliwaangusha na wenzie kama wanne hivi, yule mkubwa wao nae akabaki katumbua macho hapo ndipo wakajipanga wengi ili wanizoe kwa pamoja nilipoona na kugundua wanachotaka kufanya niliondoka mbio kwa spidi kali ambapo nilipofika mbele niliruka ukuta wa fensi ile nikawa tayari nipo nje ya nyumba ile, hapo kundi lote walijipanga vizuri iliwanizunguke na mimi nilipotoka nje sikuzubaa kulikuwa na mfuko fulan nyie mnaita rambo....nilichukua nikajaza mchanga wa kutosha tuu huku nikiwa nawangoja wajitokeze. Nilikaa kidogo akatokea mmoja nilidunda kwenye ukuta na kukita kwenye tumbo lake alianguka chini pale na kubaki akijisugua tuu tumbo lake kama anahara(sorry) kisha nikazungukia kona nyingine huko niliweza kuwaona wakiwa kama kumi na tano vile nikajisemea hapo afadhali kisha nikaruka juu huku nikiichana ile rambo na kuirusha juu zaidi kisha nikafumba macho nilipotua chini nikaanza kukimbia kuelekea katika pori moja hivi nao bila kuchelewa wakafuata njia zile ambako mimi napita. Baada ya kuona wapo nyuma yangu niliruka katika gogo fulani lilikuwa mbele yangu, nao walijaribu kuruka ila jitihada zao zilifeli kabisa wakaamua kuzunguka maana lile gogo lilikuwa kubwa sana baada ya kuzunguka walijua kazi itakayo fuata ni kumtafuta ben ambae ni mimi lakini cha kushangaza ben hawakumwona badala yake walikutana ninja akiwa na upanga wake mkononi huku ukiwa unang'aa, yule mkuu wao baada ya kuona vile alipiga magoti huku akilia kama mtoto pale chini maana anafahamu ninja ni kiumbe cha hatari sana hapa ulimwenguni kwahiyo alihisi kuzimu inamwita....lakini mimi sikumsikiliza nilichumpa juu na kuudaka mti mmoja huku nikijiandaa kumtulia kichwani lakini kama aligundua hivi alinyanyuka haraka na kuondoka spidi lakini hakujua kama amekosea njia baada ya kufika eneo fulani kuna kamba aliikanyaga ghafla akajikuta yupo juu ya mti huku kichwa kina ning'inia chini na wenzie wakiwa wanakimbia ovyo baadhi yao walijikuta wakitumbukia katika mashimo maana hawakujua chochote kuhusu msitu ule kumbe niliwapeleka makusudi ili wapate tuu mateso yale...
......katika wale watu wote walioweza kurudi ni wawili tuu ili wakatoe ushahidi kwa aliye watuma huku kabla hawaha ondoka niliwaachia ujumbe wakampe mkuu wa kituo. Bila hiana waliupokea huku wakiwa na woga saana lakini niliwaacha waondoke kwa amani huku wale wenzao wakiwa bado kwenye ile mitego na mimi nikaondoka nikiwa tayari nishakuwa kawaida maana nilijua polisi akili hawana wasije tupa bomu bure na mimi nipotelee humo haikupita mda niliingia nyumbani mida kama ya saa 11 hivi hii siku hata sikuchoka maana sikutumia nguvu yoyote kuwaadabisha wale wapuuzi
........waoooooh ben ulikuwa wapi tena kaka lao...ilikuwa ni sauti ya merry ambapo alikuwa amekaa na anna katika sofa moja na anna huku wakichezea cm yao. Sikutaka kuongea chochote kisha nikaingia ndani lakini nikiwa ndani niliitwa na merry pale sebuleni

.....nilitoka ndipo niliona wakitazama taarifa ya habari ambapo pale zile habari zilikuwa ni kama zinanihusu vile. kwa wale niliowaachia ujumbe waliufikisha na kutoa data zote kuhusu kule porini kilichowapata wenzao,,,,walikuwa wanasimulia huku wakilia tena wakionyesha wana uchungu
Mda wote huo nilikuwa bado sijakaa nilisimama tuu huku nikicheki ile taarifa ya habari""""""merry hakuweza kuendelea kutazama maana nae alijihisi kulia mana alipoa ghafla  baada ya kusikiliza ile taarifa sikushangaa mana najua kwa mwanamke ni haki yake kuwa vile

Baada kutulia kwa mda akanigeukia. Ben hao watu wahurumie tuu na sidhani kama watarudia tena...akiwa anaongea vile anna alikuwa katoa macho kama fundi saa vile sema sikujua kama mimi ndio saa au mana macho yake yote yalidokolewa usoni kwangu.
Wewe vipi mbona tunatishana geukia pembeni bhana,,,nilimwambia hivo anna kisha niliangalia pa kukaa na kukaa
Merry sorry ila bila mimi kufanya hivo anna angefanyiwa nini hata sielewi.....nikiwa naendelea kuongea simu yangu iliita niliitoa mfukoni na kuipokea ilikuwa ni namba ngeni nilipopokea tuu....itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 31

Gangstar noma
By: benchrys
31

......niliamka mapema sana ile siku akili yangu ilinituma nikawashe tv niliweza kufanya hivo ikaja breaking newz asubuhi tu hadi nilishangaa habari ilikuwa ikisema kwamba
"polisi watatu walioweza kutumwa jana kufanya uchunguzi katika nyumba namba xxxxxx wamepotea na mpaka sasa hatuna mawasiliano yeyote kisha wakaziweka picha za wale polisi na kumalizia yeyote atakae weza kuwaona atoe taarifa kupitia namba...waliitaja hiyo namba.. nikacheka pekeyangu huku najisemea daaaaah ivi na polisi sikuhizi ni watoto wa chekechea hadi watafutwe kwa taarifa kama hivi shida sana kwakeli. Nilitoka na kwenda bafuni nilinawa kisha nikarudi ndani.....

..........wale polisi waliolala kwenye gari huku ikifahamika kwamba wamepotea ilipofika asubuhi tuu waliamka na kuweza kutafuta sehem ambayo wanaweza kupata msaada ili wazibe pancha kwenye lile tairi la gari yao, walitembetemba kwa umbali fulani ndipo waliweza kupata garage na kisha hapo ndipo wakaazima vijana wachache ili wawasaidie katika kusolve tatizo lao waliondoka had eneo la tukio ambapo ipo ile gari yao kwakweli ilikuwa ni mbali hadi wale mafundi walichukia sema hawakuweza kutoa hisia zao kutokana na woga wa kuwa wale ni polisi..baada ya kutembea sana ndio walifika hadi kwenye lile gari
...duu huu mbons msumari inamaana hii njia ni mbovu namna hii.yalikuwa ni maneno ya kijana mmoja wa garage huku akiwa ameshika spana zake na kuweka kwenye gurudumu lile tayari kuanza kazi,,,,,,,,,,baada ya nusu saa tayari wakawa wameshaziba ile pancha, walifunga kila kitu kisha wakamgeukia alieenda hadi kule garage kuwaita na kumwambia mzee hapa ni elf thelathin na tano tuu kama hamtojali kisha akatulia baada ya kuongea vile yule polisi akajisemea moyoni "inamaana huu tayari umekuwa msala wangu ila sio tatizo sana, aliingiza mkono mfukoni na kutoa wallet yake kisha akahesabu ile thelathini na tano na kumkabidhi ila yule kijana akaongezea "samahani mzee hii kazi sijafanyia ofisini kwahiyo hapa inatakiwa kupewa na hela ya nauli mana tumesafili. Duuuh yule polisi ndipo alichoka zaidi na kuvuta pumzi ndefu kisha akatulia kidogo na kuuliza tena sh ngapi na hiyo. Yule kijana alimwangalia kisha akamwonea huruma kisha akasema tupatia elf tano tuu kwa wote mana inaonekana we ni mchaga. Yule kijana alipokea ile elfu tano na kuondoka na wenzie

Wale polisi walipanda gari na kuanza safari yao polisi mmoja akawasha redio ya kwenye gari akashtuka baada ya kusikia kwamba eti wametoweka tangu jana
Duuh hili jau wakuu umesikia taarifa za hawa wapuuzi...aliongea polisi mmoja
Aaaah mi naona wapo sawa kututafuta we hujui tuliondoka hatujapatikana had saizi kwenye simu zetu kwanini isionekane tumepotea...baada ya huyu kuongea hivi mmoja tuu ndie hakuchangia alibaki akiwaangalia tuu wote walimgeukia na kumuuliza ivi wewe unamatatizo mbona kimya kama bundi,,,, duuh nahisi jamaa aliboreka sana mana hata kama ilikuwa kwenye gari alinyanyuka akang'aka kama anamapepo vile. Polisi mmoja akamwambia hizo hasira ungeleta jana usiku boga wewe mtu nyoronyoro halafu unapaniki tuu...walipeana machambo hatimae walifika kituoni kisha wakaeleza kilichowakuta, mkubwa wao baada ya kuwasikiliza na kuwaelewa akawajibu safari ijayo tuongeze kikosi....

*****huku kwa ben****
Ben kama nilishajua kuwa hawa lazima watajipanga tena sikupoteza hata dakika asubuhi ilr nilienda katika nilitega mitego ya kutosha huku nikiendelea kufanya mazoezi hadi ilipofika saa saba mchana ndipo nilirudi nyumbani nilipofika nyumbani merry sikumkuta ila nikamwona dada mmoja ambae alikuwa mrefu wastan alijionyesha kuwa ni mwenye busara sana, nilimwangalia ila sikutaka kumjaji sana nilimsalimu kisha nikaingia ndani nae alifuata na kuingia sebulen huku akikaa kwenye sofa mle ndani, mimi baada ya kupepesa macho ndipo nikaona chakula kilishaandaliwa kwakuwa sikuonja kitu tangu asubuhi nilichukua jagi lililokuwa tupu nikiwa na lengo nikachote maji ninawe mikono lakini aliweza kuniwahi na kuniambia kakaangu usijisumbue acha nikusaidie tuu nikawa mbishi kwa maana ilikuwa sura ngeni machoni mwangu.
'''' samahani hata hujajitambulisha halafu unisaidie kiurahisi tuu nitakuaminije mimi wewe....nilimuuliza hivo, nae baada ya hapo akajitambulisha jina kwamba anaitwa Anna ubini sikuhitaji sana kuujua alieleza mengi ndipo nikaamua nimwachie tuu lile jagi ili akachote maji kama alivohitaji
Alichukua jagi na kutoa na mimi nilikuwa nikimwangalia tuu alifika hadi kwenye bomba na kuanza kukinga maji mimi nilipotupa macho yangu njee nikaita #anna njoo ndani haraka nilimwita hivo kisa kwa Mbali niliweza kuona kundi likija lenye watu kama hamsini hivi baada ya anna kuingia ndani kwa haraka niliamua kwa haraka ku....itaendeleaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 29

Soma kupasha macho

Gangstar noma
By: benchrys
29

........mtoto fulani alikuwa akilia sana kuomba msaada nilipomtazama vizuri ndipo nikagundua aling'atwa na mbwa basi nilimchukua haraka na kumpeleka hospital kwa usafiri wa ile pikipiki aina ya boxer nilifika hospital nikakutana na manesi kadhaa niliwaambia tatizo la yule mtoto walimpokea kisha wakaingia nae ndani kuendelea na wanayoyajua wao lakini wakiwa wanaingia ndani niliweza kumwona moja ya nesi katika wale watatu akiwa ameniangalia kama ananitilia mashaka vile sikutaka kimjaji sana nae aliondoka akaingia ndani

******eti nesi ivi huyu sio yule mvulana ambaye alikuwa anatafutwa kipindi kama miezi mitatu ivi au nimemfananisha..alisema yule nesi ambaye alikuwa akinitazama anapoingia ndani kule, nesi mwenzie akajibu kuwa tumtibu kwanza huyu mtoto halafu ndio tujue..tutamtajia hela kubwa kama ni mwanae atalipa lakini kama sio mwanae najua hawezi lipa......
Basi baada ya wale manesi kukubaliana vile walimhudumia yule mtoto vizuri kisha wakatoka nae tena hadi mahali nilipokuwepo nikawauliza ni shi ngapi huyu nesi aliyeniletea akasems "kutokana na kovu kuwa kubwa sana imetulazimu tuongezee na vitu vingine ili zoezi likamilike vizuri kwahiyo utalipa elfu sitini tu akatulia huku akiniangalia usoni na mimi wakati huo nikawa kimya kidogo lakini nikakumbuka yule nesi mwenzie aliyekuwa akiniangalia pale mwanzo, akili yangu ilikurupuka na kusema huu utakuwa mtego nikasimama kisha nikatoa wallet katika mfuko wangu wa suruali na kuhesabia zile elfu sitini kisha nikawakabidhi na kujifanya nawashukuru niliwaongezea elfu kumi nyingine kwa kigezo iwasaidie na wakati lengo langu kukwepa huo mtego. Basi nikampokea yule mtoto na kuondoka nae hadi pale nilipomkuta mwanzo nilitazama nyumba ya jirani na pale nilipoiona nikaifuata nikagonga lile geti mwanzo sikujibiwa lakini baada ya kugonga sana ndipo akatoka jamaa mmoja huku akionyesha ni mtu ambae hata si mwema kwa kumwangalia
""oya huyo mtoto umetoka nae wapi au we ni mwizi wa watoto wa watu"aliniuliza hivo. Nilimjibu mi sio kiujumla sawa tena uwe na busara hata kwa dakika moja tu ivi mtoto wenu hadi anang'atwa na mbwa nyie mpo tuu ndani mi nikajua labda ni mtoto wa mbali kumbe ni wako hadi naingia gharama kisa huruma kwa watoto ok nimelipa hela huko inarudije hiyo labda hakafu unanipokea kwa matusi hivi. Nilitulia kisha nikaendelea bro heshima na busara ni vitu muhimu sana mwanao huyo hapo nilimshusha yule mtoto na kumkabidhi....alimpokea kisha akaniuliza "ok umewalipa shi ngapi lakini kumtajia kile kiwango nikaona atahisi mimi ni mwongo nilitoa tena wallet kisha nikatoa kirisiti fulani kidogo ambacho nilipewa kule hospital nikamkabidhi alikipokea kisha akakishangaa kwa mda kisha akasema sawa ngoja aliingia ndani kisha akatoka na hela mkononi akahesabu zile sitini elfu akanipa kisha akaniongezea kama 30 elfu hivi na kusema kumbe dogo huna roho mbaya daah nisamehe sana aisee nikamjibu hata usijali ila mimi nilikuwa napita tu kwaheli kakaangu, tuliagana kisha mimi nikaondoka lakini nilipofika nje nilishangaa kuons pikipiki yangu inakokotwa na watu wawili nikawaita kwa sauti kubwa wakajifanya kama hawasikii hivi niliwafuata wote walipogundua kuwa nawafuata walisimamisha ile pikipiki tena kwa kushusha stend kabisa nilipofika jirani nao nikawauliza kiupole kama boya fulani "jamani mbona mnaondoka na pikipiki yangu mmoja alicheka kwa dharau tena na sauti kubwa moyoni nikajisemea hizi zarau sasa nikawapisha ili kuifuata pikipiki ile lakini mmoja alinizuia kwa mkono wake, dogo kuchukua hii boda ni ndoto sawa nimtazama kwa hasira kisha na mimi nikacheka kama alivocheka yeye mwanzo, baada ya kuona vile alipata hasira kisha alinisogelea na kutaka kurusha ngumi lakini niliudaka ule mkono na kwakuwa nilikuwa na hasira niliuvunja kabisa alipiga kelele kama mtoto hivi nilimwacha chini kisha nikataka tena kufuata pikipiki lakini nilizuiliwa tena na yule mwenzie huyu nae alitaka anipige teke lakini niliruka beki ilikukwepa lile teke akabaki tuu anashangaa lakini hakukata tamaa akaanza kunifuata kumbe hakujua mimi ni mtu wa aina gani, nilikimbia Kisha nikafunga breki ya gafla na kumsindikiza mbele na bonge la teke zito huku nikimbetua alitua chini kama furushi hivi hadi nikahisi kumwonea huruma..... Nikiwa naelekea kwenye pikpik yangu nikasikia sauti ya watu wakipiga makofi kushangilia nilipogeuka ndipo nikaona watu wengi wakiwa wamesimama huku wakiendelea kuniangalia baada ya hapo nikasikia wakisema... bora umewafunzaaaaaa wajinga haoooooo kila siku wanachukua tuu vitu vyetu halafu tukiwafuata tunapigwa...waliongea hivo wakaanza kuwazomea mimi nikahisi hapa inaweza kuwa zari bure kama wakija polisi lile eneo niliifuata pikipiki yangu naliipanda na kuondoka kwa spidi kali sana hadi nilipoona nimepotelea mbali ndipo nilipunguza mwendo wa pikipiki ile nilitembea taratibu hadi nafika kwa merry kwenda kwa akina naomi hata sikukumbuka tena nilipofika nyumbani nilizichukua zile tisini na kuziunganisha na nyingine kisha nikamfuata merry alikuwa kakaa tuu huku akichezea simu yake, nilimsalimia kisha nikaelekea bafuni ili nitoe uchovu baada ya hapo nilifuata chakula na kukila kwa fujo sana nilipomaliza nikajifanya eti namwuliza kama amekula aliniangalia kisha akacheka kidogo  '' ivi mimi na wewe nani amuulize mwenzie kama amekula aliniuliza hivo nikamwambia mimi kwasababu nimemaliza msosi wote mana nilikuwa na njaa hapa. Hakuongea kitu kisha akavuta pumzi na kuuliza ivi wale walionipulizia sumu wapo wapi au walikimbia nilicheka kisha nikamwambia haaa wale wote tayari ni vilema wewe usijawawazie hata kidogo walishashika adabu zao wale wote tulicheka.....

Pale nilipoondoka ule mda na pikipiki yangu ambapo niliacha watu wakiwa wanashangilia sana lilipita kama saa moja waliingia polisi huku wakiwa na gari zao maarufu kama tenga kisha wakadhikwa baadhi ya watu walioweza kukimbia walikimbia lakini wabovu walikamatwa na kusukumiwa kwenye tenga kisha safari ilianza na muda mfupi wakawa wameshafika kituoni...
Afande mmoja akasema yaani nyie mnashangilia ugomvi wa kijinga huo watu wakiuana kwenu ndio raha haya mnaweza kunieleza palitokea nini pale mama mmoja akajibu ndio afande akasema ok toa maelezo yule mama alinza hawapa wawili wali....kabla hajamaliza kuongea kuna mtu aliingia....itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 30

Gangstar noma
By: benchrys
30

.......mbona huendelei kuongea huku umesema unajua kilichotokea pale au kuna kitu ambacho mnataka kunificha, aliongea yule afande ambae alikuwa akitaka kusikiliza maelezo ya yule mama lakini chakushangaza maelezo yalisimama baada ya mzee fulani kuingia pale ndani huku akiwa na mikono yake mfukoni, yule mzee aliyeingia mle ndani akawa anazungukazunguka kisha akavuta kiti na kukaa neno la kwanza kuongea ilikuwa ni kwa afande. Yule mzee alimgeukia afande na kumuuliza mbona leo kijiji kizima nakiona humu inakuwaje,,,,,yule afande aligeuka kwa hasira sana kisha akamuuliza ivi wewe ndio mkuu wa kituo hiki ondoka tena usiniharibie siku kabisa tokaaaaaa nasema kisha akawaita vijana watatu ili wamwondoe mle ndani haikupita mda waliingia vijana watatu wakamshika yule mzee mkukumkuku kisha wakaondoka nae

*****ben na merry mda wa jion tukiwa nyumbani tunaangalia taarifa ya habari mara kuna habari moja iliweza kutushitua hadi tukajikuta tukitazamana wote mimi na merry habari ilikuwa
___kwanza walionyesha picha ya nyumba ile ya merry na kutolea maelezo kwamba yeyote aliyeko jirani akae kwa amani endapo akiona usiku kuna watu wanafanya uchunguzi wao___iliishia hivo kisha kikaendelea kipindi cha miziki kilichokuwepo mda wote ila kwa upande wangu sikuona haja tena ya kusikiliza ile miziki dakika chache tena iliongezeka habari ambayo ilikuwa ikionyesha polisi watakao kuwa wanafanya uchunguzi huo kulikuwa na polisi watatu ambapo mmoja nilipomwangalia nikakumbuka kuwa hawa ndio walio mpulizia merry sumu chumbani kwake kwa lengo wamteke. Baada ya kuona vile nikajua wazi kuwa hspa itakuwa shughuli tena sio ndogo maana yule
Polisi anashirikiana na majambazi au maharamia..
Nilitoka pale nikaingia chumba changu cha ndani nikatafuta lile begi ambalo nilipewa na babu ndipo nikachapua mavazi ya kininja na kuvaa huku nikiziandaa silaha zangu zote vizuri baada ya hapo nilichumpa nikawa nimeshadaka kimlango kidogo kilichopo juu kwaajili ya kufikia kwenye dari baada ya hapo nilipanda juu kulikuwa na mlango wa emergenc juu ya paa ndio niliotumia kutokea niliruka beki mbili mfurulizo nikatua chini upande wa nje kisha nikaenda kukaa kwenye geti la nyumba nilisimama mda mfupi nikaweza kuona gari fulani likija pale, nilitoa miwani yangu ya giza na kuivaa ili nione vizuri kila kitu

Ile gari kabla haijasogelea ile nymba nilianza kuifuata taratibu waliponiona walianza kufyatua risasi zao kwa vurugu lakini nilizikwepa zote baada ya kuona wamesha ishia risasi kwenye bastola zako wakashauriana watoa ili waje kupigana na mimi kwa mikono, walitoka huku wakiwa wamejipanga vya kutosha lakini kwakuwa ilikuwa giza kuona walipata shida kuona kila kitu, kabla ya kunifikia mmoja wao aliamua kurudi kwenye gari iliawashe taa za gari kwaajili ya mwanga. Wote walifika hadi ambapo mimi nilisimama, sikuwangoja waanze mwenyewe tuu niliwaanzilia kabla hata hawajajiandaa niliruka juu kisha nikampa kila mmoja wao zawadi ya mateke ya uso wote walianguka chini kisha wakasimama kuanza mashambulizi maana mwanzo niliwashitukiza
Alinisogelea mmoja akitaka kurusha ngumi nilikwepa kisha nilimpiga ngumi tatu mfululizo za kifua mwingine alitaka kuninyemelea nyuma niliruka begi kurudi nyuma kwakuwa alikuwa force alienda kumvaa mwenzie wote waliangukiana chini kama vipeto alibaki mmoja huyo nilidank nikatua kwenye kifua chake na kurudi pembeni aliamua kukunja ngumi akanisogelea huku akirusha teke, na mimi nilirusha teke ambapo miguu yetu ilikutana juu kwa juu,,,,baada ya mimi kuhisi lile teke halijampata vizuri niliruka juu na kumpa teke jingine la uso alipepesuka nilimfuata kwa mateke matatu mfululizo ya kifua alitua chini alipotaka kunyanyuka alikuwa ameshaishiwa nguvu hivyo hakuweza kunyanyuka akabaki kalala tuu wale wenzio walishikana na kwenda kwenye gari ili wakimbie maana kazi yao haikufanikiwa

Waliwasha gari kisha wakamchukua na mwenzao walimweka kwenye gari kisha wakaanza kuondoka kabla hawajafika mbali niliifuata ile gari huku nikiwa na msumari kisha nikaupigilia kwenye tairi nyuma kisha nikaondoka

****waliondoka ila wakiwa njiani wakaona gari linaenda kiupande kuonyesha tairi moja halina upepo walisimamisha gari wakashuka hapo waliweza kugundua tairi la nyuma upande wa kulia halina upepo. Walitafuta simu ili wampigie mkuu wao lakini kwa bahati mbaya wote simu zao haikujulikana zipo wapi....kumbe waliziangusha walipokuwa wakipambana na ben na mimi baada ya kuziona zile simu nilichukua na kuzitupa mbali sana ili hata wakitrack wapoteze tuu ramani zao.

Wale polisi baada ya kuona hakuna namna ya kufanya walipiga mahesabu wakaona hakuna namna nyingine waliingia kwenye gari kisha wakalaza viti usingizi ukawachukua kwenye gari mule hadi asubuhi

****nilipoona nisha maliza kazi yangu ya kuwazuia wale polisi sikutaka merry ajue kama nilikuwa nje, basi nilijivuta kama hatua tano ivi kisha nikatoka spidi nikaruka juu kama paka (kavu) nikavuka ule ukuta na kutulia ndani kimya kimya nikachukua kamba fulan niliyokuwa nayo nilirusha hadi kingo moja iliyoko juu ya bati kisha nikakwea hadi juu ya bati niliitingisha kidogo ikaachia kwenye ukuta, niliikusanya kisha nikaingia tena hadi ndani nikalala ilipofika asubuhi....itaendeleaaa

benchrys.blogspot.com