Jumamosi, 3 Septemba 2016

De 25

Gangstar noma
By: benchrys
25

.......nilipotazama niliweza kuona namba ya god yule aliyekuwa mmbea wa darasa maarufu kwa jina la facebook licha ya kuwa yeye halitaki. Nilipokea simu yake na kutulia kimya, yaani niliuweka uwe kama mchezo kwa kila atakaepiga simu kwangu, baada ya god kuona siongei ikamlazimu aanze kuongea mwenyewe
   Oya been vipi nambie
  Nikwambie nini atha na wewe fb
  Halafu hilo jina mwanangu staki mm
  Sio utaki sema tu uache mishe za ki fb fb vip wewe, haya unasemaje paparazi langu.hii kauli ilimchoma sana god hadi alikata simu mimi nikabaki nacheka tuu pekeangu baada ya dakika moja tena simu iliita niliipokea lakini aliyekuwa akiongea sikumwelewa hata kidogo maana sauti yake ilikuwa ya mkwaruzo sana na sikufanikiwa kumjibu chochote maana maongezi yake alikuwa akifoka tu
Aliongea sana kisha akakata ile simu nikabaki najiuliza maswali mengi tuu kwamana sikumuelewa anachokisema halafu anafoka balaa

Nkiwa home
..ivi wewe ben unatafuta matatizo watakuja kukuteka hao watu sijui mwenyewe kama unahisi unachokifanya kipo powa sana shauri yako...yalikuwa ni maneno ya naomi sijui alipata wapi habari za kuwa nimepiga watu huko, sikutaka kumwuliza ni kwanini anasema maneno kama hayo mana nilijua wazi kwamba ntakuwa nachochea mdomo wake kwa sababu ben kiufupi sio mtu wa maneno sana na ndio asili yangu hivo nilivo toka mdogo
..e bana kama wataniteka powa ila sitakubali nichunguzwe kijingajinga hivihivi sawa naomi baada ya kuongea vile nilinyanyua simu na kumpigia joel
..oya joh nambie wapi engo
..nipo tuu kihome ukowapi wewe
..road nakuja mitaa yenu
..powa mdau utanikuta mi npo tyu
..ok sio muda basi(simu ilikatwa)
Niliianza safari ya kwenda kwa joel lakini nikiwa nakata kona katika chochoro fulani nilivutwa shati langu hadi kishikizo kilikatika halafu nikabanwa ukutani huku nikionyeshewa kisu shingoni duuh nilizungusha akili fasta namna ya kujitoa lakini kila staili niliyotafuta niliona kama utanidhuru. Alikuwa mdada fulani mrefu kiasi ambaye alivalia vazi la kiislam huku akiwa amejiziba kila kona ya mwili wake mana hadi usoni alivalia miwani yenye rangi nyeusi ambapo nilijitahidi kumwangalia lakini sikuweza kumtambua hata kwa kutumia signal ya macho kwa sababu alinitingia na ile miwani
,,ivi wewe ndio dogo wa kunyanyasa watu hapa mtaani si ndio. Aliniuliza hivi kisha nikamjibu jeuri
,,kwani umeona nimemwibia mtu yeyote hadi useme nawanyanyasa, baada ya mimi kusema vile akawa kama anashika kile kisu vizuri, nikaja kugundua kuwa aliwekea upande ambao hauna makali hapohapo sikuzubaa nilimpa kufuti cha tumbo hadi akaanguka chini kisha nikanyang'anya kile kisu baada ya kuona hawezi kunyanyuka nilimfuata nikamvuta na kunsogeza pembeni ya kile kibarabara huku nikijisemea kama ni makosa bora iwe tuu kisha nikamvua ile miwani nikashituka kuona ni sura kama ya kiume nikajipa moyo nikamtoa na lile hijabu hapo ndio nilithibitisha kuwa ni mwanaume nilipomuangalia nilikumbuka kwamba ni yule ambae nilimpiga ile siku nilipotoka uwanjani nikiwa narudi nyumbani kwa merry, baada ya kugundua vile sikudili nae niliendelea na safari yangu ya kwenda kwa joel huku najiuliza maswali ivi mwanaume anawezaje kutumia sauti ya kike kama vile ila sikupata jibu na baada ya mda mfupi nikawa nipo kwa joel nyumbani..
Oya joh nishafika fungua mlango niliongea vile joel akaja hadi mlangoni na kunifungulia mlango niliingia ndani tukasalimiana lakini baadae joel akapoa ghafla akawa anaongea kinyonge hadi nikajiuliza kisha nikamuuliza na yeye unamatatizo mbona upo hivo?
Hakunijibu ila niligundua kilichomfanya apoe kumbe mkononi nilikuwa bado na kile kisu baada ya kugundua vile nilimpa na kumwambia akiweke hicho kisu,, alikipokea na kukiweka ndani
....baada ya hapo stori ziliendelea vizuri muda ulisonga nikamuaga kuwa narudi nyumbani niliondoka mdogomdogo. Nikiwa njian simu yangu yangu iliita niliitoa mfukoni ila nilipoangalia niliona ni namba ngeni sikuipokea nikarudisha mfukoni nilitembea hadi nafika nyumbani bila janga lolote kwa upande wangu baada ya kufika salama nilimshukuru Mungu maana kila ninapopita sikosi mkosi,, nilipofika nyumbani nilifuata maji nikaoga bila kujali yamoto au ya baridi.

    
Na leo ushaleta majanga yako yani we sijui kimekupata nini. Aliongea maneno hayo naomi
///naomi hayo majanga sisababishi mimi ivi labda nikuulize mtu akija na kukupiga kofi hadi unaangusha mchozi na uwezo wa kumjibu unao utamuacha au utajibu. Nilimjibu hivo nae akasema nimuache mimi yesu toa kisu natoa panga dadeki. Baada ya kunijibu hivo nilicheka kisha nikampa swali tena "sasa kama kwako wewe ipo hivo mimi itashindikaneje atha au mimi ndio yesu acha kunimaindi hivo bhana vp wewe"

Baba na mama walirudi toka kazini kwao iliingia giza tulikula tukapiga stori chache na kwenda kulala...nikiwa nimelala

****Oya mwanangu dogo mwenyewe ndio yuuuule sasa twende tukamnyake mapema kabla hajashutukia ishu sasa sio kuharibu na leo mwanangu..
Powa hapa hakiharibiki kitu jembe langu we twende ila wewe pita huku na mimi napita huku ole wako na wewe uharibu(Safari ilianza)
Dadeki shika mikono hiyo huyu boya leo wetu na nilivo na hasira nae sijui ntakacho mfanya..powa nshafunga hiyo kamba kawashe gari twende zetu dadeki mpuuzi wewe..
******kumbe ilikuwa ni ndoto nilishituka usingizini kwaajili ya ile ndoto duuuh sikuamini nilichokiona mbele yangu...itaendeleaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Alhamisi, 1 Septemba 2016

De 24

Gangstar noma
By: benchrys
24

...........niliishika vizuri ile miamba ya magoli kisha nikajizungusha ili kurudi upande wa pili hapo nikawa tayari nishawaangusha wawili alibaki mmoja. Alijifanya kidume kunisogelea mi nikawa nimesimama huku namcheki uwezo wake juu ya upambanaji, nilimsogelea huku mkono ukiwa mfukoni nae hakuchelewa akarusha teke mgongoni ila nikazidi kumsogelea tuu alijitahidi kuruka awezavyo ili anipige lakini ben nilizidi tuu kumfuata kasha nikatoa mkono mfukoni baada ya hapo alijaribu kurusha ngumi nikaudaka mkono kisha nikamvutia kwangu, alikosa balance nyie mnaita hivo sijui, tuendelee alipokosa balance ilimpelekea kupepesuka na mimi iliasiendelee nilinsindikiza na teke ili aendelee na safari yake hali ambayo ilimfanya akangukie mdomo nikajisemea aaaah potelea mbali mi sijui umetaka mwenyewe hayo yote yasingekuwapo baada ya hapo yule alikuwa akilia tuu na hawa waliopigwa na kuanguka mwanzo wakawa wananyuka mda huu baada ya kuona wananyanyuka nilijifanya kama sijawaona hivi nikawa kama naondoka hivi nao wakasemezana tukamvae kabla hajafika mbali,walikubaliana hivo kisha wakajipanga kuja kwa kasi ili wanivae tuanguke wote. Walitoka mbio kama mbwa wa jeshi kuelekea upande ambao mimi nipo waliponikaribia tu nilichumpa juu kisha nikatua nyuma yao na kuwabetua wote walitua chini kama mgomba ulioegeshwa tuu niliwaonea huruma nikaanza safari ya kurudi nyumbani......nilipitia pale ambapo nilirusha lile bagi ila nilipoingia tuu ndani nikakuta vijana wengine wawili huku wakiwa na mapanga kama ya kininja hivi, sikujali hayo yote nililifuata lile begi nikalivaa kisha nilianza kuondoka lakini kabla sijaondoka alikuja mmoja katika wale wawili huku akiwa kaelekeza lile panga kwangu, ni kitendo cha sekunde tuu nililidaka lile panga na kumshika asiweze kufanya chochote, nae baada ya kuona hana ujanja akamkonyeza mwenzie ili achukue hatua kwa kitendo kile. Lakini kabla ya kufikiria cha kufanya nikamwambia jitia mjinga mfe wote hapo kesi mimi siogopi hata kidogo kwahiyo ntafanya chochote hata weka hilo panga chini kabla sijamtanguliza huyu mwenzio mahali ambapo hatarudi,,,, hakuleta ubishi akaweka lile panga chini kisha akajifanya kama anasaluti kumbe alikuwa kaweka bastola iendayo kwa jina pisto nyuma ya mgongo wake nikiwa bado nimemshika yule mwenzake aliitoa ile pipe akaikoki lakini sikushituka ali pull triger kunielekezea mimi lakini wakati huo nilasha mgeuzia mwenzie ule upande kwahiyo alipopiga tuu risasi ilipenya moja kwa moja kwenye kifua cha yule mwenzie... Lahaura nini hiki sasa nimefanya alianza kujiuliza ni kitendo gani ambacho amekifanya "yaani nimempiga tena mwanangu duuh huu msala ntaeleza nini sasa"

mda huo yeye anaendelea kushangaa ben nilishaondoka na lile begi nakaribia nyumbani nikiwa bado njiani ilipita gari moja likiwa na mwendo wa kasi sana hadi watu wakasema watu gan hawa!!!! Kumbe walikuwa ni polisi wakielekea kule kwenye ile nyumba walikopigana watu akiwemo na Ben

****kumbe ule mda imelia risasi kuna mama mmoja alikuwa akipita pale aliposikia tuu ule mlio akapiga simu polisi ila kwa bahati polisi wamekuwa wazembe wakachelewa maana na mimi ningeshikwa

******we ben hilo begi lina nini mbona kama lina vyuma hivi ni vitu gani hivyo. Lilikuwa ni swali kutoka kwa naomi maana yeye mara huwa wa kwanza kuniona ninapoingia nyumbani,,
,,aha we lichukue kaliweke ndani mengine utajua badae. Alilipokea lile begi ili aende kuliweka ndani lilikuwa ni lile begi ambalo linasilaha za wale vijana watatu niliowaona kwenye vichochoro kule naomi akiwa anaelekea ndani.......haaaaa!!! Wewe ben umetoa wapi hivi vitu, kumbe naomi alilifungua lile begi ili ajue kilichopo ndani mule baada ya kukuta zile bastola ndogo ndio akatoa kelele za mshangao.. Baada ya kugundua kuwa kafungua nilipaza sauti na kusema:  "naomi nimekwambia ukaweke ndani mengine mtajua baadae mbona hunielewi"

Naomi baada ya kusikia vile alipitiliza hadi ndani akaweka begi kisha akaendelea na mambo ya yake.

Nikiwa nimetulia simu ilianza kuita, ilionyesha jina la merry niliipokea
;;hallow mambo ben
;;powa tyu mzima ccta
;;mi niko powa. Halafu we ben
;;ndio mi ben vipi kwan
;;mbona unanyanyasa watu wa watu mtaani kisa ni nini,aliuliza hvo merry
;;sio kwamba nawanyanyasa ila wao ndio wananinyanyasa na lengo lao kuu ni kunikamata sasa mimi siwezi kukubali hilo swala hata siku moja eti nikamatwe kizembe bila hata sababu yoyote
;;haya bhana mimi nilikuuliza kupigana ulijifunzia wapi
;;daah na wewe ukitaka kujua kitu unakumbusha kwa juhudi kweli....
;;ni lazima nikumbushe aya niambie saizi
;;haya bhana ila mbona kuna mishe naifanya na hii habari sio fupi tufanye unitafute baadae au jee
;;dah pow bhna saa mbili ntakutafuta tuu kwaheli
;;powa
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya mimi na merry akitaka nimwambie nilikojifunza kupigana wakati mimi babu alinikataza kumwambia mtu yeyote

.
.............................
Ivi huu sasa ni utani hivi inawezekanaje kile kidogo kuwapiga eti hadi mmeumia hivi inamaana...yani siwaelewi kabisa kumbukeni anazidi tuu kukusanya silaha zenu na msipokaa vizuri mtajikuta mnaozea jera endeleeni na huo uzembe mimi mkikamatwa sitajua na msinitaje maana atakae nitaja nampeleka kuzimu bila kutoa taarifa huko, halafu wenzenu watatu wako wapi mbona mpo wachache hii leo. Boss hata sisi hatujui maana waliondoka na kusema wanaenda sehemu fulani wamesikia kuwa beni yupo huko....huyu akiwa anaendelea kuongea simu ya boss iliita
;;hallo nani mwenzangu
;;unaongea na mkuu wa kituo cha polisi fulani(alimtajia jina) samahani unajika kufika hapa si zaidi ya dakika tano..kisha simu ilikatwa
Hivi haya ni mambo gani kituoni kuna nini mbona nachanganyikiwa anyway let me follow. Baada ya kuongea vile huyo wanaemwita boss alitoka katika jumba la kifahari hilo akachukua funguo za gari na kuelekea kwenye gari mojawapo kisha akaliwasha na kuondoka nalo******huku nyuma
Wafanyakazi wote walikusanyana na kujiwekea mipango ya kutoroka, walikubaliana wote bila hata kipingamizi cha upande wowote, walifungasha kila kilicho chao na kinachoweza kuwasaidia huko mbele maalumu kwa kuanza safari lakini walipofika geti kubwa la kutokea nje walijaribu kuvuta bila mafanikio wakajipanga kuwa walivunje baada ya hapo walijisogeza wote na kuanza kulipush lakini bado ikawa zero tuu ila kuna mmoja wao alipoangalia sehem akaona funguo aliiokota na kusogea hadi kwenye lile kufuri na kuchomeka ile funguo alipoizungusha kidogo tuu kufuri lilifunguka bila ubishi wakachukua mabegi ili watoke watembee zao ila walipofika tuu nje walishangaa kuona gari kubwa limepack vizuri sehemu ya kutokea na muda si mrefu walitokea polisi. sijui walijificha wapi hata sijui. Wote wakiwa na mabegi yao waliamrishwa waingie kwenye lile gari na hakuna aliyeweza kuleta ubishi wowote****** hilo ni janga lililotokea kwa wafanyakazi na boss aliyewaajili watu wamtafute ben

...........huko polisi baada ya boss yule kuulizwa maswali hakuna aliloweza kulijibu kwa kujitetea kwa akapelekwa gerezani na wafanyakazi wake(hivi ina maana hawa hawana hata idea ya kuwa nimefunfwa yaani hata mdhamana tuu hawaji kuleta duuh hii too much)alikuwa akijisemea yule boss pekeyake kule gerezani.

Ngrrrrrrrrr ngrrrrrrrr ngrrrrr huo ulikuwa ni mlio wa simu yangu aina ya Samsung ikiita niliitoa nfukoni na kuipokea lakini sikuongea chochote maana namba ilikuwa ni ngeni kwahiyi ikaniwia shida kuongea lakini cha ajabu nae hakuongea hadi simu ilikata
..upande wa pili..huyu boya mbona haongei ili tumrekodi ahh achana nae huyo tuendelee na yetu.

Nikiwa nimetulia tena simu yangu iliweza kuita tena nilipoangalia ile namba nikajisemea daaaah mambo gani haya atha alikuwa ni......itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Jumatatu, 29 Agosti 2016

De 23

Gangstar noma
By: benchrys
23

..........waoh ben umerudiiiiiii mamaaaaaaa ben huyu hapa amerudi mama njoo, ben karibu ndani tulikumiss wenzio huku hadi karibia kuumwa yaan jaman...alikuwa ni naomi ambaye alinipokea kwa shangwe hadi mi mwenyewe nilijiogopa nilizubaa kama sekunde mama nae akatoka akiwa na furaha ya hali ya juu.. Basi tuliingia ndani duuh chakula sijui kimeandaliwa mda gani hata sielewi maana nilipoingia tuu ndani haikupotea hata sekunde nilinawishwa mikono tayari kwa kuanza kula baada ya dakika chache tulishamaliza kukusanya kila chombo kilichokuwapo pale

      Jaman mbona baba simwoni yuko wapi maana nlisahau kuuliza hilo jambo
..baba yupo kazini bado hajarudi

,nilijibiwa hivo baada ya kuuliza hilo swali ok kama yupo kazini powa. Nikiwa nimekaa pale na naomi. Naomi simu yake ilianza kuita aliipokea simu ile kwa furaha huku akiniangalia, nilipoona kile kitendo nilishituka kisha nikamuuliza..
We vipi mbona mimacho kwangu vipi kwani au nimekula sumu.... Aliiweka simu pembeni kisha akaniambia kwa sauti ndogo huyu ni jane alikuwa anakusalimia. Baada ya yeye kusema vile nikatulia kwa amani maana nilijua tayari nimeuzwa
.............

Oya kale kajamaa mbona hakaonekani tena toka ile juzi sikaoni sijui kapo wapi ila ntakapata tuu hata kasijali na jinsi nilivo na hasira nako sijui itakuwaje... Aah unazingua wewe ivi kama mtu humwoni inatakiwa ujiulize yupo wapi sio unamtafuta kwa hasira kuwa mpole mambo yako yatakuwa fresh nautamnyaka tuu hata usijali jomba punguza presha huyu yupo na ni wetu wala hana kwakwenda na atakuwa amejificha
.........hayo yalikuwa ni mazungumzo ya vijana wawili wakiwa wanavuta mibangi yao sijui hata ni akina nani na ni nani wanamwongelea

Basi kwa akina ben mda ulikwenda hadi baba alikuwa tayari amesharudi ilipofika kama saa moja hivi...
Jamani natoka mara moja ntarudi sasa hata geti msirudishie.. Niliongea hivo kwa maana nlihitaji kufika kwa joel maana nilimmisi jamaa yangu lakini nlipoongea vile mama akauliza "ivi wewe umefika unamasaa tu ila unatoka kwanini huko unakoenda usiende kesho tafadhali. Basi kwakuwa aliongea mama tena kwa msisitizo nilibadili mawazo ila sikupenda kwa maana lengo sikuwa nalo moja tuu. Nilirudi ndani ila kichwani nilishapanga wakiuliza nilikokuwa naishi nitadanganya...tulikaa sebuleni masaa mengi huku tukiwa na stori nyingi kilichonishangaza hadi naenda kulala sikuulizwa swali la wapi nilikuwa naishi ilipofika saa nne na nusu niliwaaga naenda naenda kulala wote wakaridhia basi niliondoka baada ya muda kila mmoja alitawanyika kwenda chumbani kwake. Nikiwa naendelea kuutafuta usingizi kwenye simu yangu iliingia meseji nilinyanyuka kwenye kitanda nilipoegama kisha nikaifungua, kumbe alikuwa ni merry
Ben mbona kimya umefika salama kweli nijibu niwe na amani ..baada ya kusoma hiyo meseji nikafuata sehemu ya replay kisha nikarudisha,
Nimefika salama tuu nilisahau kukwambia nipo nyumbani saizi kwaheli usiku mwema nikutakie, nikaituma sio mda mrefu akarudisha na kwako pia nilidelete kisha nikaanza kutafuta usingizi tena ila usingizi haukuja

Nikakumbuka ivi kumbe kuna wasap kwenye simu yangu basi nikafungua data kama kawaida nilipowasha data ziliingia meseji ishiri na zaidi idadi kubwa zilikuwa ni za madam linda. Nilianza kufuatilia meseji moja baada ya nyingine ila nilishangaa kuona nimetumiwa picha za watu wengi kweli kisha mwishoni kukawa na ujumbe kuwa makini na hizo sura popote unapopita

Niliposoma ule ujumbe nilimakinika ndipo niliweza kumuona hadi yule niliyempiga kule mtaani kwa akina merry basi nilisoma meseji zote nikawa tayari nimemaliza kuzisoma hapo nikawaza cha kufanya kingine....nikiwa nipo bado pale nilihisi kama nje kuna mtu vile nilinyata hadi sebuleni kisha nikaka dirishani ili nijue anataka kufanya nini, mara nikaona anafuata mlango akasogea kisha akachomoa kitu kama chuma hivi sikuweza kuona vizuri anachokifanya baada ya muda mfupi mlango ulifunguka baada ya kuona vile nilirudi nyuma kidogo kisha nikaruka juu na kumtulia kifuani alianguka chini nilimsogelea na kushika pembeni mwa shingo hapo ndipo akatulia kama roba la mahindi nilimfunga kamba na kumweka stoo ambayo haina kitu chochote nililock mlango kisha nikarudi kulala kabla sijapata usingizi tena nilisikia mlio wa simu kuita kule stoo nilijua wazi ni simu huyu jambazi nilinyanyuka na kwenda kuinyakua nilipofika ikawa ndio inakata ila nikaichukua na kurudi chumbani kwangu nikiwa chumbani simu iliita tena niliipokea na kusema hebu ngoja kwanza ambapo nina liliseviwa boss baada ya kusema vile nilikata simu na kuizima kabisa kisha nikalala

*****\
Baba naomba uwapigie polisi waje hapa saizi
Baba alinipuuzia ila baada ya muda si mwingi alibadilisha mawazo na kuwapigia hayakupita hata masaa polisi walifika nikawaonyesha mtuhumiwa ni nani kisha wakamfunga pingu na kuondoka nae wamashukuru kwa kuwasaidia

......ila binadamu bhana sijui wanamatatizo gani mtu unakazi ila bado unataka na kazi ya wizi ivi kwanini hawaridhiki binadamu hawa duuh hii shida sana.. Alikuwa akiongea baba hayo maneno baada ya kumwona yule mwizi kumbe walikuwa wakifanya kazi kampuni moja......

****mama mmoja anatangaza kupotelewa na mme wake anadai aliondoka usiku bila kumuaga mahali anapoenda lakini cha kushangaza hadi wakati huu hajamwona mme wake kwa atakae mwona atoe taarifa kwa kupitia namba au atoe taarifa kituo cha polisi kilicho karibu tunaomba ushirikiano wenu ahsante*****ilikuwa ni breaking newz katika tv baada ya kuona zile picha za anaetafutwa nilicheka sana na kijisemea wewe pomole kweli unatafuta mwizi.....baada ya muda simu yangu iliita kwa namba ngeni
;;hallow
;;ya nambie ben vipi
;;powa we nan
;;mi mchizi wako bhana vipi wewe uko wapi now
;;ahaa kama ni mchizi wangu powa mi nipo tanzania jee wewe uko wapi
;;unazingua mwanangu tz kubwa bhana vipi
;;usiniendeshe sikujui halafu nikwambie nipo wapi unaumwa au.... Hallo, hallo, hallo we ben hallo,,,,, baada ya kujibu vile nilikata simu akaendelea kuita baada ya kugundua simu haipo hewani akajaribu kupiga tena nilipokea kisha nikamwambia tuonane sehemu fulani hivi hawakuchelewa wakachukua pikipiki huku wakiwa watatu na mabegi yao kuwahi lile eneo lakini mimi nilienda lile eneo kwa kupitia njia nyingine...
Duuh mbona hatokei au katuenjoy huyu mpuuzi dadeki zake tuweke haya mabegi chini maana yanachosha tu migongo. Walikubaliana na kuvua yale mabegi kisha wakaweka kwenye pikipiki zao juu ya kiti....wakati huo wote mimi nilikuwa kwenye kona moja nikiwasoma tu nilipoona wameenda mbali kidogo na zile pikipiki nilisogelea yale mabegi na kufungua ndipo nilipoweza kujua kuwa nao ni wapuuzi kumbe, ndani ya mabegi yale kulikuwa visu fulani vidogo sana ila vinauzito fulani. Nilivichukua visu vyote na kutia kwenye begi moja kisha lile begi nikalivaa mimi na kuanza kuondoka, nikiwa naondoka nyuma yangu nilisikia kelele oya kijamaa kile pale, baada ya kusikia vile nilijua wazi kuwa ni wenyewe tu  nilijifanya nakimbia nai hawakuchelewa nilipopita katika nyumba moja geti lilikuwa wazi nilirusha lile begi kisha nikaendelea kukimbia hadi maeneo fulani ambapo palikuwa na uwanja wa mpira
Walifika jirani kukaribia kunikuta. Daah niliangua kicheko baada ya kuona wanaonikimbiza et hadi hichi kijamaa kinanitafuta dah sa si kinaweza kikaishia huku huku tuu aisee ila sio mbaya njooni,, nilisogea jilani na mwamba mmoja nao walinifuata kisha.....itaendeleaaaaaaaaaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Jumapili, 28 Agosti 2016

De 22

Gangstar noma
By: benchrys
22

........ivi ni wewe uliyekuwa unapigana ni wewe au kuna kivuli chako mbona kama siamini hivi ni kweli au maigizo haya kama ni edit zimefika hadi hizi level basi mi najiuzuru kabisa aliongea maneno hayo merry akiwa haamini kama ni ben kweli ambaye alikuwa akiongelewa katika taarifa ya habari kuwa kapiga watu hadi baadhi yao wanazirai kabisa na baadhi yao inasemekana ni watu wanoogopwa sana katika mitaa.... Samahani kama nitakukwaza merry ila ukweli ndio huo maana nikiwa naenda nyumbani kama nilivokuaga kuna mtu akaniletea mambo ya ajabu sikumwacha nilimpa adhabu yake tena nilikuja nae hadi hapa nyumbani ili anipe ukweli juu ya kwanini walikuwa wananitafuta nilipata ukweli niliweza kumwachilia na kwenda uwanjani lakini nikiwa narudi kuna watu wakawa wananifuatilia nikaon upuuzi mana baada ya kumvuruga huyo mmoja ndipo nikaona bastola kwenye mfuko wake.   Nilipomaliza kutoa hayo maelezo kwa merry nikamtolea ile bastola ilibaiweke ndani

Merry hata hakuamini alivoona na kusikia yale maneno kutoka kwangu, alipokea ile bastola akaiweka ndani kisha akarudi na kuniuliza ben kwa hiyo umejifunza wapi hayo mambo ya kupigana " daah merry ni mda mfupi sana ila ni stori ndefu sitaweza kukusimulia sahizi labda kesho... Nikiwa naendelea kuongea simu yangu iliita niliipokea bila kuangalia mpigaji ni nani

;;;;;jaman mi sitakiiiiiiiii nakufa mimiiiii niachebi huko mi sitaki jaman. Msadaa jamaniiiiiiiii.. Ilikuwa ni sauti ambayo ilisikika katika simu yangu pindi tuu nilipoipokea na kuweka sikioni nilibaki nimeduwaa baada ya kusikia mtu analia mda kama ule tena kwenye simu baadhi ya maswali niliyojiuliza ni kwanini nipigiwe mimi na ni namba ngeni iliyopiga ila akili yangu ilinituma nitoke nje, na mimi bila kuchelewa nilifungua mlango na kutoka nje pengine hili tukio lipo jirani hapahapa nilipotoka nje nilisikia kama mtu akilia vilevile mbali kidogo na pale ambapo mimi nilikuwepo nilijaribu kufuata ile sauti na baada ya mda mfupi nikawa nimeshafika pale kabla ya kuongea neno niliruka na kumpiga na teke la kichwa jamaa mmoha ambaye alikuwa amembananisha msichana fulani ambae sikumtambua ukutani baada ya hapo nilimfuata yule bint na kumwambia kimbia nae hakuzubaa hata sekunde aliondoka spidi hadi nikashangaa. Nikiwa naendelea kumshangaa yule dada nilipigwa ngumi ya kifua akataka kuongeza na ya pili nilidaka mkono nikauvunja kisha nikaondoka
    Nilifika nyumbani merry bado amekaa anangoja kinachojili niliingia ndani nikafunga mlango
"wasichana wenzenu muda mwingine sijui wana matatizo gani usikuu huu mtu unatembea pekeyako vichochoroni... nilikuwa nikiongea pekeyangu maneno kisha merry nae akadakia kwani ni nani huyo
;;ahaa hata simjui na namba yangu sijui kapata wapi
;;huyo anakufahamu vizuri kabisa nawe utakuwa unamjua..... Nikiwa naendelea kuongea ikaingia meseji kwenye simu yangu nilipofungua nilikutana na ujumbe "asante ben kwa msaada wako nakushukuru ntakutafuta kesho mimi ni jane mdgo na naomi usiku mwema" nilijikuta nikicheka pekeyangu huku nikijiuliza maswali kama ni jen huku kaja kufanya pia kafahamu vipi kama mimi nipo huu mtaa maswali mengi yalinijia kichwani bila ya majibu. Nikiwa naendelea kujiuliza maswali simu yangu iliita tena kuangalia niliiona ni namba ya madam linda
;;hallo ben mambo
;;powa tuu nambie madam
;;hakuna jipya ila nataka kukuuliza huo mtaa unao kaa saivi hauna mauzauza yoyote maana naona kama kila siku habari za ajabu tuu niambie tuu maana huku kumetulia saizi unaweza kurudi tuu
;;unaniambia ukweli au na wewe umesetiwa kama akina jen walivosetiwa zile siku za mwanzo..
;;hapana ben niamini tuu yaana nakuomba
;;haya basi kesho au kesho kutwa nakuja huko nitatoa taarifa nikiwa karibu
;; haya powa usiku mwema.... Yalikuwa ni maongezi yangu baada ya kupigiwa simu na madam linda, baada ya mfupi macho yangu yalianza kuwa mazito ishara ya usingizi nilisimama nikamuaga merry kisha nikaingia kulala

*******
Jaman ivi ni upumbavu gani tunaufanya ivi tayari mmekuwa watu wajinga namna hiyo ivi nawalisha mbwa au nalisha watu ambai nao inatakiwa wajue namna ya kula wao kama wao haya kamewapiga kamtu kama kale ambako kwanza ni kadogo kwenu,mwezi uliopita mliniambia hata haonekani saizi anaonekana anawapiga watu kama nyinyi kuna maana ya mimi kuwalipa si bora nikanywee bia tuu hizi hela kama mtu nnae mtaka mimi hamuwezi kumshika kadiri nnavotaka mimi na kitu kibaya mnathubutu kumwachia hata silaha ambazo nimewapatia mnajua kesi ambayo mnajitengenezea kama akiamua kuzipeleka mahali husika..
Samahani mkuu haya ni makosa madogo tu hata hupaswi kutoa lawama kama hizo maana hata sisi wenyewe tunashangaa kama kweli kamtu kama kale kanaweza hata kupigana ila kesho ntajitahidi kumwonesha adabu na ni lazima nimkamate katoto kadogo hakawezi kutusumbua akili watu wazima kama sisi. Sio kwamba hakawezi mbona kamewasumbua sasa inamaana mlikuwa mnacheza hadi akawashika akili zenu.  .dah boss mbona inaonekana kama ni makosa ya kila siku tumekosea mara ngapi ivi hii si ndio mara ya kwanza tuu mbona umefura hivi boss hata sisi ni binadam boss naomba ufahamu hivyo.. Ok nawasubiri hiyo kesho ili nijue mwisho itakuwaje ila tambueni kwamba mnavoendelea kuzubaa tunazidi kujiharibia kumbukeni hatumtafuti sisi tuu na ndio maana yule aliyeweka tangazo kwenye tv siku chache zilizopita nasikia kafungwa sasa kwetu umakini ni swala la muhimu sana katika hii kazi. .sawa mkuu umesomeka kwa hiyo kesho mkuu.ok tuonane kesho*******
Yalikuwa ni majibizano boss akilaumu kwa wafanyakazi wake kwanini wanashindwa kumshik ben ila wakajifariji na kuachana****

    Jaman mbona nimemmiss sana mwanangu ben sijui yupo salama kweli maana nina muda sijasikia hata sauti yake aliongea hivo mama huko nyumbani kisha akanyanyua simu na kuchagua namba ya ben ili ampigie simu lakini akajibiwa mteja unaempigia hapatikani kwa sasa jaribu tena baadae alitoa simu sikioni na kuitupa kwenye kochi kisha akaondoka na kwenda kulala

........................
Siku iliyofuata asubuhi simu yangu ilikuwa ikiita baada ya kuiwasha saa 10 za usiku nilinyanyuka kiuvivu maana nilikuwa bado ninausingizi "aaa nani tena tunasumbuana asubuhi yote hii shit,,,,,,,,, nilionfea maneno hayo baada ya simu kunishitua huku bado ninausingizi.. Niliipokea simu hiyo ambayo ilionyesha jina la naomi
Hallo naomi vipi za huko
.safi tuu mbona umetususa hivo
..amna sijawasusa sema watu mnanifanya nisiwaamini maana....
.kwanini usituamini tena
.ntasema tukuonana sawa
.sawa kwakuwa maneno unayo wewe ntasubiri tuu
.nnapokuja ntakwambia ila sitaki umwambie mtu yeyote yule
.powa usijali simwambii mtu ila ufike hadi hapa nyumbani maana tumekukumbuka ile mbaya
.usijali naa

Baada ya kuongea na naomi sikupata tena usingizi niliamka na kufanya taratibu zote nikachukua begi moja na lile karatasi alilonipa babu kisha nikaanza safari ya kwenda nyumbani baada ya kumuaga merry nilitembea sana nikafika sehemu fulani niliweza kuona watu wakiwa wamejazana wakiwa kama wanashangaa kitu fulani. Macho yangu na ubongi viliungana na kuweka mpango wa lazima ushuhudie pana kitu gani pale. Nililifuata lile kundi la watu nikajifanya naangalia ila sifikii juu nikawa najipenyeza katikati ya watu hadi nilifanikiwa kufika mbele kabisa ambako ndiko kuna jambo maalumu lililowajaza watu wengi pale baada ya kuweza kuona kinachofanyika nilipata hasira sana kisha nikajikuta na mimi nikiingia pale katikati hiyo yote ilikuwa ni baada ya kumwona rafiki yangu wa shuleni akipigwa na jamaa mmoja hivi ambaye anasura kama machete hivi nitaka nilivue begi langu ila nilikumbuka  maneni ya babu juu ya utunzaji wa lile karatasi ambalo linastaili nyingi juu ya upiganaji nikiwa nimevaa begi langu niliruka juu na kutua juu ya kifua cha huyu jamaa alianguka kama boga kisha nikawa nimesimama nikimngoja aamke, alinitazama kwa hasira kisha akataka aamke haraka ili anisogelee lakini alijikuta hana nguvu tena za kunyanyuka. Akatoa amri kwa wenzake mkanateni huyo mbweha asiondoke hata hatua moja,___ nilimshika mkono joel kisha nikaondoka nae kuendelea na safari lakini kabla sijaondoka kuna watu wawili nilihisi wanakuja nyuma sikutaka kujisumbua sana kwakuwa chini kulikuwa na vumbi nilitumia mguu wangu kuchapua lile vumbi na kuwarushia usoni walipoanza kujifutafuta ikawa nafasi ya sisi kuondoka lakini kabla hatujafika mbali niligeuka nyuma nikaona kuna mtu anakuja anakimbia huku akiwa na mti sijali nilimwacha aje tuu alipotaka kurusha mti niligeuka haraka na kuudaka ule mti na kumfumua teke la uso mda mfupi akawa yupo chini hajielewi mimi na joel tuliendelea kusonga mbele wakati huo wote joel aliona kama mauzauza tu huku njiani mambo ninayoyafanya tulitembea hadi nafika mtaani kwetu jirani na nyumbani nikaanza kumuaga joel lakini nikiwa naendelea kumuaga nilimwona god yule m mbeya wa darasa kule shuleni aliniona tuu alinyanyua simu yake akawa anatafuta baadhi ya namba lakini kabla hajapiga nilikimbia na kumuwahi asije akawa walewale na yeye. Baada ya kumfikia nilinyang'anya ile simu kisha nikaangalia ni nani anataka kumpigia
    Ivi na wewe kumbe ni mmoja wao mnaotaka kunisaka mimi huku uwezo hamna baada ya mimi kuongea vile god alitoa pipe na kuniwekea kichwani kisha akasema ben upo chini ya ulinzi lakini akiwa kazubaa akajikuta pipe ipo kichwani kwake.. Kisha nikamuuliza nani yupo chini ya ulinzi baada ya kuona vile akanyoosha mikono juu kukubali. Nilimnasa tu kofi zito kisha nikatoa risasi zote na kumtupia pipe tupu bila risasi alipoona nimemtupia vile akaikota haraka kisha akaanza kuvuta triger kwa lengo anipige na risasi zile, baada ya mimi kusikia ule mlio wa pipe isiyo na nligeuka na kumwambia kama umetumwa ntawanyonga wote  nikaendelea na safari yangu hadi nyumbani nilipoingia tuu ndani......itaendeleaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 21

Gangstar noma
By: benchrys
21

..oya we dogoooo hebu simama hapo nataka niongee na wewe baadhi ya mambo ya muhimu sana mdogo wangu------we dogo ben vipi inamaana hatusomani au unazingua bhana,,,, ilikuwa ni sauti ikiniita kutoka nyuma yangu sijui alikuwa ni nani maana sikuweza kumgundua hata kwa sauti tuu moyoni nikajisemea hata sitaki mazoea na mtu yoyote maana wanaweza nikwamisha safari yangu nikajikuta naishia tu njiani humuhumu,,,,, niliendelea kutembea lakini nikiwa natembea nisikia kishindo kikiwa kinatokea nyuma yangu tena nilitaka nigeuke lakini nikatumia tuu staili ya kuhisi kwa jinsi alivonielekeza kule porini basi haikupita muda nilihisi kama kuna mtu anataka kunishika begani lakini kabla  hajafanikiwa kunishika niligeuka na kumdaka mkono wake ndani ya nusu sekunde akawa ameinamia mbele hawezi kufanya chochote
        Oya mkono huo mwanangu hujui utauvunja acha upuuzi ukiona nimejitoa hapa wewe naumiza, alisema maneno yale yule jamaa ambae nilikuwa nimemshika mkono wake kwa kumzuia asiweze kufanya chochote kile,,,,, kwa hiyo wewe kwa ndoto zako unaota kwamba hapa unaweza kujitoa kirahisi tuu haya nambie shida yako ni nini na jina langu umelijulia wapi ukijitia mjanja huu mkono nauvunja jumla, nilimwambia hivo nikiwa bado na ule mkono wake ambao haukuweza kufanya chochote kile
M m iii sijaagizwaa na mtu kukutafuta kabla hajamalizia kuongea yale nilimpa kofi zito kisha nikamuuliza nani ka kwambia kuwa umeagizwa kumbe inaonyesha dhahiri kwamba umeagizwa sasa ndio utasema hebu twende acha ujinga niliahirisha hata safari ya kwenda nyumbani nikageuza nae kurudi kule kwa merry ilinikamshikirie aseme ukweli,,,,,,,,nilitembea nae kwa kuvutana hadi eneo moja hivi ambapo nikiwa naendelea kwenda walitokea vijana wawili wakiwa na nondo mikononi mwao na kuniamrisha oya mbona umemshika mwanetu kuna noma yoyote au mwachie basi sivyo tunakuzingua hapahapa,,, waliposema maneno hayo hata sikuwaza kumwachilia sijakaa vizuri kuna moja wao alinyanyua ile nondo na kutaka kunipiga nayo lakini kwa kutumia mkono mwingine niliidaka ile nondo na kuimfumua nayo mgongoni alianguka chini huku akiwa kama anavuta kamasi ishara ya kuonyesha analia kibishi sikujali hilo nilimfunga yule niliyemshika kisha nikamfuata yule mmoja ambae kwa  hapo alikuwa anatagfuta njia ili aweze kukimbia,,,,, kwakuwa niliachana nae kwa umbali fulani alipfika mbali alianza kunipa maneno ya kunitusi kwamba sikujali nikawa namfuata kumbe kulikuwa na nyumba jirani hapohapo akaingia kwenye moja ya geti ambalo lilikuwa jirani na kufunga nilikifanya nikachukua picha ya ile nyumba kwa kutumia simu kisha nikarudi kwa wale wengine nilifika nikambeba yule mmoja ambae bado anafahamu nikafika hadi kwa merry na kumpa kiti ok huu ndio mda wa wewe kunambia ni nani kawatuma kunuitafuta kwa kunifanya nimarafiki zangu ilimtume taarifa kwake,

Baada ya kuuliza bila kujibiwa nilikchukua waya mmoja na kuunga kwenye kile kiti na kumfunga kisha nikauliza tena hakujibu ila alicheka nikaona hizi ni dharau sasa nilichukua remoti na kubonyeza moja ya kitufe alilalama na kuanza kujieleza mwenyewe baada ya kuona anajieleza mwenyewe nikamfungua nakumwambia ok nakusikiliza ni nani kawatuma kwa kuogopa ile shoti ya umeme tena ilimbidi aeleze ukweli wote kwamba..

******kuna mzee mmoja hivi  alitukamata vijana ambao tulikuwa tunatoka mtaa mmoja na yeye alitufunga mda kama wa siku tano kwenye chumba ambacho kilikuwa kina picha yako ambayo iliandikwa wanted humo ndani tulikuwa tukiletewa kila kitu baada ya zile siku akatufungulia na kusema huyu mtu ambae mmemwona katika picha namhitaji nimwone akiwa ni mzima wakati wowote kuanzia sasa nimewapiga picha nyie wote wahiyo hamwezi kukimbiliamahali popote pale mtakuwa mkiondoka asubuhi nakurudi mda wa jion kila mtu akiwa na majibu yake kama mmemwona au lah, baada ya kuongea yale maneno akatupatia kiasi cha hela kila wetu na kusema atakae jaribu kutoroka atamtumia wanajeshi ili waweze kumkamata na kitendo kitakacho fanywa kwa huyo nadhani itakuwa ni mfano kwa wengine, sisi wote baada ya kusikia maneno yale tulikuw na woga na hatukuweza kumbishia kwa lolote lile ambalo alikuwa akiambia baada ya mda kidogo siku kama mbili akatupatia namba ya simu akidai kwamba ndio namba yako wote tukawa tunajitahidi kupiga ile namba kwa wakati tukiwa na muda maana kama salio simu zetu bada ya kutununulia aliunga kifurushi cha mwezi ili tusiishiwe muda wowote ndo maana ilikuwa juzi nilipiga simu ili nikupeleleze upo maeneo gani ilinimwambie aje kukuchukua,,,,, hayo yote yalikuwa ni maelezo ya yule kijana baada ya hapo nikamuuliza kwa hiyo wenzio ni akina nani hakusita akanitajia majina mengi sana ila nikapotezea nilimwambie aondoke na asijaribu tena huo upuuzi nilimfungulia na kumwacha aende zake

Nikiwa mtaani mida ya jioni nilionakundi la watu wakinifuata nikajifanya sijawaona kisha nikaanza kuondoka taratibu lakini hawakusita walinifuata tuu
;;;;;oya mbona tunafatiliaana mnamatatizo au na mimi au, niljihami hivo moja wao akasema kwa wenzao tunaongea nae nini sasa kazi ni moja tumnyakue tuu twendezetu kwamkuu baada ya mimi kusikia vile niliondoka mbio ili wapungue mmojammoja,,, na wao wakaaanza kunikimbiza ila spidi yao ilikuwa ndogo sana katika kukimbia

Baada ya kukimbia hadi kwenye ukuta mmoja niligeuka nyuma na kukuta wamebaki watatu,,,,, nikiwa naukaribia ule ukuta nilisogea jirani na ukuta ule nilidunda kisha nikajigeuza na kuwaachia mateke ya uso wawili kisha nikamsogelea yule mmoja kum-bamiza ukutani wote wakawa tayari wapo chini kisha nikaendelea na safari yangu ya kurudi homenikiwa naendelea kwenda mbele ulitokea mwanga mkali sana ambao ulikuwa ukiumiza macho haraka nikatoa miwani ya kuzuia mwanga mkali kisha nikaivaa nakubadili njia niliyokuwa nikiifata nikiwa naendelea kwenda kuna pikipiki ilikuja kwa kasi sana kidogo inipitie miguuni lakini nilidank na kuikwepa kisha aliyekuwa akiendesha akaenda kuanguka mbele baada ya mimi kuona kile kitendo sikumfuatilia nikaendelea kutembea niktafuta njia ya kurudi nyumbani mana hii mitaa nilikuwa nimgeni

Baada ya nusu saa nilikuwa nimeshaiona njia ya kuelekea nyumbani nikanyoosha njia ile ilinifikishe nyumbani kwa merry, kwa mbali niliona kama kuna watu wengine watatu wakiwa na nguo nyeusi zote na miwani, ningeweza kubadili njia lakini lakini hakuna chochoro ambayo mimi naifahamu kwenye huu mtaa maana hadi nilifika nilitembea usiku kwa usiku basi nilitembea hadi nawakaribia hawa watu wawili ambao wote niliweza kuona wakiwa wamebeba mabegi makubwa wastani niliwasalimia wote hawakujibu nikapita nikiwa naendelea kwenda mbele mara nikahisi nayemelewa mgongoni nilianza kama kukimbia nae akaanza kukimbia gafla bin vuu niliruka beki juu sana kisha nikawa nyuma yake,,, akiwa ameduwa nilimfumua teke zito ili kumwongezea safari yake aliburuzika kama gurudumu bovu kisha nilisogea na kumvua lile begi kuangalia ndani ya begi kulikuwa na bastola ndogo ndogo niliichukua na kuchana lilebegi kisha nikaondoka kuelekea nyumbani..

Nilimkuta merry akiwa amekaa tuu kipweke huku akibonyeza simu yake nilimsalimia kisha na mimi nikajiunga kuchezea simu, merry alisimama na kuwasha tv alipowasha tuu alikutana na habari ambayo hata hakutaka kuamini nakubaki amenitumbulia macho maana ilikuwa ni breaking newz

Ivi we ben hizi habari ni kweli au wanazingua tuu,,, ni swali ambalo lilitoka kwa merry baada ya kushngaa kwa muda mrefu akiwa haamini zile  taarifa za kwenye tv,,, habari ilisema.itaendeleaaaaaaaaaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 20

Gangstar noma
By: benchrys
20

.niliipokea ile namba ngeni ambayo ilikuwa ikiita kwa ule mda ndipo nikaja kusikia sauti ya mtu wakiume ambae hata nilipojaribu kuvuta hisia ili niigundue sauti ile ni ya nani sikuweza kuigundua kabisa alikuwa akiongea mada ambazo kwa akili yangu niliona tuu ni kama  ananipotezea mda wangu kwa yale mambo ambayo alikuwa akiyaongea
;;;oya nakusikia mda wote kunifosi nikwambie maeneo ambayo mimi nipo shida yako nini nawewe ni nani mbona sikusomi mkuu!!!!!
;;;;;ahaaa mwanangu ben ee unazingua inamaana hii sauti huigundui kabisa au nsio lengo lako uniyeyushe acha kuzingua bhana uko wapi wapi wewe mimi nataka tumeet now mkuu au mimi ninanoma na wewe,,,,
;;;;;;kudadeki zako kama hujielezi na mimi nakata simu yangu mana unanimalizia tuu chaji na sina aina ya umeme wa aina yeyote huku so acha kuzingua we nani?
       Nilijitahidi kumwuliza yeye ni nni lakini hakuweza kunitajia jina lake ni nani na hata angenitajia ningejua kwamba tayari huyu ni mwongo baada ya kuongea hayo bila mafanikio ya kumjua yeye ni nani nikaona isiwe shida hata kidogo sikupoteza mdfa hata kidogo nilikata simu kisha nikamalizia kupata chakula na kwenda kuendelea na yale mazoezi ya kupasua yale maboga nilitumia nguvu kujirusha kama babu alivo fanya mara ya kwanza hadi akapasua niliweza kupasua boga moja nikarudia mara nyingi nikaweza kupasua boga na la pili baada ya hapo nikawa na uzoefu maana niliweza kupasua yale maboga kumi na zaidi ya yale aliyo nambia babu niyapasue baada ya hapo nikaanza kuondoka kwenda upande wa ile miti kabla sijafika mbali nikasikia mtu akipiga makofi ishara ya kushangilia niligeuka nyuma ndipo niliweza kumwona babu akishangilia akasema nadhani sasa umeweza hatu aya kwanza hongera sana ok hatua inayofuata nenda kwenye miti sasa na ujitahidi kuvunja nitakuwa na zawadi kwaajili yako ukiweza kila kitu vizuri alimaliza hivo kisha mimi niliondoka pale
       Huu mda niliipiga ile miti kwa nguvu sana na kwa hasira ya kupata ile zawadi ambayo babau ameniahidi kwamba atanipa kama nitaweza kupatia kila atakachonifunza nijitahidi kwa jihudi zangu kupiga hii miti lakini niliweza hatua ndogo tuu ya kuutikisa mti kwa ngumi nikajitahidi kuongeza nguvu zangu lakini nilikuwa tayari nimeshachoka nikataka niangalie mda ni saa ngapi nikakumbuka kuwa simu niliiacha kuondoa usumbufu basi nilijifunza hadi inaingia jioni ndio nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka vibaya tulikula chakula cha usiku tukalala lala

*********************

Asubuhi nilishitushwa na mlio wa simu yangu maana jana nimelala kama mzoga vile kwakuwa sikuzoea kufanya mazoezi hata kupiga pushapu
Nilikurupuka toka nilipolala na kuifuata simu ilipo kisha nikaipokea baada ya kuona ni namba ya merry ikipiga

;;;;hallo ben vipi!!
;;;;safi tuu za huko sister
;;;;huku kupo fresh sema tuu wanakusaka bado sijui wana nini hawa watu
;;;;aaaaa waache wanitafute tuu wakijisikia kuacha wataacha
      Niliongea hayo na merry kisha nikanawa uso na kuendelea na mambo mengine kiufupi niseme katika kuishi na huyu babu shughuli yangu kubwa ilikuwa ni mazoezi na siyo swala jingine niliizoea hali hiyo pia niliendelea kufundishwa mazoezi mengi zaidi baada ya hapo nikawa tayari nipo vizuri ilichukua muda kama wa mwezi mmoja hivi ndipo babu aliponiambia ben saiz unauwezo wa kuondoka hili eneo ila kama ukijisikia unaweza kunitembea lakini nitakuomba kama unakuja unipe taarifa ya kwamba unakuja kunitembelea sharti ukiniona huko mjini kwenu usje jaribu kuniita mwalimu tena na  hata ukiniona jifanye hata hunijui kabisa maana sihitaji mtu yoyote ajue haya mambo niliyokufunza huku kwenye eneo langu la siri na ndio maana sikutaka hata kukwambia hili eneo linaitwaje isipokuwa kajifunze kusoma ramani za maeneo kadhaa kupitia computer pia jitahidi kuwa mdukuzi lakini mwenye break na mambo ambayo anayoyafanya

*****baada ya babu kuongea yale yote akanionyesha mtumbwi ambao naweza kutumia ninapoondoka kurudi makwetu halafu akanikabidhi kisu fulani chenye urefu kama vile vya maninja lakini sikuona ajabu maana hivo vyote alishanifundisha jinsi ya kuvitumia kwa  kupambana kisha akanikabidhi kitu kama kisu na kuniambia humu unaweza kutunzia dawa zako unazotumia ila nimekuwekea chache humohumo mwisho akanipa kitu fulani kama karatasi na mkoba fulani mzuri kweli akanambia hili karatasi tumia njia zote unazojua mtu asilione hata kwa bahati mbaya nilimwitikia babu kisha tukapeana ishara na mimi nikaanza kuufuata mtumbwi alionionyesha na kuongoza nao kwenye ule mto wenye mamba,,, taratibu nikaanza kufuata njia kurudi kule nilikokutana na babu sikuweza kupatwa na jambo lolote hadi nilipofanikiwa kufika hapo nilishuka na kuanza kuzitafuta njia za kunifikisha nyumbani kwa merry lakini nikaona itakuwa sio vyema kama ikitokea naenda kimyakimya bila kumshitua kwenye simu nilinyanyua simu yangu na kuitafuta namba ya merry na kuipiga aliipokea kwa haraka na kuniuliza vipi umerudi nini nilimwambia ndio nimerudi upo wapi saizi akanambia hayupo nyumbani ila alinielekeza mahali ambapo ameziweka funguo na mimi nilikata simu na kuelekea nyumbani kule lakini kabla sijakamata njia vyema ndipo niliweza kumwona kijana mmoja hivi aliyekuwa akiongea na mwenzake niliposikiliza sauti nikakumbuka huyu ndiye aliye nipigia simu ili kuhakikisha nilichukua simu yangu na kupiga ile namba simu ilianza kuita kwake pale akapokea kwa shobo yap ben engo zipi mdau wangu nilimwambia kwa sauti ya chini nyuma yako akageuka na kuniona mimi ben huku nikiwa na begi fulani lefu akataka kujifanya anajua ubabe akaniamrisha ben dadeki sisi tunasanda kufanya kazi za watu kukutafuta halafu wewe unakula bata tuu na mabegi kama hayo hebu lilete mda wote nilikuwa nikimwangalia tu,,, nae hakuzubaa akanisogelea na kutaka kuvua begi, nikaona sasa huku ni kuzoeana nilifutuka na kumpiga na bonge la teke la kifua alianguka chini huku akikohoa kwa shida hapo na mimi nikaendelea na safari zangu

*******nilifika hadi nyumbani kwa merry mda mfupi tuu ndipo nikatafuta chakula mahali aliponielekeza kipo nilikila kwa fujo kweli mana nilikuwa na njaa ya safari ya kusafiri kwenye maji yale zoezi halikuchukua muda mrefu sana na baada ya hapo nilielekea kule kwenye chumba changu ambacho nilipewa pindi nafika kwa merry siku ya kwanza nilikiona kama nilivokiacha moja kwa moja nikanyosha kuelekea kwenye computer ili kuendelea kujua mambo zaidi ya yale ninayo fahamu muda ulienda merry nae akawa amerudi nyumbani tulisalimiana tukaendelea na mambo yanayotakiwa iliingia mara masaa nayo hayakukaa nyuma yakawahi ikaingia jion merry aliwasha tv ili tuweze kusikia hata taarifa ya habari japo kwa ufupi wote tulitulia ili kusikiliza
****familia moja imevamiwa na kuporwa kiasi na mali nyingine habari zinaonyesha kwamba……… sikutaka hata kusikiliza sana baada ya kuona ni nyumbani kwetu niliingia kulala kwa hasira ili siku yapili nijiandae kwenda nyumbani kwetu ambako ndio kwa baba na mama nililala lakini niliona kama usingizi hauji kibaya nikahisi kama hata saa kuna mtu anaichezea ili ichelewe kuumaliza usiku huu ila baada ya muda mrefu sana nilipitiwa na usingizi kwenda wapi tutajua mbeleni,,,, lakini kabla usingizi haujakolea vizuri simu yangu iliita nilipo ipokea ikazima shit!!! Kumbe sijaichaji niliiweka simu chaji kulala***asubuhi ilipofiika nilianza safari yangu kwenda nyumbani lakini nikiwa njiani……itaendelaaaaaaaaaaaaaaa

Benchrys.blogspot.com

De 19

Gangstar noma
By: benchrys
19

………wewee unala hadi muda kama huu ukija kwangu hata siku nyingine kama utakuwa umejisikia mwenzenu anasema hapa kazi tu ila kwangu tofauti hapa ni mazoezi tuu maana hii ndo chai kabla ya chochote kilelazima nianze nayo asubuhi sasa nifate twende kule mlimani,,,, aliongea maneno hayo babu kishanikaanza kumfuata kikwelimda ule wote nilikuwa bado nina akili zangu za usiku kwa hiyo niliona ni kama ananipanga mambo ambayo hata hayako kwenye mudi zangu kwa wakati ule nilitembea kivivuvivu lakini akanilazimisha tuanze kukimbia ‘’’’’’ ah babu ee inamaana mazoezi si kule mlimani au tunaanza hukuhuku tena
      We acha maswali mengi hebu twende kazi utaiona hukohuko wewe haiwezekani ukawa eti unakuwa mwoga mwoga kama nini sijui….. aliongea vile babu kisha tukaanza kukimbia hadi tulifika kule mlimani nilikuwa nikihemeana mdomo wazi kama mbwa ambae ananjaa halafu jua kali dddduh we kijana utakufa hebu bana pumzi hiyo hujui unapoteza nguvu baada ya yeye kuongea vile ndipo nikajua hapa inaonekana zile muvi za kichina ninazoziangaliaga leo ndio nitashuhudia kweli hadi akina doniyen jinsi wanavofanyaga mazoezi yao
Basi nilisogea mbele kidogo nikiwana babu ndipo nilipoweza kuona miti imechomekwa chini ya ardhi na kuzungushiwa kamba fulani ngumu babu akanambia badilisha hizo nguo zako kisha zivae hivi hapa kisha aknirushia manguo fulani ni mazito kama gunia lililo lowa na maji kwakuwa sikuwa na ujanja ilinilazimu niivae tuu kugonja jambo ambalo linafuatia sikaniambia kuna mazoezi kisha akasimama kwenye kilima kidogo na kuniita akaniambia inatakiwa tukimbie hadi kuifikia ile alama ambayo unaiona pale aliponiambia kukimbia nikajisemea kama kukimbia hapa amefika mwenyewe najua kukimbia vizuri tu……… safari ikaanza tulikimbia umbali mrefu kweli hadi mwenyewe nikashangaa mbona lipoonyesha niliona kama alama ipo jirani sana halafu mpaka saizi hatufiki tuu hapo
Babu, babu, babuu mi sinakuita nilimwita babu huku tukiwa tunakimbia vile lakini hakutaka kuitika na mimi nilikata shauri niliendelea tuu kukimbia baada ya dakika kamam thelathini tukawa tayari tushaion aile alama ndipo wote tulisimama nikamuuliza babu ivi hii alama inatembea na yenyewe au mbona tumefika mbali sana hadi daah babu alinijibu haitembei isipokuwa huu ndio umbali ambao hii alama ipo tusipoteze mda inatakiwa turudi nyumbani tukapate kifungua kinywa,,,, daaah tupumzike kwanza babu akaijibu ungekuwa mwenyeji haya maeneo haya ningekuacha upumzike lakini hapa ili eneo hulijui hata kidogo mimi naondoka utajua mwenyewe babu akasimama kama utani nakuanza kuondoka, baada ya kuona babu anaondoka ikanibidi na mimi nishike njia huku nikiwaza dah kwa umbali huu sinitafika hata maji mwilini hakuna ila hakuna lolote acha tuu niamshe na mimi nilikimbia kwa kasi kidogo nikamkuta akasema nilidhani unabaki siumesema unapumzika wewe au hapana ningebaki halafu nirudi na nani nyumbani

Tukiwa tumefika nyumbani tayari hata sikuwa na  hamu ya kula maana wanasema bora ukimbie mbio ndefu ndefu kuliko kubip kukimbia maana itakukost mwenyewe kwa hiyo nilipofika nyumbani hata sikitulia nikaendelea kupasha miguu kwa kuruka ruka baada ya mda kidogo nilitulia na kupata kifungua kinywa kisha tuliendelea na mazoezi kama alivoniambia mwanzo safari hii akanambia inatakiwa upasue maboga haya kwa mguu wako yaani nipige teke boga hadi linapasuka,, aliponiambia vile nikaona huu utani nikamuuliza babu ivi wewe unaweza kufanya hicho ambacho unanambia mimi nikifanye babu akanambia hivo vyote mimi naweza ndo maana nakwambia ufanye
Awe basi onyesha mfano nilikuwa nikiongea yale kwasababu maboga yale yalikuwa yapo juu kwangu mimi yaliniishia kwenye kichwa na kwa babu ilikuwa ni zadi maana yeye hakuwa mrefu kama mimi….. babu alikunja suruari yake kidogo kisha akjivuta na kupiga zinga la teke kwenye lile boga ambalo lilikuwa karibu nae kisha akanigeukia na kunambia huo nimfano ambao umehitaji sasa kazi ni kwako nakupa dakika therathini uwe umepiga maboga matano, baada ya kusema vile yeye akaondoka alienda wapi hata sifahamu mimi nikawa naendelea kujaribu kupiga yale maboga lakini hadi zilifika zile dakika alizoniambia ilikuwa bado hata boga moja sijafanikiwa kupiga na yeye ndio alikuwa anarudi nikiwa sina hili wala lile nilipiga miguu nikajikuta tayarai nishapiga magoti chini kisha akasema fata ninacho kifanya mimi nae alikaa chini akawa kama anataka kulamba ardhi kwa ulimi wake jambo ambalo haliwezekani na mimi nikajaribu lakini sikuweza kufikia kadri yeye alivyo fanya ndipo akanyanyuaka na kuja kunigandamiza mgongoni kwa nguvu nilitamani nilie lakini nilijikaza kiume tuu nilikaa vile kama dakika kumi ivi kisha nikawa kama tayari nishazoea hivi baada ya nikawa kama yeye alivofanya
Alisimama kwenda kungalia yale maboga kisha akasema inamaana hata moja tuu hujapiga niliitikia kwa kuogopa ndi-i-i—oo sijapiga maana nilijua iliniweze kuna mazoezi ambayo yatahitajika akasema sasa utaweza kwa nguvu tuu njoo huku nilimfuata akasema pitia kwa huko nilifuata alichoambia,,, ile njia niliyopita kumbe aliweka mitego ya kamba sijui maana nilipokuwa nikipita nilikanyaga vibaya nikavutwa juu kwa haraka tena kila mguu na kamba yake kisha akaja huku akiwa anacheka akanmbia kijana umakini ni kitu cha muhimu sana kisha akaondoka hapo ndio nilipoanza kutoa sauti ya kilio maana zile kamba zilizo nifunga naning’inia kila kamba ilianza kuvuta mguu wake kwa upande wake maumivu niliyoyapata hata asiulize mtu yeyote nilivutwa hadi miguu ikawa imenyooka kote baada nikawa nimetengeneza kama T nilibaki kama nusu saa tena kilio kilitulia kisha nilibaki vilevile hat sauti ya kuita babu sikuona kama kutakua na msaada wowote nilibaki tu nimetulia vile hadi maumivu yalipotulia lakini yalipotulia kamba ilirudishwa halafu ikavutwa tena kama kunitonesha hivi,, kwa wakati huu hata maumivu hay kuwa kama pale mwanzo niliona kama nisawa tuu niliwekwa vile kama dakika tano kisha nikaachiliwa tena kwa kulegezewa kamba ile ikanishusha hadi chini mwanzo nilipata shida sana kuanza kutembea ila baada ya mda nikawa safi kabisa baada ya hapo bau akaja na kusema nadhani saizi utaweza kupasua hayo maboga ila subiri kuna ile miti inatakiwa ukomazie miguu yako utakuwa ukipita ngumi na mateke nayo hadi utakapo fanikiwa kuvunja hata miti mitatu tuu safari hii nakuhurumia baada ya yeye kuongea vile niliitikia sawa kinyonge halafu nikaenda kuanza kupigana na miti ile miti yenyewe hata haitikisiki nikataka nimwambie anipe mfano napo ila roho ikasita nikaendelea kufanya peke yangu baada ya mda wamasaa akaja kuniita kwaajili ya chakula niliondoka na kumfuata huku mikono namiguu ikiwa inaniuma vibaya mno nilienda hadi ndani na kula kibishi hivo maana huku sidhani kama  kuna kudeka kwa yeyote yule

*****nikiwa nimekaa simu yangu ilianza kuita niliipokea nikasikia sauti ya mtu akiwa analia na haikuwa namba ya mtu mwingine alikuwa ni Naomi
;;haloo we naomi unalia nini
;;hallow mama  hukua anaumwa inatakiwa uje haraka iwezekanavyo, baada ya naomi kuongea vile nikajisemea dah sasa hapa inakuwaje sasa sehemu yenyewe niliyoko hata siifahamu sema tuu namtegemea huyu babu hapa sasa hapa nitafanyaje kurudi nyumbani,,,,,,nilijisemea hayo yote moyoni mwangu bila kupata msaada wowote baada ya mda tena simu yangu ikaita nilijua labda ni naomi anapiga tena niitazama simu ndipo nikaona……itaendeleaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

benchrys.blospot.com

De 18

Gangstar noma
By: benchrys
18

.........mkuu wao alikuwa tayari yupo chini akiwa anatoa povu mdomoni akiwa hajielewi kabisa..basi baadhi yao walimchukua na kumwingiza kwenye gari kwaajili ya huduma ya kwanza huku wengine wakijiandaa kuanza mashambulizi dhidi ya merry lakini merry nae hakuwa zoba maana anawaza mbali kama draft dume kwenye computer wakati wao wakijadiliana kuwa wamshike ili wampe kipigo kitakatifu na yeye alikuwa akipiga hesabu namna ya kuwatoka na kuwapa adhabu na kuwashikisha adabu mipango walivokuwa wakiipanga
::::::::::majambazi:::::
Oya wadau huyu dada asituletee miyeyusho kama mnavoona kichaa wetu tayari yupo chali hapa na sisi kukimbia haitakiwi lazima ajue sisi ni akina nani tumpe kisago cha kutosha baadhi yetu mtamkamata na wengine watakuwa na kumpa kipigo cha maana tuu..........

::::::::merry:::::::::
Duuh ivi hapa bila mimi kujiongeza wanaweza niua mana hadi hii hatua sijajua wanawaza nini kwenye vichwa vyao kwa hichi kitendo nilicho fanya ila hapana nawaomba radhi kuwa ni bahati mbaya wakinizingua naingia ndani kama naogopa hivi kisha wakijaa mlangoni kama kawa nawapa shoti tuu watoto wadogo hawa hawana lolote.......

****"samahanini jaman naomba mnisamehe ni makosa tuu ila sio makusudi naomba mnisamehe kwa tatizo hili nisameheni  jaman ni bahati mbaya tuu.....ilikuwa ni sauti ya merry akiomba msamaha kwa wale watu ili ajue msimamo wao watafanyaje...ila na wao kwakuwa walishakuwa na mipango yao hata hawakupoteza mda ili waharibu wakaanza kumsogelea merry ili wamshike nae merry kwakuwa mipango yake iliendapowa akaanza kuondoka kuingia ndani kwake kisha akalock mlango kwa ndani kisha akawaandikia kwenye kikaratasi kwamba "ondokeni hapo kama mnataka amani" lakin bado tuu wakutoka pale mlango  Hawakutoka  kwa kujitia et wanataka kuvunja mlango ili waingie kinguvu mle basi nae baada ya kuona vile hakuchelewa akabonyeza batani yake ya remote ambayo ni kwaajili ya shoti na kweli baada ya mda watu wa pale nje walianza kulalamika kama mtoto kachapwa kwa kuonelewa na mtu ambae sio mzazi wake
....

Ben nae baada ya kuhihisi kukaa ameshachoka basi akajitoa kutoka kule chini ili aweze kuonana na merry alijaribu kutoka mlango ukawa umefunya akatafuta njia nyingine ya siri ambapo hiyo njia ya siri alipopita ghafla alijikuta akiwa nje kabisa, kupepesa macho kwa mbaaala akaona kama kuna kundi la watu wanamfata ben akapiga akili
''"duuh sasa hii shida hapa nkiludi ndani washanioa bora niwaenjoy nione nikidakwa basi...... Ben niliondoka mbio kutoka pale niliposimama kugeuka nyuma bado nikaona ninafwatwa tuu nikicheki mbele hakuna njia zaidi ya poli lililonisonga sikuwa na namna niliingia ndani ya lile pori huku nikiwa makini....

Huko nyuma nako wakawa bado wakimtafuta tuu ben ila baadae walisimama ili wajadiriana Watumie njia gan ambayo inaweza kuwa rahisi kunishika mmoja wao akasema hapa tukafuate pikipiki hata mbili zinatosha wakaona ni wazo la maana kwasababu hawajui niko wapi kwa mda ule hawakupoteza hata sekunde wakawatuma wenzao wawili ili wakafate pikpiki hizo huku wengine wakiendelea kusonga mbele kwa miguu....
     Upande wa ben nilikuwa nimetembea hadi nahisi miguu yangu kuzam tumboni daah sasa hili tatizo inamaana saizi mimi naishi kama mkimbizi maisha gani nilijisemea hivo baada ya  kujiona nmechoka sana ila sikukata tamaa eti wanikamate kisa nimechoka hapa nakufa kiume dadeki zao, nilijipa moyo gafla nguvu zikaja nikaanza tena kuchanja mbuga huku nikiwa napeleka miti pembeni ili niweze kupita kwa urahisi kufika mbele palikuwa na kamto sio kakubwa sana ila kana nyasi nyingi sana mwanzo nilitaka niruke ili niende upande wa pili halafu niendelee kukinbia ila roho ikasita nilipotulia nikasikia kama vishindo nyuma yangu ila nadhani walikuwa mbali kidogo niligeuka nyuma pengine naweza ona chochote ila sikuona kitu niliporudisha macho mbele niliweza kukutana na mzee mmoja akiwa katika mtumbwi wake anasafiri na mimi sikusita nikaomba lift yule mzee hakuwa mchoyo aliniambia njoo tuu kijana twende kisha akanisogezea hadi jirani na pale ambapo mimi ambapo nilisimama nilipanda tuliendelea na safari tulienda umbali mrefu nisijue tunaenda wapi ikafika sehem fulani kulikuwa ni eneo tulivu sana hapo ndipo mzee yule alisimamisha mtumbwi ule na kutaka nishuke nikajifanya kuleta nyodo akanambia jitie mpumbavu hivohivo haya maeneo yana mamba looh baada ya kusikia vile niliruka mwenyewe kwenye mtumbwi na kutua hadi pembeni kabisa, yule akacheka kisha akasema ahaaaa kumbe mwoga hivo eeeeh utaogopaje kitu kama mamba eti. Duuuh we mzee mchawi au inamaana we huogopi mamba kabisa nilimuuliza hivo nae akajibu siogopi ndio na ndo mana nmesafiri kwenye huu mto mana huu wote unamamba kama kumi kwa idadi yaani kutoka pale nilipokukuta hadi hili eneo....yule mzee alivoongea vile nilibaki nimemkodolea macho ila yeye aliendelea ni kweli tena hata usishangae mwingine yule pale angalia kwenye maji....mamaaaaaaa weeeee ni kelele nilizotoa baad ya kumwona mamba kwenye maji tuliyotoka
  Haya tuendelee na safari kijana au jee...ah sawa babu twende tuu ila usinifanyie ubaya wowote ule..aha bhana ee sa ubaya gani nikufanyie mimi tena wewe.. We kama huogopi mamba mtu mzuri kweli wewe sidhanii..haya kijana naweza kuwa msaada kwako lakini..sawa ntashukuru zilikuwa ni moja ya stori tulizokuwa tukiongea tunapotembea sio mda mwingi tukawa tumefika eneo moja ambalo lenyewe lilikuwa ni kubwa lina sehemu zenye milima kulikuwa na mto ambao maji yake yametuama kwenye mawe meupe na maji ni masafi
    Kijana jisikie upo kwenu tena uwe huru nilifurahi kwakuwa mazingira yake yalinivutia sana mana ni kama sehemu za wahindi ila ile nyumba ya mzee yule ilikuwa kama tempo zile ambazo mara nyingi ni kwa wachina ndio zinatumika......
.....jaman huyu ben hajatoka tuu we beniiiiiiiiii, beniiiiiiiii toka huk bhana dah alikuwa nj merry baada ya kuona myda inayoyoma na bado mimj sijatoka tuu aliniambia nijifiche alinitafuta bila mafanikio inamaana alitoka wakamfukuzia au mbona huu mlango upo wazi nani katoka baada ya kujiuliza maswali hayo akanyanyua simu yake na kumpigia ben simu iliita ikapokelewa lakini mazungumzo hayakuweza kuwafanya waelewane lugha kisha merry akaona isiwe shida akatuma meseji "we ben uko wapi au wamekukamata... Baada ya mda si mwingi ben akareplay hawajishika ila nadhani bado wananitafuta katika msitu mmoja hivi na mimi nipo mbali sana naomba tunza hivo natarajia ntakuja kurudi sio mda mwingi basi merry alipika na kula hatimaye mda wa kulala ulifika na kwa ben ndivyo ilivokuwa

::::::porini ilipofika asubuhi ben akiwa amelala aliamshwa na yule babu mida kama ya sa kumi na mbili hivi

"aaah babu nini kwa sauti ya kiuchovuchovu babu akasema acha kulala huu mda wa mazoezi hebu amka usipoamka nakuwekea ngee.... Ah sawa sawa sawa mzee naamka nge!!!! Ben nae akaamka kisha ...........itaendeleaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 17

Gangstar noma
By: benchrys
17

.........niliipokea line ile ya merry ambayo haitumii kisha nikajaza zile namba ambazo wamezitaja kwenye lile tangazo niliziandika kwenye simu baada ya hapo maongezi yakawa hivi
..hallow habari za sasa bila kukosea nadhani hii ndiyo namba ambayo mmeitaja kwenye tangazo kwamba atakae mwona ben atoe taarifa kupitia hii namba si ndiyo.. Baada ya kuongea hivo nilijibiwa ndio hii ni namba ya kutolea taarifa za kuhusu kupotea kwa ben mana tumemtafuta sasa linakaribia wiki moja Kuisha,, baada ya yeye kusema vile nilimjibu ok huyo ben ni nan yako wewe mpaka uwe na bidii ya kumtafuta hivi....yule niliyekuwa nikijibizana nae akajibu acha uboya ben ni mwanangu halaf wewe unipe maswali kama hayo pu****vu kweli wewe baada ya kuongea hayo alikata Simu kwa hasira hapa pembeni merry alikuwa akicheka tuu.. Baada ya yeye kukata simu nikatuma meseji kwenye ile namba inayo someka

****pole kwa mpango wako wa kitoto mimi hapa ndio benchrys mwenyewe sasa subiria kidogo utapata majibu yako*****

Baada ya ule ujumbe kupokelewa kwenye simu yake alipiga simu tena kwenye ile namba lakini sikuhitahi kupokea akatuma na meseji tena akidai kwamba tafadhali pokea simu hiyo kisha akapiga tena simu lakini sikupokea.....

Baada ya hapo niliwatumia ujumbe nyumbani wa kwamba naomba namba za polisi za jirani,,, baada yamda mfupi nilipokea ujumbe kwenye simu yangu sikuchelewa nilizinakili zile namba kisha nikapiga....

***ya kituo cha polisi moja kwa moja nani anaongea tukusaidie.. Na mimi ili wasishituke niliwaambia kwamba jina langu naitwa bon akanijibu ndiyo bon naweza kukusaidia nipe shida yako. Baada ya yeye kusema hayo akawa tayari ashanipa uhuru wa kujieleza.... Nilimwambia lengo bila kupoteza wakati na kukata simu haikupita dadika hata tano simu yangu ilianza kuita nilisita kupokea kwa kuhofia naweza jikologa mwenyewe nilipoangalia kwenye simu niliona ni namba ngeni ilikuwa ikipiga simu sikuipokea ile simu baada ya kuita kwa mda mrefu ilikata kisha ikaingia meseji nayo hata sikutaka kuisoma mana nilishahisi lazima atakuwa huyuhuyu tu si mwingine siku hii ilipita kwa staili hii siku iliyofuatia ile namba ilipiga tena kwakuwa ile line ngeni nilishatoa niliipokea na kuweka sikioni lakini nilibaki kimya kama kawaida mpaka yeye aanze kuongea nikiridhia ndipo na mimi naitikia
"oya ben nhaje mkuu
"full nan wewe
"wewe acha kuzingua inamaana hii namba huna zarau
"kudadeki kama hujielezi nakata simu sawa
"kama kila nijieleze fwesh joh langu
"ok hamna noma tufanye nna zarau,,,, nilijibu hivo na kukata simu lakini baada ya muda nikaja kuikumbuka ile sauti maana ilikuwa ikifanana na sauti ya god aliyekuwa m mbea wa darasa ila kwanini atumie namba ngeni au nae kasetiwa boya kweli huyu yupo simpo kama yebo hivi shit.....nilijikuta nikijisemea hayo pekeyangu......

       Siku iliyofuata asubuhi mida kama ya saa tano na nusu hivi nikiwa ndani nikasikia sauti za watu kulia nje nkajiuliza kuna nini huko lakini kwakuwa sikuwa mhusika sikufanikiwa kujua chochote mana nilikuwa nipo ndani bado kwa haraka nikataka nitoke ili nikafahamu nini kimewasibu hawa watu mpka wanaliliana hadi mikelele kwa sisi wengine nikakumbuka kwamba kuna ile remoti inayohusika kwaajili ya alarm na shot kwenye hii nyumba nilitafuta ilipo kisha nikabonyeza kitufe kilichokuwa kina alama kama ya kengele hivi hapo zilitokea kelele nyumba nzima hadi mimi mwenyewe nilianza kuogopa maana ilikuwa kila kona ya ile nyumba ni kelele tuu yani...
Nilikuja kushtuka baadae baada ya kuangalia nje na kutowaona tena wale waliokuwa wanalia hapo nikajua vyema kwamba hapa nishaharibu tayari hayakupita hata masaa nilianza kuyaona magari yale ambayo yaliisogelea shule ile siku yakiwa na watu waliotinga nguo za jeshi nilishuhudia hayo yote kupitia kile kioo ambacho kipo ukutani baada ya kuona vile niliianda tena remoti kwaajili ya shoti endapo wataleta fujo zao niweze kufanya yangu akashuka baba mmoja kwenye gari ambalo lilikuwa mbele kabisa akiwa amevaa suti nyeupe huku yupo na walinzi wanne nyuma yake baada ya hapo walishuka wengine waliokuwa kwenye magari mengine huku wakiwa ns sare maalum nilipoangalia vizuri niligundua ni wengi kana kwamba hata idadi yao sikuweza kuijua kiurahisi,,,,, lakini kwa wakati nilikuwa sijifikirii mimi nilichokuwa nawaza ni kwamba merry ataingia vipi humu ndani lakini nikiwa naendelea kuwaza nilihisi kushikwa bega kabla ya kugeuka nikavuta pumzi maana mawazo yangu yalijua kwamba baadhi yao tayari washaingia hadi ndani ila nilipogeuka sikuamini kumkuta merry akiwa mule nilitamani kuuliza ameingiaje lakini sikuwa na wakati kabisa wa kuuliza baada ya hapo alipokea ile remoti kisha akasema funua pale kuna mlango kachukue mabegi yale yote kusha tumbukiza hapo wewe kajifiche kwa siku zile..... Aliposema niliona kama ashakuwa mdogo kiakili ndipo nikamuuliza kwa kumwambia merry kama ni utani huu wa leo to much mi ntafunuaje malumalu hizo si utani huu ila yeye alisisitiza kwa kusema chelewa ile kwako cjui mwenyewe we nenda kajaribu kama hapafunguki niliondoka na kwenda kufunua nilipofika pale nilitumia nguvu nyingi kuvuta kumbe hata hapahitaji nguvu "duuhh nyumba za wenyewe hizi jaman" baada ya kufungua kutokana na nilivyoviona kule chini nilijisemea hivo_basi nilifanya kadiri alivonambia kisha nilienda kujificha nilikoambiwa nijifiche

.........baada ya mimi kujificha merry alitoka nje na....... Lakini kabla hajafungua mlango hadi mwisho zilipigwa risasi za hewani mfululizo kutoka kwa wale watu. Walikuwa na maana gani hakuna aliyeweza kufahamu ila merry hakuwa mwoga alifungua mlango akawasalimia kisha akawauliza naweza kuwasaidia mnahitaji nini
"tunahitaji sisi ni kajana mmoja kwa jina ben inasemekana yupo hapa na sura yake ni hii hapa akachomoka mmoja wao akiwa ameshika karatasi kubwa yenye picha ya ben akimuonyesha merry kisha wakamuuliza jee unaweza kutusaidia kwa hilo.....
"hapana siwezi mana hii sura hata kwangu ni ngeni. Baada ya merry kujibu vile yule kiongozi wao akasema kamtazameni ndani. Wale watu wake nao wakajitia ni vipele kutaka kuingia kwa nguvu mle ndani kabla hawajafanikiwa kuingia merry akawambia nyumba yangu nyie mnajifanya kuijua ok nendeni huko ndani tuone. Walicheka dharau kisha wakasema mtu mzima hatishiwi nyau ngoja tuingie sasa, walimsukuma pale aliposimama ili waingie ndani lakini walipofika kati ya mlango na mlango walisimama kusha mmoja baada ya mwingine alianza kugeuza na kurudi nje hadi wote baadhi yao walitoka huku macho yanamachozi kiumbali,,,,
   Vipi mmeshamaliza kukagua au bado mana mmetoka mapema mno nipeni mrejesho. Hakuna aliyemjibu kila mmoja alielekea kwenye gari lake na kuweka standby kwa kuondoka, yule mkubwa wao alimwangalia merry kwa hasira akarudisha mkono wake mmoja nyuma baada ya mda kidogo ulisikika mlio "paa" hadi ben alikokuwa kajificha alistuka na wale wote walioingia kwenye magari wote walishuka baada ya kuona......itaendeleaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 16

Gangstar noma
By: Benchrys
16

.......nilikipokea kile kufaa ambacho alinikabidhi  baada Ya hapo akanambia soma maelekezo usipoelewa utaniuliza, swali la kwanza kumwuliza ilikuwa.. Hiki ni kwaajili ya nini hakusita akanijibu kwamba hichi ni kwaajili ya kupigisha short kwa mtu ambae atakuwa amejaribu kuisogelea hii nyumba endapo mimi sijapenda ujio wake siwezi nikamwacha hata kidogo mana kama hawa wanakutafuta wewe na mimi siwezi nikakubali huu upuuzi wa kuingiza majambazi humu ndani eti waichore nyumba yangu na mimi niwaache kitu kingine sikukwambia hii nyumba nikitaka ukae humu mwaka na usitoke njee uwezekano huo upo..... Kabla hajaendelea kuielezea sana ndipo nikamuuliza ni fundi nani aliyeijenga hii nyumba mana ramani yake nimeipenda sio kidogo,,,,,,
     Daah ben mimi ningeweza kujenga nyumba kama hii.. Ni kastori ila siyo karefu sana alisema hivo na mimi nikadakia kwa kuuliza nisimulie tuu merry au sitakiwi kujua kabisa???? Baada kuuliza hivo alinijibu kwamba usijali nakupa tuu hiyo stori usiwaze tulitulia kimya wote kama nusu saa hivi kisha akaanza
*****ilikuwa ni mwaka 2010 kaka yangu alikuwa anatoka jeshini ile siku ilikuwa ni siku nzuri sana kwangu maana aliniletea zawadi nyingi sana hadi baba aliuliza kuwa huko jeshini kuwa promo ya hela au kaiba hela za watu kakaangu hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kutoa zawadi alikaa pale nyumbani kwa mda wa wiki moja tuu kisha alitoweka tuu gafla na hakuna aliyejua kaenda wapi hadi wanajeshi wenzake walikuwa wakimtafuta wasijue wapi kapotelea ila kilichonishangaza mimi ni pale ambapo waliamua kuja kupangisha baadhi ya wanajeshi wenzao katika mtaa wetu hilo likanifanya nishtuke zaidi na kuanza kujiuliza maswali lukuki ila sikupata jibu lolote lile maana mtu wa kunijibu hakuwepo basi siku zilisonga zikaenda baada mwaka mmoja, nakumbuka hiyo siku nilienda mjini ili nifike super market nikanunue vitu nilipokuwa nikiusogelea mlango nilidakwa nikazibwa mdomo kwa kitambaa fulan hivi ili nisiweze kutoa sauti yoyote kwakuwa sikuwa na nguvu yoyote nilitulia kama nipo kwa kinyozi nachonga nywele hapo nilichukulia hadi eneo moja ambalo kulikuwa ni giza halafu nikasikia merry lilitajwa jina langu mda huo mimi tumbo joto natamani kukimbia lakini nilitaitiwa vibaya sikuwa na ujanja wowote kwakuwa sikuwa na namna ilinibidi tuu niitike abee we ni nani tafadhali mana zilipowashwa taa mle ndio tulikuwa sisi wawili tuu mimi na yule kaka. akanambia tafadhali usiogope chochote mimi si mtu mbaya isipokuwa sijaona njia nyingine ya kukupata zaidi ya hii......akiwa anataka aendelee kuongea nikauliza tena wewe ni nani nimeuliza hakuwa na jibu akashika kidevu chake na kukivutia juu kisha uso wote ukavulika sikuamini nilichoweza kukiona hapo woga wote ulitoweka "waoooh kumbe ni wewe nilisimama na kwenda kumkumbatia ni baada ya kugundua kuwa alikuwa ni kakaangu moses baada ya kujua ni yeye ndio tukaendelea na stori nilimuuliza sasa kwanini unajificha hivi alinijibu ile siku nimerudi nyumbani nikatoa zawad nyingi kama ulikuwa makini baba aliuliza kuwa jeshini wanatoa hela sikumjibu chochote na ukweli ni kwamba zile pesa niliziiba tena sio zile tuu ni zaidi ya zile . baada ya kaka kusema nilibaki tuu mdomo wazi  kisha akaendelea kunambia merry kuna nyumba nahitaji nikukabidhi uwe unaishi kuanzia sasa ntakwenda kukuonyesha ili uione nilimuuliza vipi kuhusu wazazi alijibu kuwa inabidi wasijue mana wakijua tuu hii nyumba itanyang'anywa nilikubaliana nae kisha tukaondoka na yeye akiwa kavalia ile sura ya bandia na hapo ndipo alikuja kunikabidhi hii nyumba****

    merry alihitimisha hivo stori yake kisha tukaendelea na vitu vingine
Ila kwa upande wangu bado nlikuwa na shauku ya kutaka kujua. Merry samahani kama ntakukwaza nna swali nataka kukuuliza hapa akanijibu uliza tuu ben ua free to ask nikwamwambia ok kwahiyo huyo bro wako alirudi tena jeshini au akarudi mtaani.. Ahaa yeye alinambia anaenda kujisalimisha na kuwadanganya ili wasimfuatilie zaidi maana hata nyumba hii hati miliki inajinihusu mimi tuu licha ya kuwa hizo hela alizoiba ndio alinunulia hii nyumba...
Mda ulisogea kidogo kisha tukaamua kwenda kuwasha tv ili tupate japo taarifa ya habari tujue kinachojiri

***mtoto anafahamika kwa jina la ben ama benchrys anatafutwa alipotea katika mazingira ya kutatanisha walipokuwa shuleni kwa yeyote atakaye mwona atujulishe kupitia namba 0712345678 au toa taarifa kituo cha polisi kilichojirani nawe mtoaji taarifa ni Hamis mkuu*** hizo ndio taarifa ambazo tulikutana nazo kwenye tv tulipokuwa tukiwasha merry akabaki kuniangalia tu nilijalibu kutulia kimya lakini ilinilazimu tuu kuongea
Merry: ben yule ndo baba ako au mbona huyu mzee namfahamu na yeye ni mwisilamu tofauti na wewe mkristo... Nilimjibu hapa ndo mana nashangaa mtu hakujui ataanzeje kutangaza anakutafuta huku hamjuani dah hii shida ila huyu dawa yake ni ndogo sana namkomesha. Nilijisemea hivo kisha merry akauliza sasa utamfanyia nini. Nilimjibu sorry unaline ya simu ambayo hutumii alijibu ndio ninayo utanyaje nishirikishe tuu ben.... Ngoja nitachukua hiyo namba kisha.........itaendeleaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com