Jumanne, 16 Agosti 2016

De 15

Gangstar noma
By: benchrys
15
.........Ngrrrrr ngrrrrrr huo ulikuwa ni mlio wa simu yangu nilinyanyuka kiuvivu ili niweze kujua ni nan anapiga simu mda kama ule halafu ukizingatia namba ngeni.. Niliichukua simu yangu kisha nikaslide iliijipokee lakini nilipopokea hiyo simu sikuweza kutoa sauti yoyote wala kuongea chochote baada ya mda kidogo alianza yeye mwenyewe,,,,,, hallo ben vipi mbona sikiizi adimu sana hata huonekani yani upo wapi rafiki yangu....ilisikika vyema hiyo sauti masikioni mwangu nikaja kugundua kwamba huyu ni jane lakini kwanini atumie namba ngeni sikupata jibu lolote na sikuongea chochote hadi maongezi yanaisha mana nilijua lazima amesetiwa ili aulize ili ijukane niliko kitu ambacho mimi sikuwa tayari kukifanya, nilikata simu nikarudi kulala ila baada ya dakika chache iliingia meseji kwenye simu yangu nilinyanyuka tena kuifungua hapo ndipo ilikuwa ni namba ya jane imetuma meseji inayosomeka "duh nashukuru hujatoa jibu lolote mana mimi huku nimetekwa wakinibana nitaje uliyoko na sitaki unitajie kabisa kwaheli usiku mwema" baada ya kusoma hii meseji nilivuta pumzi ndefu ndio nikala ila kwakuwa walisha niharibia usingizi sikuona hata haja kulala maana macho mda huo yalikuwa magumu basi nilichokifanya nikwenda kuwasha computer ya mule chunbani ambamo nimewekwa ilikuwa ni computer aina ya dell yenye uwezo wa kujitosheleza kabisa cha kwanza nilingia internet kisha nikatafuta maps lengo ilikuwa ni kujaribu kutaka kuyasoma mazingira kupitia computer baada ya mda mfupi ilianza kunionyesha baadhi ya maeneo usiku ule sikulala nikawa tu na computer hadi ilipofika asubuhi.....

.......ilipofika asubuhi nilitoka nje lengo nikaangalie hata kulivo tu ila merry akanambia usitoke huko ben nilimuuliza kwanini tena akasema hebu tazama pale ukutani duuh hata sikuamini baada ya kuwaona baadhi ya watu ambao tuliwaona kwenye huku wakiwa na sura za kikatili kabisa nikamuuliza merry sasa tuna fanyaje hapa akasema wewe rudi kule ndani funua kapeti unaona mlango kisha jifiche huko chini tumbukiza na mabegi yote sawa...niliitikia sawa kisha nikafanya kama kadiri alivonambia.

****aaaah hakuna lolote hapa huyu mjinga hayupo ilieneo tumepoteza mafuta ya bure tu, oya vichaa wangu ee twenzetuni asituzingue bhana... Hayo yalikuwa na maneno ya wale majambazi,,,,, Kumbe walijua ile nyumba ni ya vyumba vitatu kumbe kuna vyumba vingine vya siri ndani na ndio ambako mimi nilijificha huo baada ya dakika chache merry aliingia kule na kusema haya saizi toka lakini usitoke nje mimi naenda kwenye shughuli zangu ila wewe hapo kinachokupasa nikukazia macho yako pale ukutani tuu mana hapo kila kitu cha nje lazima kionekane hapo....."""" hii nyumba ilijengwa kijanja sana ndio kitu nilichokuja kukigundua mana chumba nilichopangiwa hata uwe mchunguzi vipi huwezi gundua haraka kwamba huko ndani kuna chumba isitoshe huko ndani nako kuna chumba kingine cha chini niliupenda sana huu mfumo wa ujengaji....

****huko nyumbani leo walitembelewa na wageni ambao hawafahamiki machoni pao baba na mama aliwakaribisha vizuri kabisa wakapata kifungua kinywa pamoja kisha wakaanza kuongea
Baba: karibuni jaman ningeomba kwanza kuwafamu ninyi ni akina nan na shida yenu ni nini,
Mgeni: sisi ni walimu katika shule ya hapo mbele i mean anaposoma na mwanao ben.... Kabla hajamalizia kuongea yule mgeni baba akapachika swali jingine mnasema nyie ni walimu mbona hizi sura ni ngeni hata pale shuleni sijawahi kumuona hata Mmoja wenu mlifika lini??? Swali hilo lilimpa wakati mgumu yule mgeni aliyeanza kutoa maelezo... Mbona kama unaanza kuwa na wasiwasi ok nambia shida iliyowaleta yule mgeni alianza kujing'atang'ata... A    aammm eee i  po hivi mzee wangu kabla hajatoa maelezo yoyote baba akasema kwa amani naomba mpotee haraka,,, hawakuwa na jinsi iliwabidi tuu waondoke lakini wakiwa wanatoka kuna mmoja kati ya wale watatu aliangusha karatasi... Kumbe mama nae alikuwa nje aliiwahi kuokota akaingia nayo sebuleni lakini ile anaangalia ndipo aliweza kuona picha ya mwanae ben akajiuliza hawa ni watu wa namna gani kutembea na picha ya mwanangu.
     Kumbe katika yale maongezi yaliyokuwa yakiendelea kati ya baba na wale wageni yalirekodiwa na naomi ambae alikuwa dirisha la nyuma ameweka simu yake kama paparazi...
Na hiki ndicho kitu ambacho mimi pamoja na baba tulimpenda sana huyu naomi kichwa chake kipo fasta sana kufikiria.....baada ya mambo yote kuisha kila mtu aliendelea na mishe zake dakika zilisogea masaa yalipita ikawa imeshafika jion meery nae alikuwa akitoka huko kwenye mgahawa wake,,,,_,,,,, lakini mimi nilikuwa nikijiuliza maswali hivi huu mgahawa ndio ulio msababishia hadi anajenga nyumba kama hii kiukweli sikupata jibu lolote maana ni kichwa mtu mmoja hakiwezi kutafuta majibu ya mtu mwingine
      Merry alifika pale nyumbani akiwa ni mtu mwenye furaha sana tulipiga stori nyingi sana hadi ilipokuwa inkaribia mda wa kwenda kulala lakini tukiwa tumekaa mimi niling'aza macho yangu ukutani na merry pia aling'aza macho yake ukutani vilevile harafu akasema mabwege hawa ngoja niwape dawa yao alichukua kitu fulani kama kikokotoo au nyie mnaita calculator ya ni hivo kisha akabonyeza baadhi ya namba na kumalizia kwa kusema hii nyumbani ni yangu sikujenga ili mnitenbelee kilio chema.....baada ya kubonyeza ni kweli nilianza kusikia vilio kule nje kutoka kwa wale watu kisha akasema ben siumeona nnachofanya kiukweli hii nyumba sihitajigi mlinzi mana nao ni wezi tuu niliitikia vizuri baada ya hapo......itaendeleaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 14

Gangstar noma
By: benchrys
14
.....hallow mambo gani hayo tunafanyiana hiyo motonyo inakuja au haiji pia kumbuka kuja na hiyo maiti ili tuteketeze kupoteza ushahidi ila acha upuuzi kwanini unaziba uso au leo network tatizo mana mimi huku hata sikuoni" nini maana ya imo video caller.. Mdau huo yeye anaongea hayo yote mimi nilitulia kimya nisiongee chochote baada ya kimsikiliza sana nilikata simu kisha nikairudisha nilipoendelea kukagua ule mkoba kuna mfuko nilikuta kuna picha za watu ambao baadhi yao niliweza kuwa fahamu kwa sura zao maana walikuwa ni watu wa mtaani kwetu baadhi ya picha hizo hata mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao wameunganishwa kwenye zile picha ni jambo ambalo lilinishitua sana kuona na mimi picha yangu ipo swali ambalo nililipata kwa haraka ni kwamba hizi picha kazipata wapi,,.. Nikiwa naendelea kujiuliza maswali hayo simu yangu ghafla ilianza kutoa mlio ishara dhahiri ya kwamba kuna mtu alikuwa akipiga nilinyanyua simu yangu ili nijue ni nani anapiga hiyo simu kwa mda huo nilipoangalia niliiona namba ya joel ikinipigia simu kwa mda huo nilikumbuka maneno ya madam linda pamoja na meseji aliyotuma naomi kupitia whasapp baada ya hapo nikaweka tahadhali kwangu mwenyewe kisha nikaipokea simu hiyo nilipopokea simu hiyo sikutaka kuongea chochote joel ilimubidi aanze mwenyewe kuongea
Hallow ben vepe wewe!!!! Aliongea kama mara nne hivi na mimi sikuitikia kitu lakini nikiwa makini atasema nini ndipo niliweza kusikia sauti nyingine ya jibaba likiongea kwa kukoroma "huyo boya lako mbona haongei acha kutuyeyusha dogo utapishana na mapene hivihivi huku unajiona shauri zako liliongea hivo lile jitu lenye sauti nzito joel hakuwa jibu akaendelea oya ben eee mbona huongei mdau wangu hizo ni dharau au kitu gan mwanangu" ... Hata kama joel aliongea kama analalamika lakini kwa upande wangu hata sikuona hata haja ya kumjibu neno hata moja maana kwa wakati huo nilikuwa na malengo mawili moja niwasikilize nini watasena na pili washindwe kuamini kama ile ni namba ya simu  baada ya hapo nilikata simu na kuiweka chini........ 

......turudi huko nyumbani mama alikuwa akilia na kutupa lawama kwa serikali kwamba bora wangetoa tuu taarifa kuwa kila mzazi atafute shule ambayo ataweza kumsomesha mwanae kuliko kupotezeana nguvu katika familia kwa namna kama hii.. Wakati huo naomi na baba wakiwa wanajaribu kumtuliza asilie na kumpa matumaini kwamba mwanae ben yuko salama tu mahali hata asijipe mawazo ya kumfanya alie sana.. Baada ya mda kidogo mama alikuwa tayari amesha acha kulia..

****** hivi tangu lini umeanza kuufanya uzembe wa namna hii yaani umempata ndege ameingia hadi kwenye mtego halafu mwisho eti amekimbia isitoshe ameiba na baadhi ya vitu vyako.. kabla Hajamaliza kuongea alimpiga kibao kikali nyie mnaita kofi hadi yule aliye kuwa akiambiwa vile akakaa chini huku akimwangalia kwa huruma kama ndege aliyeko kwenye mtego anamwona mtegaji ndio anakuja.... Hayo maneno yalikuwa ni lawama kwa yule baba ambae alinipokea kwake na kutaka aniue usiku ule kumbe yule nae licha ya kuwa alikuwa na nyumba nzuri lakini nae alikuwa na boss wake ambae anampa hizo kazi za kuua lakini kwa ben alikosa hiyo bahati ya kumwua.... Baada ya kuambiwa yale maneno yote ndipo akaamka na kumjibu yule boss wake kwamba samahani sana hata mimi sielewi ni uzembe gani nimefanya lakini i promise siwezi rudia tena na wala hili kosa halitojirudia tena naomba unisamehe tu kwakweli.,, boss wake huyo hakuwa na la zaidi akamwambia kama umekiri kweli haina tatizo nenda endelea na mambo yako ukamilishe ratiba nyingine.
Walipeana mikono kisha wakaagana na kila mmoja kutoka lakini yule ambae ilionekan amefanya makosa akatoka kinyumenyume jambo ambalo watu wengine waliokuwapo pale hawakuelewa kumbe mwenzao alikuwa na maana yake staili hii ya kutoka ilimsaidia yeye kama boss amemsamehe kwa kinyongo ili anapoondoka anpige shaba basi hata ukifanyika uchunguzi picha ya aliyemuua ibaki kwenye mboni za maiti.....

****turudi kwa ben na merry...dada merry ee samahani nilikuwa naomba msaada wako hapa niliponinajasho kweli mwilini humu maana nmetembea umbali mrefu kweli leo hii. Naweza nikapata hata maji tuu ili nikaoge ikiwezekana nilimuuliza merry nae akanijibu hata usijali kama ni kuoga we usiogope mana hata nje hutoki alinionyesha bafu iliko, nikamshukuru na kuelekea huko bafuni baada ya mda kidogo nikawa nimesha toka bafuni....
Ben aliniita merry. Naam mimi ben nakusikiliza,, akanambia mwenzio ulipoenda bafuni nilikuwa naangalia huu mkoba lakini kuna kitu nimekiona sijakielewa labda wewe kama unakijua ni hiki hapa,,, baada ya kusema hivo akakitoa hicho kitu alipokitoa ukiangalia kwa haraka unaweza sema ni peni/kalamu ya kubonyeza,. Niliishika ile peni kisha nikaiangalia vizuri nikaja kugundua kwamba hii sio peni bali ni kifaa cha kurekodia nakasema duu peni gani inasehemu ya kuweka memory pamoja na earphone hii sio peni halafu cheki kuna alama za maiki humuhumu na chaji hii ni recorder sio peni baada ya hapo tulichukua na earphone ambazo zilikuwa pamoja na ili peni tuliunganisha kisha mimi nilivaa sikio moja pamoja na merry alivaa sikio jingine hapo ndipo kuna sauti zilianza kusikika  maneno ambayo ilikuwa ni kama mjadala wa simu baina ya watu wawili nilisikiliza yale maneno kwa umakini nilichokuja kugundua ni kwamba inaonekana wanampango wa kwenda kuvamia nyumba moja lakini sikujua ni nyumba nani maana ilionekana kwamba walishatoka wanaongea mimi nilisikiliza nikiwa ndio wanamalizia kuongea walipoacha kuongea nikajisemea wasije wanaenda kuvamia nyunbani kwetu jambo nililolifanya ni kutuma meseji kwa madam kwamba "nakuomba kama hutojali tuma polisi wakafanye ulinzi nyumbani kwetu pamoja na hapo kwako maana kuna mpangi m-baya unaendelea nakuomba madam ujitahidi" kisha niliituma muda huo merry alikuwa ashaanza kupata usingizi nilimuwahi kabla hajalala niliita merry!! Eee ben nini bhana nilimwambia hujanionyesha kwa kulala halafu wewe unasinzia amka alijibu ahaa tena bora umenikumbusha mimi nalala huku wewe mlango wako huo hapo hiko ndio chumba ambacho itakuwa ukilala twende nikakufungulie alisimama kisha akaenda kunifungulia mlango... Waoh!!! Nlijisemea hivo kimoyomoyo baada ya kukifurahia kile chumba mle ndani kulikuwa na computer screen ya flat kama kawaida ila mimi niliipenda sana computer. Aliponionyesha akanambia upo huru kutumia kila kitu humu ndani ndio maana nimekupa hiki chumba kwaajili yako ukiona hakikufai utanambia ila kesho na sio leo maana hapa nmechoka aliondoka kuelekea chumbani kwake lakini nilichukua simu yangu nikatuma meseji kwa baba na mama pamoja naomi kwa kuweni makini huu usiku mnaweza vamiwa ila mkiona polisi wamekuja onyesheni ushirikiano niwatakie usiku mwema.... Kisha nikaituma baada ya mda naomi akareply powa ila...hakumalizia na mimi kwa kuon hajamalizia ile meseji sikijipa shida nikalala lakini ilipofika usiku.......itaendeleaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 13

Gangstar noma
By: benchrys
13
......pigeni huyoooo pigeni huyoooo,,,,,,, zilikuwa ni kelele za watu wa mtaa ule ambapo kuna mtu mmoja ambae walikuwa wakimkimbiza kwa kelele zilizokuwa zikisikika mwiziiiiiiiiiiii piga huyo nikiwa na yule mhudumu kuelekea huko kwake huyu mwizi alipita kwa spidi kumbe lengo ilikuwa anataka annyakue ule mkoba wa lakini sielewi ni nini kilichonifanya hadi nikakaa chini yule jamaa alipopita nikagungua kwa kitendo alichokiobyesha akiwa mbali kidogo mana alikuwa kanyoshea kidole kwenye ule mkoba wangu huku akiangalia kwa macho ya uchu kuonyesha ameboreka na kitendo cha kuukosa ule mkoba wangu.....

,,,,,,,,hivi ulisema unaitwa ben
Ndio naitwa ben ila yaliyonikuta ni kama hayo.. Aliniuliza hilo swali yule mhudumu hapo na mimi nikajipa nafasi ya kutaka kujua jina lake na mimi.. Samahani lakini unaitwa nani vile nilimuuliza akanijibu anhaa mimi naitwa merry aliponitajia jina sikuwa na haja ya kutaka kujua ubin wake mana jina tuu linanitosha.
Kwa hiyo wewe ni mkazi wa haya maeneo nilimuuliza akanijibu ndio lakini sina mda mrefu sana tangu nije hapa, tulipiga stori nyingi hapo nikakumbuka kwamba hapa naweza kutwa na majanga wacha niichaji simu yangu kwanza..... Samahani dadaangu unachaja ya smatphone. Ndiyo ninayo ila saizi nimewekea simu yangu labda tujalibu kuchajia kwenye deki mana mimi sijazoea kuchajia deki, alinijibu hivo merry baada ya kumwomba chaja ya simu nilitoa simu yangu mfukoni lakini kabla ya kumkabidhi nilimtafuta madan linda simu iliita akapokea kisha tukaendelea kuongea,,,,
Hallow madam,, yaa nambie ben uko wap,, aaah eneo lenyewe hata jina silijui,, ahaa powa ila kama upo mahali salama nakuomba ujifiche hkohuko kwa mda mrefu mana huku hata walimu saizi hatuna ruhusa ya kwenda pale shuleni isitoshe unatafutwa picha za zimebandikwa karibia kila sehemu hasa kwenye nguzo za umeme wanadai kwamba aliyetoroka ile siku ni wewe tuu na katika wale wanajeshi waliokuja na yule baba mwenye visa na serikali anakusaka kwa namna anazojua yeye maana walimkamata rafiki yako jane ili wambane wamuulize kama anajua chochote kukuhusu wewe lakini jane aliwakatalia kwamba hajui baadae nilienda kuamlia mana wakawa wanasema awape namba zako za simu nikaona kama anazo anaweza toa halafu ikawa kesi tena, halafu kuna baba mmoja anaongea kistaarabu hivi wanasema ananyumba kubwa mtaa tofauti na hapa ni mbali kidogo kuwa makini katika mizunguko yako unamopita,,,,, hayo yalikuwa na maneno ya madam pindi nilipompigia simu alinambia huyo mtu wa kuwa nae makini nilimwambia anitumie picha yake huyo baba kupitia whatsapp alikubaliana na mimi kisha akanambia najua utakuwa kipindi kigumu sana ntakutumia pesa kidogo zitakusaidia nilikubaliana nae kisha nilikata simu huku nikiwa na shauku ya kutaka kujua hiyo sura ya huyo baba ambae inatakiwa niwe makini

****ben huyo ni dada ako au mbona unamwita madam, aliniuliza hivo madam mimi nikamjibu huyu ni mwalimu linda mwalimu ambae anafundisha kwenye hiyo shule yetu somo la kiswahili. Merry akasema inaonekana huko imeshakuwa shida mimi nilimjibu tuu kwa mkato kuwa haya yote yatakwisha tuu Mungu ni mkubwa naamini........hazikupita dakika nyingi iliingia meseji kwenye simu yangu upande wa whatsapp nikajua kwamba huyu lazima atakuwa ni madam nilinyanyua simu yangu kutoka pale kwenye sofa ili nifungue niione hiyo picha ila mambo yalikuwa tofauti na vile ambavo mimi nilitegemea itakuwa nilipofungua ile meseji kumbe alikuwa ni naomi ambapo aliandika ujumbe uliosomeka
"ben kama upo sehemu salama nakuomba usije thubutu kumwambia mtu yeyote wa huku mtaan kwetu mahali ulipo mana kuna watu wamesetiwa ilikukupeleleza mahali ulipo ili uje ukamatwe kama unankumbuka yule kaka ambae alikuwa akitaka kuniharibu ile siku kule hadi ukaniokoa kaajiliwa na huyu baba ambae anabishana na serikali kwa hiyo anatafuta njia ya marafiki zako ili akupate ulipo.. Ukiisoma hii meseji naomba uifute bye ��"

     Baada ya kusoma hii meseji nikawa tayari nishapata mwanga fulani kwamba huyu baba inaonekana amekodi na majambazi ili kutekeleza hii kazi yake..... Huo mda wote nilikuwa na begi langu mgongoni ni aina ya begi ambalo lilionekana ni la gharama sana nikiwa nangoja hii meseji ya madam nilimwomba merry niende chumba cha ndani nashukuru merry nae alikuwa ni mwelewa akanambia powa aliloki milango yote kisha akasema nifwate nilimfuata hapo akaenda hadi hadi sehemu moja ambapo mimi nilijua kuwa naingia kwenye kabati la nguo kumbe ulikuwa ni mlango wa kuingilia kwenye chumba kingine cha ndani kabisa.
     Nilipoingia kule ndani ndipo nikalivua lile begi langu ili kujua kuna nini cha zaidi mle ndani ukiacha zile bullet box pamoja na pisto ile niliyoibakwa yule baba kwanza nilifungua zipu zote lakini kabla sijaanza kikagua iliingia meseji WhatsApp kwenye simu yangu ilikuwa ni meseji ya madam linda ambayo ilikuwa ikionyesha picha ya mtu lakini nilipojaribu kuangalia vizuri ile picha nikagundua kwamba yule ni yule baba ambako ninefikia jana akawa anahitaji kuniua sikupoteza mda nikamjibu
"duh mungu mkubwa aisee huyu mtu jana usiku nililala kwake lakini alitaka kuniua kwa kunichoma kisu lakini nilipogundua ilinibidi nitumie akili yangu kwa kuweka shuka ili liwe kam binadam kisha nikajificha uvunguni" niliituma

Hapo nilianza kupekenyua lile begi kumbe hili begi ndio maana lilikuwa zito hivi ndani ya begi kulikuwa na laptop fulan ndogo hivi aina ya HP na chaji cable yake pia cd mbili ambazo ziliandikwa window 7 na nyingine windows8 Sikutaka kuwa na papara kwakuwa laptop nazijua haikunipa shida sana kabla ya kuwasha nilitoa betri ili kama inafanya recodi ipoteze mawasiliano baada ya hapo nikaifungua tena ili nijue nini kipo zaidi lakini nilishutuka baada ya kusikia mlio wa simu kutoka kwenye lile begi nilitafuta hii simu ipo mfuko upi baada ya mda kidogo nikawa nishaipata katika ile simu inapoita niliona sura ya mtu kwenye kioo inapoita nikajua wazi huu mtego nilichokifanya niliziba camera ya mbele kisha nikapokea.....itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

De 12

Gangstar noma
By: benchrys
12
Nilihisi kama navamiwa hivi maana mtu aliyekuwa anayaka kuingia mile ndani nilimolala mimi alikuwa ananyata kitendo hicho kilinifanya mimi nimakinike kujua hapa ni nini kitaendelea nikiwa nimejifunua lile blanket nikaamua kuachia kaupenyo kadogo ili niweze kuona ni nini kinakuja mle ndani mara mlango wangu ulisukumwa kwa utatibu kama mtu ambae anavizia kukamata kuku vile nikaona hapa kama hawa sio watu wema na mimi acha nijitetee nilifanya kama nastuka hivi yeye akatoka haraka akijua sijamwona ni kweli sura sikuielewa, alipotoka nje huku ndani mimi nikakunja shuka moja liwe mfano wa mtu kisha nikalilaza pale kitandani halafu mimi nililala uvunguni huku nikiwa macho mda wote ilikujua ni nani ambaye ananinyemelea huu usiku. Haikupita mda mrefu sana alirudi tena mle ndani kwakuwa nilikuwa chini ya uvungu niliweza kuona mwanaume mmoja akiwa kavalia dereki/kitambaa sehemu ya mdomo wake akiziba uso wake kwa style hiyo nilitulia kimya hata mlio wa pumzi usiweze kutoka nje au kusikika kabisa nje huko asije akastuka kisha nitafutwe ambako nipo nikiwa naendelea kutazama alitoa kisu kidogo akakiangalia akawa anajishauri kisha akarudisha mfukoni na kutoa kisu ambacho kina urefu wa aina yake kilikuwa kisu kama jambia ila chenyewe ni chambamba chenye mng'ao wa makali ya kukata niliweza kuona mana taa ya nje ilikuwa ikitoa mwangaza....baada ya hapo akakinyanyua juu na kukishusha mahali ambapo kulikuwa na mwili ambapo kwa uelewa wake alijua kwamba ni mimi kisha akachomoa na kuondoka mle ndani kwa mwendo wa kujiamini kabisa hapo nikawaza hivi tayari ningekuwa tayari naiona ahera nilimshukuru sana mungu wangu kisha nilianza kupanga mikakati ya kutoroka usiku uleule..... baada ya yule mtu kutoka chumbani mle aliingia ndani na kuzizima taa zote ambazo zilikuwa zimewashwa kwa mda wote ule alipozima tu zile taa mimi nilitafuta simu yangu kisha nikaangalia mlango cha kushangaza niliona geti lipo wazi nilitoka nje nliona kuna gari limesimama nilipojaribu kuangalia  ndani sikuona mtu nilichungulia vizuri nikaona kitita cha hela kwa akili yangu ya haraka nikawaza kwamba kama walinikaribisha ili waniue mungu wangu mkubwa hapo niliingiza mkono hadi mle ndani ya gari na kuchukua kile kitita cha hela pia kulikuwa na bastola ndogo pisto mnaita niliinyakuwa nayo pamoja na kibox fulan kilichosomeka bullets box niliweka mfukoni na kutokomea kwenye kiza nikiwa mbali niliweza kuona yule baba aliyenikaribisha akiingia katika lile gari huku ile dereki ameshusha ipo shingoni niliweza kujua kwamba ndio yeye aliyekuwa akininyemelea kule ndani ili anichome na lile bisu lake

Usiku ile nilitembea pekeyangu hadi nilipofika katika sehemu moja hivi ambayo palionekana kuwa ni tulivu kwa mimi kujipumzisha nilikaa chini huku nikiendelea kujiuliza haya mambo yote kisa nini mana shule imvamiwa sababu hata sielewi nikiwa naendelea kuwazua nilianza kuona mwanga za mapambazuko kuonesha kwamba ilikuwa tayari ni asubuhi.....nilinyanyuka na kuendelea kutembea nisijue naenda wapi tayari ikawa asubuhi nilipishana na watu wengi ila kwakuwa sikuwa na nguo za shule hakuna aliyeweza kuniuliza swali lolote mana walikonipokea kule walinipa hadi nguo za nyumbani ili nizivae ule usiku mida ilienda sana kisha ikawa tayari imeshatimia saa saba za mchana nilinyanyua simu yangu na kumtafuta naomi "mteja unae mpigia hapatikani kwa sasa tutamtaarifu kwa sms atapokuwa hewani" nimajibu niliyopewa na watu wa mtandao sikukata tamaa nikamtafuta baba ila sikufanikiwa nikamtafuta tena na mama sikufanikiwa duuuh ndio nini hii...nilitafuta namba ya madam linda nae alikuwa hayupo hewani kwa mda huo wote niljihisi nipo dunia ya ajabu sana nikakumbuka rafiki yangu wa shule joel nilipiga kwenye namba yake simu yake iliita bila ya kupokelewa nilikata tamaa nikarudisha simu mfukoni...

Oya we dogo unaenda wapi. Kuna aliniuliza lile swali lakini nilijifanya kama haongei na mimi vile nikapitiliza tena nikiwa ni kama mtu mwenye haraka sana nilipoona nishapotelea nilianza kukimbia huku nikiwa na begi langu ambalo nilikimbia nalo kwa yule mzee mwenye roho yake mbaya haonei huruma binadamu mwenzake na kuthubutu kutaka kuua hili begi nililobeba mgongoni mwangu ndio nilimo weka pesa na silaha hivi vitu ambavyo nimetoka navyo kwa yule muuaji...
......ilipofika mida kama ya saa nane na nusu hivi nilihisi njaa inaanza kuchakaza tumbo langu hapo nikatafuta sehemu ambayo ni salama kwangu na kisha kwenye zile hela nilitoa noti ya shilingi elfu tano na kuiweka mfuko ambao kama nifika sehemu yenye mgahawa nikila tuu naingiza mkono mfukoni na kutoa pesa zoezi hili liliisha haraka tuu kisha nilianza misele ya kuutafuta mgahawa ili niweze kuridhisha tumbo langu nitembea hadi nikajiuliza inamaana watu wa hii mitaa hawajawahi kujua nini maana ya mgahawa,,,,
Baada ya kutembea sana ndio niliweza kukutana na sehemu moja yenye banda la mabanzi huku nje kukiwa na tangazo lililosomeka "jiachie new mgahawa" baada ya kuona hivo nikalifuata lile banda ambapo nilikutana na dada moja aliyenikaribisha,
Karibu kakaangu naweza kukusaidia unahitaji nini. Asante kuna chipsi dadaangu, nilimuuliza hivo akajibu kuwa chipsi zipo ila ni za kupasha hapo nilimwambia ah usijali zipashe tuu na mayai inakuwa bei gani alinijibu kuwa ni shilingi elfu mbili tuu kwakuwa ni mayai ya kisasa nikamwambia anikaangie na mayai....
Hapo alianza kufanya yake huku akiendelea na stori haikuwa shida maana mle ndani tulikuwa wawili tu akaniuliza naelekea wapi nikaona huyu asinipe zari nae ila baada ya kuwaza sana nikampa full mkanda jinsi ilivo akanipa pole kisha ninapoendelea kungoja alinipa soda niendelee kushushia ninapongoja chipsi zile sio nda mwingi alileta kwakuwa zilikuwa tayari nilizipokea na kumkaribisha na yeye..ah usijali ben mimi hapa nashinda na msosi ko mda wote nipo full usijali we kula tuu lakini mi nakuomba usiendelee na safari yako hiyo mana unaweza potea kabisa na wewe huku si kwema sana kaka ben nilimwambia kwahiyo utanisaidiaje, kuhusu sehemu ya kuishi we usijali ntakusaidia tu kwakuwa ilikuwa inaelekea jion akasema leo nawahi kufunga alifunga ule mgahawa kisha tuliondoka lakini tulipokuwa njiani.........itaendeleaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com