Gangstar noma
By: benchrys
6
Madam umee ese ma nikungoje niliuliza kwa kigugumizi swali hilo kwa madam linda mana nilihisi huyu pengine ndio anataka atimize lengo lake la kulazimisha apajue nyumbani ili awape wazazi ukweli wote juu ya mambo ambayo nayafanya huko shule l..mimi nikiwa nawaza hayo joel nae alikuwa akiningoja kwasababu tulishapigiana simu kuwa siyo mida mingi ntakuwa nishafika kwao mana siyo mbali sana kutoka pale sisi nyumba yetu ilipo nikiwa nimesimama huku nikiendelea kumngoja yule madam mara simu yangu ikaanza kuita ngrrrrr ngrrrrrr nikainyanyua na kuipokea nikijua wazi kwamba huyu atakuwa ni joel anataka kuulizia mbona nachelewa kufika hivo lahaula kumbe hakuwa joel niligundua hilo jambo baada ya kuipokea ile simu na kuanza kuongea.....hallo vipi jo...kabla sijamalizia kusema joel ili nikamilishe kusema hilo jina nikazuiliwa kuendelea kuongea na sauti ambayo niligundua kabisa hii siyo sauti ya joel mana ilikuwa ni sauti ya mkwaruzo tena kavu kama ambae chai yake ni kokoto au anashindia bangi tuu kila siku ndipo aendelee kuongea....
Oya mdogo wangu upo wap saizi ninamishe na wewe kama upo tayari tukutane ili tuchonge mipango yote iende fresh,,,,,,,,mbona hunijibu au hujanisikia. Sikujibu nilibakia kimya bila kujibu chochote hapo ndipo akili yangu kidogo iruke maana huyu madam madam kanambia nimngoje halafu kibaya hadi saivi hatokei nikiondoka itaonekana ninadharauu na tena nikabaki hapa kisha nije kukutana na majanga tena mana aliyepiga hii simu simjui na shida yake nini..hayo yalikuwa ni mawazo ambayo yalianza kusumbua sasa kichwa changu uchaguzi ni wangu huu niepuke kipi na nikiache kipi duh.. Nionekane namdharau ticha au nimpuuzie joel au nimpuuze aliyepiga hii simu Nilkuwa katika wakati mgumu kulingana na jambo lililo....licha ya kuwa ticha ataniadhibu ila hakitaharibika kitu chochote ila kwa huyu boya ambae simjui lazima anaweza kuwa ni mpuuzi yule alitemteka yule bint mbona sauti zao kama zinalingana hivi anaweza kuwa anajua niliko mahali salama hapa ni homu tuu...nilikuwa nayafikilia hayo ndipo nkachukua uamuzi wa kuondoka pale tena kwa haraka lakini nikiwa nimetoa hatua kama tano hivi ilisikika sauti ya kike tena nadhani alikuwa ni madam linda nikiwa na haraka kama mtu mwenye safari halafu kakumbuka kuwa amesahau nauli na gari mda wa kupita unakaribia,,,nikageuka kumbe ni kweli alikuwa madam
Mbona unakimbia huku nmekwambia uningoje hapa kuna tatizo lolote. Muda hio yeye anaongea hayo nlikuwa nikimwangalia tuu na kubaki kimya bila kujibu lolote mawazo niliyokuwa nayo kama yule aliyepiga simu yupo jilan itakuwa matatizo kama sio kwangu basi madam anaweza kudhurika nae maana mwenye roho mbaya haangalii nani ni wakumdhuru, nikamwambia madam samahan tutaongea kesho shuleni ndio ntakupa full mkanda jinsi ilivo na ndio maana unaona hapa nnaharaka kama ivi. Sikutaka kupewa hata ruhusa nikasema madam wahi nyumbani muda m baya huu kisha nikaondoka huku nikiwa nakimbia kama nimetumwa nikakomboe hazina mahali,, mda mfupi nikawa tayari nishafika nyumbani niliingia ndani nikiwa nahema kama mtu aliyepona kunyakuliwa na tai
Nikiwa nyumbani hata sijapumzika simu yangu ikaanza kuita niliipuuzia sikutaka kuangalia hata jina la anaepiga simu huo mda...we ben inamaana hiyo simu inayoita siyo yako au...naomiiiiiii we naomiii.ilikuwa ni sauti ya mama akimwita naomi, mimi nikauliza mama inamaana naomi bado yupo hapa hadi leo tena mda huu. Mana nilijua atakuwa tayari amesharudi kwao mama akanijibu kwani kunatatizo? Ndio mi naona ni tatizo inamaana wazazi wake watakuwa hawamtafuti tuu mi naona tutakuwa tunawasumbua tuu,,mama akasema we mwanangu usiwaze kuhusu hilo tulishaongea kwamba ataishi hapahapa maana yupo likizo isitoshe baba yako kakubali na mimi pia nimekubali.. Hapo ndipo na mimi baada ya kupewa hilo jibu nikaenda kuichukua simu yangu iliniangalie ni nani alikuwa anapiga, nilipoangalia nikaona namba ngeni nikajisemea atakuwa yule mpuuzi ila nikaona tena kuna meseji imepokelewa nikaifungua kutaka niisome namba iliyoituma ile meseji haikuwa na jina kwamaana ni namba ngeni nikaendelea kufungua hapo ndipo nikauona ujumbe USIJE UKAOGOPA....nikiwa naendelea kusoma ile meseji nikaitwa beeeeen alikuwa mama akiniita tena akisisitiza nifanye haraka nikafanya kama alivomaanisha nikafika mahali alikuwa amesimama
Ben umeanza urafiki na vijana wahuni sio. Hapana, sasa inakuwaje hadi tunapata mashitaka ya namna hii.. Mbona mimi sina rafiki zaidi ya joel. Anhaa ndio mnazurura pamoja huyo joel eti, na kwanini we ni mwanafunzi harafu uwe na rafiki ambae sio mwanafunzi. Hapana joel tunasoma wote.....nilipojibu hivo nikatupa macho nje hapo nilishtuka na nikajua kwanini mama anauliza hivo ndipo nikamwambia kama ni huyo wa nje ndiye aliyetaka kumdhuru yule bint naomi,,,,,kwa sauti ya au tuseme mwizi maana huyu si mtu mwema, mama akasema subiri mimi namwondoa kwa aman tuu ila akileta ubishi ndipo ntatumia hiyo njia.
Samahani sana naomba tuu uondoke tena kwa amani mana ben hamjuani njia ile pale kama ni siku ya kudhurika kwa ben sio leo kwaheli eeee..aliongea hayo mama kwa yule jamaa. Huyo jamaa hakutaka kuleta ubishi akageuka na kuanza kuondoka lakini alipokuwa akishuka katika ngazi wote tulishtuka baada ya kuona akiwa bastola kiunoni, haraka nilipokea simu ya mama na kuchukua picha inayoonyesha ile bastola kiunoni...itandeleaaaaa
benchrys1996@gmail.com
&
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni