Gangstar noma
by: benchrys
10
......Niliiweka ile simu chaji kisha wote tukaingia ndani na kuendelea na taratibu nyingine kiufupi ulikuwa ni wa sisi kufurahisha vinywa vyetu kwakuwa chakula kilikuwa tayari kipo mezani hatukua na budi kuanza kukila hii jion wote tulikula tukiwa ni wati wenye furaha sana hususani naomi ambae anasubilia masaa kadhaa tu nae aanze kuitimia simu yake ambae amenunuliwa na baba tulikula huku tukiendelea na stori baada ya dakika kadhaa tulikuwa tushatosheka vilitolewa vyombo mi nikawaaga kuwa naenda kujisomea maana ni kama siku ngapi hivi sijashika daftari mida ya jion kwajili ya kulipitia hata kidogo niliondoka na kwenda sehemu ambayo ni maalumu kwaajili yangu. nikiwa nimesoma karatasi mbili simu yangu ilitoa muungurumo wenyewe mnasema vibrate yaah ni hivohivo ni ishara ya kwamba kuna meseji iliingia kwenye simu yangu maana niliset hivo kuepusha usumbufu wa watu ambao watanitafuta muda nikiwa najisomea... Niliinyanyua simu na kuangalia ni meseji gan hiyo ndipo nikakutana na ujumbe kutoka kwa madam NIMEKUTUMIA TAYARI SALIO NINI TATIZO BEN DEAR!!!! niliposoma hivo nkajikuta nikicheka pekeyangu nlicheka kwa sauti hadi baba alisikia akaniuliza wewe umeingia huko kusoma au kuchat upuuzi. Hapana baba mi nipo nasoma tuu hii ilikuwa ni bahati mbaya tuu nilijibu hivo kisha kila mmoja akatulia hapo ndipo nikaichukua tena simu yangu na kumrudishia madam... Nielekeze jinsi ya kujiunga kifurushi cha data tu mana nimesahau kujiunga kisha nikaituma nikaendelea na kusoma ila mawazo yangu yote yalikuwa tayari yameshahama kabisa baada ya kuisoma ile meseji ya madam sikukaa sana iliingia meseji nyingine ambao ilikua ikitoa maelekezo jinsi ya kujiunga kifurushi cha data lakini nilipoona tu jinsi ya kuangalia salio na mimi kabla ya kujiunga ndipo nikaangalia kwanza salio langu iliporudi meseji ikanambia nina gb 2.7 Nikajisemea hapa hata sijaribu kutoa hela ili nijaze vocha hapo nikaelekea playstore na kuandila whatsapp niliidownload haraka nilivokua na hamu ya kuitumia hata kusoma nilisahau kabisa na kuendelea na internet yangu.... Baada ya mda mfupi ilikuwa tayari ishakubali kukaa kwenye simu yangu nikawa nafuata maelekezo jinsi ya kujiunga zoezi hili nalo halikuchukua mda mrefu tayari nikawa nipo whatsapp nikamtumia madam kuwa nimefanikiwa akaridisha meseji poa nakuchek nilikaa kidogo kuna mlio ulitoka kwenye simu yangu akili yangu ikanituma au ndio meseji ya wasap huko nikafungua kwenye neno whatsapo lililopo kwenye simu ndipo nikaona jina madam kama nilivo save, ndipo nikafungua kumbe ilikuwa ni meseji iliyoandikwa mambo... Kwa kutumia uzoefu nikamjibu shwari tyu
Ushalala...Hapana nipo najisomea tuu hapa
aya bhana kwakuwa ni mwanafunzi ila mi nishalala,alidisha meseji iliyoandkwa hivo huku kaambatanisha na picha yake akiwa na nguo yake ya kulalia siku jaji sana nikamrudishia usiku mwema naye akareplay lakini safari hii alitumia njia tofauti meseji ilikuwa ni kwa sauti na siyo maandishi.... Ni mimi nikawa na shauku ya kujua amefanyeje nilimuuliza unafanyaje kutuma hivi akanielekeza na mimi nikajaribu nadhani niliweza
*****
Siku ya pili nikiwa shuleni asubuhi sana madam aliniita kusema ben ole wako nikuone na....... Kabla hajamalizia aliitwa na mkuu wa shule hapo nilibaki na maswali kibao ole anione na nini atha mbona simwelewi aaah anyway atajua mwenyewe mda ulienda tukawa tayari tupo darasani nikiwa nimekaa jane alikuja nyuma yangu akiwa na uso wake wa furaha na mimi sikusita nilimwoneshea furaha mana ugomvi wangu na yeye tayari ulishaisha kisa ni kumwokoa dada yake naomi
Mambo ben....
Powa tuu nambie jen... Mbona sikuhizi ni kama upo busy sana mana toka juzi ndio nimekuona halaf wanasema hujashinda shule hata mara moja aliuliza hivo jen ndipo nikamjibu mimi nipo sema hujawahi kunitafuta tuu ndo mana hukuwa ukiniona hujui mambo ya skul sometime inabidi tuu uwe mpole kaa maji ya mtungi.. Jane alicheka na kusema powa ben but nnarequest baadae naomba kabla ya kwenda home tuonane nilimjibu hakuna tatizo sema sio ujifiche kwa wenzako mimi nikatafute sijawahi kufanya hivo.. hapana usijali nitakufuata mwenyewe hata usijali alijibu hivo na kuelekea kwenye meza yake aliyopangiwa ile anakaa kwenye kiti mkuu wa shule aliingia na kusema ben... No kabla ya vyote hizi kelele ni za nini mshamaliza au mmesahau darasa lenu la mtihani,,, hapo kimya kikatawala darasani. Mkuu aliendelea nawauliza wenyewe hamnisikii au ndio kiburi mnaniletea kiburi mimi si ndio sasa ngojeeni kidogo nakuja.. Aliondoka kisha akarudi akiwa na fimbo kadhaa mkononi mwake akasema tunaanza na upande huu... Duuh yani huyu mwalimu anaona akimwadhibu mwanafunzi lazima atumie njia ya viboko....Mkuu aliendelea wote jiandaeni....,, Ila kabla hajaadhibu hata mwanafunzi mmoja madam linda aliingia na kusema jaman discussion mmeshamaliza au bado ben bila woga niliitikia bado tulikuwa tukiendelea tumepumzika kwaajili ya mkuu ameingia,,,, hapo mkuu aliishiwa nguvu mana anajua tulikuwa tunapiga tu kelele madam aligeuka kwa mkuu na kusema samahani mkubwa umeongea nao tayari au unaendelea mkuu alijibu nishamaliza kisha akatoka nje huku anatikisa tu kichwa, alifika hadi ofisini aliingia ndani na kutoka kisha.... Itaendeleaaaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni