Gangstar noma
By: benchrys
9
......Jane unaundugu nae au ndo tabia zenu za ajabu hapa skul, madam aliniuliza hili swali hadi nikajifikiria hivi madam hadi anauliza swali kama hili kawaza nini ila sikuwa na chaguo ilinibidi nimjibu tuu. Hapana madam sina uhusiano nae wowote isipokuwa tuu.... Enhee kitu gani madam alidakia kabla sijamalizia hapo na mimi akili yangu iligutuka ikajibadili fasta mana niazimia kuwa nitamweleza kwanini tupo jirani ila alipodakia nikamjibu shotcut kuwa ndo mana nilikwambia kwenye meseji kuwa nitakueleza shuleni na wewe shuleni hujaja mimi ningekuelezaje haya panga siku nyingine ya kukutana ili nikueleze, madam akajibu wewe mimi kukuamini inaeza kuwa ngumu kidogo maana naona wewe ni kama janja moja hatari so kunidanganya hutaona kama kitu kigumu sana kwako..Ahaa nawewe usiponiamini powa tuu mana mnaona kama sisi tulizaliwa tunadanganya mimi nimekwambia panga wakati wa kukueleza hupangi unanipa tuu hali ya kujiona mimi ni mwongo so nikikueleza utaamini kipi sasa kama mapema hivi hutaki kuniamini halafu umeagizwa na mwalimu wa nidhamu au ni uamuzi wako tuu..Hili swali lilimfanya madam atulie kidogo hadi nikahisi kakata simu ile
Hallo,hallo,hallo nilisema hivo mara tatu bila kuitikiwa nikatoa simu sikioni ili niangalie kama tayari ishakata nilipoangalia nikagundua kuwa bado ipo hewani tuu nikairudisha tena sikioni,,, madam alivuta pumzi kwa nguvu kwa nguvu kama mtu aliyewekewa kisu shingoni kisha kikatolewa tena kwamba amenusurika kifo Kisha akaendelea kuongea ivi ben kumbe ambavo mimi najiona sikuamini kumbe na wewe huni amini pia ivi....Kabla hajamalizia kuongea nikadakia kuwaamini nyie ni ngumu sana lakini mbona hujajibu swali la, nilirudia tena kuuliza lile swali la mwanzo halafu nikauliza samani lakini au unashuguli nyingi ndo maana ukaweka simu na kuitulizia kisha ukavuta pumzi kuonyesha umechoka? naona ni bora ungefanya kwanza kazi ndipo unitafute au unaonaje,, madam akanijibu baadae sitakuwa na dakika for sure but i think we will chat au unasemaje madam alisema hivo nikamwambia kwa leo sina kifurushi chochote wala salio kwahiyo itakuwa ni ngumu kuchat, niliongea hivo huku nikijua kabisa kuwa nadanganya kisha akaniuliza halaf ben mbona whatsapp sikuoni na wakati unasimu yenye uwezo wa kuwa na vitu hivyo vyote nikamjibu kwamba siwezi kujiunga na pia hata nijiunga walimu nyie ni lazima muanze kuninyanyasa mana sijui mnaroho gani nyie hadi sometime siwasomi yani hapana wewe jiunge mwalimu atakae kujadili tuu nitajua mimi cha kujibu.........Hadi hapa tulipofikia kwa haya maongezi kati yangu na madam nilikuwa tuu najiuliza mbona huyu madam leo simsomi dakika 37 anaongea tuu na mwanafunzi wake inamaana hawamtafuti watu kwenye simu yake au nlikuwa nikijadili hayo Wakati tukiendelea kuongea nimwambia sorry naomba nikabadili kwanza nguo za shule akaitikia akasema sawa ben ila ntakutumia vocha ili ujiunge whatsapp sawa ee baadae mpendwa eee! ilinichukua mda kidogo kujibu yale maneno kwa uvivu nikamwambia ok kwaheli nayeye akaitikia kwa sauti kama mtu mwenye dalili ya kulia hivi sawa benii badaee....
Hivi ben ulikuwa unaongea na nani tunapiga simu ipo bize tuu karibia saa sasa mda wote huo mtu unaongea tuu duh watoto wa sikuhizi ni shida tupu sijui mnamatatizo yaani hadi kazi iliyotakiwa tuifanye pamoja tumesha maliza sawa boss wetu..Samahani tuu nilikuwa naongea na mwalimu tuu akawaananipa maelekezo na ndio mana tumeongea mda mrefu. Nilimjibu hiyo mama baada ya kuniuliza na kunambia vile kisha nikauliza hakuna kazi nyingine ya kwangu niimalizie.. Nimekwambia tushamaliza
****Duuuuuuh we ben huyu madam linda na wewe inakuaje tena anakutaka nini.. Halaf naomi tuheshimiane sawa maneno gan hayo sasa ananitaka kwani mi msosi au ni ajira ambapo atahitaji salary kutoka kwangu kwanza kwanini uniulize swali kama hili. wakati Huo yeye alikuwa kashika simu yangu, ok umesema kwanini nimekuuliza hivi chukua hichi kidude vaa sikioni halaf ningojee mda huo nilikuwa nimevaa prova kama wenyewe mnasemaga kwahiyo kile kidude nilkivaa yeye akiwa kashika simu yangu sijui alifanya nini nikaanza kusikia yale maongezi niliyokuwa nikiongea na madam kwanza nilishituka nikamuuliza hichi ni kinini akanijibu inaitwa bluetooth, na haya maongezi yameingiaje humu akanijibu mbona yapo kwenye simu yako sijataka niweke sauti juu wasije wakasikia na wengine hapa halaf iwe noma kwako ben. Nikasema inamaana simu yangu inarekodi mnapoongea au akanijibu ndio hivo duuuuuh huu kumbe upuuzi wa hali ya juu aisee
Tukiwa tunaendelea kuongea na naomi iliingia meseji, ben meseji yako hii bhana ee ifungue tuu kwani kunatatizo! akaifungua kisha akataka kucheka kwa ngumu akatulia baada ya kusikia mlango ndani unafunguliwa alikuwa ni baba anatoka sebuleni mana mda huo wote sisi tulikaa kwenye msingi wa nyumba yetu nyinyi mnaitaga kiti ilikurahisisha lugha....Naona mnabadilishana mawazo safi sana hivo ndio inafaa sio kila mtu anaishi nyumbani hapa kipekeake tuu. Aliongea hivo baba kisha akauliza kwa naomi 'naomi nawewe unasimu au? hapana baba sina pole naona ben anasumbua tuu ngoja niwape wote unapenda ipi akajibu hata ikiwa kama ya hii ya ben ntafurahi tuu, baba akajibu ok safi baba alionekana ni mtu mwenye furaha ile jion. Ben mi natoka mara moja sasa hivi narudi hata geti msifunge.. Haikupita mda akarudi akiwa na box la simu aina samsung garaxy kama ambayo mimi naitumia akasema ben jee utafurahi naomi akiwa na simu kama yako nikamjibu nimefurahi ndiyo baba wote tulinyanyuka na kumkumbatia baba baba akasema chukua utamchajia mwenzio unakumbka yako nlikwambia uchaji masaa mangapi ndio si ni masaa sita baba akasema kumbe unakumbuka safi sana.....Itaendeleaaaaaaa
Ijumaa, 5 Agosti 2016
de 9
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni