#Najifunza_wandishi
Benchrys kipindi nilipokuwa miaka ya ambayo yeyote ni lazima awe shule za vidudu/ shule ya msingi nilikuwa kama done au mtu ambae ni kama uncontrollable kutokana na sifa ambazo nilikuwa nazo mtaani jambo lililosababisha hata wazazi kutoniamini kwa lolote hata kama nikiongea kitu ambacho ni ukweli, Na hilo ni jambo ambalo lilinipa hasira sana maana kama naongea ukweli lakini bado inaonekana mimi ni muongo haina maana ya mimi kujirudi kuwa kama watoto wengine ambao mtaani wanasifika mtaani kwamba ni watiifu (hayo yote nilikuwa nikiwa darasa la tano.
Ilikuwa siku moja nimetoka shule naingia nyumbani Baba na Mama wakawa wananiuliza ben mwanetu umetoka wapi saizi? Nimetoka shuleni niliwajibu hivo,Hapo kwa pamoja wakaitikia kwa kusema umevizia muda ambao wenzio wanatoka shuleni ndipo na wewe ukaamua kuja hapa nyumbani Kiukweli hii kauli iliniuma sana na kunifanya nianze kujiuliza maswali mengi sana katika kichwa changu na kujiongezea msongo wamawazo na njaa maana mda huo nilikuwa bado sijala chochote kutokana na njaa ambayo ilinipata pale shuleni. Baba mi nilikuwa shuleni hata uwapigie walimu uwaulize kuhusiana na mimi kama nimehudhuria vipindi au sijahudhuria Hapo Mama akasema ivi wewe umeona sisi watoto wadogo kama walivo hao wenzio mpaka unatita wazazi jua kwamba tunafahamu njia zenu nyingi ambazo hata mwenyewe huzielewi kama sisi ni rahisi sana kugundua, Ivi inamaana leo shuleni nilikuwa ni mimi au nina kivuli changu ambacho leo nilikituma hko shuleni, yalikuwa ni mwaswali ambayo nilikuwa nikijiuliza mda ambao mama alikuwa akiongea ila sikutoa sauti yoyote wala jibu lolote lile kana kwamba nimeungana na yeye kwa asilimia zote kwamba anachokisema ni cha ukweli na ni ukweli mama akaendelea kuongea kuwa wewe ambapo hujibu chochote inamaana kwamba ni ukweli hukuwa shuleni. Hapo nikaleta kiburi na kujibu kwamba inamaana kama mimi inaonekana nawaambia kuwa nilikuwa shuleni halafu nyie bado tuu mnaniambia niache kuwadanganya basi endeleeni kuongea mkiniamini na mimi nitajibu tena kitu ambacho ndio ukweli,
Ivi we mtoto unaemjibu hivo ni nani aliuliza mama ambapo mimi sikutoajibu lolote lile kwa mda huo nikaona leo au hakuna chakula maana sielewi kinachoendelea hapa nikajiamini na kuuliza kwani kunanini ambacho kimetokea mpaka msiniamini kwamba mimi nilikuwa shuleni kuuliza hivo nakawa kama ndio nimechokoza moto uendelee hapo na Baba akasema Mwanetu ben tunakupenda lakini inaonekana dhahili kwamba mambo yako bado tuu hutaki kuyabadilisha, Akavuta pumzi na kuendelea na kuongea ok sawa kama basi iko hivi hapa mchana mimi na mama ako tukiwa katika lanch kuna polisi wawili waliingia kabla hajaendelea nikadakia na kuuliza POLISI tena kwa mshangao mkubwa maana tangu utoto wangu naambiwa polisi ni watu hatari sana kwakuwa wanafunga watu gerezeni. Baba akaendelea ndio polisi walikuja hapa na kuulizia wewe uko wapi, baba akiwa anasema anasema vile nikatamani hata nikimbie au hata nizimie maana nikaona anaponiambia habari kama zile ni kama haelewi mimi moyoni mwangu nawaza nini kuhusinana na hao polisi ambao anawataja, yeye akawa anaendelea kuongea kwamba wanadai umevunja kioo cha gari yao mda huo wakiwa wanapita barabarani kwaajili ya mambo yao kwahiyo wanadai kwamba wanakutaka wakupate wewe iliwajue chakufanya na wewe au sisi tulipe kiasi acha hela ambacho wametaja lakini kiukweli kiasi hicho walichotaja sisi kama wazazi wako hatuna kabisa na bado tunajiuliza inakuaje ili kuepuka swala la wewe kuepuka hapa na kuchukuliwa na hao watu mi bado nikaona ni kama wananitania tyu maana nilikuwa sielewi chochote walinilewesha pale waliponitajia kuhusu polisinikawa mdogo ghafla, mara ikawa imeshatimia jion mama akaanda chakula lakini hata hamu ya kula sikuiona kabisa maana bado nilikuwa nikiwaza kuhusu hao polisi nitajiepushaje kwenye mikono yao baba na mama wakawa wanaongea kwamba itabidi wanihamishe shule lakini wakajakubishana tena baada ya mama kuulizaa utahamishia wapi wakati polisi na hawa watu wanaohusika kuhamisha wanauhusiano wakasema inatakiwa nitulie kwa mda kidogo hadi mambo yakiwa sawa ndipo niludi hapo shuleni. Baada ya muda ndipo wakaniita na kuniambia lile swala ambalo walikuwa wakijadili kwakuwa na mimi ni muoga juu ya polisi nikajikuta nikikubali kiurahisi kabisa pasipo kinyongo chochote hata sikkukumbuka tena suala la shule ambalo ilibidi niendelee nalo
Sasa inatakiwa utambue kwamba hata hilo jina lako Benchry inabidi ulibadilishe kabisa lisjefahamike huko utakako enda nikakubali kwa kuitikia sawa nikiwa nawaza kwamba nimeshajiepusha kwenye mikono ya polisi katika umri wangu mdogo kwa kosa ambalo hata silielewi kama mimi nimehusikaje maana huo muda nilikuwa zangu shuleni na wanafunzi wengine ila sio mbaya najua watafuatilia ukweli hadi waupate nilikuwa nikijifariji hivyo pekeayangu nilipokuwanimekula kwa kujilazimisha nimeingiandani kwangu (chumbani) kwaajili ya kujipumzisha maana sfarai yote ilipangwa kuwa itakuwa asubuhi ya keshotena mapema wasije wambea wa mtaa wakatuona basi nikapanda gari hadi mjini ambapo nilikuwa ni mgeni kabisa hata wa kumwuliza sikumwona maana pale wote naona ni wenyeji na wamechangamka mimi pekeayangu ndiyo bonge la mshamba
Nikakaa sehemu moja ambayo niiona ni kama ndiyo inafanana na mimi kulikuwa kwenye geredumu moja la gari ambalo lilikuwa limeungua upande lakini nikakumbuka kabla sijaondoaka nyumbani niliambiwa kwamba nisije kutaja jina langu la benchrys na badala yake nijiite Joel na kweli ilikuwa hivo kila atakae pita na kuuliza we mbona mbona umekaa tu hapa unaitwa nani nikawa najibu kuwa naitwa Joel ingali najua kuwa jina langu langu halisi naitwa Ben, baada ya mda kidogo nikawa nimeweza kuiona sura ya Baba akiwa anakuja kwa mbali nikamfuata ila akanipa ishara ya kwamba hataki watu wajue kuwa yeye ndiye baba angu kiurahisi badala yake akanionyesha sehemu ambayo ikawa salama mimi na yeye kuonana na kunionyesha mahali pa kuishi kwa mda
Tulipofika nyuma ya nyumba fulani ndipo akaniita na kuniambia kwamba nihesabu nyumba kama nne kutoka pale tulipo simama ndipo nikagonge na hapo ndipo nitakuwa nikikaa kwa kipindi hicho chote, nikafuata maelekezo aliyonipa nikafika nakuona nyumba moja iliyokuwa ni kifahari sana maana mule ndani ilikuwa kama wanaishi ni kama wanajua dhahiri kwamba wameshafika lakini kabla ya kugonga mlango ule nikavutwa sweta langu kwa akili ya haraka nikajua ni baba kumbe mawazo yangu yalienda tofauti kabisa ni baada ya kuona polisi akiwa na SMG kwa hasira ambazo hata mimi niliogopa akasema.......itaendelea
Safiiii
JibuFuta