Jumapili, 17 Julai 2016

de 1

NGangster noma
Mwandishi: benchrys
1
Nikiwa na umri wa miaka 14 nilikuwa ni mtu ambae hata siku moja huwezi nikuta nyumbani hata kwa bahati mbaya hali ambayo iliwakwaza sana wazazi wangu kila siku wakawa wananisihi nijalibu kupunguza uzururaji kwa maana nilikuwa bado ni mwanafunzi wa sekondari katika shule moja iliyoko njombe mkoa mpya kwa sasa, kiukweli sikuweza kuwa muelewa kwa haraka kama inavo takiwa kwa binadam ambae anaitwa mtu mwenye nidhamu na uelewa. Jaman hivi mtoto kaenda wapi tena saivi wakati huu ndio mda wake wa kuludi kibaya tulicho mwekea tayari hakipo inaonyeshA dhahili kwamba asharudi ila ndio haonekani na alikoenda hata sijamwoma, dah huyu hili badae litakuwa tatizo tena kubwa sana tuu.. Hayo yalikuwa ni majibizano kati ya baba na mama ilikuwa ni mida ya saa tisa mchana, hiyo siku nilipofika nyumbani nilikuwa haraka sio kidogo nikabadili nguo kisha nikafakamia chakula na kuondoka hali iliyowafanya wao hata mmoja wao asinione hata nilipofika wala mda gani nimekula na kuondoka ndio maana wakawa wanaulizana mahali ambapo nimeenda.
   Dah mwanetu upo quick ni kinoma dah ushafika hizi engo tayari dah we noma au leo unataka uwahi kurudi home nini mana daily we mchelewaji, hayo yalikuwa ni maneno ya jamaa yangu joel. Usijali basi tuu mtu ukiShaamua kitu inabidi ujitahid kujisukuma ww mwenyewe nilimjibu hivyo
Basi powa joh langu njoo gheto mi nazama ndani
Powa sio kesi mdau wangu ila na we inabidi uwefasta kidogo co uchelewa teina
Aaaah wewe kitakacho nichelewesha ni nini sasa. Yalikuwa ni majibizano kati yangu na rafiki angu joel.   
    Dah kasimu kangu safari hii kazito hadi kananiboa yani dah, nilisema maneno hayo wakati joel anakula mana mi nlishakuwa full toka naindoka nyumbani.........Alipomaliza kula tukaanza safari ya kuelekea kituo cha internet kwa computer(internet cafe) njiani tulipiga stori nyingi za uongo na ukweli tukiwa karibu na kituo hicho tukakutana na god huyo alikuwa ni moja ya wanafunzi ambao tulikuwa darasa moja tatizo lake ni moja yeye hata mwalimu ashinde anafundisha anaweza kuondoka hajaelewa kitu chochote lakini ni mtu mwenye dharau kwa wanafunzi wenzake halafu ni wakujipendekeza kwa walimu aonekane yeye ndio mtu ambae ni bora kuliko wengine wote, kikweli hata nilipomwona sikutamani hata kumsalimia maana mi nlikuwa mtu ambae siwapendi sana wanafunzi au watu ambao ni vipele iwe mtani au shuleni. Oya ben mwanangu hata kama unamdisi huyo jamaa msalimie tuu huo anaofanya ni utahila wa mda mfupi anavunga we ngoja hapa tupo form two na sidhani kama kweli hadi mwakani tutakuwa wote darasa moja au kidato kimoja, maneno hayo aliyaongea jamaa yangu baada ya kugundua dhahiri kuwa namchukia sana huyo god kipele wa darasa hata kama ni wakiume.
    ngrrrrrrrrrrrrrrr........Ulikuwa ni mlio wa simu yangu aina ya samsung ambayo nilipewa na mjomba nilipofaulu kwenda kudato cha kwanza kwaajili alifurahishwa sana.
     Hallow ivi we mtoto umeenda wapi sisi huku tunakutafuta na hamna anaejua kuwa umeenda wapi acha kutusumbua hebu rudi haraka sana hapa vichwa vyetu vinawaza mambo mengi sana sio kwamba tunawaza kuhusu wewe tuu nakupa dakika kumi na tano nadhani zinakutosha sana kufanya mambo yako na kurejea hapa,,, Ilikuwa ni sauti ya baba baada ya kupiga simu inaonekana alikuwa na hasira sana na ndio maana hajataka hata salamu yangu, aliongea vile na kukata simu. Nikaona isiwe taabu acha tuu niende nyumbani mana kama ni siku nishaharibiwa na huyu god bora nsingekutana nae tu
Oya ben vp mbona kama huyo jamaa yako kashakuvuruga kabisa acha upuuzi bhana hebu twen zetu huko, aliongea hayo maneno joel ila kwangu sikuona kama yanamaana nikamwamba ee bhana ee minaenda zangu home nimepewa dakika tano tuu hapa niwe nishafika nyumbani we unataka niharibiwe siku yangu kama hivi hadi usiku nao niharibiwe vp wewe mzazi ni mzazi bana tofauti na wewe. Maneno haya inaonyesha kama yalimuudhi sana jamaa yangu joel ila nikaona sio kesi sana kama kashamaindi acha amaindi..Kwa hiyo mi kesho ndo kuonana tena bye nilimuaga na kuondoka lile eneo huku nikiwa mbiombio hadi watu baadhi walioniona wakabaki kunishangaa maana haikuwa kawaida yangu kukimbia au kijichosha kwa mazoezi.Jamaa yangu mmoja akanitania oya unawahi uwanjani au mbona upo mwendo hivo sikujibu niliachana nae na kuendelea kukimbia.....

***
Jamani nyie mbona waonezi niacheni bhana uwiiuu vibakaaaaa jaman naomba msada jaman msaada, we tulia tena usije tuletea zari hapa nishakwambia kimya"ilikuwa ni sauti ya bint mmoja akijaribu kuomba msaada huku akifokewa na sauti za kiume ambao inaonekana kabisa ni watu ambao wanaroho mbaya na si watu wema. Nikatulia kidogo akili yangu ikaniagiza okota hata tofali au jiwe kisha nenda huko ambako sauti ya msaada inatokea basi na mimi moyO wa kuwa mtiifu ukaja nikaokota mawe matatu ambayo yanaweza kuwa silaha yangu au msaada kabisa kwa bint huyo, nilipookota nikaenda katika ile chocho ndipo nikamwona huyo jamaa na bint wakiendelea kubishana nika kamata jiwe moja vizuri na kumpga nalo yule jamaa alipigeuka haraka nikashika jiwe la pili nikampiga nalo kichwani palepale akaanguka chini nikamwita yule bint na kuondoka nae huku tukiwa tunakimbia ili hata yule jamaa akiamka  asimwone mtu eneo lile tukakimbia na kupita kona fulani nikasikia sauti ya kimbea na unoko kabisa 'kantangazeeeeeeeee leo naona kuna wamefumwa ila kwa kudumisha upendo wamesepa wote shushuu' nilikariri tuu sura yake na kundelea kukimbia lakini nikiwa naendelea kumbia ghafla bin vuu nikaona.....Itaendelea

benchrys1996@gmail.com

Na
:benchrys.blogspot.com

.......

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni