Jumatatu, 1 Agosti 2016

De 7

Gangstar noma
By: benchrys
7
...baada ya kupiga picha nilihisi kama yule jamaa anadalili za kugeuka hapo na mimi nikatuna lengo nisigundulike kitu ambacho nimekifanya mana laiti angejua kuna nimempiga ile picha basi ingekuwa hatari kama sio hata mtaani pasingetosha maana hakuna mtu m baya yeyote ambae anapenda siri zake zivuje na vitu kama hiyo miguu ya kuku aka pisto hatakama unamiliki inatakiwa asione mtu yeyote kwa maana hiyo yeye ni kwamba alikuwa kafanya kosa kuiweka vibaya hadi sisi tuliiona, Hapo akawa tayari ameshatoka hadi nje ya geti la nyumba yetu hapo na sisi tukawa kidogo tupo sawa mana wasiwasi ilikuwa kama @kigeuka haraka na kutufyatulia hizo risasi....
  Tukaendelee na mambo mengine mana hii ni mida ya kula giza hili tayari lisha ingia. Alisema mama tukiwa pale nje nakuanza kuondoka ndipo na mimi nikaelekea sebuleni hadi pale nilipoiweka simu yangu nikaangalie ile meseji ambayo sikuimalizia kusoma lakini cha kushangaza nilipofika pale nilipo iweka simu yangu sikuikuta kwa haraka nikahisi au Naomi kaichikua!!! Kama kaichukua anafanya nayo nini simu yangu. Ni baadhi ya maswali niliyo jiuliza bila jibu "Naomiiiiii upo wapi" hee we ben kuna tatzo au alisema hivo mama baada nimemuita naomi kwa sauti ya juu sana nahisi sauti ilisikika hadi nyumba ya tatu maana nilijivuta sana kuita hilo jina.. Hapana mama hamna tatizo ila nilitaka tuu nimwulize simu kama yupo nayo nikiwa naendelea kuongea naomi nae alikuwa akija huku kashika simu mkononi kidogo nimwuulize ulikuwa kufanya nayo nini ila kabla sijauliza yeye alianza kuongea kwamba ulipoitwa na mama nilichungulia kupitia dirisha nikamwona yule kaka nikajisemea lazima niwe na ushahidi hata wa picha lakini kuwafata hapo nje ikawa ngumu lakini nilipoangalia kwenye kiti ndipo nikaiona simu yako sikujali ulikuwa unafanya nayo nini nikaichukua na kuingia kwenye camera ili nimpige picha huyo mkaka aliyekuw hapo nje samahani kama nimekuudhi ben.. Na mimi baada kusikia kuwa alichukua ili apige picha nikasema ok basi kama lilikuwa ndio lengo lako powa hamna tatizo nione hizo picha ulizo piga au hujapiga. Naomi akajibu picha nimechukua moja tuu ila nimechukua video iangalie hiyo hapo, akanikabidhi simu ndipo nikaangalia ile video aliyochukua 'kumbe unaakili safi sana gud' nikajikuta nampongeza tuu. Mda wote huo mama nae alikuwa akicheki kinachojiri nae alipoangalia akasema kumbe sisi tungeacha tu
(Usiogope mimi ni mwalimu wako linda na nilikuwa nakuomba kesho unapotoka shule wanafunzi wakitawanyishwa tukutane ofisini kwangu usianze kushangaa sana wala usijiulize wapi nimepata namba yako hayo yote niulize hiyo kesho, kingine sihitaji umshirikishe rafiki rafiki yako jane kuhusu hili Ombi nikutakie usiku mwema BEN)  <ni meseji ambayo nilianza kuisoma mama akaniita kumbe alikuwa ni madam linda sikujua namba yangu kaipata wapi ila alieleza kwamba kama kumwuliza niulize hiyo kesho siku ya ijumaa baada ya wanafunzi kutawanyika lakini nikahisi ni yule god Mwanaume kipele wa dasara letu nilipokuwa sijajua tabia yake nilimpa namba yangu ya simu maana aliniomba kwaajili ya mawasiliano..
   Mama na baba wakiwa sebuleni mimi nilikuwa nje sikutaka kukaa ndani kuepuka usumbufu ila nilipoulizwa nilidai kwamba mtandao wa internet humu ndani unasumbua lakini baada dakika kadhaa nikahisi kama kuna mtu amebifwata nje nilkokuwa nikageuka mwili mzima kuangalia nilimwona naomi akiwa anasogea nilipo nikajifanya kama sijamwona hapo akaita kwa sauti ya chini ben nnaswali naomba kuuliza, niulize sawa mbona upo nje mda huu unaumwa au, hapana mimi siumwi, sa kama huumwi mi naona bora ukajumuike na sie wenzio ndani twende,,,,, aaah bhana ee we nenda nitakuja sasa hivi, ok ila nnaswali jingine ila utanisamehe, sio shida we uliza tuu. Sawa powa ivi wewe na madam linda mna...... Ile kabda hajamalizia kuuliza hili swali ambalo sikulielewa tulihisi kama kuna kishindo kizito pale getini halafu na punze za mchanga zilituangukia wote tuliingia ndani kwa spidi kama robot zimeagizwa kuua vile baba akauliza huko nje inakuaje mbona kama kuna vishindo navisikia alitaka kutoka nje nikamzuia baada ya mda zilisikika kama sauti za watu uwanjani duuh nikasema leo tumevamiwa hapo ndipo nilipohitaji msaada wa linda yule madam nilinyanyua simu na kureplay ile meseji kwamba sawa nimekuelewa ila naomba utume upige simu polisi waje hapa nyumbani tunavamiwa kisha nikaituma ilipopokelewa tuu simu yangu ilianza kuita bahati nzuri niliiwekea silent mode ilikuwa ikiita bila sauti sikuipokea bali nilikata na kutuma meseji kuwa usipige tafadhali hiyo meseji nayo ilipopokelewa ndipo akarudisha kwamba nimeshatoa taarifa nyie zimeni taa za nyumba nzima tena anzeni na taa za ndani nikafanya hivo wale waliokuwa nje yaani majambazi walianza kujibizana kuwa hawa jamaa mbona wanazima taa msimu wenyewe ndio huu cheki ilivokuwa giza mishen yetu itaharibika hapa mimi niliposikiliza zile sauti zao niliigundua kuwa na yule aliyekuja jioni nae yupo tena inaonyesha yeye alikuwa kiongozi wao mana alikuwa akiwaanlisha sana wenzake
Mda kidogo ikaingia tena meseji ya madam kuwa mkiona tuu polisi washaingia washeni taa za nje tuu nikamjibu powa madam

*****nikiwa sehemu yenye switch ya taa za nje tu nikaona licha ni kwa umbali sana kama taa kwenye usawa wa geti mara sauti mpo chini ya ulinzi hapohapo mlipo Atakaekimbia ndio amekwisha. Ilikuwa ni sauti ya askari mmoja na mimi nilipojua kuwa polisi wamefika nikawasha taa za nje zote mda mchache wale majambazi wakawa wameshafungwa pingu wote kwa pamoja. Mimi nikajisemea afadhali saizi ndio kwanza nikalale mana hapa roho ilikuwa juu juu.. Hapo gari la polisi kwa jina la TENGA huku wanaita hivo sijui kwingine mnasemaje lilikuwa tayari lisha ondoka na wale majambaz....
   We ben aliita mama jina langu, naam mama umesema unaenda kulala?? Ndio mimi naenda kulala, unaenda kulala! Leo umekula wapi mwenzetu. Haaa hivi kumbe sijala nilisahau kuwa sijala kweli mimi ni jinga looooh!! hapo ikawa kazi moja kutafuta pot ilinijue msiso ulikonikiuona niukomeshe kwanini nimeusahau ingali nautaka bado kabla sijauona wakasema na nyama umalize nikawajibu mlijuaje thijui..nikawa nishaliona pot lenye chakula na mboga nikagundua hapa ni wali na nyama ya ng'ombe furaha yangu yote ndipo ilipoisha mana hii nyama siitumii
   We mbona mboga umeacha au imechacha, amna haijachacha, saa kwanini huli au haijaiva niliona ananizubaisha tu nilimwambia ngoje nishibe nilikatazwa kuongea ninapokula sorry naomi aha powa
   Nilipomaliza kula sikutaka kuongea na mtu yeyote niliishika simu na kutuma meseji kwa madam linda kwaajili ya kumshukuru kwa msaada wake kisha nikaingia kulala ili niitafute siku ya kesho nikiwa nimelala......itaendeleaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni