Jumanne, 16 Agosti 2016

De 12

Gangstar noma
By: benchrys
12
Nilihisi kama navamiwa hivi maana mtu aliyekuwa anayaka kuingia mile ndani nilimolala mimi alikuwa ananyata kitendo hicho kilinifanya mimi nimakinike kujua hapa ni nini kitaendelea nikiwa nimejifunua lile blanket nikaamua kuachia kaupenyo kadogo ili niweze kuona ni nini kinakuja mle ndani mara mlango wangu ulisukumwa kwa utatibu kama mtu ambae anavizia kukamata kuku vile nikaona hapa kama hawa sio watu wema na mimi acha nijitetee nilifanya kama nastuka hivi yeye akatoka haraka akijua sijamwona ni kweli sura sikuielewa, alipotoka nje huku ndani mimi nikakunja shuka moja liwe mfano wa mtu kisha nikalilaza pale kitandani halafu mimi nililala uvunguni huku nikiwa macho mda wote ilikujua ni nani ambaye ananinyemelea huu usiku. Haikupita mda mrefu sana alirudi tena mle ndani kwakuwa nilikuwa chini ya uvungu niliweza kuona mwanaume mmoja akiwa kavalia dereki/kitambaa sehemu ya mdomo wake akiziba uso wake kwa style hiyo nilitulia kimya hata mlio wa pumzi usiweze kutoka nje au kusikika kabisa nje huko asije akastuka kisha nitafutwe ambako nipo nikiwa naendelea kutazama alitoa kisu kidogo akakiangalia akawa anajishauri kisha akarudisha mfukoni na kutoa kisu ambacho kina urefu wa aina yake kilikuwa kisu kama jambia ila chenyewe ni chambamba chenye mng'ao wa makali ya kukata niliweza kuona mana taa ya nje ilikuwa ikitoa mwangaza....baada ya hapo akakinyanyua juu na kukishusha mahali ambapo kulikuwa na mwili ambapo kwa uelewa wake alijua kwamba ni mimi kisha akachomoa na kuondoka mle ndani kwa mwendo wa kujiamini kabisa hapo nikawaza hivi tayari ningekuwa tayari naiona ahera nilimshukuru sana mungu wangu kisha nilianza kupanga mikakati ya kutoroka usiku uleule..... baada ya yule mtu kutoka chumbani mle aliingia ndani na kuzizima taa zote ambazo zilikuwa zimewashwa kwa mda wote ule alipozima tu zile taa mimi nilitafuta simu yangu kisha nikaangalia mlango cha kushangaza niliona geti lipo wazi nilitoka nje nliona kuna gari limesimama nilipojaribu kuangalia  ndani sikuona mtu nilichungulia vizuri nikaona kitita cha hela kwa akili yangu ya haraka nikawaza kwamba kama walinikaribisha ili waniue mungu wangu mkubwa hapo niliingiza mkono hadi mle ndani ya gari na kuchukua kile kitita cha hela pia kulikuwa na bastola ndogo pisto mnaita niliinyakuwa nayo pamoja na kibox fulan kilichosomeka bullets box niliweka mfukoni na kutokomea kwenye kiza nikiwa mbali niliweza kuona yule baba aliyenikaribisha akiingia katika lile gari huku ile dereki ameshusha ipo shingoni niliweza kujua kwamba ndio yeye aliyekuwa akininyemelea kule ndani ili anichome na lile bisu lake

Usiku ile nilitembea pekeyangu hadi nilipofika katika sehemu moja hivi ambayo palionekana kuwa ni tulivu kwa mimi kujipumzisha nilikaa chini huku nikiendelea kujiuliza haya mambo yote kisa nini mana shule imvamiwa sababu hata sielewi nikiwa naendelea kuwazua nilianza kuona mwanga za mapambazuko kuonesha kwamba ilikuwa tayari ni asubuhi.....nilinyanyuka na kuendelea kutembea nisijue naenda wapi tayari ikawa asubuhi nilipishana na watu wengi ila kwakuwa sikuwa na nguo za shule hakuna aliyeweza kuniuliza swali lolote mana walikonipokea kule walinipa hadi nguo za nyumbani ili nizivae ule usiku mida ilienda sana kisha ikawa tayari imeshatimia saa saba za mchana nilinyanyua simu yangu na kumtafuta naomi "mteja unae mpigia hapatikani kwa sasa tutamtaarifu kwa sms atapokuwa hewani" nimajibu niliyopewa na watu wa mtandao sikukata tamaa nikamtafuta baba ila sikufanikiwa nikamtafuta tena na mama sikufanikiwa duuuh ndio nini hii...nilitafuta namba ya madam linda nae alikuwa hayupo hewani kwa mda huo wote niljihisi nipo dunia ya ajabu sana nikakumbuka rafiki yangu wa shule joel nilipiga kwenye namba yake simu yake iliita bila ya kupokelewa nilikata tamaa nikarudisha simu mfukoni...

Oya we dogo unaenda wapi. Kuna aliniuliza lile swali lakini nilijifanya kama haongei na mimi vile nikapitiliza tena nikiwa ni kama mtu mwenye haraka sana nilipoona nishapotelea nilianza kukimbia huku nikiwa na begi langu ambalo nilikimbia nalo kwa yule mzee mwenye roho yake mbaya haonei huruma binadamu mwenzake na kuthubutu kutaka kuua hili begi nililobeba mgongoni mwangu ndio nilimo weka pesa na silaha hivi vitu ambavyo nimetoka navyo kwa yule muuaji...
......ilipofika mida kama ya saa nane na nusu hivi nilihisi njaa inaanza kuchakaza tumbo langu hapo nikatafuta sehemu ambayo ni salama kwangu na kisha kwenye zile hela nilitoa noti ya shilingi elfu tano na kuiweka mfuko ambao kama nifika sehemu yenye mgahawa nikila tuu naingiza mkono mfukoni na kutoa pesa zoezi hili liliisha haraka tuu kisha nilianza misele ya kuutafuta mgahawa ili niweze kuridhisha tumbo langu nitembea hadi nikajiuliza inamaana watu wa hii mitaa hawajawahi kujua nini maana ya mgahawa,,,,
Baada ya kutembea sana ndio niliweza kukutana na sehemu moja yenye banda la mabanzi huku nje kukiwa na tangazo lililosomeka "jiachie new mgahawa" baada ya kuona hivo nikalifuata lile banda ambapo nilikutana na dada moja aliyenikaribisha,
Karibu kakaangu naweza kukusaidia unahitaji nini. Asante kuna chipsi dadaangu, nilimuuliza hivo akajibu kuwa chipsi zipo ila ni za kupasha hapo nilimwambia ah usijali zipashe tuu na mayai inakuwa bei gani alinijibu kuwa ni shilingi elfu mbili tuu kwakuwa ni mayai ya kisasa nikamwambia anikaangie na mayai....
Hapo alianza kufanya yake huku akiendelea na stori haikuwa shida maana mle ndani tulikuwa wawili tu akaniuliza naelekea wapi nikaona huyu asinipe zari nae ila baada ya kuwaza sana nikampa full mkanda jinsi ilivo akanipa pole kisha ninapoendelea kungoja alinipa soda niendelee kushushia ninapongoja chipsi zile sio nda mwingi alileta kwakuwa zilikuwa tayari nilizipokea na kumkaribisha na yeye..ah usijali ben mimi hapa nashinda na msosi ko mda wote nipo full usijali we kula tuu lakini mi nakuomba usiendelee na safari yako hiyo mana unaweza potea kabisa na wewe huku si kwema sana kaka ben nilimwambia kwahiyo utanisaidiaje, kuhusu sehemu ya kuishi we usijali ntakusaidia tu kwakuwa ilikuwa inaelekea jion akasema leo nawahi kufunga alifunga ule mgahawa kisha tuliondoka lakini tulipokuwa njiani.........itaendeleaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni