Gangstar noma
By: benchrys
13
......pigeni huyoooo pigeni huyoooo,,,,,,, zilikuwa ni kelele za watu wa mtaa ule ambapo kuna mtu mmoja ambae walikuwa wakimkimbiza kwa kelele zilizokuwa zikisikika mwiziiiiiiiiiiii piga huyo nikiwa na yule mhudumu kuelekea huko kwake huyu mwizi alipita kwa spidi kumbe lengo ilikuwa anataka annyakue ule mkoba wa lakini sielewi ni nini kilichonifanya hadi nikakaa chini yule jamaa alipopita nikagungua kwa kitendo alichokiobyesha akiwa mbali kidogo mana alikuwa kanyoshea kidole kwenye ule mkoba wangu huku akiangalia kwa macho ya uchu kuonyesha ameboreka na kitendo cha kuukosa ule mkoba wangu.....
,,,,,,,,hivi ulisema unaitwa ben
Ndio naitwa ben ila yaliyonikuta ni kama hayo.. Aliniuliza hilo swali yule mhudumu hapo na mimi nikajipa nafasi ya kutaka kujua jina lake na mimi.. Samahani lakini unaitwa nani vile nilimuuliza akanijibu anhaa mimi naitwa merry aliponitajia jina sikuwa na haja ya kutaka kujua ubin wake mana jina tuu linanitosha.
Kwa hiyo wewe ni mkazi wa haya maeneo nilimuuliza akanijibu ndio lakini sina mda mrefu sana tangu nije hapa, tulipiga stori nyingi hapo nikakumbuka kwamba hapa naweza kutwa na majanga wacha niichaji simu yangu kwanza..... Samahani dadaangu unachaja ya smatphone. Ndiyo ninayo ila saizi nimewekea simu yangu labda tujalibu kuchajia kwenye deki mana mimi sijazoea kuchajia deki, alinijibu hivo merry baada ya kumwomba chaja ya simu nilitoa simu yangu mfukoni lakini kabla ya kumkabidhi nilimtafuta madan linda simu iliita akapokea kisha tukaendelea kuongea,,,,
Hallow madam,, yaa nambie ben uko wap,, aaah eneo lenyewe hata jina silijui,, ahaa powa ila kama upo mahali salama nakuomba ujifiche hkohuko kwa mda mrefu mana huku hata walimu saizi hatuna ruhusa ya kwenda pale shuleni isitoshe unatafutwa picha za zimebandikwa karibia kila sehemu hasa kwenye nguzo za umeme wanadai kwamba aliyetoroka ile siku ni wewe tuu na katika wale wanajeshi waliokuja na yule baba mwenye visa na serikali anakusaka kwa namna anazojua yeye maana walimkamata rafiki yako jane ili wambane wamuulize kama anajua chochote kukuhusu wewe lakini jane aliwakatalia kwamba hajui baadae nilienda kuamlia mana wakawa wanasema awape namba zako za simu nikaona kama anazo anaweza toa halafu ikawa kesi tena, halafu kuna baba mmoja anaongea kistaarabu hivi wanasema ananyumba kubwa mtaa tofauti na hapa ni mbali kidogo kuwa makini katika mizunguko yako unamopita,,,,, hayo yalikuwa na maneno ya madam pindi nilipompigia simu alinambia huyo mtu wa kuwa nae makini nilimwambia anitumie picha yake huyo baba kupitia whatsapp alikubaliana na mimi kisha akanambia najua utakuwa kipindi kigumu sana ntakutumia pesa kidogo zitakusaidia nilikubaliana nae kisha nilikata simu huku nikiwa na shauku ya kutaka kujua hiyo sura ya huyo baba ambae inatakiwa niwe makini
****ben huyo ni dada ako au mbona unamwita madam, aliniuliza hivo madam mimi nikamjibu huyu ni mwalimu linda mwalimu ambae anafundisha kwenye hiyo shule yetu somo la kiswahili. Merry akasema inaonekana huko imeshakuwa shida mimi nilimjibu tuu kwa mkato kuwa haya yote yatakwisha tuu Mungu ni mkubwa naamini........hazikupita dakika nyingi iliingia meseji kwenye simu yangu upande wa whatsapp nikajua kwamba huyu lazima atakuwa ni madam nilinyanyua simu yangu kutoka pale kwenye sofa ili nifungue niione hiyo picha ila mambo yalikuwa tofauti na vile ambavo mimi nilitegemea itakuwa nilipofungua ile meseji kumbe alikuwa ni naomi ambapo aliandika ujumbe uliosomeka
"ben kama upo sehemu salama nakuomba usije thubutu kumwambia mtu yeyote wa huku mtaan kwetu mahali ulipo mana kuna watu wamesetiwa ilikukupeleleza mahali ulipo ili uje ukamatwe kama unankumbuka yule kaka ambae alikuwa akitaka kuniharibu ile siku kule hadi ukaniokoa kaajiliwa na huyu baba ambae anabishana na serikali kwa hiyo anatafuta njia ya marafiki zako ili akupate ulipo.. Ukiisoma hii meseji naomba uifute bye "
Baada ya kusoma hii meseji nikawa tayari nishapata mwanga fulani kwamba huyu baba inaonekana amekodi na majambazi ili kutekeleza hii kazi yake..... Huo mda wote nilikuwa na begi langu mgongoni ni aina ya begi ambalo lilionekana ni la gharama sana nikiwa nangoja hii meseji ya madam nilimwomba merry niende chumba cha ndani nashukuru merry nae alikuwa ni mwelewa akanambia powa aliloki milango yote kisha akasema nifwate nilimfuata hapo akaenda hadi hadi sehemu moja ambapo mimi nilijua kuwa naingia kwenye kabati la nguo kumbe ulikuwa ni mlango wa kuingilia kwenye chumba kingine cha ndani kabisa.
Nilipoingia kule ndani ndipo nikalivua lile begi langu ili kujua kuna nini cha zaidi mle ndani ukiacha zile bullet box pamoja na pisto ile niliyoibakwa yule baba kwanza nilifungua zipu zote lakini kabla sijaanza kikagua iliingia meseji WhatsApp kwenye simu yangu ilikuwa ni meseji ya madam linda ambayo ilikuwa ikionyesha picha ya mtu lakini nilipojaribu kuangalia vizuri ile picha nikagundua kwamba yule ni yule baba ambako ninefikia jana akawa anahitaji kuniua sikupoteza mda nikamjibu
"duh mungu mkubwa aisee huyu mtu jana usiku nililala kwake lakini alitaka kuniua kwa kunichoma kisu lakini nilipogundua ilinibidi nitumie akili yangu kwa kuweka shuka ili liwe kam binadam kisha nikajificha uvunguni" niliituma
Hapo nilianza kupekenyua lile begi kumbe hili begi ndio maana lilikuwa zito hivi ndani ya begi kulikuwa na laptop fulan ndogo hivi aina ya HP na chaji cable yake pia cd mbili ambazo ziliandikwa window 7 na nyingine windows8 Sikutaka kuwa na papara kwakuwa laptop nazijua haikunipa shida sana kabla ya kuwasha nilitoa betri ili kama inafanya recodi ipoteze mawasiliano baada ya hapo nikaifungua tena ili nijue nini kipo zaidi lakini nilishutuka baada ya kusikia mlio wa simu kutoka kwenye lile begi nilitafuta hii simu ipo mfuko upi baada ya mda kidogo nikawa nishaipata katika ile simu inapoita niliona sura ya mtu kwenye kioo inapoita nikajua wazi huu mtego nilichokifanya niliziba camera ya mbele kisha nikapokea.....itaendeleaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni