Jumanne, 16 Agosti 2016

De 14

Gangstar noma
By: benchrys
14
.....hallow mambo gani hayo tunafanyiana hiyo motonyo inakuja au haiji pia kumbuka kuja na hiyo maiti ili tuteketeze kupoteza ushahidi ila acha upuuzi kwanini unaziba uso au leo network tatizo mana mimi huku hata sikuoni" nini maana ya imo video caller.. Mdau huo yeye anaongea hayo yote mimi nilitulia kimya nisiongee chochote baada ya kimsikiliza sana nilikata simu kisha nikairudisha nilipoendelea kukagua ule mkoba kuna mfuko nilikuta kuna picha za watu ambao baadhi yao niliweza kuwa fahamu kwa sura zao maana walikuwa ni watu wa mtaani kwetu baadhi ya picha hizo hata mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao wameunganishwa kwenye zile picha ni jambo ambalo lilinishitua sana kuona na mimi picha yangu ipo swali ambalo nililipata kwa haraka ni kwamba hizi picha kazipata wapi,,.. Nikiwa naendelea kujiuliza maswali hayo simu yangu ghafla ilianza kutoa mlio ishara dhahiri ya kwamba kuna mtu alikuwa akipiga nilinyanyua simu yangu ili nijue ni nani anapiga hiyo simu kwa mda huo nilipoangalia niliiona namba ya joel ikinipigia simu kwa mda huo nilikumbuka maneno ya madam linda pamoja na meseji aliyotuma naomi kupitia whasapp baada ya hapo nikaweka tahadhali kwangu mwenyewe kisha nikaipokea simu hiyo nilipopokea simu hiyo sikutaka kuongea chochote joel ilimubidi aanze mwenyewe kuongea
Hallow ben vepe wewe!!!! Aliongea kama mara nne hivi na mimi sikuitikia kitu lakini nikiwa makini atasema nini ndipo niliweza kusikia sauti nyingine ya jibaba likiongea kwa kukoroma "huyo boya lako mbona haongei acha kutuyeyusha dogo utapishana na mapene hivihivi huku unajiona shauri zako liliongea hivo lile jitu lenye sauti nzito joel hakuwa jibu akaendelea oya ben eee mbona huongei mdau wangu hizo ni dharau au kitu gan mwanangu" ... Hata kama joel aliongea kama analalamika lakini kwa upande wangu hata sikuona hata haja ya kumjibu neno hata moja maana kwa wakati huo nilikuwa na malengo mawili moja niwasikilize nini watasena na pili washindwe kuamini kama ile ni namba ya simu  baada ya hapo nilikata simu na kuiweka chini........ 

......turudi huko nyumbani mama alikuwa akilia na kutupa lawama kwa serikali kwamba bora wangetoa tuu taarifa kuwa kila mzazi atafute shule ambayo ataweza kumsomesha mwanae kuliko kupotezeana nguvu katika familia kwa namna kama hii.. Wakati huo naomi na baba wakiwa wanajaribu kumtuliza asilie na kumpa matumaini kwamba mwanae ben yuko salama tu mahali hata asijipe mawazo ya kumfanya alie sana.. Baada ya mda kidogo mama alikuwa tayari amesha acha kulia..

****** hivi tangu lini umeanza kuufanya uzembe wa namna hii yaani umempata ndege ameingia hadi kwenye mtego halafu mwisho eti amekimbia isitoshe ameiba na baadhi ya vitu vyako.. kabla Hajamaliza kuongea alimpiga kibao kikali nyie mnaita kofi hadi yule aliye kuwa akiambiwa vile akakaa chini huku akimwangalia kwa huruma kama ndege aliyeko kwenye mtego anamwona mtegaji ndio anakuja.... Hayo maneno yalikuwa ni lawama kwa yule baba ambae alinipokea kwake na kutaka aniue usiku ule kumbe yule nae licha ya kuwa alikuwa na nyumba nzuri lakini nae alikuwa na boss wake ambae anampa hizo kazi za kuua lakini kwa ben alikosa hiyo bahati ya kumwua.... Baada ya kuambiwa yale maneno yote ndipo akaamka na kumjibu yule boss wake kwamba samahani sana hata mimi sielewi ni uzembe gani nimefanya lakini i promise siwezi rudia tena na wala hili kosa halitojirudia tena naomba unisamehe tu kwakweli.,, boss wake huyo hakuwa na la zaidi akamwambia kama umekiri kweli haina tatizo nenda endelea na mambo yako ukamilishe ratiba nyingine.
Walipeana mikono kisha wakaagana na kila mmoja kutoka lakini yule ambae ilionekan amefanya makosa akatoka kinyumenyume jambo ambalo watu wengine waliokuwapo pale hawakuelewa kumbe mwenzao alikuwa na maana yake staili hii ya kutoka ilimsaidia yeye kama boss amemsamehe kwa kinyongo ili anapoondoka anpige shaba basi hata ukifanyika uchunguzi picha ya aliyemuua ibaki kwenye mboni za maiti.....

****turudi kwa ben na merry...dada merry ee samahani nilikuwa naomba msaada wako hapa niliponinajasho kweli mwilini humu maana nmetembea umbali mrefu kweli leo hii. Naweza nikapata hata maji tuu ili nikaoge ikiwezekana nilimuuliza merry nae akanijibu hata usijali kama ni kuoga we usiogope mana hata nje hutoki alinionyesha bafu iliko, nikamshukuru na kuelekea huko bafuni baada ya mda kidogo nikawa nimesha toka bafuni....
Ben aliniita merry. Naam mimi ben nakusikiliza,, akanambia mwenzio ulipoenda bafuni nilikuwa naangalia huu mkoba lakini kuna kitu nimekiona sijakielewa labda wewe kama unakijua ni hiki hapa,,, baada ya kusema hivo akakitoa hicho kitu alipokitoa ukiangalia kwa haraka unaweza sema ni peni/kalamu ya kubonyeza,. Niliishika ile peni kisha nikaiangalia vizuri nikaja kugundua kwamba hii sio peni bali ni kifaa cha kurekodia nakasema duu peni gani inasehemu ya kuweka memory pamoja na earphone hii sio peni halafu cheki kuna alama za maiki humuhumu na chaji hii ni recorder sio peni baada ya hapo tulichukua na earphone ambazo zilikuwa pamoja na ili peni tuliunganisha kisha mimi nilivaa sikio moja pamoja na merry alivaa sikio jingine hapo ndipo kuna sauti zilianza kusikika  maneno ambayo ilikuwa ni kama mjadala wa simu baina ya watu wawili nilisikiliza yale maneno kwa umakini nilichokuja kugundua ni kwamba inaonekana wanampango wa kwenda kuvamia nyumba moja lakini sikujua ni nyumba nani maana ilionekana kwamba walishatoka wanaongea mimi nilisikiliza nikiwa ndio wanamalizia kuongea walipoacha kuongea nikajisemea wasije wanaenda kuvamia nyunbani kwetu jambo nililolifanya ni kutuma meseji kwa madam kwamba "nakuomba kama hutojali tuma polisi wakafanye ulinzi nyumbani kwetu pamoja na hapo kwako maana kuna mpangi m-baya unaendelea nakuomba madam ujitahidi" kisha niliituma muda huo merry alikuwa ashaanza kupata usingizi nilimuwahi kabla hajalala niliita merry!! Eee ben nini bhana nilimwambia hujanionyesha kwa kulala halafu wewe unasinzia amka alijibu ahaa tena bora umenikumbusha mimi nalala huku wewe mlango wako huo hapo hiko ndio chumba ambacho itakuwa ukilala twende nikakufungulie alisimama kisha akaenda kunifungulia mlango... Waoh!!! Nlijisemea hivo kimoyomoyo baada ya kukifurahia kile chumba mle ndani kulikuwa na computer screen ya flat kama kawaida ila mimi niliipenda sana computer. Aliponionyesha akanambia upo huru kutumia kila kitu humu ndani ndio maana nimekupa hiki chumba kwaajili yako ukiona hakikufai utanambia ila kesho na sio leo maana hapa nmechoka aliondoka kuelekea chumbani kwake lakini nilichukua simu yangu nikatuma meseji kwa baba na mama pamoja naomi kwa kuweni makini huu usiku mnaweza vamiwa ila mkiona polisi wamekuja onyesheni ushirikiano niwatakie usiku mwema.... Kisha nikaituma baada ya mda naomi akareply powa ila...hakumalizia na mimi kwa kuon hajamalizia ile meseji sikijipa shida nikalala lakini ilipofika usiku.......itaendeleaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni