Jumatano, 3 Agosti 2016

De 8

Gangstar noma
By: benchrys
8
....ngongongo, ngongongo oya fungua mlango vipi wewe,, aah bhana ee nimelala mimi sitaki kusumbuana naomba uondoke. Mlango wangu ulikuwa ukigongwa kwakuwa nilikuwa sihitaji usumbufu sikuufungua ili isije ikatokea na kesho nichelewe shule kama ilivokuwa hii siku.......
  Wengine wakiwa sebuleni pale ule usiku,, kumbe ben nae ni mwoga daah yaan ameenda kulala mapema eti kisa kesho asije chelewa kama leo ila sio mbaya asafishe hata jina lake kuwa amewahi kulala,
Asafishe jina wapi ben akili yake inamtosha yeye pekeake tuu wengine hata hamuiwezi ni bora mkamwacha tu ila habari ya kusafisha jina hilo swala gumu mana utampa heko leo halafu kesho lisha haribu. Walikuwa wakijadili hayo pale sebuleni wakati nipo chumbani kwangu waliongea wakawa wamesitisha ile mada
'hivi mimi mwenzeni ule mda tumetaka kuvamiwa ilionekana ben kama kuna mtu alikuwa akichati nae na kumpatia plani zile zote na ndio maana polisi wakapata urahisi katika kuwakamata wale majambazi mi hapa mpaka sahizi ninajiuliza ni nani rafiki yake anaejua plani zile za kushujaa mana yeye anadai rafiki yake ni joel tuu huyo joel kajifunza wapi hizo njia,,,lilikuwa ni swali ambali liliulizwa na mama ambapo lilifanya pale wote waliokuwa wamekaa wali hukuchukulie uzito kwa namna fulani licha ya kuwa hawakupata majibu yaliyosahihi..
Au atakuwa na rafiki yake tofauti na joel ambae ashawahi kuvamiwa ndio akatumia hio njia kuwakamata
**** ben nikiwa nimelala nikawa naota wale wote waliokamatwa washarudi nyumbani kwetu kwa lengo lipi sijui wamatokaje? Na kama waneachiliwa ni kwa misingi ipi""" oya wewe dogo nadhani ndiye uliyefanya mpango hadi tumedakwa alivoongea tuu akachomoa kitu fulani kama kiboko hivi kutaka abitandike nacho ila ananyanyua juu na kutaka kushusha mwilini mwangu ben nilijizingusha mithili ya paka aliyedondoshwa kutoka juu anakaeibia kufika chini kisha kwa haraka  ikapokonya ila fimbo yeye baada ya kuona vile akatikisa kichwa na kusema kwahiyo leo unataka kujitia wewe ni mkorea ambae mwili wake ni kama puto subiri ngoja nikuonyoshe we si ninja ee hapo akachomoa kisu akawa ananisogelea lengo anichome na kile kisu duu kikweli ben nilikuwa nina nguvu hadi mimi nilijishangaa kuona napambana na watu  kama  ni mpiganaji wa vita uwanjani, aliposogea na kisu nikazunguka kama upepo ghafla akahikuta ashapokinywa kile kisu halafu nimemwekea yeye kooni hapo ndipo akaanza kutetemeka na kuomba msamaha,,
Tafadhali naomba usiniue!!! alisema mana nilimtaiti kana kwamba akitikisika tu basi ncha ya kisu itakuwa ishazama kwenye shingo yake..ok unasema nisikuue labda nitake kujua huyo unaemtafuta kibaya alichokufanyia wewe ni nini
Hakukuku    ku na kibahya alichonifanyia sasa.
Sasa tatizo lako wewe kwake ni nini? Hapana nisamehe sitamuwinda tena......nilimwachilia akaondoka spidi kali kama mwizi kaiona chochoro ambayo haina mtu.
Nikiwa nimekaa nikaona kundi la vijana linakuja wakiwa na mapanga fulani yaliyo nolewa hadi yanang'aa nikajua hili ni kundi la yule jamaa tu sio watu wengine nikaingia ndani haraka na kuulock mlango kisha nikachukua manati na golori na kupandisha kwenye mlango wa dharura ambao upo juu ya dari na kuvuta kipande cha bati ili nitoke nje,, nilipotoka nilienda mbali kidogo nikashika golori na kuweka kwenye manati ile na kumkadiria mmoja wao sehemu ya mgongo katikati ilipompiga akabaki anagaragara kama mtoto chini wote wakaona hii ishakuwa shida wakaondoka na mimi nilitumia njia ile ile kurudi ndani na kuhifadhi manati kisha nikafungua mlango wangu baada ya hapo nikaona haina haja ya kukaa nje nikaenda sebuleni nikiwa nimekaa simu yangu ilianza kuita..
**** dah kumbe nilikuwa katika ndoto nasimu ndio iliyoniamsha hadi nimeshituka na ndoto iliisha kwa staili hiyo usiku huu niliuona kama ni mfupi kwangu mana kulala nlichelewa halafu ndoto niliyoiota sio ya kufariji hata kidogo...
    Ilipofika asubuhi niliamka kama kawaida na kumkuta naomi alishaamka ameandaa hadi kifungua kinywa.
Habari za athubui naomi nilimsalimia hivo. Powa nzuri tuu leo umeamka na kithembe au hahaha acha hizo nani anakithembe bhana mbona nimeongea vidhuri tyu au nakosea kutamka maneno.....nilikuwa nikifanya makusudi kuongea vile....hapana hujajosea, sasa mbona unasema nina kithembe mi sio fani yangu kuwa na kithembe.... Hahaha nawe acha utani kuwa mtu ambae fani ya kuwa na kithembe kunywaga chai uwahi skuli tuu....haya powa ngoja nikanawe kwanza kisha ndio ninywe chai.
    Woah!!!!!! Uko vizuri chai hii kutafuno kama isingenibidi niwabakizie wengine walai ningeifuta tuu maana tame enhee..... Ok basi powa mi naenda shule bhana badae nikiwa nataka kuondoka.. We ben,   naam ivii.... Au basi ntakuuliza badae tuu saizi nenda shule. Niliondoka kuelekea shuleni nilipofika kitu cha kwanza niliipata namba yangu halafu nakaanza kupepesa macho kumtafuta madam linda mahali alipo sikumwona ikabidi niulize kwa wenzangu kama wamemwona..... Aaaaaa ben ee acha utani madam mineno asubuhi yote hii unamtaka wa nini kama alikupa homework unaeza kumpelekea hata badae, niliwasikiliza hivohivo kisha nikasitisha lile ziezi la kumtafuta mda wa kuingia darasani ulifika ila bado sikumwona nikaanza kujiuliza inamaana leo hajaja anaumwa au maana hata taarifa sijapata na wakati ananamba yangu ila siyo shida sana, hali ilikuwa hivo hadi ulipofika mda wa kurudi nyumbani nikiwa naniandaa kuondoka akaja godson mpambe na mbea wa darasa letu
    Ehee FASEBOOK nambie unataka ukatoe taarifa gani tena mana leo umenifata mimi hapa sio bure tu haya nambie.. Duh kumbe god lile jina ambalo nilimwita hakulipenda akasema. Ben kudadeki nakuheshimu sana nani ni facebook hapa haha eti nani facebook we kazi yako sikutoa taarifa tuu kama facebook ukicomplain powa haya nipe shida yako god akajitia kuleta kiburi akaondoka kwa hasira anapoondoka nikamtupia tena  oya shauri yako sikuhizi hadi mwanamke mwenyewe hatubembelezi sembese wewe boya nani akubembeleze tembea p****y wewe
    Nikaendelea na safari ya kwenda home siku niliiona kama ya ajabu mana hata joel sikuongea nae hadi naondoka kurudi nyumbani nilipofika nyumbani kabla ya vyote nilitaka kuchukua simu na kutafuta madam ila nilipoichukua ndio nikagundua nilitafutwa vya kutosha kulikuwa na missed call 12 message 15... Nikishakula nitazisoma zote sio saizi nikaingia ndani nilibadili nguo na kurudi ili nile nikiwa naendelea kula simu yangu ilikuwa ikiita nikainyanyua ndipo niligundua alikuwa ni madam nikaipokea.... Shik.... Mambo ben. Nilikuwa nikitaka kusalimia shikamoo nikatulizwa na salamu yake ambayo ilikuwa na ujazo wa namna yake... Halafu akaendelea kuongea ben, ndio mimi ben unasemaje. Halaf ben usinijibu hivo mimi mwalimu wako sawa, sawa niliitikia kisha yeye akaendelea nilikuwa nataka nikuulize hivi........ Itandeleaaaaaaaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni