Jumapili, 11 Septemba 2016

De 27

Gangstar noma
By: benchrys
27

.........kulikuwa na polisi wanne ambao waliwekwa kama walinzi kwenye ile hospital kwahiyo rasta ule mda wote walikuwa wakimtazama tuu jinsi anavojitia yeye ndiye kidume katika ile hospital jukumu walilochukua wao hata hawakutaka kujisumbua sana walimtuma mmoja wao ambae alikuwa kashika zile fimbo maalumu ambazo zina cheni ndani yake baada ya hapo alimpiga katika bega lake la upande wa kushoto huku yule mwenzake ambae wapo pamoja akibaki kushangaa, lakini nae haikupita mda mrefu akajikuta akiwekelewa pingu kwenye mikono yake huku akiamrishwa asonge mbele tens bila kuuliza swali lolote lile. Kiukweli hii siku rasta na mwenzie ni siku ambayo waliifurahia sana lakini kutokana na majanga haya wakajikuta wakiilaani vibaya maana hawajui hatima yao kitakuwa nini....mana wameibiwa hela pamoja na funguo za gari wakajitahidi kuwahi hospital ili wasimpoteze ben ila bado wamemkosa kibaya zaidi wamemaliza hata kiasi kidogi cha pesa ambacho walikuwa nacho.....
    
    Walifika kituon wakiwa na wale maafande wa ile hospital kusha wakaamrishwa washuke, kwakuwa walikuwa chini ya ulinzi hawakuweza kubisha kwa lolote walifuata masharti yote.  Lakini baada ya mda kidogo akaja afande mmoja ambae alionekana kidogo ni mkarimu kupita wale wengine wote alimsogelea rasta na yule mwenzie na kuwauliza
:nawaona nyie wote hapa ni wageni samahani ningetaka au niombe kujua ni nini kiliwasibu
:rasta kwa kimbelembele akajifanya kujua sana kwa kutolea maelezo ya uongo....kiukweli afande hapa tulikuwa tumekuja kumwona mgonjwa wetu ambae kabla ya kufikishwa tulielewana na dereva kwamba ajitahidi kukumbuka chumba namba ngapi, na baada ya dereva kusema hafahamu lolote mimi nilijua labda labda katuuzia mgonjwa wetu ndipo nilipatwa na hasira kisha nikampiga lile kofi..alieleza vile rasta

Afande..ok chukua simu yako ili uwape taarifa ndugu zako juu ya jambo hili. :rasta baada ya kuambiwa vile akaona huyu afande inaonekana hana msaada kwakuwa yeye pale hakuwa na simu kutokana na simu yake kuipasua kule hospital

Samahani afande hapa sina simu labda nimuombe mwenzangu maana tulikuwa wote....aliongea vile rasta

Ndio nini sasa simu yako iko wapi hadi uazime ya mwenzako...afande aliongea
Rasta nae akajibu iliangua kule hospital kisha iliharibika kabisa..kwakuwa afande alikuwa ni mtu mwenye busara akamruhusu kuazima simu ya huyo mwenzake.  Basi rasta alimwita mwenzake kisha akamwomba simu lakini hawakufanikiwa na pia afande aliondoka baada ya kusikia kuwa mwenzie na rasta nae hana simu mahali pale kwasababu nae simu yake iliachwa kule kwenye gari ambalo funguo zipo na ben........

********
********
      Ivi jamanj humu ndani inakuaje kipindi hiki!!!! We naomiiiiiiiii uko wapi hebu njoo kuna jambo nahitaji kukuuliza hapa....alikuwa akiongea mama huko nyumbani baada ya kuona mambo yasiyoeleweka mule ndani
Bee mama nimefika...naomi
  Mama: hapa kuna jambo nimeliona halafu hata sijalielewa sijui ni nini hiki sasa, hivi hizi bastola humu ndani zinatokea wapi?
:naom: kiukweli mama hicho kith alirudi nacho ben sikumoja hivi ambapo aliwahi kurudi kama unakumbukua ile siku amerudi sa 9 ndipo alirudi na hivo vitu mimi sielewi alipata wapi kwakweli
Mama: ok sawa nitamuuliza wee endelea na shughuli zako...lakini alipokuwa akiondoka alimtumia meseji ben ikisema kwamba ""mama ameziona zile pisto ulizorudi nazo ile siku akaniuliza ni vya nan ila nimemwambia kuwa ni vyako, ukiona nomekosea nisamehe tuu bure ben""

Nikiwa nimekaa kwa merry baada ya kutoka kutembea huko kwenye simu yangu iliingia meseji, nilipoifungua ndio alikuwa naomi niliifungua nikakutana na ujumbe ule aliouandika kunipa taarifa za bunduki zile ndogo ila sikichukulia uzito wowote nilimuandikia ""akikuuliza tena mwambie ahifadhi ndani vizuri" kisha nikaituma kwa naomi.. Kwakuwa iliingia giza nienda ndani na kuendelea kucheza na computer ya kule chumbani kwangu, sikukaa sana merry aliniita kisha tulipa chakula na kuelekea kulala

********nikiwa usingizini*****

.....dogo safari hii utakamuliwa hadi utumbo maana kama ni kutusumbua akili umetusumbua vya kutisha nadhani wakati umeisha sasa. Aliongea mmoja na mwingine kisha mmoja akasema...niko tayari hata nigombane na ukoo wako wote ile tuu nikamilishe hii kazi sijui kama unsnisoma we dogo alipomaliza akanibamiza kofi jipya la 5g duuuuh kidogo nilie maana wakati huo wote nilikuwa nilikuwa nimekalishwa chini huku nimefungwa kamba kwenye nguzo fulani...nikiwa na hasira sana niliomba sana Mungu alete miujiza hii kamba hata ikatike itakuwa powa sana..huku wao wakiendelea kunitupia maneno mengi

Aaaah   mungu mkubwa nilijisemea kimoyomoyo tena kwa furaha mana kuna mbwa sijui alitokea wapi alianza kutafuna ile kamba kwakuwa ilikuwa usiku hakuna aliyeweza kuinasa hadi nilifanikiwa kukimbia lakini nikiwa natoka njee sikuweza kuamini nilianza kujisemea pekeyangu hivi hapa nimekwepa au ndo nishatumbukia....hayo maneno yalitokana na hali iliyokuwapo njee ya nyumba kulikuwa shimo kubwa ambalo sikujua hata limechimbwa mda gani, nilisogeza mguu kutaka kujua n nini kipo mle nikiwa nasogeza mguu wangu udongo ule ulianza kuvunjika ukielekea kwenye lile na mimi hapo nilitereza kutumbukia kwenye shimo***nikaja kustuka kumbe nlikuwa naota usiku ule duuh.. Nilichukua saa na kuangalia ilikuwa ni saa 10 na nusu usiku kwa kuwa nlikuwa bado nnausingizi nilivuta blanket tena ili nilale ndani ya dakika tano tayari nilishachukuliwa na rafiki wa wengi ambae ni usingizi
    Ilifika asubuhi niliamka lakini nikiwa naelekea bafuni nilipita jirani na chumba cha merry nikasikia sauti ya mtu analia, sikujali sana nikapita ile naludi bado niliona bado ile hali ila bado sikujali sana nikaingia chumbani kwangu nikavaa nguo nyingine na kutoka ndipo nlimkuta merry amekaa sebuleni akiwa bado analia, nilimsogelea taratibu ili kumwuliza lakini nilipofika tuu jirani naye pale kwenye aliyumbisha kichwa na.... Itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni