Jumapili, 11 Septemba 2016

De 28

Gangstar noma
By: benchrys
28

......merry aliyumbisha kichwa pembeni na kulala kitendo ambacho kilinifanya nisijue ni nini cha kufanya niliita kwa sauti #meriiii zaidi ya mara saba lakini sikuweza kuitikiwa kwa sauti yeyote nikajiuliza inamaana alikuwa anaumwa au mbona hivi..kiufupi sikuwa na jibu sahihi niliichukua simu yake ilinijue kama kuna namba yoyote ya dsktari ili aweze kuja atoe msaada kama ikiwezekana nilipochukua simu yake ilikuwa na lock za pattern hii too much nilinisemea mwenyewe baada ya kuona vile nikaamua niondoke ili niende hata kwa majirani pengine naweza pata msaada
Nilifungua mlango kisha nikatoka nje lakini kabla sijapiga hatua nyingi nilihisi nyuma yangu kama kuna kitu kimepita kwa mwendo wa haraka niligeuka na kurudi nyumbani ile nafika mlangoni nilisikia sauti ya mlango kubamizwa kabla ya kufungwa niliuwahi na kuingia ndani ndipo nilikutana na mtu ambae kwa kumwangalia alikuwa kajazia sana maeneo ya kifua, nae alipohisi nimeingia alicheka kwa dharau kisha akanigeukia lakini kwa kuwa babu alinipa staili nyingi za kupigana kule porini nilijua tu kuwa nae anataka anifanye mbabe pale. Baada ya kuniangalia na kucheka kwa dharau akanisogezea uso wake karibu na wangu akawa anaongea kwa sauti ya chini
""""dogo humu ndani kama ulikuja kuleta shobo zako leo hutoki humu ukiwa hai sitahitaji kujua wewe ni nani na huyu ni nani yako hayo unafahamu wewe mimi ilimradi nikamilishe kazi yangu kwa amani na usalama zaidi na ndio maana nikampulizia huyu ile dawa hadi amelala hivi na hapo hajielewi kabisa hebu njoo huku"""

Baada ya kumaliza kusema yale alinishika kwenye shati langu wenyewe mnaitaga t shirt sijui sana, baada ya kunishika vile alinisogeza hadi sehemu fulani ambayo ilikuwa na uwazi katika ile nyumba hapo ndipo aliniachilia ile t shirt yangu kisha akasema ngoja kazi nikuonyeshe sio swala la mda mrefu wait......kisha akaondoka ila mimi baada ya kuangalia niliona kwenye dirisha ambalo nipo jirani nalo hakuna nondo isitoshe lipo wazi ni kitendo cha haraka sana nilikwea lile dirisha na kuingia ndani kisha nikatokea chumba cha mery na kufika sebuleni muda huo kabla ya yule mbabe kuingia maana nilishajua dhumuni lake,,,,sikuzubaa nilimnyanyua merry na kumpeleka kule kwenye chumba cha siri kwenye ile nyumba kisha nikatoka haraka nikiwa na nguo maalumu za kung fu fighter kama masta fulani wa kichina nguo hizi nilipewa na babu kule porini

       Baada ya mda kidogo yule mbabe alikuwa akifungua mlango ili kuingia ndani. Nilijiandaa pindi aking'aza tuu sura yake ndani lazima ajute baada ya sekunde tu aliweza kuufungua mlango lakini alirudishwa nje alikotoka kwa mateke mawili mazito moja likitua kichwani na jingine kifuani......alitua nje kama peto la mtumba baada ya hapo na mimi nilinfuata huko nje nikiwa namngoja ili asimame tuoneshane

Alinyanyuka kwa hasira sana kisha akachomoa kisu mfukoni mwake na kuanza kunisigelea lakini kidume hata sikutishika hata kidogo nikabaki tu nimesimama huku nikimngoja ili nijue anachotaka kufanya nae bila woga alisogea akiwa katanguliza kile kisu chake.....aliponikaribia tuu aliongeza mwendo wake kunifikia lakini kabla hajafika nilichumpa juu na kujigeuza kama paka nilipokuwa natua chini kisu tayari kilikuwa mikononi mwangu nae kwakuwa alishakariri kuwa mimi boya kama wengine akajua hii ilikuwa bahati mbaya tuu akajipanga na kunisogelea tena kwa spidi ila kabla hajanifikia niliruka na kuzunguka mara tatu hewani kisha nikampiga mateke mawili ya uso hali iliyomfanya apepesuke kama mgonjwa wa maralia kali na kwenda chini kama kipeto kisichokuwa na maana sana mda wote huo mimi nilikuwa kimya kikazi zaidi
Baada ya kutua huko aKapata nguvu tena na kujivuta ili anisogelee tena nilimwangalia kisha nikafanya kama naondoka kuelekea getini nae ndipo akajua amepata wakati mzuri wa kunivaa kumbe nilimwekea kama mtego wa kumpeleka hadi kabisa ya nyumba ile___nilipiga hatua chache nae akawa kwa mwendo wake tayari yupo jirani na mimi, nilidunda katika ukuta wa pale jirani na geti akiwa hana hili wala lile nilitua moja kwa moja kwenye mgongo wake kwakuwa geti lilikuwa wazi aliweza kupitiza hadi nje kabisa ya hii nyumbani hakutamani hata kugeuza uso wake mana alikuwa akinizarau lakini shughuli  aliyoipata hakuweza kuamini kabisa kama amemfunza adabu Kamanda mzima......

******huko nyumbani naomi akiwa katumwa dukani akanunue baadhi ya mboga akiwa njiani alibetuliwa bila kujielewa alianguka chini puu duuh alilia sana lakini baada ya dakika chache akakakuta akinyanyulia na mtu baada ya kugeuka kumbe alikuwa ben kafikaje hadi hayo maeneo hakuna anaejua.....baada ya kumnyanyua nilimruhusu aendelee na safari yake ili nichuane na huyu aliyembetua ngwala nae baada ya mimi kumnyanyua naomi na kumruhusu aende ilionekana ni kitendo kilichomuudhi sana akanisogelea na kunishika roba shingoni kama kunitisha lakini alishangaa kuona mimi nacheka tu akataka anipige zinga la kofi lakini ni kama kitendo cha sekunde alikuwa tayari kakunjwa mkono wake yaani akileta fujo nilimwambia navunja....hakuwa na la kufanya ilibidi aombe samahani na mimi nilimwachia aendelee na safari zake niliifuata pikipiki niliyokuja nayo aina ya boxer kisha nikaendelea na safari zangu nilitembelea mitaa mingi sana siku hii badae niliamua kurudi nyumbani.
..naomi nae alipofika nyumbani aliwaeleza yaliyomkuta njiani.......nikiwa bado katika usafiri nikielekea nyumbani kwa naomi simu yangu ilikuwa ikiita lakini kabla sijaipokea mbele yangu niliweza kuona.......itaendeleaaaAa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni