Gangstar noma
By: benchrys
30
.......mbona huendelei kuongea huku umesema unajua kilichotokea pale au kuna kitu ambacho mnataka kunificha, aliongea yule afande ambae alikuwa akitaka kusikiliza maelezo ya yule mama lakini chakushangaza maelezo yalisimama baada ya mzee fulani kuingia pale ndani huku akiwa na mikono yake mfukoni, yule mzee aliyeingia mle ndani akawa anazungukazunguka kisha akavuta kiti na kukaa neno la kwanza kuongea ilikuwa ni kwa afande. Yule mzee alimgeukia afande na kumuuliza mbona leo kijiji kizima nakiona humu inakuwaje,,,,,yule afande aligeuka kwa hasira sana kisha akamuuliza ivi wewe ndio mkuu wa kituo hiki ondoka tena usiniharibie siku kabisa tokaaaaaa nasema kisha akawaita vijana watatu ili wamwondoe mle ndani haikupita mda waliingia vijana watatu wakamshika yule mzee mkukumkuku kisha wakaondoka nae
*****ben na merry mda wa jion tukiwa nyumbani tunaangalia taarifa ya habari mara kuna habari moja iliweza kutushitua hadi tukajikuta tukitazamana wote mimi na merry habari ilikuwa
___kwanza walionyesha picha ya nyumba ile ya merry na kutolea maelezo kwamba yeyote aliyeko jirani akae kwa amani endapo akiona usiku kuna watu wanafanya uchunguzi wao___iliishia hivo kisha kikaendelea kipindi cha miziki kilichokuwepo mda wote ila kwa upande wangu sikuona haja tena ya kusikiliza ile miziki dakika chache tena iliongezeka habari ambayo ilikuwa ikionyesha polisi watakao kuwa wanafanya uchunguzi huo kulikuwa na polisi watatu ambapo mmoja nilipomwangalia nikakumbuka kuwa hawa ndio walio mpulizia merry sumu chumbani kwake kwa lengo wamteke. Baada ya kuona vile nikajua wazi kuwa hspa itakuwa shughuli tena sio ndogo maana yule
Polisi anashirikiana na majambazi au maharamia..
Nilitoka pale nikaingia chumba changu cha ndani nikatafuta lile begi ambalo nilipewa na babu ndipo nikachapua mavazi ya kininja na kuvaa huku nikiziandaa silaha zangu zote vizuri baada ya hapo nilichumpa nikawa nimeshadaka kimlango kidogo kilichopo juu kwaajili ya kufikia kwenye dari baada ya hapo nilipanda juu kulikuwa na mlango wa emergenc juu ya paa ndio niliotumia kutokea niliruka beki mbili mfurulizo nikatua chini upande wa nje kisha nikaenda kukaa kwenye geti la nyumba nilisimama mda mfupi nikaweza kuona gari fulani likija pale, nilitoa miwani yangu ya giza na kuivaa ili nione vizuri kila kitu
Ile gari kabla haijasogelea ile nymba nilianza kuifuata taratibu waliponiona walianza kufyatua risasi zao kwa vurugu lakini nilizikwepa zote baada ya kuona wamesha ishia risasi kwenye bastola zako wakashauriana watoa ili waje kupigana na mimi kwa mikono, walitoka huku wakiwa wamejipanga vya kutosha lakini kwakuwa ilikuwa giza kuona walipata shida kuona kila kitu, kabla ya kunifikia mmoja wao aliamua kurudi kwenye gari iliawashe taa za gari kwaajili ya mwanga. Wote walifika hadi ambapo mimi nilisimama, sikuwangoja waanze mwenyewe tuu niliwaanzilia kabla hata hawajajiandaa niliruka juu kisha nikampa kila mmoja wao zawadi ya mateke ya uso wote walianguka chini kisha wakasimama kuanza mashambulizi maana mwanzo niliwashitukiza
Alinisogelea mmoja akitaka kurusha ngumi nilikwepa kisha nilimpiga ngumi tatu mfululizo za kifua mwingine alitaka kuninyemelea nyuma niliruka begi kurudi nyuma kwakuwa alikuwa force alienda kumvaa mwenzie wote waliangukiana chini kama vipeto alibaki mmoja huyo nilidank nikatua kwenye kifua chake na kurudi pembeni aliamua kukunja ngumi akanisogelea huku akirusha teke, na mimi nilirusha teke ambapo miguu yetu ilikutana juu kwa juu,,,,baada ya mimi kuhisi lile teke halijampata vizuri niliruka juu na kumpa teke jingine la uso alipepesuka nilimfuata kwa mateke matatu mfululizo ya kifua alitua chini alipotaka kunyanyuka alikuwa ameshaishiwa nguvu hivyo hakuweza kunyanyuka akabaki kalala tuu wale wenzio walishikana na kwenda kwenye gari ili wakimbie maana kazi yao haikufanikiwa
Waliwasha gari kisha wakamchukua na mwenzao walimweka kwenye gari kisha wakaanza kuondoka kabla hawajafika mbali niliifuata ile gari huku nikiwa na msumari kisha nikaupigilia kwenye tairi nyuma kisha nikaondoka
****waliondoka ila wakiwa njiani wakaona gari linaenda kiupande kuonyesha tairi moja halina upepo walisimamisha gari wakashuka hapo waliweza kugundua tairi la nyuma upande wa kulia halina upepo. Walitafuta simu ili wampigie mkuu wao lakini kwa bahati mbaya wote simu zao haikujulikana zipo wapi....kumbe waliziangusha walipokuwa wakipambana na ben na mimi baada ya kuziona zile simu nilichukua na kuzitupa mbali sana ili hata wakitrack wapoteze tuu ramani zao.
Wale polisi baada ya kuona hakuna namna ya kufanya walipiga mahesabu wakaona hakuna namna nyingine waliingia kwenye gari kisha wakalaza viti usingizi ukawachukua kwenye gari mule hadi asubuhi
****nilipoona nisha maliza kazi yangu ya kuwazuia wale polisi sikutaka merry ajue kama nilikuwa nje, basi nilijivuta kama hatua tano ivi kisha nikatoka spidi nikaruka juu kama paka (kavu) nikavuka ule ukuta na kutulia ndani kimya kimya nikachukua kamba fulan niliyokuwa nayo nilirusha hadi kingo moja iliyoko juu ya bati kisha nikakwea hadi juu ya bati niliitingisha kidogo ikaachia kwenye ukuta, niliikusanya kisha nikaingia tena hadi ndani nikalala ilipofika asubuhi....itaendeleaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni