Jumanne, 27 Septemba 2016

De 36

Gangstar noma
By: benchrys
36

----ilipofika saa nane usiku usiku nilihakikisha kila mtu tayari ameshalala niliamka na kutokea dirishani kwangu nilidank hadi nje na kuruka ukuta wa nyumba ile kisha nikaenda na kuwasha gari kisha nikaenda kulitelekeza katika kichaka fulani kinachoelekeana njia ya kituo cha polisi kisha nikarejea tena nyumbani na kulala hadi asubuhi

___ilipofika asubuhi taarifa za habari kwenye vyombo mbalimbali zilikuwa zikiongelea kuhusu uvamizi wa nyumba ya mwepelwa ambapo aliweza kusaidiwa na mtu inaesadikika kuwa ni ninja lakini ni aina gani ya ninja hawakuweza kujua na kusema kuchunguzi unaendelea kufanyika ili kuwadaka watu hao ikiwezekana wamkamate hata huyo ninja kwa kutumia mitego yao, wakiwa wanaedelea na taarifa ya habari ilionekana kuna taarifa nyingine ya dharura kwamba polisi waliotumwa kwaajili ya kupata taarifa zaidi za hiyo nyumba iliyovamiwa ni kwamba saizi asubuhi ndio wanaingia kituoni na wamefika bila gari. aliitwa polisi mmoja ili atoe maelezo kuhusu kilicho wapata ikaonekana kila polisi ni kama anaona aibu kwa maana kwa polisi kama umetumwa halaf ionekane umeshindwa kazi wewe utaonekana huna maana tena/// baada ya mkuu wa kituo kugundua kuwa hakuna anaetaka kuwa wa kwanza kutoa maelezo ili taarifa ikamilike akatoa amri kwamba watahojiwa kwa taratibu zao kisha habari nyingine ziliendelea

*******nikiwa nimekaa naangalia baadhi ya taarifa kwenye simu yangu mara simu yangu iliita aliyekuwa anapiga alikuwa ni madam linda. Duh ivi hii namba ilikuwa bado ipo tuu aisee (nilijisemea pekeyangu maana ni mda mrefu sana sijaongea nae) kisha nikaipokea na kuweka simu sikioni
--hallow madam
- hallow mzima ben
-- mimi mzima tuu sijui hali yako
- mm nko pouwa sijui hali yako maana ni kitambo sana tangu tuwasiliane umenisusa hadi basi ani
--amna sijakususa mimi sema life linakaba vp wazima wote lakini
- huku wazima uko wapi now
-- nipo kwa wazazi
- ohoo ntakutembelea (alivoongea hili swali hata sikutaka kulijibu kabisa maana nilijua naweza anza kufanyiwa uchunguzi bure)
--sawa ila lini utatembelea huku/// baada ya kuniuliza hivo akasema jumapili hii ndio atakuja mtaani kwetu ndipo tuonane

Kiukweli hata sikuhitaji kabisa tuweze kuonana na nikapanga taratibu za kumdanganya hata baba ili tuu niondoke ile siku ya jumapili maana hii ilikuwa ni siku ya jumatano, siku zilienda hadi jumamosi. Hii siku nilikuwa bize kidgo kwa kufua nguo zangu ili kesho ikiwezekana niende kwa merry nikakae kwa siku kadhaa.
Ilifika hadi jioni ambapo nilipoangalia nguo zangu zote zilizofua tayari zilikuwa zisha kauka nilizianua na kuingia chumbani kwangu ili nizipange vizuri kwaajili ya kesho lakini nikawaza nitatokaje huku sijamwandaa baba kuwa naondoka

Siku iliyofuata ilikuwa ni jumapili asubuhi wote walienda kanisani lakini waliniacha pale ambapo waliponiuliza nikawaambia ntaenda misa inayofuata yaani ya mchana basi waliondoka baadaya mda kidogo kukawa kimya pale nyumbani nikiwepo mimi tuu
Ndipo nilichukua kikaratasi kidogo na kuandika ujumbe fulani kisha nikaweka kwenye meza na kuondoka na kibegi changu kidogo. Haikunipa shida sababu nilishaongea na merry usiku wa jana safari yangu ilianza kuelekea kwa merry huku nikiwa na kibaiskel changu cha kupora kwa yule aliejifanya anajua kupigana

Nikiwa njiani nilishutushwa na mlio mkali wa honi kwenye barabara ila sikumwelewa ni makusudi au mana nilikuwa pembeni kabisa ya barabara baada ya hapo akanifuata na gari lake na kubana upande wa pembeni ili nisiweze kuendelea na safari yangu nilipomwangalia vizuri niliweza kuona sura ya god akiwa ndio mwendeshaji wa lile gari

Oya facebook sasa mambo gani hayo ya kuchelewesheana safari bhana hebu toa katakataka kako huko
Aisee ben ee hebu acha kunifurahisha huko sasa hili gari na kabaiskel hako kipi ni takataka sasa unaniletea wazimu toa m*****nge nini wewe/////nilipata hasira baada ya kuona ananiletea mambo ya dharau huku mtu nina safari zangu na isitoshe ni mbali ninapo fika. Alipogundua kuwa nimekasirika alifunga kioo cha gari lake na kupiga lesi nyingi sana kwakuwa ilikuwa gari chakavu eneo lote lilikuwa ni moshi tuu kisha akashuka kupitia upande mwingine alizunguka nyuma ya gari mimi nikiwa bado nangoja atoke nilishituka nafungwa na kamba mwili wote kisha nikapakiwa kwenye gari. gari liliondoka hadi nyumba fulan ivi, ile nyumba nilipoingalia vizuri nikakumbuka ile siku yametokea maafa shuleni nyumba ambayo niliomba kujihifadhi lakini wao wakawa na lengo la kunitoa uhai, hapo ndipo nikapata akili kwamba yule mzee alikuwa bado akifanya mpango wa kunikamata ila sikuhofia maana kipindi kile nilikuwa bado boya sana+++++/safari ilinyoosha hadi kule ndani nikiwa vilevile nimefungwa baadaya muda wakanishusha na kuniweka kwenye chumba fulani hadi ilipofika giza, waka panga tena mipango ya kuniteketekeza kwa bahati niliwasikia nikapanga jins ya kujifungu pale. Niliweza kuangalia pembeni kulikuwa na mlango ambao haupakwa rangi ipo finishing tuu au cement basi nilijivuta hadi pale nikaanza kujiburuza pale hadi kamba zote zilikata kisha nikabadilika na kuwa ninja nikachukua mkanda na kuufunga kiunoni kuonyesha sia mzaha na mtu dakika chache mlango ulifunguliwa.. kitendo cha sekunde tu nilichomoa star(nyota) na kuirusha ambapo ilikita kwenye tumbo yule aliyekuwa akifungua mlango tayari akawa yupo chini huku damu zikimtoka nyingi sana kwa mda huo hakuwa na pumzi tena baada ya hapo nikatoka na kunyata hadi kule sebuleni ambapo nilikuta yule mzee akiangalia movie ya anord (predator) mnaifaham hivo kupitia dirishani niliingia ndani ndani kama upepo na kumkaba shingo dakika chache akawa kuzimu nae baada ya hapo nilifuata hadi geti kubwa ile natoka nje nilisikia sauti za ving'ora na taa za mwanga mkali-----itaendeleaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni