Jumatano, 5 Oktoba 2016

De 37 (end)

Gangster noma
By: benchrys
37(mwisho)

--------nilitoka hadi nje ndipo nilisikia vingora vikilia huku na taa za mwanga mkali vikinimulika
Sikupoteza mda kabisa niliruka beki juu sana na kutua tena chini waliokuwa wamezunguka lile eneo walibaki tuu kushangaa mana pale hapakuonekana kitu tena
Mtu kapotea kimiujiza hapohapo wote walitawanyika nakusambaratika kila upande ili kama nikionekana tuu nidakwe ( duuuh kwakweli hawa polisi sijui waliahidiwa zawadi gani endapo wakinishika)

Tukiwa maeneo fulani kuna watu walikuwa wakipiga stor zao za kawaida

Duh ivi na nyinyi mmesikia kuhusu ninja ambae anaharibu mapolisi na baadhi ya watu wanaojifanya kujipendekeza kifarafara
Aaaah acha ndoto hizo wewe ivi hii Tanzania kabisa iwe na ninja badae utasema spider man nae ameonekana tanzania acha kutushika maskio wewe
Sio kwamba nawashikamskio ila ndio ukweli, duuuh kweli hata redio  hamsikilizagi majumbani kwenu
Acha hizo sasa mi redio nisikilize inanifaidisha nini sikuizi ni mwendo music kene flash basi hizo habari za redio achana nazo ushamba huo

Ndo maana hakuna unalo fahamu jinga wewe

Aaaah mi siwezi kubishana na wewe mtoto wa mama vipi wewe kalale huko

Dadeki powa mimi mtoto wa mama we siulinyonya kon ya babaako(alijibu hivi bada ya kuona ameambiwa mtoto wa mama)

Gafla tuu pakawa hapakaliki tena ngumi za mavumbini zilianza. Wakati huo wote mimi nilikuwa nimekaa pembeni nawasikiliza tuu jinsi wanavobishana hadi saizi wanabishana lakini kwa kutotaka kuwa shahidi nikasimama na kuondoka hata kama haya maeneo sikuwa mwenyeji baada ya mimi kuondoka bila kuaga hata kwa mtu mmoja. Gafla watu wakakuta wakipigwa virungu na maafande fulani watatu
Vijana kazi za kufanya ni nyingi nyie mchana huu mnapigana kama kuku mnaakili nzuri kweli nyinyi nawauliza mnaakili
Maneno hayo yalikuwa yameambatana na virungu 

Ben nikiwa nyuma ya ukuta  fulani hivi niliweza kusikia sauti ya vilio vya watu wakilia sana nilirukia hadi juu na kuchungulia ni nini kinaendelea upande mwingine ndipo nikaona wau wakipokea kipigo. Hapohapo nilichange na kuwa ninja nikiwa na lengo nikawa tishe tuu

Maafande wakiwa wanatoa ile dozi hevi wakashangaa ninja anakuja mbele yao waliondoka mbio na kusahau vile virungu vyao nilibaki nikicheka tuu lakini gafla nikakuta tunazingirwa na watu waliovalia nguo za kijeshi huku wakiwa wanaonyesha dhahiri kwamba hawapo kimzaha na mtu mana kuna jamaa alijipitisha alipokea teke moja na kwenda kuanguka mbali sana na mimi nikajisemea kama kudakwa hadakwi mtu naondoka na roho za watu leo
Wakati huo nimechuchumaa mguu mmoja chini nikabadilisha style na kukaa kama muislam akiwa kuswali (wanaohusika wanajua) na kuweka ishara fulan katika vidole vyangu kishanikanyanyuka kwa kasi ya ajabu
Wale wanajeshi wakajipanga alisogea mmoja nikampiga ngumi ya uso ambapo alipepesuka na kwenda kuangukia kwa mwenzake wakaja wawili niliruka beki mbili mfululizo juu huku nikizunguka kama gurudumu nikaduna chini na kutua katika vifua vyao wote walianguka chini huku wakikohoa mmoja nilishuhudia akitokwa na damu mdomoni lakini sikujali kuliko nikamatwe

Baada ya hapo nikaona wote wakija nilichomoa upanga wangu na kuanza kuwafuata lakini hawa wote walikuwa na roho za nini sijui mana woga kwao walishatupaga na ulikopotelea wamesahau
Nilianza kuuzungusha ule upanga lakini kwa uwezo wao waliweza kukwepa nilipoona hii njia kama ni mbaya niliruka beki juu na kupita kwenye vichwa vyao ili nipate nafasi ndoto tuu baada ya kuwapita wote nilitoa cheni iliyokuwa imefungwa na gorori nzito za vyuma na kuanza kuwatandikia zoezi lilitembea kwa mda wa dakika kama ishirini baada ya hapo wote walikuwa chini tena wapo hoi kabisa

Niliondoka humu nikiwa na furaha ya kuwa sijakamatwa lakini kufika mbele nilikutana mwanajeshi mmoja ambae alikuwa kasimama katika ya barabara aliponiona akaanza kupiga makofi akinishangilia ninapo kuja ila sikujali nikaendelea kumfata tuu

Baadaya hapo akanisimamisha kwa alama ya vidole nikasimama
Wewe ndie unajifanya mwanaume sana sasa leo nataka tuone mimi na wewe nani zaidi
Baada ya kuongea yale alidank juu na kunipiga teke zito la kifua, teke lile lilinipeleka moja kwa moja hadi chini hadi sikuamin sijakaa vizuri ngumi ya uso lakini alikosea kunipa upenyo wa kusimama niliposimama
Alidank tena ili arudie ile style ya mwanzo lakini alifeli nilimuwahi kwa kupiga kwa nguvu sana katika kiuno chake akatua chini kama gogo nilimgoja asimame aliposimama nikaona asinipotezee mda hapo nikawa namchanganyia mateke ngumi huku vyote vikiwa ni vizito hadi baadae akawa hawezi kusimama ndipo akaaanza kuropoka
NIMEJITAHIDI KUKUTAFUTA KWA KILA NAMNA LENGO NIKUDAKE LAKINI NAONA KAMA NI UJANJA UMENISHINDA UMENIVUNJA MGUU NA MKONO TAFADHALI USIENDELEE UTANIUA BURE WEWE NI ZAIDI YANGU
HATA MLIOKUWA MKISOMA NAO BAADHI NILIWAUA NA WENGINE NILISHA WATEKA KITAMBO baadaya kuona ameongea hivo nikamuuliza moja ya watu uliowaua akataja jane nilipata hasira sana nilitoa upanga na kufyeka shingo yake kama nyasi
Pumbavu umeniulia msichana ambae nilishampenda na dada ake nitamueleza ni nini niliposema hivo niliondoka na kupotelea nikiwa katika nyumba ya merry siku ya tatu taarifa ikatangaza
Aliyekuwa akionekana kama ni ninja ameweza kumteketeza jambazi sugu na gaidi ambae alikuwa anaisumbua serikali kwa kipindi chote na kwakuwa ninja tumeshamfahamu tutamfata kwa wakati wetu na kumpa pongezi yake
Siku iliyofuata nilipigiwa simu na kuitwa katika ofisi fulani nikakabidhiwa pesa na cheki ya benk ambayo ilisoma hela nyingi sana, niliwashukuru na kuondoka kisha maisha yakaanza upya ndani nyumba yangu mpya na magari kadhaa niliyonunua na moja la kupewa****
XxxxxxxxxxxxxxxxxxTHE ENDxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni