Ijumaa, 23 Septemba 2016

De 35

GANGSTAR NOMA
By: benchrys
35

nilielekea nje huku nilkiwa na mwendo wangu wa kunyata ambapo katika wale waliokuwapo nje hata mmoja wao hakuweza kuniona lakini mimi kila mmoja niliweza kuhisi alipo hapo ndipo nilidank na kutua katikati ya uwanja bila kishindo chochote kile kwakuwa nilishafahamu ni watu gani hata kaikunipa shida sana nikautoa upanga wangu na kuburuza chini kwenye uwanja wetu lengo langu ilikuwa zitoke cheche ili wote washituke warudi nyuma kisha pambano lianze.
      Oya huko nyuma mmesikia nini mimi nimeona kama mwanga fulani hivi au twendeni turudi wote,,,,ilikuwa ni sauti ya mmoja wa wale ambao walivamia nyumbani usiku ule baada ya kuhisi kuna kitu ambacho kipo ndani mule sio cha kawaida, basi wote waliachana safari yao ya kutaka waingie ndani nakurudi nyuma iliwaweze kukizuia kile ambacho mwenzao kakihisi,,,,,,,,

Baada ya mda mda mfupi zilikuwa ni sauti za watu wakilalamika kwa maumivu makali ambapo baba na mama na Naomi ambao walikuwa sebuleni walitaka kutoka nje ili wajionee ni nini kinaendelea lakini Naomi akawaambia kuwa wanaweza kudakwa na kutekwa lakini mama akawa mbishi zaidi kwanza ndio aliwasha taa kubwa ya nje ndipo akashuhudia ninja akipigana na watu kama kumi na tano mama alibaki ametoa tuu macho asimini anachokiona kisha akazijiba mdomo maana alitamani apige kelele kwa jinsi alivoona yule ninja akichakaza watu kama ameagizwa akakate mianzi kwa dakika chachelakini nikiwa napambana na hawa wapuuzi niligeuka nyuma nikaweza kuona mmoja wao akielekea sebuleni sikuzubaa nilitoa nyota(star) moja na kuirusha kuelekea kule kisha nikaendelea kuwapa adabu hawa wachache waliopo hapa. Kilisikika tu kishindo cha mtu kuanguka chini puuuu! Alikuwa ni yule ambae alikuwa akielekea kwenye nyumba baada ya kukutwa na ile nyota upande wa mgongo sijui alizima au ndio RIP tutajua,,,,, baada ya dakika chache lile kundi lote tayari wakawa wapo chini huku baadhi yao wakiwa na majeraha makali sana, kufumba na kufumbua tayari nilikuwa nishapotelea gizani hata asijue mtu nilikoelekea

*****ilipita mda kidogo geti lilikuwa likigongwa sana kwa fujo ambapo kila aliyekuwapo ndani aliogopa kufungua kisha zikasikika sauti hodiiiiiiiiiiiiiiiiii jaman kunauzima humu ndani, ilikuwa ni sauti ya jirani mmoja ambae yupo jirani na nyumba yetu ile,,,, lakini kutoka huku ndani hakuna sauti yeyote ambayo ilitoka kuwaitikia wale ambao walikuwa wakibisha hodi kule nje
Majirani walijitajidi kupiga hodi kama nusu saa na lisaa hivi lakini hawakufanikiwa baada ya hapo wakaamua kuyapanga mawe makubwa ili waweze kupitia juu wakafungue mlango ili waingie ndani, kwakuwa njee kulikuwa na baadhi ya mawe hawakupata shida sana waliyakusanya na kuyasogeza kisha walimchagua mmoja wao ambae ni mrefu ili aweze kupanda na kuingia ndani akafungue mlango jitihada zao zilifanikiwa vizuri kabisa mda mfupi akawa tayari ashaingia ndani akaweza kuiona miili ya watu wakiwa hoi sana hata wasiweze kuongea lakini kwakuwa alikuwa jasiri nae kinamna fulani akafuata ambacho kimemfanya aingie mle ndani,, aliwaangalia sekunde tuu kisha akafungua lile geti nakuwaachia na wengine waingie ili nao wajionee bila kusimuliwa na mtu mwingine baada ya kuwatazama wale watu kwa dakika chache baadhi yao wakaingia ndani iliwakajue kama kuna wenyejji au laa alifika baba mmoja na kugonga mlango wa sebuleni ndipo akakutana na sura ya beni ikitoka kumkaribisha huku nikijifanya ninawoga waajabu sana,,,,,,utajiuliza ndani nimefikaje kumbuka kuwa ninja ana njia nyingi za kuweza kupita sehem,,,,,,,,,yule baba akaanza kwa kuniuliza mbona mlikuwa hamuitiki tunapoita,,,
Tulikuwa tunaogopa wasije wakawa ni wenzao ndo mana hatukuitika. Nilimjibu hivo kisha akaingia ndani lakini alipokuwa anaingia tuu ndani waliweza kuonekana na polisi kama wanne hivi wakiingia ndani mle huku wameshika vitambulisho vyao, kisha mmoja akaanza kwa kujitambulisha naitwa afande kindu nimepata taarifa kwamba hapa kuna habari mbaya kwahiyo nilkuwa nahitaji wanafamilia watatu kwaajili ya ushaidi kwahiyo baba, mama na mtoto mmoja inatakiwa tuondoke..kabla hajamaliza kuongea baba akamwambia hivi nyie maafande sometime mnaona kama wananchi ni watu mbumbumbu sana hivi kirahisi kabisa saihizi ni giza kama mda unavoonyesha ni saa tatu na nusu nani anaeweza kushuhudia au kusimulia mapigano ya ninja hasa mda kama huu wa gizawale maafande baada ya kusikia ni ninja walistuka na kutazamana maana walikumbuka kuwa wamewahi kutumwa sehem wakachunguze kisha walipewa kichapona ninja halafu na hapa inaonekana ni ninja ndio kaja kuharibu tena;;;;;;wakiwa wanaendelea kushangaa mimi nilipita na kutaka kutoka nje afande mmoja akanidaka, dogo sasa unaenda wapi usiku huu na kama unavoona nje kuna majeruhi kibao tuu usije ukadakwa huko bure mana ninja sio watu wazuri hata kidogo ila baada ya kuongea aliniachia chansi yakujitetea ndipo nikamjibu nilitoka kulala ilikuwa saa mbili nilipotaka kutoka haja nikaona geti lilmefunguliwa niliogopa nikarudi tena kulala kwahiyo saiz nataka niende tuu haja niachieni bhaana huku nikionyesha kama kweli nimezidiwa nikampokonyoka nakutoka nje baada ya mda mfupi nilirudi tena ndani lakini nilishangaa kuona pale nje hakuna mtu hata mmoja na ndani hakuna polisi wala wazazi niliduwaa ghafla kisha nikaingia ndani nikachukua simu yangu na kuitrack namba ya Naomi kupitia google map nikaweza kugundua kuwa yupo njian kuelekea mjini sikuweza kujua ni safari ya wapi,

Nilienda hadi katika chumba ambacho kinakaa na pikipiki za baba ndipo nikachukua pikipiki aina ya boxer na kungoa kibanko cha namba kisha nikaanza safari kufuata uelekeo ule baaada ya kitambo furani nikaweza kuona gari fulani aina ya tenga huku likiwa na watu kama saba ndani yake ndipo nikaongeza mwendo wa pikipiki ile na kulipita kama upepo vile kishanikapotelea huku nikijua lazima wafuate tuu hii njia hii nilishuka na kipaki ile pikipik katikati ya barabara ili kumzuia anaepita kisha nikaondoka,,

Polisi walipofika pale walisimama na gari lao kisha waangaza huku na huko lakini hawakuwezza kumwona mtu yeyote walichokifanya ni kupakia pikipiki na kuoiweka kwenye gari kisha wakawasha kuendelea nasafari yao ndani ya dakika kama kama mbili usiku ule waliweza kuona mtu kasimama mbele huku akiwa na suti nyeus yaan vazi la kininja wakajadiliana yupo katikati ya barabara tumgonge tuu kama ni kesi sijui iwe tuu dereva nae akaongeza mwendo wa gari lakini akashangaa huyo ninja hata hana wazo la kuikwepa ile gari, akili ikamruka kabisa hivi huyu ni mtu au jini alipokaribia kwa huyo ninja akakwepesha kidogo lile gari ili apite pembeni lakini yule ninja nae akageukia ule upande polisi yule aliyekuwa akiendesha akaona hana namna akafunga brek ya haraka miguuni mwa yule ninja yule ninja akasogea na kuwaambia wote tokeni nje hakuna liyeweza kubisha hata kidogo wote walitoka kisha akamwita dereva na kumwambia geuza gari dereva nae hakuleta ubishi akapanda na kuligeuza kisha akaambiwa ashuke

ok sasa nazani kutuoni ni jirani safari njema nyinyi pandeni huku vidole vikiwaelekea wazazi pamoja na Naomi na nyie nyie safari njema nitawasogezea tuu gari lenu ndio msaada wangu kwaheri niliingia kwenye gari na kuondoka na baba na mama safari nzima hadi nafika nyumbani ilikuwa ni kimya hakuna anaweza kuongea chochote maana hawajui huyo ninja ni nani ambae karibia kila mda anatokea kama msaada kwao nilipofika nje ya geti niliwaambia kuwa mie nashuka kisha nikafungua mlango wangu na kupotelea,,, niliruka ukuta wa nyumba na kupitia dirishani kisha nikazama ndani nikabadili nguo na kujifanya kama ndio natoka kuangalia gari ni la nani huku baba, mama na Naomi wakishuka nao kila mtu alishuka kivyake kisha wakafunga geti wote tukaingia kulala ilipofika usiku mda wa saa..itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Maoni 1 :