Gangstar noma
By: benchrys
3
Kufungua mlango hakuona kitu chochote hukubkulikuwa na kelele na fujo nyingi za kugonga mlango kama kuna ugomvi au mgambo kaibiwa na ameshaona adui yake nyumba ndio hii hapa,, ivi huu ni uchawi au mambo gani ya kujienjoy namna hii au macho na masikio yangu ni mabovu alisema hivo baba kisha akatugeukia sisi akasema hivi jamani simmesikia makelele sasa hivi hapa za makelele ya mtu kugonga hapa lakini nafungua hakuna mtu...Mi nikasema baba pengine umetazama vibaya mana hata mimi nilikuwa na wasiwasi mana zile fujo za kugonga nakajua hapa ndani hapata kalika ila siyo shida sana tufunge mlango tuendelee....Mama akasema hivi hukuwa umeanza kuelezea hata kidogo, baba akafunga mlango akaludi kukaa na mimi nikaendelea kuhadithia baada ya hapo baba akageuka kwa yule dada akamwambia pole sana bint,,, yule dada akajibu asante nashukuru pia namshukuru na mwanao ila huko nyumbani najua watakuwa wanawasiwasi kuhusu mimi niko wapi hadi mda huu, yule dada aliposema vile baba akadakia akasema sio mbaya sana ni bora upo hapa salama kuliko ungekuwa huko ambako wangekuharibu tuu...Akawa amejaribu kumtoa katika mawazo yale bint alipoonyesha katuliza akili ya ndipo na mimi nikajikakamua kuuliza hivi jina lako nani? kiukweli niliona nimejitahidi mana mimi katika mda au kipindi hicho nilikuwa mzito sana kunyanyua mdomo na kumwuliza swali licha ya kuwa nilikuwa ni mtu wa makundi ambayo mara nyingi ni ya kubishana. Naitwa Naomi chesko ok mana ndio tumetoka mbali ila sikufanikiwa kukuuliza niliongea maneno hayo baada ya yeye kutaja jina lake.. Ila kilicho nishangaza ni pale nilipoona ametaja jina langu'' ivi we ben mbona nasikia unachelewa sana kurudi nyumbani.......
Jaman huu mda wa kulala ben siunajua kesho inabidi uwahi shuleni au imesahau alisema baba. Kwa upande wangu nliona kama kanirahisishia kujibu lile swali lililo ulizwa na naomi kweli baba ila unakumbuka ulinipigia simu iliniwahi hapa nyumbani lakini katika harakati za kurudi ndio nimekutana na hili zogo hujaniambia kulikuwa na nini' nilijitia mfuatiliaji kidogo ni kweli tangu narudi baba hajanambia kwanini waliniita mda ule tena akiwa kama anajazba fulani
Aha Basi kulikuwa na kakazi fulani kadogo ila mbona kwa kuchelewa kwako tumeshafanya,,,, naomi kwa kisikia vile akasema nambeni mnisamehe Kwa kumchelewesha kuja kufanya hiyo kazi mana mimi ndio nimekuwa kikwazo kwa hilo tatizo. Mimi mawazo kichwani yakaanza kupembua kama mwanasaikolojia hivi 'wenyewe wanasema mi sifahamu sana' inamaana huyu dada anaigiza au ndio mkarimu na mnyenyekevu hivi dah unaweza ukaaibika hapa bora nikalale tuu tuinane kesho, hayo ni maneno nilikuwa nikijisemea mimi mwenyewe katika kichwa changu nyie mnasema kimoyomoyo lugha hizi bhana,, basi nikawaambia jamani mi naenda kupumzika hapa nimechoka sana bora nikapumzike tuu. Baba akadakia ila leo kama mazoezi umefanya na ushukuru tulishaandaa maji ya kuoga. Baba kusema vile naomi akacheka alishindwa kujizuia. Haa na mimi nikaona hatakama nimeaga lazima nijue huyu kacheka nini
Naomi: niliita hivo akaitikia abee ben siumesema unaenda kulala wewe. Ndio naenda kulala ila...... Kabla sijamaliza kuongea mama nae akasema wee ole wako na kesho tujisumbue kukuamsha huku saizi hapa unazugazuga kwenda kulala. Hapa naomi alitamani acheke ila akajishinda kwa kuzuia mdomo wake na kitambaa alichokuwa nacho basi na mimi ndio nikagundua huyu ananicheka mimi tuu, licha ya kuwa mama alivosema kamoyo kangu hakakupenda nikaona sasa naona uzalendo unanishinda, sasa nnamachaguo mawili nikalale huku sijui anachekea kitu gani au nikomae hadi niulize.. Kichwa hapo kilipata kazi ya kuchafua lipi litakua jema ili nilale kwa amani na usingizi wanfu uwe safii. Baada kufikilia ndio nikajikakamua tena na kuuliza we naomi naona unacheka nini au umekumbuka tulivokuwa tunakimbia ukanifananisha na vile vitom na jerry acha mambo yako bhana
Nikweli baba alivosema leo umefanya mazoezi ndio nikakumbuka hadi ulivompiga yule jamaa na jiwe! hapo hadi mimi mwenyewe nikajikuta eti naanza kucheka huku nilisema kwamba naenda kulala
Acha hizo usiku mwema kwaheli jaman nikawa nasukuma mlango wangu ili niingie kulala naomi akasema kumbuka kuomba ben na sisi sote utuombee, nikajibu kuhusu hilo hata msijali hapo ndipo nikaingia chumbani kwa nikaanza kujiuliza ivi nani kaniruhusu kuanza utani na wadada kama hivi.. Mda si mwingi sana nikawa nishapitiwa na usingizi kama unavojua mambo kama haya ni emegenc tuu mara haukwambii fumba macho ulale ila mwenyewe utajikuta ushalala
***Naomi hiki ndicho chumba ambacho utalala utatusamehe hatupo vizuri maisha yetu hiyo ilikuwa ni sauti ya mama alikuwa akimwonesha naomi chumba cha kulala nashukuru sana niwatakie usiku mwema wenye amani naomi alisema kama ishara ya kumuaga mama.....
***Ivi we dogo kwanini unapenda uonekane kama wewe ndio bonge gentlemen hapa unajua tunauwezo wa kukugeuza hata kitoweo ok yule dem umesepa nae umempeleka wapi nahitaji nausiposema hapa hapa naanza na kukung'oa meno kama unabisha sema unabisha au kaa kimya tuu nakupa dakika tano kuwe kumesha sambazwa majibu ya maswali hayo kwenye masikio yangu nakungoja wewe mwenyewe dakika moja tayari ishaisha kama upo braza ee uliangalia vibaya mi sijaondoka na demu wako mbona tunaoneana hivo kama angu. Sijakaa vizuri nilipokea zinga la kofi hadi nikajikuta nimepiga magoti kama dakika tatu ivi,, hapo ndipo akili yangu ikawa imerudi jamaa yule akasema nadhani muda umekwisha tayari ok nambie umempeleka wapi huyo demu. Sikutoa jibu lolote lile akasema wewe unaona mimi ni kanumba au ray nipo kwenye muvi naigiza sasa ngoja akatoa kamba mfukoni akanifunga kwenye nondo ya dirisha kisha akasema ningoje nakuja mpuuzi wewe. Aliporudi alirudi na koleo na nyundo moyo ukaanza kunienda mbio kisha akatoa kisu mfukoni akakiburuza ukutani kikawa kinatoa kama moto hivi, Ok chansi ya mwisho sema mimi kimya tuu nilibaki. Nikiwa bado sijafunguliwa nilipigwa ngumi ya tumbo kidogo niteme utumbo nje nilipiga kelele mamaaaaa nakufaaa......
***Kumbe nilikuwa naota nilishituka asubuhi kuna jua kwa umbali nikajua wazi nimechelewa shuleni, nikajivuta kiuvivu ili nitoke nje duh nilipofungua mlango tuu.........Itaendelea
benchrys1996@gmail.com
&
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni