Jumatano, 20 Julai 2016

de 2

Gangstar noma
by: benchrys
2
Haraka  tugeuke bana mbona huku ndio mateso tupu cheki sasa dah mbona tunafukuzwa hku nyuma angalia, aliongea yule dada huku akiwa kama anahuzunika kutokana na kuhisi kama atadhulika zaidi mana mbele kuna jamaa ambae ni anatisha mana amejazia mimi nikijicheki dah yani sina hata ubavu wenyewe wanasema kimbaombao basi akili yangu ikajipiga haraka namna ya kujitetea kuangalia chini kama kawaida nikakutana na jiwe moja ambalo nililiona kwangu litanifaa kwa kujitetea basi nikainama fasta na kuliokota lile jiwe yule jamaa alipoona nimeshaokota jiwe akagutuka na kugeuza safari yake ya kutukimbiza basi safari ikaanza upya mbio hadi nilipofika nyumbani nikiwa na yule dada wote tukiwa tunahema kama mbwa anatamani nyama..
    nyie vipi tena mbona tunashituana tu hapa kuna nini huko mlikotoka mana hata siwaelewi hata kidogo mnahemeana tu kama manini sijui, hayo yalikuwa ni maneno ya mama yeye ndio alituona tukiwa tunaingia pale kwa fujo kama tunakimbizwa na mbwa mwenye kichaa. Basi nikasema mama huko tulikotoka ni shida tupu huyu unaemwona hapa simjui nadhani hata yeye hanijui ila twende hata sebuleni tukae kisha niwaelezee vizuri, mama akasema huo muda mnaokuwa mnatoa hiyo habari yenu nadhani utakuwa mda wangu wa kupika mana nadhani mnajua saizi ni saa ngapi mda huo ilikuwa ni kama saa kumi na mbili na nusu simu yangu ilikuwa ikionyesha hivo, ndio hivo na kukimbia kote ila simu yangu nilikuwa makini nayo kama unavojua nipo tayari nisahau vingine ila sio simu na ndo mana hata wanaosahau kuweka alarm wakilala sio kwamba hawajui umuhimu wa kuwahi kuamka ila kujali tuu kitu hicho..Basi mama akaanza kazi ya kupika chakula muda ukafika tukaanza ila yule dada akawa kama anaogopa hivi nadhani hiyo yote ilikuwa kwasababu ni mgeni pale..Usiogope jisikie upo kwenu dada yangu,,,

****yule jamaa ambae alikuwa anataka kumfanyia unyama yule bint muda ukawa umefika kuzinduka akawa anajinyoosha ....Aaaaaamu aaha shit kudadeki nipo wapi hapa kuna mzee alikuwa anapita maeneo hayo akacheka sana
Dah bangi sijui za wapi hizi mtuu unashituka sahizi kuwa ulilala tena eneo kama hili dah
Kijana habari yako, huyo mzee alimsalimia kwa kibaunsa hicho hakujibiwa''' kijana habari za saizi nakusalimia, yule jamaa akamwangalia halafu akaguna wazee wengine bhana utalazimishaje salamu kwangu kama lazima siinatakiwa nikusalimie mwenyewe aha... Ok salamu sio lazima sana ulikuwa unatakaje mana naona salamu nyingi sana ndio nakusikiliza sema,,jamaa alisema hivo kwa hasira sana hadi yule mzee akaina hapa yaweza kuwa majanga mengine bure...Ok sikuwa na shida yoyote ila nilikuwa nakusalimia tuu hakuna lolote lile kwaheli mwanangu mzee aliondoka pale kwa wasiwasi mkubwa maana asije akapata majanga bure maana ilikuwa mda wa jion hakuna atakae msaidia

****tukiwa nyumbani tulikuwa tushamaliza tayari ukawa ndio mda wa baba na mama kuanza kusikiliza jambo ambalo ndio lilitupata ila mimi nikawa bado najiuliza yule dada kwao inaezekana watakuwa wana mtafuta ila nikajisemea sio shida sana angekuwa mtoto labda ndio ingekuwa ni tatizo kubwa, hapo nikaanza kuelezea jambo lililo tupata mara mlango wa pale ukagongwa tena kwa fujo..Fungua mlangoooooooo nasema funguaaa mlango nasema wote mle ndani tulikuwa kimya kama tumelowa maji hivi, baba akasimama na kufungua mlango lakini baada ya kufungua mlango......Itaendelea

benchrys1996@gmail.com
&
benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni