Jumamosi, 23 Julai 2016

de 4

Gangstar noma
By: benchrys
4
...Usishtuke sana bro vipi wewe kumbe mwoga hivo
mbona jana nilikuona bonge la shujaa moja ambae naweza kumfananisha hata na johnsina mana ulifanya kazi ngumu tena inayohitaji akili mana ungecheza vibaya tu basi na wewe ungeunganishwa kwenye kibano, aliongea maneno hayo Naomi baada ya mimi kutoa mshituko mkali nilipoona mlangoni kwangu kuna mazaga mengi ya usafi mana nikijicheki bado nina akili zangu za usiku kiukweli nilishituka hadi nikafunga mlango wangu tena na kutaka kuludi kulala dahh kweli akili za usiku hazifai ila ambacho niliona so ni pale aliponipa dongo kuwa mimi ni mwoga hivo sikulipenda lile neno basi ndio hivo nikatulia tu....Muda huo wazazi walikuwa bado hawaamka ama kweli jana tulichelewa kulala nilijisemea kwenye nafsi yangu....
   Ben vipi mbona huu muda bado upo hapa nyumbani inakuwaje au shule ndio imefunga tena kwako tuu mana leo nashangaa kukuona hapa nyumbani,,, mbona hunijibu ivi sinime taja kwamaana naongea na wewe hizo ni zarau au. Haya yalikuwa ni maneno ya mama baada ya kuamka na kunikuta bado  mimi nipo pale nyumbani ilikuwa ni saa tatu kasoro na muda kuingia darasani na kuanza vipindi ni saa 8:00 kwa hiyo nilikuwa tayari nishachelewa tayari mama akasema shule lazima uende na wala huwezi shinda hapa kajiandae haraka'
   Dah leo mwanetu umechelewa kiNoma au ndo ushaanza na majukumu huko home kwenu saa tatu ndio unafika skuli kama ushadata we sema...Joel aliongea maneno ambapo nae kwakuwa nilizinguana nae jana halafu tena leo ananipa maneno ya kashfa namna hii sikumjibu kitu chochote ila baada ya muda kidogo nilikaa na kuwaza kuwa haya maisha tuu "no one is perfect" nikajikuta tuu nikitamka hilo neno la kimombo pekeyangu ndipo nikajizindua kama nilikuwa katika maeneo mengine kabisa na pale darasani mana toka nyumbani ni kama nimeharakishwa mkiki mkiki hapo ndipo nikajinyanyua na kumjibu joel,,,,,dah mwanangu we acha tuu usione nimechewa hivi leo kuja skuli mi jana ilikuwa ni majanga tuu. Joel akadakia kuna nini tena kilikupata joh langu mana ulipofika hata hukunicall au hukuwa na bando mzeiya. Awee niachie kashfa hizo bhana kisa nini mpaka nisiwe na bando et sema jana nimeupa faida mtandao tuu....yaani nilipofika darasani zikawa ni stori tuu nikasahau kuwa mwenzangu alikuwa darasani toka muda mrefu na mimi ndio kwanza hata kipindi kimoja sijahudhuria mi nikaendelea na stori,, unajua nini mwanangu ile jana pale nilipoachana wewe siuliona nimeondoka kama chizi hivi pale mshua alipiga simu ya kuniita home lakini napita kona hivi nikasikia sauti ya dada akipiga kelele za kuomba msaada sikuwa na noma kwenda kupiga chabo nikaona boya moja sijui lilikuwa linataka kupiga mtungo au mi nikaokota mawe na kulipiga nayo lilipotua chini tuu nikamnyakua yule dada na kuanza kusepa kabla haijawa noma;; nilikuwa nikimwelezea hivyo jamaa yangu joel. Joel , dah kweli ulikutana na zali ila bora kama ulimwokoa na bora kama ulienda nae homu kwa usalama wenu..Ndio tulifika hadi homu licha ya kuwa barabarani ilikuwa jau bado mana kulikuwa na boya lingine linatukimbiza ila nalo nililidhibiti kwa jiwe moja tuu likatokomea ila kufika homu ilikuwa fresh
    Ben samahani nina swali nataka nikuulize samahani lakini kama hutojali...nilipoona jina langu limetajwa kuwa kuna swali isitoshe ni sauti ya kike roho yangu ikanipa majibu bila hata kusikia swali lenyewe, moyoni nikajisemea kudadeki wenye mapepo ya unafiki nao washaanza sasa ngoja nimsikilize halafu aniharibie siku yangu hapo ndipo atanijua vizuri hata kama sipendagi bifu na watu...Ok wewe unataka kuuliza swali gani na wakati unajua mimi hata kipindi kimoja hapa sijakipata bado nyie mshasoma ndo mana mnatuletea sisi wengine mambi ajabu ajabu hapa nakupa dakika mbili tuu uliza hilo swali ila isiwe ni swali la masomo mana nitaamsha mapepo yangu...Niliongea maneno hayo  baada ya kuona sura ya m baya wangu ndiye mwenye shida ya kuuliza lile swali alikuwa ni msichana kwa jina la Jane ambae nilikuwa sihitaji kuongea nae hata kwa bahati mbaya hata pale nikubali kuongea nae kwa sababu Joel jamaa yangu aliniambia nimpunguzie jazba na nimsikilize tuu kilichofanya huyu dada nimchukie ni siku moja nikiwa darasani kichwa changu hiyo siku sijui kilitembelewa na wadudu gani maana kilikuwa kinaniuma tena sana katika orodha ya watu wasumbufu ikaonekana na mimi ni mmoja wao licha ya kuwa nilkuwa mgonjwa lakini nilipokea adhabu ambayo walisema wanafidia kwa wanaosumbua siku zote adhabu ilikuwa ni kubwa tena ni viboko pamoja na kazi za nje nilifanya hadi natamani kulia mana hata huyo mwalimu nilipojaribu kumwambia kuwa mimi naumwa hakuweza kunielewa hata kidogo ilkuwa ni kama siku ya kunikomesha shule nilijihisi kama bora niwambie wanifukuzishe shule mana huu  ni utumwa sitaweza kuuvumilia hata dini yetu inasema samehe 7x70 niliona kama hawajui lolote ila basi kamakawaida mimi ni mtu wa kujifariji daily nilifanya ile adhabu hadk namaliza lakini kwa kinyongo sana......
***Nimesikia hapo na rafiki yako mnasema kwamba kuna mtu ulimwoKoa jana nilitaka kujua anaitwa nani kama uliuliza hata jina lake mana mimi nyumbani nina dada yangu jana hajarudi na tumejitahidi kumtafuta ila hatujafanikiwa kumpata hata yaliyo mkuta hatujui mana alikuwa akienda kutafuta mahitaji kwaajili ya usiku, naomba unitajie jina tuu licha ya kuwa najua kuwa inanichukia toka kipindi lakini na mimi sikuwa mimi nadhani ni utoto nao unachangia samahani ben.aliongea maneno hayo jane tena msikitiko mkubwa nilipata roho ya kumsamehe lakini roho na mdomo vilikuwa ni vitu viwili tofauti kabisa maana moyo ulitoa majibu mazuri ila katika kuyafikisha kwa mhusika ikawa ni vingine kabisa,,,kwahiyo ukiwa na shida kubwa ndio unakumbuka kuwa kuna mtu ulishawahi kumkosea huo utoto unaosema ulichangia mchango wake ulifikia sh. ngapi mana mi hata sikuusikia huo mchango, nilimjibu hivyo jane kwasababu nikikumbuka adhabu ile ya siku ile laiti angekuwa yeye angeweza zimia lakini mwanaume nilikomaa. Hivi unafahamu kwamba ile siku nilkuwa naumwa sana nilimuuliza hivo ila jane hakujibu zaidi ya sorry ben forgive me, sikuwa na mengi nikaamua nimsamehe tuu ila sikumwambia kuwa nishakusamehe yeye akawa analia tuu analiwa huku kajiziba uso wake na kitambaa na zile sauti za fyuu zikisikika nadhani alikuwa akilia. Hapo mimi si najua kama ni dada yake yupo home hakuna kinachoharibika, nikauliza wee jane ilibakiza supu ndo unamalizia au mana nasikia tuh fyuu nahisi pale nilimkatisha hata hamu ya kuendelea kusimama pale jirani na mimi kwa kuuliza lile swali ambalo kiukweli lilikuwa na la kitahila na ni lama udhi tena yaliyo kithiri..
    jamani humu dasani kuna ugomvi au inakuaje nahitaji kujua nambieni kinacho endelea humu mana naona jane pale analia inakuwaje?! wanadarasa wote walibaki kimya wasijibu lolote lakini kidogo nikasikia sauti ikisema jane kabla wewe hujaingia alikuwa kasimama na benchrys labda ungemuuliza huyo ben anaweza kuwa na majibu..Hapohapo nikamwangalia jane nae alikuwa akiniangalia na kutoa ishara ya kuwa nisiseme lolote tuliyokuwa tukiongea nikaona huu sasa utakuwa msala mwingine mana mi gari linalo tembeza nyota yangu nahisi bovu ndio mana kila siku kwangu ni majanga tuu.....Inaonesha nyie mshaanza upuuzi tangulieni ofisini kwangu pale wewe ben na mwenzio jane kisha......Itaendelea

benchrys1996@gmail.com
&
benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni