WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 13
Ilisikila sauti paaa!!! Kisha vika fuatiwa na vilio vya watu
Songa>>>>
Kila mtu pale tulipokuwa tumesimama alitawanyika na isieleweke kaenda wapi, na mimi isionekane zube sana nikaondoka na kuelekea kule ambako imesikika ile sauti nilijivuta hadi kufika kule ambapo niliweza kuona vijana watatu ambao wamejaza vifua kama breast za wanawake (sitaki swali) wakiwa wamesimama wakitoa kichapo ambapo mmoja kati ya wale alikuwa amehika bomba moja ambalo kwa mda huo lilikuwa likitoa moshi, nilijaribu kulitafsiri lile bomba lakini sikupata jibu lolote lile zaidi ya kujua labda atatumia kumpiga mtu ila bado nikabaki na swali kwanini litoe moshi halafu amelishika kwa raha kabisa, hili jambo sikulielewa kabisa nikajikuta nikisogea hadi mbele ili niwezekujionea mwenyewe vizuri kabisa.
NANI MWINGINE ANAE TAKA ALETE UBISHI JUU YETU SISI, KILA SIKU TUNAWAAMBIA HUU MTAA LAZIMA UWE NA HESHIMA JUU YETU SISI THREE SOJAZ SAWA HILI KUNDI LICHUKULIENI KAMA NDIO RAHISI WENU. SASA NAMMALIZIA NA HUYU BOYA ALIYEBAKI.
Baada ya kuongea vile alimdaka dada mmoja ambae muda wote nilimwona amekaa kiwoga woga sana,. Baada ya kumdaka yule dada alikuwa analeta ubishi aliokea kofi moja ambalo kwakutazama tuu lilikuwa ni zito sana hata mwingine ungepigwa lazima uombe maji ya kunywa. Hichi kitendo kilinikwaza sana na nilishindwa kabisa kujizuia nika paza na mimi sauti
;;;;;oya bro huyo dada kakosa nini hadi umpe adhabu kama hiyo hivi huoni kama huo ni unyama unaomtendea huyo,. Baada ya mimi kuongea vile akanijibu
;;kwa hiyo ulikuwa unaamuaje sasa au unataka uje kuwajibika wewe, no mind kama unataka nipo tayari kumwachia huyu Malaya aende halafu ubadiri siunajiweza
;;;;;kudadeki kwahiyo akili yako wewe ni kunyanyasa wanawake tuu si ndio ok sio shida sasa basi., kama wewe unajiita mwanaume unae taka uheshimike kila mtaa mi nipo tayari kukushushia hiyo heshima fara wewe.
;;hahahaha we mbuzi ivi unanibipu nadhani umeona uwe ray kwa kutafuta kiki ya kubishana na mimi? Si nakuuliza we toto la kahaba
;;;;;;toto la kahaba ndio lenye akili ya kishost kama wewe huku ni boy acha nyodo njoo tuonyeshane sio maneno mengi maan hayajengi vipi
Baada ya mimi kuongea vile alimwachia yule dada kwa kumrusha huko kisha akawa ananifuata akiwa kafura, watu wote katika hili eneo walianza kusogea pembeni ili washuhudia ni nini kitaendelea hapa wale ambao wao kazi yao ni upambe kama kawaida walianza
Bro akujui huyo dadeq zake anaona sisi tunaeheshimu kama ni malofa hivi hebu mwoneshe tuu boya huyo
Nae kwakuona kapewa sifa akawa bichwa hiloooo alitoka spidi na kuja kujirusha ili atulie na teke kwenye kifua changu. Lakini kabla hajafika nilruka kavu kisha tukakutana juu kwa juu na kwakuwa hakuwa na stamina ya kutosha akatulia mgongo chini.
Hapo hata kelele zilianza kupungua kutoka kwa wale wapambe. Lakini bado alionyesha ubishi alinyanyuka na kutaka asogee na ngumi aliporusha mkono niliudaka na kuuzungusha hapo ilisikika tuu sauti ya kaaaa kwenye mwili kisha kikafuata kilio kama mtoto, huku mwanzo alikuwa akiongea bezz zito tena la kujiamin kana kwamba yeye ndie general ya majeshi.
Baada ya pale nikataka kuondoka nikijua tayari nishamkomboa yule ambae hta kitendo ambacho alitaka kufanyiwa sidhani kama ni kizuri
Niliangalia mahali pa kutokea nikawa nimeweza kuona upenye fulan niliufuata lakini kabla sijatoka nilirudishwa pale katikati nateke zito kisha ikasikika sauti HAHAHAHAHAH WE UNATAKA KUUTAWALA MTAA AMBAO UNAWENYEWE KAMA UMEPIGA HUYU MMOJA BASI SISI TUTAANGAMIZA PAMOJA NA FAMILIA YAKO YOTE
Nikiwa bado nipo pale chini nikaona watu wakija pale na mapanga hapahapo gafla nikanyanyuka na kusimama kama mtu ambae ametoka katika usingizi na ameota ndoto ya kutisha sana
Wale wote wenye mapanga wakaanza kunifuata. Wakati huo nikiwa nawaza sina hata silaha, lakini nikakumbuka kuwa kuna njia ya kuwafanyia mauzauza kisha kila kitu kinakuwa fresh. Wakati ule wapo jirani ilikuwa kama CD ya kichawi inatazamwa.,., nilidank juu sana waliokuwa chini waliona kama cheche tuu zinawaangukia, mara mtu nikatua tena chini nikiwa sio mimi tena. Safari hii nilikuw na nguo za kininja zenye rangi ya nyeusi na nyekundu hapo ndio watu wote walibaki tuu wameshika midomo yao kuonyesha hawaamin walichokiona wenye smart phone nao ulikuwa ndio mda wao wa kuanza kushoot video maana wamezoea ninja assasin kwenye tv tuu lakini leo wanaona live kwa macho yao
Baada ya kutua chini pale nilichomoa upanga wangu nikiwa sina lengo la kumwacha hata mmoja kati ya wale wenye mapanga zoezi lililofuata hapo ni kichapo tuu kila aliejitahidi kunivizia na panga lake hakuna alicho ambulia zaidi yakufyekwa au kuvunjwa kiungo mojawapo
Waliokuwa wanaangalia kuna jamaa mmoja ambae ndie aliye nipiga lile teke la kunirudisha pale katikati huyu ndio sikutaka hata time nae aliposogea tuu nilidank na kutua kichwani kwake huku nikimshindilia kiwiko cha mkono ambacho kina ujazo wa aina yake kisha nikaruka na kumbetua kabla haja tua chini nilimwongeza teke ambalo lilimpeleka juu sana anapotua chini nikamtegea kisu nae akatua juu yake (kama mwoga fumba macho)
Waliokuwa pembeni wale washabiki baadhi yao walianza kuondoka taratibu huku wakirudi makwao na baadhi wakificha sura zao
Nilipomaliza zoezi lile kulikuwa na ukuta jirani hapohapo. Upanga wangu ukiwa mkononi niliutumia kuandika YOU HAV E TO KNOW (WHO AM I) kisha nikapotelea katika maeneo ambayo hata ungekuwa makini kiasi gan ungeondoka chenga huelewi chochote.
Dakika chache mbele nikaja kuonekana tena katika kijiwe fulani cha kushona viatu
Daaah ivi kumbe hata Tz kuna maninja
Daah mwanangu ivi yale yalikuwa mauzauza au ni kitu gan maan ilikuwa kama muvi.
Halaf nakumbuk kama umerekodi hiv lile tukio
Aaaah kweli halaf ckucheki ngoja nicheki saa hizi hapa
Alitoa simu katika mfuko wake wa suruali ilikuwa ni tecno h6 nadhani aliyotumia kushoot video ile
Basi watu wapale walijisogeza kuiangalia huku na mimi nikiwa ni mojawapo kati ya waliokuja kuitazama. Aliiwasha hii video ikaonyesha tuu pale ambapo walikuwa wanaongea kisha nikaruka juu sana kwa kudanki kuendelea ilikuwa ina scratch tuu
>>>>aaaaaah mwanangu hapo umeharibu uhondo wote duhh
Sasa kama memory yako inavirus siungeacha tuu kutuonesha shit smart phon nzima memory inavirus unazingua bhana
.,.,watu walichukia sana kile kitendo cha simu kustak kuonyesha ile video huku wao walikuwa na hamu nayo ile mbaya
Lakini mimi huo mda wote nikawa najiuliza inamaana hawanijui au sura sio yangu huku na kule ni tofauti. Maana hapa ningepata maswali kibao kuhusu uwezo huu lakini sikujua kuna nini hadi wanisahau wakati tulikuwa wote muda si mrefu kabla ya tukio. Nikiwa bado simu yangu ilianza kuita kuitazama ni nani-----itaendeleaaaaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni