WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 12
Baada ya hapo walitoa silaha na kuanza kuifuata ile gari____
Songa nayo
------wale wanajeshi waliasogelea hadi jirani ya lile gari kubwa ambalo lilikuwa na walinzi ndani. Lakini walishangaa kuona kimya kimetanda sana katika gari hili ila kwakuwa ni wanajeshi wakajipa moyo na kuingia katika gari lile ndani wakiwa na imani lazima watamuona mtu ambae anawaletea mauzauza hapa
Oya kinju mbona hakuna kitu humu ndani, ngoja niwashe hata tochi ili nione./ baada ya hapo aliwasha tochi yake ambayo ilikuwa na mwanhamkali sana lakin hakuweza kumwona mtu mle ndani zaidi aliona tayari mlango wa upande mwingine nao upo wazi.
Kwa kuona hivo akajua walinzi wanawaogopa, alipaza sauti
JITOKEZENI TUMEKUJA NA BOSS WENU KUWENI NA AMAN HATUPO KUWADHURU NYIE. HEBU NJOONI TU. Alipoongea vile ndipo akaanza kujitokeza mlinzi mmoja hadi mwingine hadi wakafika idadi kamili inayotakiwa ambapo bamboo kwa mda huo hatazamiki hata kidogo usoni kaumia hadi huruma kama ungemuona huwezi kumwangalia mara mbili
Walijaza mafuta katika lile gari na kutaka kuanza safari ya kurudi nyumbani lakini kila walipojaribu kupiga starter hakuna kulichojibu.
Mwanajeshi mmoja alishuka chini na kuangalia huku akiwa na tochi yake lakini hakuona tatizo lolote. Wakabadilisha mawazo labda wote wapande gari la boss wao ambalo amekujanalo,. Walikubaliana na hilo wazo kisha wote wakaondoka na kulifuata lile gari kisha wakapanda na mwanajeshi mmoja akakaa siti dereva kuonesha kwamba yeye ndie wa kuendesha aliweka funguo na kunyonga hakuna hata mwanga uliotoka ilionyesha dhahiri kwamba hili gari halina betri kwa mda huu. Ila kwa kujiaminisha alishuka na kuangalia, na kweli beri kwenye gari tayari ilikuwa imesha chomolewa
Mwanajeshi huyu alifura kiasi kwamba akasema huyo anaemchezea akili laiti akionekana hana kichwa
)()( kudadeki nitapeleka mtu kuzimu mimi, tafadhali wewe kilaza hebu jitokeze mwenyewe kabla sijaanza kukusaka)()( aliongea mwanajeshi yule kama mwenda wazimu lakini hakuna aliyemjibu hata kwa hewa tuu
Masaa yalisonga mbele bila kukawia, toka saa tatu mda walio kuja huku hadi sasa tunaangalia saa ni saa saba na robo na hakuna magari yanayoweza yakapita haya maeneo mda kama huu, mwanajehi baada ya kuchanganya akili akaona huu upuzi hakuna wa kulala hapa porin.
Alinyanyua simu yake na kuandika namba fulani kisha akazipiga
-_-_-__-yaa ndio mkuu, tupo eneo la mawenzi sijui huu mtaa wanaita, yaa ndio njoo, au tuma watu, ndio, ok sawa simu ikakatwa
Baada ya dakika chache kuna magar yapatayo manne yalitinga katika hili eneo, kisha wanajeshi wakashuka wasio na idadi na kuanza kuingia katika pori hili huku wakikata baadhi ya miti ambapo wakati huo wote nilikuwa nikiwaangalia tuu, na baada ya muda mfupi tuu walimaliza maeneo yote yakawa wazi. Nikaona isiwe shida kama nilipambana na yule kiumbe nikamshinda nitashindwaje na hutu tuumtu twa kawaida.
Baadaya hapo nilichumpa toka pale niliposimama na kutokezea katika kaeneo ambako kalikuwa wazi ambapo ni barabarani.
Wanajeshi wote walishituka na kugeuka. Ile wanaangalia nyuma yao waliona ninja akiwa na maski fulani ya rangi kama silver ilingaa kutokana na kuwa walikuwa na tochi za mwanga mkali usiku ule.
Kwa kuwa walikuwa wengi sana walijivuta kwa mshikamano hadi pale ambapo mimi nipo huku wakiwa na iman ni lazima wanikalishe tuu.
(hebu kaa hapo hapo upo chini ya ulinzi) ilisikika sauti ya mwanajeshi mmoja ikiniamrisha ninyooshe mikono juu eti nimesalenda kwao.., kimoyomoyo nikasema sio masharti ya ninja hayo kunyoosha mikono juu. Kisha nikawageukia kuwatazama.
Silaha zao zoote zilikuwa zikiniangalia mimi kuashiria kwamba siwezikufanya kitu chochote kile ili kujinusuru, lakini nikaiona njia moja ya tuu ambayo ilikuwa ni kuwapiga changa.
Baadaya kugeuka nilichuchumaa chini
Wanajeshi wakiwa wananitazama pale nilipochuchumaa ulitokea mwanga mkali na mlio kama wa bomu,. Kufumba na kufumbua mwanaume nlishapotea mda mrefu sana. Ule usiku walitafuta lile eneo lote lakini hawakuona mtu yeyote yule. Baada ya hapo waliamua kuondoka wote katika lile eneo na kurudi makwao.
Safari ilikita moja kwa moja hadi nyumban kwa boss na kuwaacha pale pamoja na walinzi wake. Walimchukua boss kwa kusaidiana kisha wakamweka sebuleni. Huku wakimwamsha kwa fujo na kwa bahati nzuri walifanikiwa kumwamsha hadi aliamka, kisha walimfanyia utaratibu wote na baada ya dakika chache wote waliingia kulala hadi asubuhi
_____________________________
Ilipofika asubuhi boss aliamka na kuwasha tv apate angalau taarifa ya habari
Habari ya kwanza kusikika
)))))asubuhi hii katika mtaa wa mawnzi kuna magari mawili yameonekana yakiwa yamewakamoto, tukio hili inaonekana limefanywa usiku wa kuamkia leo na mhusika bado hajajulikana mpaka sasa, jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo(((((
Boss baadaya kusikia habari ile palepale alizimia. Mhudumu mmoja ambae alikuwa anapita kwa aajili ya maandaliz ya chai ndio aliyekuwa wa kwanza kuona lile tukio, aliwaita walinzi ili ikiwezekana wamfikishe hospital akapewe huduma.
Walinzi walipofika pale waliita gari na kumpeleka kituo cha afya na sio katika hospital kubwa kitedo ambacho kilimshangaza yule mhudumu, alipata shauku ya kuataka kuuliza lakini aliushinda mdomo wake-----
Asubuhi tunaamka katika nyumba ambayo na bon amepanga,.
Kuna wadada wawili walikuwa wamekaa wakiotea jua wakiwa wamekaa kizembe kabisa.
======ivi shoga mbona huyu kaka haamki hadi sasa hivi
==nyooo ko wewe umejikalisha kimitego hivo ili umpate,.
===sasa hayo yametoka wapi sasa ndio jibu la swali langu au
=yametoka wapi mdomoni au we unatolea mata***ni, hebu nitokee hapa fyuuu
== powa natoka ila hadi nimwone
=Dadeki na hatoki huyo hujui anamwogopa bashir tena na wewe enheeee sijui>>
Katika hii nyumba hawa wadada wawili sijui ni wanalaana au vipi maana wao ni maneno tuu mda wote lazima watupiane
*******tukiwa mbali kidogo na huu mtaa tunamwona bon akiwa na vijana kama wanne hivi ambao walikuwa ni boda boda na mmoja yupo tuu sijui anafanya kazi gani.
.oya broo mishe gan unapiga kitaa hiki
Daa bado sijapata mishe maana bado ni mgeni
. daah pole ila sio shida_____kabla hajamaliza kuongea ilisikika sauti paaaa!!!
Kisha vikafuatiwa na vilio vya watu baada ya -----itaendeleaaaaaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni