WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 11
---------ilikuwa ikionyesha dhahiri kwamba kuna polisi tayari washaingia pale ndani na taarifa wamepata wapi hakuna aliyeweza kujua baadhi ya watu ambao walikuwa bado hawaja ingia ndani walishikwa na kuwekwa ndani ya gari ambalo linafahamika kama tenga. Kisha afande mmoja akasogeza gari jirani kabisa na uwanja, na kuanza kufungua milango ya kila mmoja.
Usiku huu ilikuwa ni fujo tuu katika hii nyumba
Baada ya dakika kumi na tano walikuwa tayari wameshakusanya wapangaji wote na kuwapakia kwenye tenga
Aisee hapa kuna chumba kimoja naona kama bado hatuja pita(aliongea afande mmoja kumwambia hivo mwenzie)
Ok nichumba kipi hicho kipara
Chumba cha mwisho kwenye karibia na kona. Ahaa we nyoronyoro nenda kagonge fasta (alimwamulisha afande mwenzie)
Yule afande ambae alionekana ni mwembamba sana hadi wanamwita nyoronyoro aliondoka ili akaangalie katika kile chumba na amchukue na aliyeko ndani waende kituoni
Ngo ngo ngo fungua mlango (kimya) nasema fungua mlango,.,. aliongea kwa ukali lakini hakuna sauti ambayo iliitikia wala mlango haukufunguliwa alichokifanya kuulazimisha kufungua akafanikiwa. Lakini ile anaingia tuu ndani alibamizwa na mlango hadi akajikuta anarudi tena nje. Hadi hapo hakuwa na hamu tena ya kuendelea kufuatilia hili swala la kutaka kujua aliyeko humu ndani, aliondoka na kurudi hadi kule kwa wenzake.
Oya kimbao mbona unarudi bila abiria inakuwaje au umeshakula hongo hukohuko.
-nianchie upuuzi hebu nenda kwanza wewe ivi unadhani wewe ulisahau kwa bahati mbaya kwenda katika kile chumba.
Unamanisha nini?
- nimesema nenda kamchukue aliyeko ndani. Baadaya kubishana sana yule ambae alikuwa kama ndio kiongozi alitoa uamuzi wa kwamba tuachane nae tuu.
Lakini wapangaji wengine nao wakapaza sauti zao
NYIE MAAFANDE NDIO HAMNA AKILI KWELI YAANI MHUSIKA MUMWACHE HALAFU TUCHUKULIWE SISI WENGINE AMBAO HATA HATUHUSIKI SASA HAPA HATOKI MTU, MTAKALO AMUA AMUENI TUU WOTE TUNASHUKA HU UJINGA SASA>
Baada ya kuongea vile alianza kushuka mmoja baada ya mwingine hadi gari likawa tupu. Maafande walijaribu kutumia ubabe lakini hakuna aliyyeweza kuwaridisha mle ndani. Walipoona wameshindwa waliamua kuondoka na bashir pekeyake na kwenda nae kituoni ili akawasaidie maelezo kwa kitu kilicho tokea.
Gari lilianza safari na kituo cha kwanza kilikuwa katika kituo cha afya ambacho hadi ule mda kilikuwa bado kipo wazi, na kumpa huduma ya kwanza bashir ili waendelee na safari yao. Baadaya kufika kituoni bashir alifikishwa na kupelekwa mahali maalumu kwaajili ya maelezo. Lakini alipofika tuu polisi mmoja ambae alikuwa ni wa kike akajisemea asante mungu KAMA HILI JAMBAZI LEO LIMELETWA
Hongereni kwa kazi nzuri maafande maana huyu alikuwa ni msumbufu sana. Kisha akapelekwa katika chumba kingine bila kuulizwa chochote
_______upande wa walinzi kule barabarani_______
Oya nyie jamaa hapa naona boss leo ni kama hana msaada hivi, mnashauri tufanyaje sasa tutembee kwa mguu au jee.
Kudadeki acha ujinga hata kama ramani tunayo umajua huu mtaani wa akina nani wewe kama utatembea kwa mguu safar njema bamboo sawa sisi hatuna noma hata kwenye gari tutalala tu
Duuuh ila nae anazingua sa siapokee simu tu tuelewe tunafanyaje-----wakiwa wanaendelea kujadiliana mara simu ya bamboo ilianza kuita, alipoitazama alifurahi baada ya kuona namba ya boss ndio iliyokuwa ikipiga simu kwa muda ule, aliipokea
_-_-_yaah boss, ee ndio, enhee, sawa ok, lakini mbona hakuna m-pesa hili eneo, ya ni bora uje nayo tu, ok asante, sawa tutakungoja tuu, asante. Kisha simu ilikatwa.
Bamboo alifurahi, na wenzake kidogo furaha yao ilirudi maana walikuwa wakiwaza watalaleje hapa polini na isitoshe sio wenyeji. Lakini waliposikia boss anakuja ili waondoke walishukuru sana kisha wakaingia kwenye gari na kuanza kumngoja ili atokee wajaze mafuta kwenye gari safari ya kurudi nyumbani ianze.
Walikaa kwa mda kama wa nusu saa wakaona boss hatokei bamboo akataka anyanyue simu ili ampigie tena boss. Lakini gafla akaona simu yake imepokonywa sikioni mwake, kwaakili yake alijua labda ni utani waliojizoesha na wenzake ndio wamechukua simu. Alimgeukia mwenzake ili amwambie aache utani wa kijinga lakini akajikuta akipokea makofi tuu
Bamboo alianza kuona maruweruwe. Wakiwa bado hawaelewi chochote mara wakaona kama mbele yao kuna taa zinawaka na kuzima huku zikiwa fuata wote wakajificha chini ya viti vya gari lile ili ule mwanga usiwamulike. Lakini mauzauza hayakupungua mara wakahisi kama wanamwagiwa maji kwenye migongo yao tena maji ya barid kama barafu kitendo kilichomfanya kila mmoja wao kunyanyuka ili ajipukute hayo maji. Kitendo cha kunyanyuka tuu kioo cha mbele cha gari lile kilipasuliwa.
Wote wakabaki wameduwaa tuu mara wakaona mtu ananyukia mbele ya gari lile
Bamboo alishika usukani ili aanze kuendesha amharibu huyo aliyekuwa ananyanyukia mbele ya kioo. Lakini gari haikuwaka. =.alisahau kama mafuta yalikuwa yameisha na ndio walikuwa wanamngoja boss awaletee mafuta
/////kweli bahati mbaya haina mwenyewe na kifo cha nyani miti yote huteleza/////
Bamboo baada ya kuona vile akaamua kujitosa na kuchumpa pale dirishani kwenye kioo cha mbele ya gari ambacho kilipasuliwa, lakini kabla ya kutoka nje alirudishwa na teke ambalo lilimpeleka hadi siti ya nyuma kabisa huku akitulia mgongo. Bamboo alilalamika sana kuilaani hii kazi ambayo alipewa na boss wake leo..,,,/; kwa mbaali wakaweza kuona mwanga wa gari inakuja katika lile eneo
______)kwenye hili gari tunaona boss wa akina bamboo akiwa na wanajeshi wawili ambao wameshiba sana(_______
Aisee mkubwa gari lako ndio lile au
Yaah ni lenyewe vipi kwani
Mbona naona kioo cha mbele kama kimevunjwa vile (alikuwa ni mwanajeshi mmoja ambae alikuwa katika lile gari na boss wa bamboo)
Ngoja tusogee jirani kwanza
_-_-gari lilifika hadi pale kwenye gari ambalo lipo na walinzi. Wanajeshi wale walikuwa wa kwanza kushuka ambapo mmoja alizunguka ili amfungulie mlango boss, mlango ulifunguliwa na boss akawa anashuka kwa maringo sana ili akajue nini kinaendelea kwa walinzi wake. Lakini alipotoa kichwa tuu na kushusha mguu mmoja hapohapo alianguka chini wanajeshi hawa walipata wakati mgumu sana maana hawajui ni presha ya boss au kitu gani, walimnyanyua ili wajue cha kufanya.
Baada ya kumnyanyua mwanajeshi mmoja aliingia nae tena katika gari huku mwanajeshi mwenzake akifungua buti na kutoa madumu mawili ya mafuta ili akajaze katika lile gari lililochukua walinzi ili waondoke kukamilishakile ambacho kimewaleta
Huyu polisi ambae alikuwa na boss baada ya kumwangalia vizuri aligundua kuwa boss amedwingwa sindano ya usingizi. Alimwita mwenzie, akaja
Aisee hapa inaonekana pana hatari hebu tumwache boss tuacheki hicho kinyago kinacho tuchezea(baada ya hapo walitoa silaha zao na kuanza kufuata gari------itaendeleaaaaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni