WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 10
-----yule aliingia ndan na kuwasha tochi katika simu yake ili aangalie hela mahali ambapo anaziweka kila siku, lakini alishangaa kuona hakuna kitu chochote zaidi zimebaki tuu zile nguo ambazo zilikuwa jirani na ile sehemu ya kuhifadhia hela zake.
Hadi hapo mzee alichanganyikiwa kabisa asiamini kama kweli hela zake hazipo pia akabaki anajiuliza ni nani aliyefanikiwa kuingia hadi ndani ya kile chumba chake na kuondoka na pesa zake.
Licha ya kujiuliza maswali hayo yote lakini hakupata jibu ila akajipa moyo wa kuendelea tuu kutafuta pengine ataziona, ukiangalia umeme haupo katika hii nyumba ndio kitu kilicho mfanya ajipe moyo upya wa kuendelea kutafuta pengine ameangalia kwa pupa hadi hajaona kitu chochote.
Alitafuta hela zile kwa mda wa nusu saa lakini hakuziona, baadaya hapo akatoka na kukaa sebuleni huku kukiwa ni giza ila simu yake ndio iliyokuwa inamwongoza huu mda wote.
Upande wa walinzi nao walingoja sana hadi baadae wakakata tamaa kabisa, bamboo kama kawaida akanyanyua simu yake na kutafuta namba ya boss na kupiga,
Mzee akiwa nyumban amekaa pale kwenye sofa lake mara akasikia simu ayke inaita tena akanyanyua tena ili aone ni nani anae mpigia, alipoona ni mlinzi wake bamboo hata hakuhangaika kuipokea ile simu mana alishajua hawa shida ni mafuta na sio kitu kingine.
;;;kwakweli usiku huu ulikuwa ni mbaya sana ambao hata wasingeweza kuusahau hata mara ,moja
;;;IVI HAWA NAO WAPUUZI INAMAANA HAKUNA HATA GARI MOJA LINALOPITA KATIKA HIO NJIA MBONA WANATAKA WANIFANYE KUCHANGANYIKIWA HAPA SHIT;;;;
aliongea boss alipokuwa amekaa pale sebuleni baada ya simu kutoka kwa mlinzi wake bamboo kukatika
mzee akiwa amekaa tena simu yake ikaita tena
ya ndio nimekutafuta sijui ulikuwa wapi kijana wangu,
aah sawa mimi hapa nina tatizo kama hutojali sijui kama unaweza kuja hata sasa hivi hapa nyumbani, ok nitshukuru sana kijana wangu nakutegemea usiniangushe kwakweli, aaaaah ok, ok, nashukuru sana(simu ikakatwa)
baadaya muda kuna alipiga hodi mzee alikaribisha ili aingie ndani
daaaah mzee hapa naona shida yenyewe hata huna haja ya kuniambia inajieleza yenyewe aisee pole sana, ngoja nikutatulie haraka. Kijana aliingia kwa maneno mengi sana ambayo mzee hata hakupata chansi ya kuongea. Akabaki ametulia tuu kumngoja tuu kijana huyu akamilishe hii kazi ndipo waongee zaidi.- baadaya dakika chache umeme uliwaka ambapo mzee alifurahi sana akamfuata huyu kijana na kumwambia----; yaaah hebu njoo ukae kwanza mana hapa sikujua kabisa ntafanyaje hapa
sawa mzee wangu hizi kazi za tuu kwetu kama hela ipo
aaaah we usijari pesa sio tatizo sana, ehee niambie unahitaji sh ngapi mana umenisaidia sana
-----mzee alifurahi huku akihitaji aambiwe kiasi cha pesa ya kulipa kwa kurekebishiwa umeme wake katika nyumba kijana nae kwaajili ndio kazi yake hakuzubaa akamwambia
++mzee hapa kwakuwa umeniita usikukama huu utanipa elfu hamsini tuulikitokea tatizo niite tena.
Mzee akamwambia hebu ningoje hapohapo kwanza nakuja. Kisha akasimama na kuelekea ndani ili akafuate pesa amlipe huyu kijana
Baadaya kufika ndani ndipo alijua kuwa simu yake haikumdanganya kuwa ndani kwenye briefcase yake hakuna pesa yoyote
Kidogo azimie lakini watu wakubwa tena mapedeshee kama hawa hawawi na akiba ndogo akaenda kufungua begi fulan hivi kubwa kiasi
Ile anafungua tuu lilichanika begi lote huku vitita vya pesa vikidondoka chini akahesabia kiasi kama cha laki mbili na kuondoka nacho
Alirudi tena sebuleni na kumkabidhi yule kijana zile pesa na kumwambia asante mara kadhaa
Tukirudi kwa ben na bashir hii nyumba huu usiku zilikuwa ni kelele tuu
Wakati huo bashir alikuwa anatoa damu puani hadi mdomoni huku akiwa hana hata nguvu za kusimama tena
Kama kawaida wadada na maneno yao
Hahahaaaaaaaaaaaaaa babu uuu leo yamekupata unajifanyaga kidume sana kwa wenzio leo kajamaa kadogo kadogo kama hako kamekukalisha boya wewe
;;;;;mh amina tulia bhana kelele hadi unaboa ujue hapa atakuwa anakariri wanaomletea shobo shauri zako
Ohoooooo tena achunge akitaka kunipiga tuu nipo tayari nikaolelwe na huyu mgeni hata kama sijamfahamu. Wenzie baadaya kusikia hivyo walicheka sana huku wakimwambia shauri zako
Bashir baada ya kumwonesha na kumfunza adabu, nilijua wazi kwamba yule mwanamke wake labda atamsaidia kumwondoa pale lakini mke wake mwenyewe ndio kwanza alikuwa anapiga tuu stori na wenzake
;;;;; enheee shoga imekuwaje hadi shemeji yetu inakuwa hivi tena, aliuliza hili swali dada mmoja ambae walimtaja ni qeen.
Aaah shoga wewe acha tuu huyu mgeni si akaja kugonga na kuuliza wapi ambapo anaweza kupa msosi usikuu huu ili ale akalale bashir kama kawa na nyodo zake akajibu pumba lakini mimi nikaona sio vyema nikamwelekeza mahali ambapo anaweza kwenda na kula, huyu mkaka aliondoka, huku nyuma sasa bashir amenimaindi vibaya na kujisemea akirudi huyo boya wako nawachinja wote. Mimi sikuwa na la kusema
Basi huyu mkaka aliporudi akawa amekuja kutoa shukran bashir siakajifanya kumpandishia mimi nimewasilikiza wamebishana hadi wakasema watoke nje ili waoneshane, mambo ndiokama unavoona saizi hivi mtu tayari chini_-_--___-
Huu ni uboya ivi we unadhani mimi nikamtoe pale huku mimi mwenyewe kila siku napata shida tuu za kupokea kichapo bila sababu yoyote leo na yeye aonje bhana
(aliongea maneno yale mke wa bashir ambapo alikuwa amekaa na wenzake katika gogo ambalo lipo kwenye moja ya ukuta wa nyumba ile na baadaya mda wapangaji karibia wote waliondoka na kurudi ndani kwao huku mdada anaeenda kwa jina la Asha akisema kesho lazima awe redio ya mtaa kutangaza kuwa bashir jana usiku alipigwa kama mtoto na mgeni ambae ameingia jana hiyohiyo kwenye nyumba hii) lakini wenzake wakasema shauri yako na mwenzio amina nyie inaonekana mnataka kumbip bashir atamalizia hasira zake kwenu jifanyeni hamjamfahamu tu. Moja wao aliongea maneno yale na kuingia ndani kwake na mimi baada ya kuona kama adabu tayari nimeshamfunza nilinyanyuka na kuingia chumbani kwangu ili nilale na kesho nianze kazi ya kulipa visasi kwa wale ambao wanahusika na kututeketezea familia zetu bila sababu yoyote ile.
Niliingia ndani kwangu na sikutaka hata mmoja ajue nimeondokaje hadi kuingia ndan
Hii sikunililala kwa tahadhali sana, maana najua kabisa hii nchi yetu ya Tanzania wambea hawapungui.. unaweza sema kitu kitabaki siri kumbe kuna watu washapiga simu hadi kituo cha polisi ili kukuchomesha wewe ambae sio mwenza
Nilipoingia ndani nikachukua ile karatasi ambayo nilikabidhiwa na mama ili niipitie nijue ni nini ambacho kipo ndani yake
Nilisoma kwa mda wa dakika kama tano, mara nikasikia sauti kutoka nje wote mpo chini ya ulinzi hakuna mtu kutoka nje------itaendeleaaaaaaaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni