WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 09
---------sasa siungejenga nyumba yako mwenyewe (huku msonyo ukisikika)
Kiufupi haya maneno maneno yalimuingia sana huyu jamaa. Akajisemea ivi leo hii mimi basher ndo naambiwa upumbavu huu na mwanamke hizi dharau au kitu gani.
Baada aya kuongea hayo akamgeukia tena ile kwa spidi kama amechomwa na sindano au mwiba. Hali hii ilionyesha kabisa kwamba anahasira sana kwa jinsi alivokuwa. Ndipo ikasikika sauti samahani bashir nisamehe
Pumbavu ivi unapata wapi ujasiri kama huo eti mimwanaume mingine, kwahiyo huyo mgeni wewe atakusaidia nini wewe. Sasa namngoja arudi ili niwaonyeshe wote kuwa bashir ni mwanaume wa shoka.
Na kweli baada ya kuongea vile akakaa kwenye kochi fulani ambalo lilikuwapo mule ndani akimaanisha kwamba ananingoja mimi ili nirudi chumbani kwangu yeye anifuate
______kwa bon_____
-- baada ya kufuata yale maelekezo ambayo nilipewa na mke wa huyu jirani yangu nilienda mojamoja kwa moja hadi lile eneo na kuagiza kitu ambacho nilikuwa nakihitaji kwa wakati ule.
Nikiwa nimetulia nangoja mama ntilie aje aniletee chakula mara nikasikia kelele nje, watu wengi wa mle ndani walitoka ili wakashangae lakini mimi hata sikuwa na habari maana nilienda kwa shida ya kula na kula na sio mambo mengine. Ile nimekaa nangoja, niliona mda unazidi kuenda tuu lakini siletewi chakula changu nikasimama ili niangalie mahali ambapo yupo lakini sikuona chochote. Lakini baada ya dakika chache nikmwona nae akiingia toka nje. Kwa maana nae alienda kuangalia tukio lililo kuwepo kule nje. Niliboreka lakini basi hakuna namna yoyote ile maana mimi ndio mwenye shida. Ilinipasa kungoja tuu
Baada ya dakika chache ndio chakula kiletwa. Nilikula kwa fujo sana mda wa dakika moja nikawa tayar nimeshamaliza nikalipa hela na kuondoka nikienda nyumbani.
Nilifika nyumbani lakini kabla ya kwenda ndani nikapitia kuwashukuru kwa malekezo
Ngo, ngo, ngo
Yaa nani unagonga, aliuliza hivo bashir
- aaah ni mimi jirani yako hapa
Ok powa ingia tuu
- asante. Kisha nikaingia hadi ndani.
Nimekuja sina mengi ila nawashukuru tuu kwa msaada wenu nimefanikiwa kupaona asante. Kwaheli mimi naenda kwangu
Oya dogo ngoja kwani (alisema hivo bashir na mimi nikasimama tena kwa heshima zote)
IVI UNAJUA MASHARTI YA UNAPOENDA KUPANGA NYUMBA HIZI UNATAKIWA KUWAJE (aliuliza hili swali bashir lakini sikujua namaanisha nini)
Bro swali lako linamaana gan mbona kama sikusomi
--ahaa hunisomi utanisoma tuu subiri baadaya muda
Kudadeki usjitie kidume kwa wageni huku hujui mimi ni nani hata siku moja bado sijamaliza tena naomba tuelewane hapa sijaja kwaajili yako na kama ni hela ya pango hujanilipia kwahiyo fanya yako na mimi nifanye yangu sawa bro heshima ni kitu cha sana naona unaelekea hatutakuwa sawa hata kidogo(nilimwambia hivo nae akanijibu)
Powa ila mazingira ya watu hata sikumoja usijitie unajua sana, tena kama mimi ukinizingua nakumwaga ubongo kabisa bila hata kukuangalia usoni unasura ya kupastor au ki gangster sawa mdogo wetu
(niliona huyu anataka kunipanda kichwani tena hata heshima hana)
Sawa sio shida sana tuache maneno mengi kama madem wakitaa chenu twende njee saizi ili tukajue ni nani zaid na ni nani boga lililooza kabisa.
Bashir kichwani akajisemea leo ndio pa kuchukua ujiko kwa haka kaboya kengine ivi hakanijui nini ngoja kwani.
Alipojisemea hivo alimama na kunifuata hadi pale nilipokuwa na kusema sawa hebu twende. We jogoo la shamba huwezi kunitishia maisha yangu kama hukuchunguza kabla ya kuja kupanga hapa ndio utafahamu vyema huyubashir ni nani
Wakati huo wote yule mwanamke wake alikuwa akitusikiliza na kutuangalia bila kuongea kitu chochote kile
Mimi na bashir tulisimama na kutoka hadi nje ambapo kulikuw ana uwanja katikati ya ile nyumba.
Bashir alikuwa na maneno mengi sana hadi na baadhi ya wapangaji wengine walitoka ili wajue kuna nini hadi bashir anapigamakelele ya namna hii.
Kwa macho yangu nikawa nashuhudia milango ikifunguliwa na baadhi ambao walizima taa zao wakawa wanaziwasha ili waweze kushuhudia ni nini ambacho kinaendelea usiku huu
/////shoga angu leo kama siokuna timbwili hapa ngoja tulicheki atakae bondwa kama kawa kesho ntakuwa gazeti kitaa kizima yani.
Sema wee shoga nakuaminia kama ni ukiwembe tuu unajua
Acha zako mbona hata wewe uko hivo unakumbuka ile ulipozusha kuwa umenifumania.
Aaaah kausha bhana usije ukanikosesha mtanange huu bure////// ni wasichana wawili ambao majina yao hayajafahamika bado
Baada ya wapangaji kutoka pale bashir akaona huu ndio wakati wake wa kuonyesha uanaume wake maana wapangaji wote walikuwa wakimfahamu_______
______kwa baba______
Baba akiwa ametulia nyumbani amesha maliza taratibu zote mara simu yake ikawa inaita
Ngrrrrrrr x5
Naam haloo
Ndio mkubwa vipi ile mipango imekaa vizuri
Mipango gani
Mzee usifanye umesahau
Aisee hebu nikumbushe kwani wewe ni nani (simu ilikatwa na maongezi yaliishia hapo)
Baba hadi hapo hakuwa ameelewa ni nani aliyepiga simu kwa wkati ule na kuongea habari za mipango imekaa vizuri alizima tv na kuingia kulala
__________________________________
Tukirudi kwa yule mzee kwenye lile jumba tunamwona mzee ambae ni boss ndo anafahamika hivo
Yupo uwanjani anazunguka tuu peke yake huku nyumba ikiwa haina umeme na mafundi wote wapo bize kwa wakati ule.
Akiwa anaendelea kuzunguka mle ndani kama yeye ndie mlinzi mara simu yake ilianza kuita alipoangalia ilikuwa ni namba ya mlinzi wake mmoja bamboo jina lilisomeka hivo kwenye simu,. Ila mzee hakupokea maana aliona watakuwa wanampotezea tuu mda asijue wanataka kumwambia kitu gani,
Simu iliita hadi ina kata bila kuweza kupokelewa, lakini bamboo hakukata tamaa alipiga tena simu safari hii iliita hadi inakaribia kukata ndio ikapokelewa.
Samahani boss gari mafuta yametuishia na hatukutembea na akiba yoyote sijui kama unaweza agiza mtu aje atuletee huku tuko hapa barabarani.;;.;.; bamboo aliongea bila nukta maana alijua lazima huyu boss atakata tuu simu ile na kutofanya chochote kile.
Boss alijibu hebu ngoja kama dakika tano hivi natoa majibu, kisha simu ilikatwa nae akaingia tena ndani ili------itaendeleaaaaaaaaI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni