WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 08
-------baada ya kuita walinzi kwa mda mrefu kashangaa hata mmoja haji kuitika ule wito ndipo akachukua uamuzi wa kusimama ili akawaone mweyewe kule nje. Alishituka baada ya kutoka kule nje aliwakuta walinzi wote wakiwa wamewasha wimbo kwenye simu na kuanza kucheza
Yule boss wao baada ya kuwaangalia akajisemea ivi mkiwaachisha kazi itaonekana mnaroho mbaya sana kama mabos sijui niwamwage ubongo nao????
Lakini baadaya kufikiria sana akasema hapa sio bure lazima kuna kitu nyuma ya pazia himaya yangu imesha ingiliwa tayari.
Alisogea hadi pale walipo na kumshika mlinzi mmoja na kumwambia nenda kauzime mziki huo ili tuongee yule mlinz kwa kuwa ni boss aliongea aliamua kufanya hivyo
Aaaaaa bamboo mambo gani sasa hayo hebu washa mziki
Bamboo aligeuka na kuwaambia angalieni au hamumuoni boss baada ya bamboo kuongea yale walinzi wote walishtuka na kusimama kisawasawa ili wamsikilize boss wao maana walijua kabisa hapa tayari tumesha haribu
;;;;;jaman ivi ni mambo gani mnayoyafanya saizi hapa, mmekuja hapa kufanya kazi au kucheza hizo nyimbo zenu za kibongo mnazoita bongo freva sijui(baada ya boss kuongea yale alivuta pumzi akatulia kisha kaendelea) ok sio mbaya naomba kujua kwa hivi mnavofanya mwishoni mnanidai ujira wenu au na mimi niwachezee hivohivo. Mlinzi mmoja aliropoka kwakusema
Boss mziki ulikuwa mzuri sana
Wenzie walimgeukia na kumwangalia sana yule aliyekuwa jirani nae alimuwasha bonge la kofi ikifuatiwa na ngumi ya tumbo hadi yule aliyeropoka akakaa chini kwa maumivu(((maana kati ya ngumi ambazo ukishitukizwa unaweza kuzirai ni pamoja na ngumi ya tumbo)))
Boss aliendelea kuongea
Cheki kama huyu mwenzenu yaani ameahau kabisa nini kimemleta hapa ili aje kukifanya eti mziki ulikuwa mtamu. Ok nimewaita tokea mda mrefu sana lakini hakuna aliyeweza kusikia wakati huo nawaita sasa sijaelewa ni kwa sababu ya huo mziki au ni kitu gani sijui lakini nili taka mje sebuleni mkawatoe wenzenu na kuwapeleka mahali ambako mimi nitawaonyesha..
Baada ya kuongea yale alianza kuondoka akiwa na maana inatakiwa wamfuate ambako yeye anaenda ambako ni kule sebuleni
Baada ya kufika sebuleni kila mlinzi alibaki ametumbua tuu macho yake kuwaangalia wale ambao kwa mda ule walikuwa wamelala chini huku wakiwa na damu kwenye vichwa vyao maana walipigwa risasi za kichwa kilamtu. Walinzi hawa hata kama wamelinda kwa mda mrefu sana lakini hakuna hata mmoja ambae amewahi kupoteza uhai wa kwa namna yoyote ile kwa hiyo wote waliona kama ni tukio la ajabu sana ambalo boss wao amelifanya.,
Walipomaliza kuwakusanya wale maiti waliwapeleka moja kwa mojahadi kwenye gari moja ambalo lilikuwa limezibwa upande wote na ndani ya hilo gari ni giza totoro ambalo tungefanaisha na gari la kubebea maiti lakini kwa hili lilikuwa likimilikiwana mtu binafsi.
Boss aliita bamboo hebu njoo ili nikupe maelekezo mahali ambako inatakiwa kupeleka hiyo mizoga. Bamboo bila kuchelewa alimfata boss na kupewa maelekezo mahali kwa kupeleka ule mzigo ambao ni watu, baada ya hapo safari ilianza na yule boss wao akawa anarudi sebuleni lakini katika hali ya sinto fahamu akashangaa mlango ambao inatakiwa aingie unafungwa kwa ndani. Alikimbia ili penginepo aweze kuuzuia lakini jitihada zake hata hazikufanikisha jambo lolote lile na badala yake aliuacha ufungwe tuu
Kwa wakati huu boss hapa nyumbani alibaki yeye pekeyake bila hata mlinzi yoyote yule kwahiyo kwakuwa mlango wa upande mwingine nao aliufunga kwa ndani na kibaya hakuchukua funguo hata moja ikambidi akae tuu pale nje huku akifikilia ni jambo gani atalifanya ili aweze kuingia tena ndani
Alikaa sana masaa yalienda hadi inaaanza kuingia giza hapo ndipo akaona mlango unafunguliwa tena lakini mtu anaefungua hakuweza kumwona. Kwakuwa ni nyumba ya kwake alijisemea hata nikifia kwenye nyuma yangu sio mbaya kuliko nikafia nje huko. Hayo yote alikuwa akiongea huku anaingia ndani ya nyumba ile ambapo ndan ilikuwa giza sana. Alipojaribu kuwasha taa hata moja hakuna taa iliyokubali kuwaka, alijitahidi kubonyeza swichi mara kadhaa lakini hakuna kilicho badilika akaanza kutafutiza simu yake alipoiweka ili ampigie fundi umeme aje arekebishe hadi kuipata simu yake ilichukua nusu saa kwa kuwa ilikuwa ni giza mle ndani hapo ndipo akatafuta jina la fundi umeme ili apige
-/-/-/-/ mteja unaempigia hapatikani kwa sasa tafadhali jabu tena baadae. Thank you for_____hakutaka kusikiliza zaidi. Alikata simu na kutafuta jina jingine la fundi umeme lakini nae majibu yakawa
Mteja unaempigia anaongea na simu nyingine tafadhali jaribu tena baadae alijitahidi kungoja na hatimae simu ikakatwa
_______________________________
Tukiwa katika maeneo fulani ambao ni giza totoro tunamwona ninja fulani akiwa kashika kileo na kukata waya wa nguzo ambayo ilikuwa jirani na mnara kisha akaruka beki tatu mfululizo ambazo zinamfikisha hadi chini na baada ya hapo anaondoka na kuendelea na safari
********************
Wale walinzi baadaya kuondoka walitembea hadi lile eneo ambalo waliambiwa wakatupe zile maiti walifika hadi lile eneo na kutupa zile maiti na kuanza safari ya kurudi ambapo saa zao zilikuwa zikionyesha kwamba ni saa tatu na dakika kumi na tano
Baada ya hapo walianza safari ya kurudi nyumbani ambako ndio kwa yule boss, walifika hadi maeneo fulani gari lilzima na kugoma kabisa kuondoka walipojaribu kuangalia wakagundua kuwa mafuta yamewaishia na hawakuwa na akiba ya dumu hata la lita tano tuu, kwahiyo walichokipanga ni kuomba kama gari likipita waombe msaada wa kufika hadi kituo cha mafuta ili wanunue
______kwa boN________
Baadaya mambo yote niliyoyafanya mchana ambayo ni yale mauzauza ambayo yalikuwa yanatokea kwa boss pale nyumbani kwake nilitafuta hadi sehemu ambayo yeye anatumia kwaajili ya kuweka hela zake na kuchota kiasi fulani cha pesa ambacho kiliniwezesha kupata chumba cha kupanga kilichokuwa mbali kidgo na pale kwa boss.
Usiku niliingia katika kile chumba ili nilale lakini nikagundua kuwa ninanjaa sana kwakuwa hapa palikuwa na watu wengine niligonga mlango mmoja na kumkuta bro mmoja ambae alikuwa na mke wake. Aliponikaribisha niliingia na kuuliza mahali ambapo naweza kupata mgahawa ili nipate angalau hata chakula mana mimi ni mgeni katika mazingira haya.
Yule bro akasema ungeenda kuuliza kwa balozi mana yeye ndiye anaejua mitaa yake yote.,., duuh hili jibu liliniudhi sana nikamwambia poa kaka angu nashukuru kwa jibu lako kwaheli nikawa natoka.
Mke wake ambae alikuwa nae kwa mda huo akasema nenda mtaa wa nyuma huo pana ukuta mmoja unataa kubwa hili mlango wa tatu ndio kuna mgahawa. Nilimshukuru kisha nikawa naondoka huko nyuma
Kwahiyo wewe ndio unajifanya unajua sana kusaidia hawa mafara wanaoingilia mitaa ya watu na kutusumbua.
- hata wewe unaweza ukawa fara kinacho kufanya ushobokee nyumba ya watu ni nini siujenge ya kwako mi mwanaume mingine bhana sijui ipoje((huku msonyo ukisikika)) yaani wewe kabisa una-___---itaendeleaaaaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni