Ijumaa, 21 Oktoba 2016

Who am i

WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 18

Tulipoishia>>>>>

Walimsogelea lakini ile kumgusa tuu walisikia kishindo kizito sana juu ya gari moja walilokuja nalo pale wote walishtuka na kuangaza macho ule upande ambao kimesikika kile kishindo, lakini hawakuweza kuona chochote mmoja waoa kachukua saa na kuangalia ni saa ngapi mda ilikuwa inaonyesha ni saa 9 na nusu usiku
  Mmmmh ila kuna watu hapa duniani wapo kwaajili ya kuwapa watu mateso ivi mwenzenu sijawahi kufikilia kuwa nitakuja kufanya kaza ya ulinzi lakini leo ndio mara yangu ya kwanza ivi wenzangu mmeonaje kuhusiana na hili swala la sisi kulala kama mapopo hivi huku tukilinda magari ya mtu bila malipo yoyote yale huu uboya.(alikuwa akiongea mwenzo mmoja)
    Aaaaah na wewe unangea nini bhana mimi nawaza kama yule jamaa akija tena hapa ambae ametupa kichapo itakuwaje mana saizi yenyewe mauza uza kibao mara vipite vivuli tuu kama hvi saiv kishindo sijui ni cha nini, shit huu uboya mi naamsha hata sasa hivi ambaye yupo tayari twenzetu
Baada ya kuongea vile alianza safari yale na kwa kuwa nyumbani kwao hakukuwa mbali sana wote waliungana na kuondoka lile eneo bila kumwacha hata mmoja wao

____ilifika asubuhi boss wao alikuja na kuanza kukagua kama waliweza kumwona baba lakini cha ajabu alifika na kuyaona tuu magari yake yakiwa pekeyake pale
Kwa mawzo yake alielewa kwambayawezekana wamelala ndani ya magari kwahiyo bado watakuwa hawajaamka
Akalifuata gari moja na kuchungulia kwenyekioo lakini hakuona kitu akafuata jingine nalo aliona ni hivo hivo. Hapo akajua kwamba hapa wala hakuna mtu alianza kuongea pekeyake
IVI HAWA WATOTO WA MTU GANI, WAMEKIMBIA NA KUACHA MAGARI YANGU HAPA HUKU NILIWAPA KAZI YA KUFANYA. SASA NTAMTAFUTA MMOJA BAADA YA MWINGINE.
Baadaya baadaya hapo alitoa simu mfukoni na kumpigia mtu mmoja
Yaa ndio mheshimiwa, aah ndio, sasa nilikuwa nahitaji mtu wa kuendesha scaveta kama watu watatu hivi nataka wakaniondolee sehemu moja hivi vyombo vyangu, ok sawa ukipata nambie, yaah hakuna tatizo kabisa, ok asante sana.
Baada ya hapo akashusha simu yake na kuingilia moja ya gari kisha akaondoka nalo

_____ilipofika mda wa kazi baba kama kawaida aliondoka na kwenda kazini kwake na kuniacha pale nyumbani
Na mimi nilipoangalai ratiba zangu nikagundua kwamba hii ni siku nzuri ya kwenda kumwangamiza yule mganga ambae ndio hufanya kazi  na akina babu na bibi ili kuwapoteza ndugu zetu
Nilichukua begi langu na kuweka baadhi ya vitu kisha nikachukua karatasi na kuandika maneno fulani kwa kalamu ambayo yalisomeka
SAMAHANI BABA NAJUA UTAJIULIZA SANA NIMEONDOKA NA KWENDA WAPI,. ILA UKWELI NI KWAMBA NIMEENDA MAHALI KWAAJILI YA KUTEKELEZA MAAGIZO AMBAYO NILIACHIWA NA MAMA MARA YA MWISHO KUONANA NAE,.. BY BON
Kisha nikaifunga na kuweka sebuleni kwenye meza yake ambayo mara nyingi hupeda kukaa na kujisomea vitabu vyake. Na baadaya hapo nikaondoka na kwenda katika duka moja ambalo lilikuwa linajishughulisha na kuuza pikipiki nilinunua pikipiki moja aina ya boxer nilipohakikisha kila kitu kipo sawa nianza safari yangu rasmi ya kwenda kwa mganga
Safari hii ilichukua masaa kama saba hadi kufika maeneo ambayo nilikusudia lakini nikakumbuka kuwa mganga huyo anaishi jirani na mtaa wa mawen ambako niliacha vitu vyangu baada ya kuondoka na kwenda kwa baba.
Baada aya hapo niliamua kugeuza na kwenda pale lakini nikapitia ili kuapata baadhi ya mahitaji yangu, nilifanya hivo kisha nikaenda hadi pale nyumbani

Nilipofika niliwaona akina asha na mwenzake amina wakiwa wamekaa tu nje wanaotea jua la jion
Uso wa asha ulionyesha unafuraha sana lakini hawezi hata kusema anishingilie kwa maana hata jina langu hakuna anaelijua katika ile nyumba

Baadaya kufika niliapaki pikipiki yangu nje na kuingia ndani huku nikiwa na badhi ya mafurushiyangu niliyotoka kununua huko ila nikakumbuka hakuna jiko humu ndani nilitoka tena nje na kuchukua pikipiki yangu kisha nikaelekea kwenye maduka yanayohusika na kuuza majiko. Nilifanikiwa kuliona duka moja ambalo ndio walikuwa wamepanga majiko mengi sana nje pale, mwendo wa fasta tuu nilisimama na kufuata lile duka ili niulizie jiko lakini nikiwa ndio nafika mlangoni nyuma nilisikia mtu anapiga lesi kwenye pikipiki yangu. Akili yangu ilinituma kwamba hapa nitaibiwa halafu nishindwe kufanya kazi ambayo imenileta hadi huku.
Haphapo niligeuka na kurudi hadi kwenye pikipiki nae alipoona narudi kwakuwa kuondoka alisha chelewa akaamua kushuka akiwa nalengo anipige ili yeye apate kuondoka na pikipiki
Alifika kichwakichwa tuu na kunirishia ngumi asijue mi mtu wa namna gani
Ile maurusha tuu mkono niliudaka haraka na kuuvunja kisha nikamwacha pale akiwa na maumivu ya kuvunjwa mkono yani ilikuwa ni ndani ya nusu dakika tu tayari mtu ashaachiwa ukilema kisa wizi
Niligeuka na kurudi tena kwenye majiko kisha nikachagua jiko linalonifaa na kuchukua pikipikikisha nikaondoka na kurudi nyumbani ile nimekaa nyumbani mda kama wa saa tatu hivi nikawa sauti kutoka nje watu wanaongea
+++nilisikia anakaa  hapa tena nahisi ni humu ndani kama siyo ngoja kwanza tukagonge ili tuone kama kweli
Sema mwanangu inatakiwa tuingie kwa akili sana mana asije akawa ni mtu wa hatari mana ukifuatilia tangu anaingia tuu siku ya kwanza usiku ni mtu ambae hata hapendi ujinga ujinga na mtu licha ya kuwa anaonekana ni mpole sama kwa usoni.
Kudadeki acha uoga wewe inamaana tumetembea tuu bure mwenzetu amevunjwa mkono halafu tulifumbie tuu macho suala kama hili kwa upande wangu mimi sikubaliani hata kidogo yani ama zake ama zangu liwalo na lile.(walikuwa wakijibizana hivo wasijue kwambakila wanachoongea nimesha kisikia tayari
Baada ya hapo walifika hadi mlangoni kwangu na kuanza kugonga kwa fujo kweli
Ngongongongo
Nani unagonga (niliuliza kisha nikajibiwa
Binadamu..ok sawa kama wewe ni binadamu nahisi mimi ni binaugali au maji sawa kaa hapohapo kama mlinzi kama huwezi kujitambulisha sawa
Halafu acha uboya hebu fungua mlango vipi wewe utajuaje kama mimi ni balozi?
Sidhani kama balozi unauhuru wa kutoa majibu ya chooni kama hayo kwa usalama wako nakuomba tuu ondoka (niliwaambia hivo  badaya kuona kama wananiletea nyeusi tuu)
Na hapa haondoki mtu sasa hadi kieleweke tuu(walinijibu )
Poa ngojeni kwanza kitaeleweka tuu hata msijali nisubirini nyie si ndio wasumbufu wa nyumba za watu.>baada ya kuongea vile nilinyanyuka na kutokea dirishani kisha nikawazungukia hadi mlangoni na kuanza kuwafumua tuu makofi kama naadhibu mwanangu hivi. Baada ya kuona makofi tuu wamelizika waliamua kuondoka mbio na kurudi makwao

Baada ya hapo kwa kuwa nilishukuwa nimekula na kushiba safi kabisa nilichukua pikipiki tena na kuondoka hadi kwa mganga kisha nikapaki pikipiki mbali kidogo kisha nikaingia hadi ndani bila hata hodi------itaendeleaaaaa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni