Ijumaa, 21 Oktoba 2016

Who am i

WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 14

Tulipoishia>>>>

-----simu ilianza kuita nikaitazama ni nani lakini sikuweza kujua namba kwa maana ilikuwa ni ngeni machoni kwangu lakini niliipokea hivohivo, baada ya kuipokea zilisikika tuu sauti za makelele ya watu kibao.
Aaah msinizingue shit,. Kasha nikakata simu na kuanza kuondoka mdogo mdogo kuelekea kule nyumbani ambapo nilipanga____-

Katika uchochoro mmoja ivi kulikuwa na kikundi cha watu ambao walikuwa na mazungumzo yao :-
Aaaah kichaa waangu ivi huyo ngeni ni mtoto wa kahaba gani anae weza kuingilia tuu mitaa ya watu kiholela hivo
Ddduh man hata mimi sijampata hata jina lake ila acha tukamcheki mamake zake huyu, lazima niondoke na kiwiliwili chake nikaange homu kama kitimoto mana kitambo saaana
(kumbe walikuwa ni wavuta bangi ambapo katika hawa wavuta bangi na bashir alikuwa ni mmoja wao) baada ya kuongea saaana walijipanga kwa kuchukua silaha zao kama mapanga, nyembe, makwanja, wengine fimbo kama unavojua wavuta bangi wakisha panga kuleta vurugu. Baada ya hapo wakaanza safari na kiongozi wao alikuwa ni bashir ambae alishika jambia kama silaha yake

____- bon_ wakati naingia tuu pale nyumbani mdada alinifuata akijitambulisha huku hajaulizwa
Kakaangu mimi naitwa amina, mwenyeji wa hapa hapa samahani sijui wewe unaitwa nani mana kama majirani ni vyema kufahamiana vizuri
Niliona kama ananipotezea tuu mda wangu nikataka niondoke ili niingie ndani,. Jamani kaka angu acha dharau naongea na wewe.
Ahaaaa mawazo yapo mbali sana hapa umesemaje kwani, nilimuuliza kama sijasikia vile
Ilimpa wakati mgumu sana kuanza kuongea tena lakini akajikaza hivohivo, nimesema hivi-----kabla hajaongea simu yangu ilianza kuita tena, sikupoteza mda nikaipokea bila hata kuangalia ni nani ambae alikuwa anapiga kisha nikasikia sauti tokea upande wa pili nakuhitaji uje hapa nyumbani sasa hivi tena bila kuchelewa
Nilijua dhahiri kuwa hii ni sauti ya yule mzee kwenye jumba lile ambako nilipelekwa baada ya kutekwa. Niligundua kwakuwa nafahamu kuwa simu ninayo itumia ilikuwa ni ya mwanae aliiacha baada ya kwenda shuleni

Niliposikia amesema vile hata sikujibu chochote nikakata simu ile.
Enhee ulikuwa unasemaje nilimuuliza amina lakini hakujibu chochote na kuondoka spidi huku akiingia ndani kwake. Kumbe kile kikundi cha mateja tayari kilikuwa kishafika pale

Boya lenyewe ndio lipo wapi au umetuenjoi tuu hapa bashir onyesha fasta bhana ninahamu ya damu///aliongea teja mmoja kwa bashir ili bashir aonyeshe huyo aliye mpiga ni nani huo muda wote nilikuwa nimesimama tuu huku nikiwaangalia
Bashir nae hakusita kwa kutumia jambia lake akanyoosha kuelekea kwangu kwa maana mimi ndio mhusika wa tukio hili.
Yule teja kwa kimbelembele akajileta huku kashika upanga wake mkononi na kusema kijana piga simu ya kuaga kuwa wewe wakuandalie tuu kaburi kwa maana saiz wewe unaenda kuwa kitoweo changu nakupa dakika moja inatosha. Baada ya hapo akatoka kipisi cha karatasi ambacho ndani yake kuna bangi alikiwasha na kuvuta kisha akampa mwenzake ili nae apige pafu
Kisha akanigeukia tena./ muda umeisha kisha akanyanyua panga lake lakini anashusha tuu panga lilipigwa teke na kwenda kutua juu ya bati za nyumba ile kisha nikampiga makofi kama naadhibu mtoto. Baada ya hapo nilimpa ngumi ambayo ilimrudisha nyuma kidogo nikaongea na teke la tumbo alipepesuka na kwenda kuwasukuma wenzake kule walikosimama. Kudadeki zenu kwahiyo mmejituma kuja kufanya ujinga kama huo hapa eti. Nilikuwa naongea huku nikiwafuata waliko, nao kwakuwa walikuwa na silaha wakajiaminisha na kunyanyua silaha zao. Mmoja akajifanya kuleta shobo za kuwa wa kwanza kunipiga alipewa zawadi ya ngumi ya taya akaanguka chini huku akiwa kashika tu mdomo kwakuwa alikuwa ameshika fimbo niliinyanyua na kuanza kuwachezeshea muda wa dakika tano tuu ulitosha kuwakalisha wote chini. Nilipomaliza nilijaribu kupapasa macho yangu ili nimwone, lakini jitihada zangu hazikufanikiwa, sikumwona na wale mateja waliondoka na kupotelea wapi sijui

-------baba ivi simu yangu niliiweka humu ndani lakini siioni iko wapi maana nimetafuta sana na sijaiona (aliuliza mtoto wa mzee yule ambae waliniteka) e bwana wewe unalia na simu ya laki tano mimi niliibiwa milioni saba unaona kama unahaki ya kulia? Na kibaya simu yenyewe inapatika hebu ngoja nipige tena. Alinyanyua simu na kutafuta ile namba tena ili apige lakini haikuwa inapatikana
Kama ni line nilishasajili nyingine kuepusha usumbufu usiwepo kabisa kisha nikaifuta kila data zikiwemo account zake zote

Kama unavoona namba saizi haipatikani (aliongea baba ake)
Basi itabidi ninunue nyingine kesho, kwanini usiende sasa hivi nikupe hela kabisa, sawa nipe tuu naenda hata saizi. Basi mzee alisimama na kwenda ndani kisha akatoka na kitita cha hela kikiwa kimefunga na lababend (kama mnavosema) kisha kamkabidhi yule mwanae akanunulie simu, alipokea na kuondoka.

Katika duka moja tunamwona yule kijana wa mzee yule ameingia kununua simu mara akakumbana na dada Fulani na kuangusha simu ya yule dada ambapo simu ilianguka na kupasuka kioo lakini huyu dogo hata hakujari akapita na kuingia ndani. Lakini mhudumu kwakuwa aliona akamuuliza // wewe kaka mbona umeharibu simu ya yule dada lakini unajifanya kama huoni vile// ebwana ee wewe fuata kinachokuweka hapa huyo dada ndio kazi yako au unajifanya msamaria mwema wa kileo acha uboya nahitaji nokia lumia 850 hapo kama ipo.
Lakini yule mhudumu akakazania kwa kuendelea kuongea
//kakaangu acha dharau yule nae ni binadamu hujui saizi hapo tayari umemharibia hana mawasiliano tena?
Ivi wewe sista vipi mbona inaonekana hatuelewani kwahiyo simu inagharama gani ambazo wewe zinakupa uchungu namna hii, simu ipo haipo niambie niondoke aliongea kwa hasira sana yule dogo
// ok simu zipo nadhani gharama zake unazijua ni m ngapi
Wewe usijari kama hela ipo ya kutosha tuu nipe simu niiangalie nikiridhika nayo fwesh
./././mhudumu alitoa box moja la simu na kumkabidhi ili aweze kutazama. Dogo alilipokea kuangalia kisha akatoa kitita kizima cha hela zile na kumwambia hesabu zako nipe chenji zangu. Mhudumu. Alizipokea na kuhesabu huku akiwa na lengo la kumkomoa alihesabu zinazotakiwa kisha akahesabu za simu ya yule dada kisha akakamrudishia chench ambayo ilikuwa ni laki tisa na themanini na kumwandikia risiti.
Unaitwa nani mteja
Naitwa enock mlanje. Alijibu hivo kisha yule mhudumu akaandka jina kwenye risiti lakini kwenye kiasi cha hela akaandka in u$ dollah kisha akamkabidhi.
Karibu sana. Enock aliondoka kwa furaha asijue kuwa kaibiwa.,
Enock akiwa njiani kuna gari moja jeusi lilikuja na kusimama mbele yake kisha muda wa dakika tuu kadakwa na kuingizwa ndani ya gari lile ambayo ilienda kumwacha katika viunga vya posta. Enock alishuka ndani ya gari huku akiwa analia sana huku akiwaza gari lake alilokuja lipo mbali na kama simu bado ni mpya hawezi kutumia kufanya chochote ila akawaza aingie kwenye duka moja ili apate msaada-------itaendeleaaaaaa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni