Ijumaa, 21 Oktoba 2016

Who am i

WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 17

Tulipoishia>>>>>

Baada ya mimi kutoweka pale ile gari ilisogea hadi jirani kabisa kisha akashuka yuke baba aliyeyejitambulisha kwa jina la mkuti kule ofisini kwa baba
JAMANI YULE KIJANA YUPO WAPI NAMHITAJI ILI NIKAMPELEKEE BABA AKE MAITI YA MWANAE MAANA ANANILETEA DHARAU AMBAZO HATA SIZIELEWI(laiti angejua jinsi alivokuwa anawaboa hawa wafanyakazi wake ambao aliwapa ile kazi hata asingethubutu kuongea yale ambayo anayaongea kutoka mdomoni mwake mda huu
Jamani hivi sinawauliza nyinyi au siongei na nyinyi mimi tayari nimeshakuwa chizi au. Licha ya yeye kuongea maneno mengi mfululizo lakini hakuna aliyeweza kunyanyua mdomo wake ili atoe angalau hata jibu maana wote pale walikuwa wanaugulia maumivu ambayo wameachiwa kama zawadi na bon a.k.a ninja halafu yeye anawaletea nyeusi. Mmoja uvumilivu ulimshinda akaamua kupwayuka tuu
<<<<mzee kama uliona kazi sio lazima sana kuifanya ni bora ungeniacha niendelee kusafisha tuu mitaro kule ulikonikuta sio kuanza kuagiziana watu ili watufanye vilema tena bila hata faida hata ya mia mbovu, sihitaji niongee sana cha kufanya nipe tuu changu kwa maana umenisumbua tuu na hakuna nilichokipata

Boss wao baada ya kumsikiliza sana akaona huyu tayari asahaanza kuwa kichaa au kachanganyikiwa na maisha hadi anapwayuka maneno kama haya.
Aisee nimekusikiliza sana lakini hata sijakuelewa kwa lolote labda saizi hapa naomba kujua unamaana gan kuongea maneno kama hayo ambayo unayaongea. Baada ya kuongea hivo akamgeukia mwingine lakini wote sura zao zilikuwa zimekunjamana mbaya hadi boss akaanza kujiuliza maswali inamaana hawa watu wameamua kumnunia, ila bado akajiuliza inamaana ile pesa aliyowapa haijatosha chochote au ndio mbongo huwaga hawezi kulizika akapepesa macho huku na kule ili amwone yule ambae alimkabidhi ile briefcase yenye hela za kuwapa wenzake lakini hakumwona, akaanza kutembea tembea kidogo kwa mbele aliweza kuna mtu amelala chini kama amekufa vile lakini aliposogea hadi jirani aliweza kugundua kuwa bado anahema akajaribu kumsogelea jirani nakumtikisa ili aone kama anaamka, kwanza akashtuka kuonandio yule ambaye alimkabidhi ile briefcase yenye pesa zile. Lakini akabaki na maswali inakuwaje hadi yupo katika hali hii. Alijaribu kumwamsha ili hata mawili tuu lakin hakuamka, hapo boss andio akajua kwamba huyu kazimia lakini bado hajajua ni kwasababu gani hadi amezimia pia akawa anajiuliza mbona na wale wengine wapo katika hali ile
Akiwa anaendelea kujiuliza akageuka nyuma kuangalia vifaa vyake kama vipo sahihi bado kwanza aliangalia lile gari ambalo walikuja nalo akaona vioo vya upande wote vina vumbi la hatari sana kana kwamba hata kama ndani kuna kitu huwezi kuchungulia na kuona chochote kidogo nae achanganyikiwe

_____bon_____
Muda wote baadaya kumaliza kazi ya kuwatuliza wale wafanyakazi wa mkuti niliingia ndani na kufungua ile briefcase kisha nikaanza kuhesabia pesa ambazo zilikuwa mle ndani ya brifcas nilihesabu huku masaa yakiendelea kwenda ila nikakumbuka baba sio mda mrefu sana anaweza akarudi sasa akifika hawa bado wapo hapa nje lazima waanze kumsumbua na mimi sitaki hata mtu mmoja ajue kuwa bon ni nani katika upande wa mkono, nilichokifanya ni kupiga simu kwa baba na kumwambia leo itabidi kidogo achelewe kurudi hapa nyumbani kisha nikamwelekeza ni kwanini namwambia hivo,,. Baba nae alinielewa kwa haraka kisha akakata simu nakuniambia atakapo kuwa anarudi atanambia kupitia simu kisha simu ikakatwa

Huku nje baada ya kukaa kwa mda mrefu kumbe ni kweli walikuwa wanamngoja baba ili wajue siri ya hili eneo kumbe hakuna siri yoyote ile isipokuwa tuu wameingia kwenye mikono mibaya na kujikuta wakikunjwa kama chapati inaandaliwa kunywewa na supu

Walikaa sana masaa yalienda hadi ikafika usiku wa saa nne hivi wakajisemea hapa hakuna mtu kutoka hadi tujue hatima ya huyu mzee
Ila mmoja waoa akasema>kinachomchelewe nini mbona sijawahi kuona mzee akiwa ananajaribu hata kunywa au kwenye sehemu za starehe sijawahi kumwona
    Ivi kuna binadamu ambaye unaweza ukakariri tabia yake kwa jumla we kaa hapo hadi arudi ili na sisi tupate chetu sawa chogo
  Kudadeki tutazinguana hata kama ni usiku tena maeneo ya watu nani chogo tabia kama una*****

Wewe nikaushie huko hasira nyingi halafu hujiwezi mamaza mengine bhna

Halafu nyie acheni uboya huo(kilisikika kibezi kikitokea upande mwingine wote waliogopa kumbe alikuwa ni mwenzao) nae baada ya kuona wameogopa na kutulia akacheka na kuwaambia mnajifanya mnachimbana kumbe wote manyoro tuu shit

____kwa bashir ___mda wa saa mbili kama nusu tunamwona bashir akiwa anatoka kwa asha wpangaji wenzake wakamwona kisha wakaanza kucheka baada ya kuona anajinyoosha kama alilala juzi vile na miayo mingi kweli ila aaaaaamh kama anataka kummeza mtu vile

Hahahahahaaaaaa bashir kichaa lao mbona upo hasso hivo vipi tena ulikuwa na mtanange au (alikuwa ni rafiki yake mmoja kwa jina la john
Licha ya kuongeleshwa hayo maneno mengi lakini bashir hata hakujibu chochote maana kwanza alikuwa akachoka sana isitoshe alikuwa na njaa sana mana toka azimishwe mchana hajaamka hadi saizi ndio anakurupuka
Alienda moja kwa moja hadi kwenye chumba akitegemea atamkuta mke wake lakini chaajabu aliona hata taa imezimwa kuonesha dhahiri kwamba humu ndani hakuna mtu kwa wakati huu. Aliingia ndani na kuwasha taa yake lakin bado hakuona mtu ila alishangazwa baada ya kuangaza mle ndani aligundua kuwa kuna baadhi ya mabegi hayapo mle ndani. Alianza kama kichaa au kapandwa na mapepo doriii, dorii hadi wapangaji wengine wakawa wanajiuiza inamaana dori bado yupo tuu
Kumbe mke wa bashir aliitwa dori na inaonyesha dori ameondoka kaenda wapi haieleweki
Bashir akabaki mdogo zaidi basi hakuwa na njia nyingine aliamua kuchukua pesa yake na kwenda kwa mama ntilie ili akapate chakula alale ili aione kesho

____bon__nikiwa nimekaa tuu mle ndani meseji iliingia kwenye simu yangu nilipotazama niligundua kuwa ni baba., nilinyata hadi kwenye geti kumbe nae alikuwa kabana kwenye maua ambayo yalikuwa jilani na geti nilipofungua tuu geti mara moja nae akaingia ndani kisha tukafunga geti tukala la kisha mimi nilienda kulala na kumwacha baba pale sebuleni
Na huku nje wale waliopanga kukutana na baba bado tuu walikuwa wakingoja huku wakiwa na imani kwamba bado hajarudi na ndani ya nyumba nipo mimi tuu pekeyangu

Wakiwa bado wanazunguka nyumba yetu mara wakahisi kama kuna kitu kimepita tena kasi hadi kinaacha upepo wote walistuka na kuwa makini sana ili kukiangalia kama kitapita tena lakini hakikupita tena.
Ni kama saa sita usiku yule aliyekabidhiwa hela na boss ndio alikuwa anazinduka akiwa na maumivu sana upande wake wa mgongo mana ndio ile ngumi ilikokita. Alianza kujinyoosha kwa kupiga kelele kama mtu anatapika vile na kulia humohumo hadi wale wenzake walishtuka ila wakagundua kuwa ni mwenzao ndio anaamka walimfata na kumshika, lakini ile kumgusa tu-----itaendeleaaaaa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni