WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 16
Tulipoishia>>>>
Bashir baada ya kugonga mlango na kuona hafungiliwi aliamua kuusukuma kwa nguvu ili aingie ndani kumfunza adabu huyo asha ambae yeye mara nyingi ni mshabiki kipindi kama bashir akiwa kakutana na majanga hasa ikitokea amepigwa na mtu fulan
Bashir alitumia nguvu hadi alifanikiwa kufungua ulemlango lakini alipoingia ndani kabla hajaweza kuona chochote alipigwa na kitu kizito kichwani kwake kilicho mpelekea hali ya kuweweseka na kuanguka chini puuuuuu kama mzigo kisha asha akaanza kushangilia kuwa ameweza kujitetea na mbaya wake baada ya hapo asha alitimuka na kutoka nje hadi hadi kwa rafiki yake amina hata kama walipigana ila bado utani kwao ulikuwa ni wa damu kabisa
Shogaangu nifungulie mlango basi
Jiheshimu wewe umefumaniwa au inakuwaje mbona upo haraka hivo
Ahaa we acha tuu nifungulie kwani tuongee bhana,. Usinizingue hebu ngoja kwan nifanye yangu ndio nafungua kaa hapohapo kama mlinzi sawa., daha kwakuwa ni kwako nakaa ila usinzingue., asha hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumngoja tuu amina amfungulie mlango wake
Mlango ulifunguliwa amina akaingia ndani huku akiwa kama hajiamini hivi,.. mana bada ya kuingia tuu ndani aliufunga mlango tena kwa ndani kisha akaanza kumwelezea
Ivi wewe leo unanini wadudu wako leo inaonekana umewapa maji ya moto haya niambie kinachokukimbiza namna hii nini
Shogaangu we acha tuu bashir alikuja akangonga mlango wangu sikufungua maaana nlishajua kabisa anataka anipe kipigo
Basi akalazimisha had amefungua___alieleza maelezo yote kisha wakacheka sana kwa maana asha alivofanya alionekana kama shujaa sana kwa kumkomoa bashir licha ya kuwa amezimia wao walishajua ataamka tuu.,>>>>
>>>>ilipofika asubuhi nyumbani mimi na baba tulifanya utaratibu wote kisha baba akaelekea kazini kwake hukuakiniacha tuu pale nyumbani sikukaa sana nikaondoka na kwenda kwa joel ambae nilipotezana kitambo kidogo
Ngo ngo ngo hodiiiii
Hodiiii wenye wenye nyumba
///mmmmh hii mbona kama sauti ya bon hivi ngoja nikacheki kwani,. Alikuwa akiongea vile joel mda ule yupo na babaake.
Joel alisimama na kuja hadi mlangoni ambapo hakuamini kukutana live na uso wa beni maaana ni miezi mingi sasa imepita tangu nipotee na kutangazwa kwenye baadhi ya vituo vya redio lakini bado sikupatikana
Dahaa babaaaaa ni bon kweli aisee daah nambie mwanangu mbona adimu sana ulipotelea wapi mana kitambo kinoma
Dah mdau mi nipo mbona sema mambo ya hapa na pale tuu ndiyo yanafanya hadi hatuonani nilimjibu vile huku nikijua kabisa hata weza kuridhika kabisa na hili jibu. Kisha akaendelea kuongea
Bon unazingua mishe za hapa na pale huku tangu skuli watu tulikutafuta kinoma mahafali yenyewe ulisepa hukuonekana, au ulipata mishe kabla hata hujapata cheti cha umeme?
Usijali ntakutonya tuu ngoja nikamcheki mshua si yupo humo ndani au
Yah yupo ndani((((tuliingia ndani huku tukiwa bado tunaongea mambo meng tuu kisha nikafika na kumsalimia baba yale lakini nae alionyesha anashauku ya kujua wapi ambako nilipotelea kwa mda wa karibia mwaka mzima sijaonekana hadi wananitafuta bila mafanikio,. Lakini wote niliwaambia ni stori ndefu sana
Tukiwa tunaendelea kupiga stori pale kwa akina joel mara gafla tuu nilipitiwa na usingizi na kuanza kuota nyumbani kuna greda na d6 yapo yanavunja nyumba. Hii ndoto ilinishtua sana hadi nikajikuta nikinyanyuka pale kwenye kiti huku nimechoka sana
We bon vipi mbona kama hatupo wote hapa unasinzia ndani ya dakika tano na kushituka kama ulilala jana vipi bhana kuna tatizo au(aliuliza hivi babaake wa joel lakini sikujibu kitu nikasimama na kuwaaga kuwa mi naenda wote hawakuweza kuelewa ni nini maana ya hili jambo lakini ukweli wote ulikuwa ndani ya moyo wangu
Samahani mambo yakiwa vizuri badae nakuja hata kukesha tuu ila kwa saizi naomba niende nyumbani. Sikuhitaji ruhusa nikafungua mlango na kuondoka ili nikaone nyumbani kupo katika hali gani. nilipiga hatua za haraka haraka sana kwa mda mfupi tuu tayari nikawa nimeshafika nyumbani.
Nilipofika nyumbani nilishangaa kuona kuna magari ya wide road yapo pale huku pembeni kuna greda moja na d6 moja kwa mbaaaali nikaona kile kigari cha kushindilia nacho kikija usawa wa pale nyumbani
Sikutaka kubaki kimya nikaamua kuuliza
ETI SAMAHANI HIVI VITU VINAELEKEA WAPI
Aliyekuwa jirani akanijibu vimesha fika
Nikamuuliza tena inamaana hii nyumba inavunjwa nae akanijibu ndio tuliagizwa na boss
Mara akaja mzee mmoja na briefcase kisha akamkabidhi mmoja wao na kuwaamuru kuwa huyu kijana mwangamizeni kwa haraka sana inavowezekana pale pale wote walinigeukia na huku wengine wakiwa na sepetu a.k.a spedi nyie mnaita na kuanza kunifuata nazo nikaona namna yakufanya hapa ni kukimbia tuu na sio njia nyingine
Baada ya kuona upenyo nilitoka spidi kali kama upepo wote pale walibaki tuu wakishangaa wasijue nimeenda wapi wakiwa wametulia bado wanafikiria nitakuwa nimeenda wapi ili wanifuate watimize kauli ya mkubwa wao
Mara ukaja upepo mkali sana eneo lote lilikuwa ni rangi ya vumbi tuu hii ni style ambayo niliisoma katika kile kitabu kidogo ambacho niliachiwa na mama ninapoagana nae mara ya mwisho kule kwenye lile jumba
Baada ya upepo kuvuma wengi walianza kujiziba usoni kuzuia vumbi
Hadi yule aliyepokea ile briefcase yenye hela alijisahau ile anageuka aangalie zile hela ile briefcase ndo kwanza akaona inazamia kwenye upande wa pili wa paa la nyumba hakuweza kuamini akataka apwayuke kwamba watu waingie mle ndani lakini kabla hajaongea chochote alitulizwa na ngumi yenye uzito kama tufe kisha akatua chini puu akiwa hana hata fahamu kitendo kile wengine nao walikiona baada ya hapo wakamwona ninja akiwa katokea upande ambao upepo ulikuwa umetokea hapohapo wote waklidamka na kuanza kusogelea silaha zao ambazo ni sepetu mapanga wenye spana walichukua spana zao na kujipanga ili wapambane nami sikakawia nilitoka na mwendo wa kasi huku nikiruka juu na kuzunguka nikaachia mateke kwa watu watatu mfululizo ambao walienda kuwasukuma na wenzao kama watatu tena. Baada ya hapo nikasimama kati ili mtanange uanze na hii siku nilishawapania wakijifanya wabishi sana nachinja mmoja wao ili uwafundishe na wengine.
Walianza kujongea huku wakizishika silaha zao kiufundi lakini mimi nilitoa tuu nyororo moja yenye goroli kibao na kuanza kucheza nayo, kila ambaye ilimpata alikuwa ni lazima akajifiche kwenye magari ya kazi niliwafunza wote hadi wote tayari wakawa wapo hoi kisha nikaongea kwa sauti fulani ya bezi la kulazimisha
ONDOENI UCHAFU WENU TENA NISIWAONE KABISA KATIKA HILI ENEO kisha nilimshika mmoja na kumrusha kule
Katika hawa wote hakuna aliyeweza kugundua kama ni mimi mtoto wa MPL ndio ambaye nimefanya hivi maana wote waliamini mimi nilikimbia mapema kabla ya zari kumbe niliwapangilia.
Wakiwa wanaanda magari yao ili waondoke wakampe taarifa boss wao, mara waliona kwa mbali kuna gari linakuja, kwakuwa hata mimi hilo gari sikulitambua sikupoteza mda nilichumpa juu sana na kupotelea kusiko eleweka lakini ndio ilikuwa ndo njia ya mimi kuondoka pale------itaendeleaaaaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni