WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 15
Tulipoishia>>>>
------baada ya kuingia duka lililokuwa jiran nae aliweza kujieleza ili apatiwe msaada wa kupata simu ili apige nyumbani
Nani akuamini wewe na wakati unajua kabisa umeniona pale duka la simu ukanipiga kibega tena kwa maksudi na yule dada anakuambia ila ukajifanya unaleta maringo kana kwamba hela zako ndio zinazosumbua sana watu wote (aliongea vile yule dada ambaea alikuwa katika m pesa fulani kule mjini
Dadaangu nisamehe na mimi ni binadamu tuu kama ni simu nitalipa tuu ila naomba msaada huo nisaidie
Yaani hapa enock alikuwa mdogo ghafla tuu mana yeye hakuweza kuriri sura ya mtu ambae amemharibia simu yake. Baada ya kuomboleza sana ndio alipewa msaada wa kuongea na simu alimpigia baba ake nyumbani na kumwambia amevamiwa na kuporwa hela zote lakini simu tuu ndio imeachwa, kwakuwa alikuwa ni mtoto wa pekee kwa huyu mzee mda huohuo tuu ziliingia hela mpesa kwa namba ya yule dada kisha wakaitoa, enock alishukuru sana kwakuwa alisaidiwa, baada ya kuhesabu hela ambazo alikuwa akihitaji alichukuwa kiasi kama cha laki tano na kumkabidhi huyu dada ambae amemsaidia, kisha akasimamisha bodaboda ambayo alitaka imfikishe hadi eneo ambalo lilikuwa na gari yake, mambo yalipokamilika akapanda gari na kupitia sheli ili ajaze mafuta kisha akarudi nyumbani salama kabisa
_____kwa baba______
Wiki moja liliisha na wafanyakazi wote walikutana tena katika ofisi zao na kuendelea na kazi zao kama kawaida. Ilipita muda kama wa mwezi mmoja hivi walitembelewa na baba mmoja ambae alijitambulisha kwa jina la Mkuti, akadai yeye ni mwekezaji hivo alikuwa anatafuta eneo ambalo ni zuri ili aweze kufanyia shughuli yake. Lakini katika mapendekezo yake akapendekeza eneo ambalo ni karibia na nyumbani. Baba baada ya kusikia vile akamwambia kwa hilo eneo hata haitawezekana kabisa kwa sababu lile eneo ni dogo sana na pia lilishakuwa na mipango ambayo tayari imeshaanza kufanyiwa utekelezaji, kajaribu sehemu nyingine
Lakini yule mgeni kwa jina la mkuti akaonyesha kama hajaelewa kabisa kuhusu kuzuiliwa na maelezo hayo alichowajibu ni kwamba ataenda kuongea na watu wa serikali ili wamuangalizie kuhusu hilo eneo. Baada ya kuongea vile akaondoka hata hakuhitaji kuanza kukaa tena pale wasije wakaendelea kumzuia zaidi
Aliondoka na kwenda kutimiza kama alivoahidi pale kwenda kuongea na wakubwa ikiwezekana hata kwa hongo ili tuu apate anachokihitaji yeye. Baada ya kuongea nao walikubaliana vizuri kabisa kisha simu ikapigwa kwa baba kumpa zile taarifa za kukatwa kipande cha eneo lake, baba hakutaka kukubaliana nao kabisa lakini kwakuwa walisha kula hongo ya pesa ndefu wakaamua kutumia comand kwamba atake asitake ni lazima tuu eneo likatwe kisha simu ikakatwa hivo
Baba alibaki akijiuliza maswali mengi sana pale ofisini lakini hakupata jibu lolote akiwa ametulia simu yake ilianza kuita namba ngeni aliiangalia kwa kuwa alikuwa na mawazo sana akataka aikate lakini roho ikasita akaipokea
Akiwa amepokea akabaki ameduwaa asiamin kituanachokisikia kwenye simu ile,
Nini wewe bon uko wapi kwa sasa, ahaa basi njoo hadi ofisini kwangu kabisa, ya nipo ofisini ndiyo, ok nakungoja ukifika gonga tuu sekretari akakuleta hadi ndani
----duh bon kaondokaje kule tutajua tuu----
Baba akiwa amekaa ofisini kwake mara mlango ukagongwa
Yes karibu
Waooooooh alinyanyuka na kunikumbatia kwa furaha mana ni kama mwaka umeisha tangu tupotezane pale nyumbani. Ulikuwa ni mda wa furaha sana baba alisahau kama kunamtu ashamtibua mda si mrefu sana,
Baba aliondoka na mimi pale ofisini na kulekea nyumbani lakini tukiwa bado hatujafika nyumbani tupo njiani kuna gari lilikuja na kusimama mbele kisha akashuka jamaa mmoja ambae alionyesha sio mtu mwema hata kidogo. Alikuja hadi kwenye kioo cha gari ambalo sisi tupokisha akasema kwangu wewe dogo sogea kwanza namhitaji huyo mzee kwanza ninashida nae. Lakini nikaleta ubishi kidogo kwa kumwuliza kwani kama unamfahamu na unashidanae si bora ingamfata kwa busara tuu sio kumzuia hata asiende mbele,
Dogo acha shobo nimekwambia ninashida na huyo mzee wewe mbona shobo nyingi au wewe ndio powa shuka wewe basi ili nikupe shida yangu ambayo nahitaji huyu mzee aifanye.
Baada ya yeye kusema vile nikamwambia ok nashuka ili niikamilishe hiyo shida yako.
Niliufungua mlango wa gari na kushuka kwenye gari nae akanivutia hadi mbele ya gari ya gari lake baada ya kufika kule akasema sasa nakupa dawa ya shobo zako we siunajitia mwehu sana eeee sasa ngoja, baada ya kusema vile alikunja ngumi huku akijiandaa kunipiga tumboni, nikawa namwangalia tuu bila kuchelewa akanipiga ngumi ya kwanza ya tumbo lakini sikushtuka akapiga ya pili sikushtuka bado alitaka kupiga ya tatu niliudaka mkono wake na kuunyonga ikasikika tuu sauti (koooo) kilichofuatia hapo ni kilio. Nami sikupoteza mda nikarudi kwenye gari kisha nikarudisha nyuma kidogo na kuipisha ile gari yake hadi tunafika nyumbani. Tulifika na kufanya taratibu zote kisha tukala na kulala_____
_____katika ile nyumba ambayo anakaa bashir kulikuwa na mabishano makubwa sana ambapo bashir alikuwa kazongwa na wpangaji wote huku wakimpa vipondo tuu
Dadeq zako kwa hiyo saizi umeamua uache zile bangi zako na huyu jamaa ungeendelea kuleta shobo zako za kike angekuua wewe eti street fighter jiite hvohvo na saizi.
kantangazeeeeee kweli kila mbabe na mbabe wake. Bashir umepoa kama unasubiri upulize pola, aliongea vile asha kisha amina akamdakia ivi wewe asha mbona na wewe shobo nyingi kama umejigundua unashombo wakikunyonyoa tu kilio kama umekutana na popobawa, lione kwan
afu wewe shoga au bashir unakuwaga na promise nae mana kila siku ilaonekana kama unajisikia mbaya mno nikiongelea kumhusu kuwa wazi tuu manfongo wewe..
hheheee shoga tena unikome nini.
Hujasikia au ndo mideko. Ushuzi kweli wewe
Amina na asha walisimama na kushikana ilionyesha kwamba kila mmoja ameshindwa kuvumilia yale maneno waliyokuwa wakipeana. Hapakukalika kabisa katika hii nyumba kama kawaida ya wadada wanapopigana matusi ya nguoni ni kawaida timbwili lilitembea kwa mda wa dakika kumi kila mmoja akawa ameenda ndani kwake kwa hasira sana.
Bashir akiwa ameenda kwenye chumba cha bon akakuta mlango upo wazi alijaribu kugonga lakini hakuna aliye jibu wala kufungua mlango. Kwakuwa alikuwa na hasira sana na bon alifungua kwa tahadhali sana na kuingia ndani ambapo aliona kuna vitu vichache tuu mle ndani ilikuwa ni kitanda, godoro na mablanket na shuka zaidi ya hapo hakuna akajisemea leo huyu lazima ajute humu naondoka na kila kitu siachi hata kimoja.
Baada ya kuongea vile akagusa kitanda kwenye kona ili akikague kama kipo vizuri lakini anagusa tuu alipigwa na shoti ya umeme,kumbe ulikuwa ni mtego tuu umewekwa kwa yeyote atayefanya anataka kuingia mle ndani na kuondoka na kitu, bashir kuona vile alikata tamaa tena ya kutaka kujua zaidi akashika mlango kwa umakini akauvuta na kutoka nje, anapotoka mlango ulirudi kwa kasi sana na kumbonda hadi alienda kutulia kichwa.
HAHAHAHAHAHAHA. HAHAHA BASHIR VIPI TENA., kumbe kile kitendo kuna jamaa walikaa nje pale walikishuhudia vizuri kabisa bila chenga. Baada ya hapo bashir aliondoka kwa lengo akamfunze adabu asha ambae anamdomo sana. Alifika hadi mlangoni kwa asha na kugonga baada ya kuona hafunguliwi alisukuma mlango kwa nguvu kisha------itaendeleaaaaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni