Ijumaa, 21 Oktoba 2016

Who am i

WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 19

Tuliposhia>>>>

---baada ya kuingia kwa mganga bila hata hodi ghafla nikabadilika na kuwa kuwa ninja, niliweza kujiona kupitia kioo ambacho kilikuwa mbele yangu
Kiukweli nilikuwa natisha sana hadi mwenyewe nilijiogopa usoni hata kipande kidogo changozi hakikuwa kinaonekana ila kulikuwa na maski ambapo inangaa sana huku kwenye alama za macho kukiwa na vitobo vitatu kwa kial jicho ambapo kila kitobo kilionekana kinatoa kama miale ya rangi tofauti kijani, nyekundu na nyeupe
Ilikuwa nikigeukia upande huu tuu unawaka mwale tofauti hii hali hata mimi mwenyewe sikuweza kuielewa ila nilijali mimi ni nini kimenileta

Wakati huo mganga nae alikuwa anapiga piga kama kangoma fulani ambako kamepakwa baadhi ya rangi. Alipiga kwa mda fulani huku akiwa anaongea na baadhi ya maneno ambayo baadhiniliyasikia na mengine hata sikuweza kuyasikia na kuyaelewa lakini niligundua kuwa huyu hizi nyimbo zake ni za kushangilia kitu fulani lakin bado sikujua anakishagilia anachokishangilia ni nini
Baada ya hapo alikitupa kile kingoma chake kidogo mbali kidogo ambapo mimi nilipoangalia niliona kama ni ukuta lakini cha ajabu kilekingoma kilipitiliza na kitua upande wa pili na kwa gafla tuu pakawa na uwanja mkubwa sana

Kwa akili yangu nilishajua kwamba kuwa wadudu lazima anatumia kupiganishia kitu ambacho kinataka kushindana na yeye na ndio maana anafanya huu uchawi ili ajihadhali mapema na kitakacho tokea hapa
Baada ya hapo nikiwa nimesimama mara nikweza kuona mnyama wa ajabu sana ambae hata sikuwahi kufikilia kama ipo siku nitaweza kumwona katika macho yangu

Mnyama kwa kumwangalia alikuwa na meno yasiyopungua kama mia mbili ikiwezekana ni zaidi hata ya hayo
Alitoa sauti ambayo ilisababisha hadi tetemeko kubwa sana katika uwanja ule baada ya hapo akaanza kun fuata kwa mwendo wa maringo
Na mimi kwa haraka hata sikulaza damu niliuchomoa upanga wangu huku kwa mbali nikimwona mganga anacheka huku ameshika kitu fulani mithili ya mkia wa ngombe na kuuzungusha kwa satili ambayo yeye aliijua zaidi
Mara yule kiumbe alijizungusha baada ya kumwona upande wake wa nyuma alikuwa na mkia wenye unene kama gogo la nguzo ule mkia ulikuwa ukija kulikuwa na upepo ukivuma kam kuna ndege aina ya helkopta ipo upande wa juu yangu akili yangu iliweza kugundua kwamba huu unatakiwa unitandike
Ule mkia ukiwa jiran niliruka juu ili kuukwepa ambapo ukaenda kugonga nguzo moja ambayo ilikuwa jiran na uwanja ule na baada ya hapo ile ilivunjika na kudondoka chini hii ni kuonyesha ule mkia uzito wake na nguvu zake ni hatari tupu

___upande wa pili baba tayari alikuwa amesha rud kutoka kazini kwake jioni akafika na kuanza taratibu zake huku akiita boniiiiiiiiiiiiiiiii, boniiiiii uko wapi mbona sikuoni

Na baadaya kuona kimya aliamua kuchukua simu yake na kunipigia iliita kwa mda mrefu sana kisha akapokea majibu
MTEJA UNAEMPIGIA HAPOKE_____
Hakutaka kusikiliza sana akakaa simu na kisha akaendelea kufanya mambo yake mengine, kwa wakati huo ilikuwa ni saa kumi na mbili za jion
Baada ya kufanya kila kitu kilicho kuwa katika ratiba zake
Ulikuwa mda kamili wa yeye kula ili aweze kulala au kujisomea vitabu vyake
Muda wote huo alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana. Kuhusu mwanae bon ameenda wapi hadi mda huu aliangaliaa saa yake ilimwonesha ni saa mbili karibia na nusu ila akahisi labda nitakuwa nimeenda kwa joel kwa maana ndio mahali ambako mara nyingi napenda sana kwenda kutokana na kwamba tulikuwa na urafiki wa kitambo sana
Baba alikuwa kisha akafunga safari ya kwenda kwa akina joel, lakini akakumbuka kuwa pale nje palikuwa na vifaa vya utengenezaji wa barabara, aliamua kuzungukia ili akaangalie kama wameishia wapi katika hiyo kazi yao ya kufanya uwekezaji kwenye nyumba ya mtu.
Baada ya kufika kule nyuma ya nyumba yake aliona hakuna kitu chochote
Alicheka sana huku akijisemea MLIJUA KUNA MAJINI NA BORA MMEONDOKA WENYEWE ASANTE MUNGU KWA UAMUZI ULIOUTOA.alifurahi sana  kisha ndio akashika njia ya kwenda kwa akina joel alitembea kwa mda mfupi tuu na baada ya dakika kama tano na sekunde tayari alikuwa tayari ameshatia mguu pale, ambapo alipokelewa na baba ake na joel
Ooooooh karibu baba bon
- ah asante nimekaribia kwema lakini
Hapa kwetu kwema kabisa sijui utokako
- nako nadhani kutakuwa ni kwema hivo hivo
Haya karibu ndani ila mbona umetembea pekeyako na bon umemwacha wapi tena
Baba baada ya kusikia hivi akajua kwamba mwanae bon na hapa hayupo hapo ndio mawazo yaliongezeka zaidi akazidi kujiuliza kichwani mwake maswali mengi zaidi na asipate jibu lolote, ila kwa safari hii alijifariji kuwa
Aaaah mawazo ya nini wakati sio mtoto mdogo___akiw anaendelea kufikiria bado baba joel akauliza tena lile swali lake +=bon umemwacha wapi pekeyake (

Hivi unavoniona nimekuja hapa huku nikijua kuwa bon nitamkuta hapa lakini kumbe na hapa hayupo tena

Duuuh hili tatizo sasa kwahiyo unaenda ktnagza au unaacha tuu(aliuliza baba joel
Safari hata sihangaiki kutangaza inamaana bon bado mtoto mdogo namna hiyo kila siku niwe namtangaza tuu si hata vituo badae vitanichoka maana vinaona kila siku matangazo yangu tuu kwenye redio tena kuhusu mtoto ambaye akili zake ziko sawa kabisa, huwezi jua ni kwanini ameondoka pengine akirudi atasema alikoenda hebu tusubilie tuu (aliongea baba

Kisha baba joel akajibu sawa kuonyesha amekubaliana na mwazo ya baba
Jamani majirani basi mimi niwakimbie au mnasemaje(alikuwa baba akiaga na kusimama lakini baba joel akasema ngoja nikusindikize hadi kwenu maana wewe upo wewe tuu kila siku
Sikumoja moja hahahahahahhaaaa. Walicheka pamoja kisha wakaanza safari ya kwenda nyumbani walifika hadi nyumbani ambapo baba joel alifika moja kwa moja pale kwenye meza ya baba ambayo anatumia kujisomea vitabu vyake,.
   Jirani naweza kuangalia chochote hapa au marufuku kugusa kitu
Ahaa kwenye hiyo meza wewe angalia tuu ikiwezekana kaa kabisa hadi kesho hadi utakapo ridhika kuangalia

Baba joel baadaya kuruhusiwa kuangalia chochote kadiri alivoomba alikaa na kuanza kupitia vitabu vile lakini akiwa anaendelea kutazama kuna karatasi fulani aliona maneno yanayoishia BY NON, kwa haraka akaliwahi na kutaka ajue kuna nini ndani yake alipofungua alikutana na ujumbe ambao ulimfanya amwite baba ili wasome pamoja. Waliusoma ila wakabaki wanajiuliza mama yake alimwona wapi

Tukirudi kwa mganga tunamwona bon amelala chini akiwa hana nguvu kisha-----itaendeleaaaaa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni