Soma kupasha macho
Gangstar noma
By: benchrys
29
........mtoto fulani alikuwa akilia sana kuomba msaada nilipomtazama vizuri ndipo nikagundua aling'atwa na mbwa basi nilimchukua haraka na kumpeleka hospital kwa usafiri wa ile pikipiki aina ya boxer nilifika hospital nikakutana na manesi kadhaa niliwaambia tatizo la yule mtoto walimpokea kisha wakaingia nae ndani kuendelea na wanayoyajua wao lakini wakiwa wanaingia ndani niliweza kumwona moja ya nesi katika wale watatu akiwa ameniangalia kama ananitilia mashaka vile sikutaka kimjaji sana nae aliondoka akaingia ndani
******eti nesi ivi huyu sio yule mvulana ambaye alikuwa anatafutwa kipindi kama miezi mitatu ivi au nimemfananisha..alisema yule nesi ambaye alikuwa akinitazama anapoingia ndani kule, nesi mwenzie akajibu kuwa tumtibu kwanza huyu mtoto halafu ndio tujue..tutamtajia hela kubwa kama ni mwanae atalipa lakini kama sio mwanae najua hawezi lipa......
Basi baada ya wale manesi kukubaliana vile walimhudumia yule mtoto vizuri kisha wakatoka nae tena hadi mahali nilipokuwepo nikawauliza ni shi ngapi huyu nesi aliyeniletea akasems "kutokana na kovu kuwa kubwa sana imetulazimu tuongezee na vitu vingine ili zoezi likamilike vizuri kwahiyo utalipa elfu sitini tu akatulia huku akiniangalia usoni na mimi wakati huo nikawa kimya kidogo lakini nikakumbuka yule nesi mwenzie aliyekuwa akiniangalia pale mwanzo, akili yangu ilikurupuka na kusema huu utakuwa mtego nikasimama kisha nikatoa wallet katika mfuko wangu wa suruali na kuhesabia zile elfu sitini kisha nikawakabidhi na kujifanya nawashukuru niliwaongezea elfu kumi nyingine kwa kigezo iwasaidie na wakati lengo langu kukwepa huo mtego. Basi nikampokea yule mtoto na kuondoka nae hadi pale nilipomkuta mwanzo nilitazama nyumba ya jirani na pale nilipoiona nikaifuata nikagonga lile geti mwanzo sikujibiwa lakini baada ya kugonga sana ndipo akatoka jamaa mmoja huku akionyesha ni mtu ambae hata si mwema kwa kumwangalia
""oya huyo mtoto umetoka nae wapi au we ni mwizi wa watoto wa watu"aliniuliza hivo. Nilimjibu mi sio kiujumla sawa tena uwe na busara hata kwa dakika moja tu ivi mtoto wenu hadi anang'atwa na mbwa nyie mpo tuu ndani mi nikajua labda ni mtoto wa mbali kumbe ni wako hadi naingia gharama kisa huruma kwa watoto ok nimelipa hela huko inarudije hiyo labda hakafu unanipokea kwa matusi hivi. Nilitulia kisha nikaendelea bro heshima na busara ni vitu muhimu sana mwanao huyo hapo nilimshusha yule mtoto na kumkabidhi....alimpokea kisha akaniuliza "ok umewalipa shi ngapi lakini kumtajia kile kiwango nikaona atahisi mimi ni mwongo nilitoa tena wallet kisha nikatoa kirisiti fulani kidogo ambacho nilipewa kule hospital nikamkabidhi alikipokea kisha akakishangaa kwa mda kisha akasema sawa ngoja aliingia ndani kisha akatoka na hela mkononi akahesabu zile sitini elfu akanipa kisha akaniongezea kama 30 elfu hivi na kusema kumbe dogo huna roho mbaya daah nisamehe sana aisee nikamjibu hata usijali ila mimi nilikuwa napita tu kwaheli kakaangu, tuliagana kisha mimi nikaondoka lakini nilipofika nje nilishangaa kuons pikipiki yangu inakokotwa na watu wawili nikawaita kwa sauti kubwa wakajifanya kama hawasikii hivi niliwafuata wote walipogundua kuwa nawafuata walisimamisha ile pikipiki tena kwa kushusha stend kabisa nilipofika jirani nao nikawauliza kiupole kama boya fulani "jamani mbona mnaondoka na pikipiki yangu mmoja alicheka kwa dharau tena na sauti kubwa moyoni nikajisemea hizi zarau sasa nikawapisha ili kuifuata pikipiki ile lakini mmoja alinizuia kwa mkono wake, dogo kuchukua hii boda ni ndoto sawa nimtazama kwa hasira kisha na mimi nikacheka kama alivocheka yeye mwanzo, baada ya kuona vile alipata hasira kisha alinisogelea na kutaka kurusha ngumi lakini niliudaka ule mkono na kwakuwa nilikuwa na hasira niliuvunja kabisa alipiga kelele kama mtoto hivi nilimwacha chini kisha nikataka tena kufuata pikipiki lakini nilizuiliwa tena na yule mwenzie huyu nae alitaka anipige teke lakini niliruka beki ilikukwepa lile teke akabaki tuu anashangaa lakini hakukata tamaa akaanza kunifuata kumbe hakujua mimi ni mtu wa aina gani, nilikimbia Kisha nikafunga breki ya gafla na kumsindikiza mbele na bonge la teke zito huku nikimbetua alitua chini kama furushi hivi hadi nikahisi kumwonea huruma..... Nikiwa naelekea kwenye pikpik yangu nikasikia sauti ya watu wakipiga makofi kushangilia nilipogeuka ndipo nikaona watu wengi wakiwa wamesimama huku wakiendelea kuniangalia baada ya hapo nikasikia wakisema... bora umewafunzaaaaaa wajinga haoooooo kila siku wanachukua tuu vitu vyetu halafu tukiwafuata tunapigwa...waliongea hivo wakaanza kuwazomea mimi nikahisi hapa inaweza kuwa zari bure kama wakija polisi lile eneo niliifuata pikipiki yangu naliipanda na kuondoka kwa spidi kali sana hadi nilipoona nimepotelea mbali ndipo nilipunguza mwendo wa pikipiki ile nilitembea taratibu hadi nafika kwa merry kwenda kwa akina naomi hata sikukumbuka tena nilipofika nyumbani nilizichukua zile tisini na kuziunganisha na nyingine kisha nikamfuata merry alikuwa kakaa tuu huku akichezea simu yake, nilimsalimia kisha nikaelekea bafuni ili nitoe uchovu baada ya hapo nilifuata chakula na kukila kwa fujo sana nilipomaliza nikajifanya eti namwuliza kama amekula aliniangalia kisha akacheka kidogo '' ivi mimi na wewe nani amuulize mwenzie kama amekula aliniuliza hivo nikamwambia mimi kwasababu nimemaliza msosi wote mana nilikuwa na njaa hapa. Hakuongea kitu kisha akavuta pumzi na kuuliza ivi wale walionipulizia sumu wapo wapi au walikimbia nilicheka kisha nikamwambia haaa wale wote tayari ni vilema wewe usijawawazie hata kidogo walishashika adabu zao wale wote tulicheka.....
Pale nilipoondoka ule mda na pikipiki yangu ambapo niliacha watu wakiwa wanashangilia sana lilipita kama saa moja waliingia polisi huku wakiwa na gari zao maarufu kama tenga kisha wakadhikwa baadhi ya watu walioweza kukimbia walikimbia lakini wabovu walikamatwa na kusukumiwa kwenye tenga kisha safari ilianza na muda mfupi wakawa wameshafika kituoni...
Afande mmoja akasema yaani nyie mnashangilia ugomvi wa kijinga huo watu wakiuana kwenu ndio raha haya mnaweza kunieleza palitokea nini pale mama mmoja akajibu ndio afande akasema ok toa maelezo yule mama alinza hawapa wawili wali....kabla hajamaliza kuongea kuna mtu aliingia....itaendeleaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni