Ijumaa, 23 Septemba 2016

De 32

Gangstar noma
By: benchrys
32

.........kwa haraka nilifunga mlango huku anna akiwa mle ndani kisha nilitoka huku nikiwa pekeyangu wale polisi na watu wa kawaida walishangaa kisha mmoja wao ambae alionekana kuwa ndio kiongozi wa wote akasema hapa tumepoteza tuu mda wetu kuja hapa hicho kiboya ndio hiki au akanyanyua simu yake na kupiga sehemu
""""hallow boss mambo gan haya sasa kutuleta katika ujinga huu ujue tumepoteza mda bure tuu hapa......ok huyo uliyemkuta mkamate kisha njoo nae hadi hapa kituoni""""
Kwakuwa alitumia cm ya ile isiyo na siri niliweza kusikia kila kitu walichokiongea. Yule mkuu wao pale akaita polisi watatu huku akiwaamrisha hebu shikeni kinyago hicho kikatoe maelezo kule.....kabla hata mmoja hajatoka kunifata nikasema hapa hamuondoki na mtu safarj njema..baada ya mimi kusema hivo yule akacheka kwa sauti kubwa hahahahahahaha niliweza kugundua kuwa hizi ni dharau nilimkazia macho hadi alitulia kucheka kisha akawaambia tena ivi nyie sinimesema mkamateni huyo,, aliongea vile kwa kufoka sana hadi waliogopa na kuanza kunifata. Walijichagua polisi watatu kisha wakawa wananisogelea lakini walichoshangaa ni kuona nimeganda tuu kama siwaoni, polisi mmoja akasogea zaidi ili anikamate lakini akiwa hata hajatulia alipata teke lenye heshima kwenye kifua chake hadi aliwaangusha na wenzie kama wanne hivi, yule mkubwa wao nae akabaki katumbua macho hapo ndipo wakajipanga wengi ili wanizoe kwa pamoja nilipoona na kugundua wanachotaka kufanya niliondoka mbio kwa spidi kali ambapo nilipofika mbele niliruka ukuta wa fensi ile nikawa tayari nipo nje ya nyumba ile, hapo kundi lote walijipanga vizuri iliwanizunguke na mimi nilipotoka nje sikuzubaa kulikuwa na mfuko fulan nyie mnaita rambo....nilichukua nikajaza mchanga wa kutosha tuu huku nikiwa nawangoja wajitokeze. Nilikaa kidogo akatokea mmoja nilidunda kwenye ukuta na kukita kwenye tumbo lake alianguka chini pale na kubaki akijisugua tuu tumbo lake kama anahara(sorry) kisha nikazungukia kona nyingine huko niliweza kuwaona wakiwa kama kumi na tano vile nikajisemea hapo afadhali kisha nikaruka juu huku nikiichana ile rambo na kuirusha juu zaidi kisha nikafumba macho nilipotua chini nikaanza kukimbia kuelekea katika pori moja hivi nao bila kuchelewa wakafuata njia zile ambako mimi napita. Baada ya kuona wapo nyuma yangu niliruka katika gogo fulani lilikuwa mbele yangu, nao walijaribu kuruka ila jitihada zao zilifeli kabisa wakaamua kuzunguka maana lile gogo lilikuwa kubwa sana baada ya kuzunguka walijua kazi itakayo fuata ni kumtafuta ben ambae ni mimi lakini cha kushangaza ben hawakumwona badala yake walikutana ninja akiwa na upanga wake mkononi huku ukiwa unang'aa, yule mkuu wao baada ya kuona vile alipiga magoti huku akilia kama mtoto pale chini maana anafahamu ninja ni kiumbe cha hatari sana hapa ulimwenguni kwahiyo alihisi kuzimu inamwita....lakini mimi sikumsikiliza nilichumpa juu na kuudaka mti mmoja huku nikijiandaa kumtulia kichwani lakini kama aligundua hivi alinyanyuka haraka na kuondoka spidi lakini hakujua kama amekosea njia baada ya kufika eneo fulani kuna kamba aliikanyaga ghafla akajikuta yupo juu ya mti huku kichwa kina ning'inia chini na wenzie wakiwa wanakimbia ovyo baadhi yao walijikuta wakitumbukia katika mashimo maana hawakujua chochote kuhusu msitu ule kumbe niliwapeleka makusudi ili wapate tuu mateso yale...
......katika wale watu wote walioweza kurudi ni wawili tuu ili wakatoe ushahidi kwa aliye watuma huku kabla hawaha ondoka niliwaachia ujumbe wakampe mkuu wa kituo. Bila hiana waliupokea huku wakiwa na woga saana lakini niliwaacha waondoke kwa amani huku wale wenzao wakiwa bado kwenye ile mitego na mimi nikaondoka nikiwa tayari nishakuwa kawaida maana nilijua polisi akili hawana wasije tupa bomu bure na mimi nipotelee humo haikupita mda niliingia nyumbani mida kama ya saa 11 hivi hii siku hata sikuchoka maana sikutumia nguvu yoyote kuwaadabisha wale wapuuzi
........waoooooh ben ulikuwa wapi tena kaka lao...ilikuwa ni sauti ya merry ambapo alikuwa amekaa na anna katika sofa moja na anna huku wakichezea cm yao. Sikutaka kuongea chochote kisha nikaingia ndani lakini nikiwa ndani niliitwa na merry pale sebuleni

.....nilitoka ndipo niliona wakitazama taarifa ya habari ambapo pale zile habari zilikuwa ni kama zinanihusu vile. kwa wale niliowaachia ujumbe waliufikisha na kutoa data zote kuhusu kule porini kilichowapata wenzao,,,,walikuwa wanasimulia huku wakilia tena wakionyesha wana uchungu
Mda wote huo nilikuwa bado sijakaa nilisimama tuu huku nikicheki ile taarifa ya habari""""""merry hakuweza kuendelea kutazama maana nae alijihisi kulia mana alipoa ghafla  baada ya kusikiliza ile taarifa sikushangaa mana najua kwa mwanamke ni haki yake kuwa vile

Baada kutulia kwa mda akanigeukia. Ben hao watu wahurumie tuu na sidhani kama watarudia tena...akiwa anaongea vile anna alikuwa katoa macho kama fundi saa vile sema sikujua kama mimi ndio saa au mana macho yake yote yalidokolewa usoni kwangu.
Wewe vipi mbona tunatishana geukia pembeni bhana,,,nilimwambia hivo anna kisha niliangalia pa kukaa na kukaa
Merry sorry ila bila mimi kufanya hivo anna angefanyiwa nini hata sielewi.....nikiwa naendelea kuongea simu yangu iliita niliitoa mfukoni na kuipokea ilikuwa ni namba ngeni nilipopokea tuu....itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni