Gangstar noma
By: benchrys
33
..........hallow ben nakuomba utoke nje hapa ninamazungumzo na wewe mara moja wala hatatotumia mda sana done quick ee nakungoja ben...ilisikika sauti ya kike ambayo niliisikia vyema kwenye simu ile iliyopigwa ambapo namba ilikuwa ngeni..katika ile simu kwenye yale maongezi nilimsikiliza lakini sikuweza kijibu chochote mana nilijua wazi mitego haitoi taarifa hata siku moja nilimsikiliza kisha nilikata simu, baada ya hapo niliingia chumban na kutoka huku nikiwa nimevalia zile nguo za kung fu nilizotoka nazo kwa babu kule nilifika sebuleni nilimkabidhi merry simu yangu huku nikimwambia msifungue mlango hadi niwape ruhusa mana hawa watu wanatafuta maisha ya watu
Nilitoka nje huku nikiwa makini kama watakuwa wamejificha sehem wakinivizia wasiweze kabisa, nilifungua mlango na kutoka nje merry nae akaufunga kwa ndani....
....ivi dada huyu ni nani yako halafu mbona inaonekana hii nyumba kama inachunguzwa sana pana nini hapa..lilikuwa ni swali la anna kwa merry ambapo merry alimwambia tu anna mdogo wangu ni stori ndefu sana mda ukifika nitakusimulia usijali.....huko nje.....
Baada ya mimi kutoka nje sikuweza kumwona mtu yeyote lakini nilishajua kwamba hawa wamejificha ili wanivizie ni kweli baada ya mda kidogo nilihisi mtu akija nyuma yangu kwa spidi sana nadhani lengo lake anivae tuanguke wote chini iliwenzie waje kunishika lakini ilikuwa tofauti sana. Baada ya kugundua vile nilimkadiria akiwa jirani nilidanki na kutulia nyuma yake huku yeye akiwa mbele na mimi nyuma yake alipogeuka tu alikutana na teke la shavu lililo mfanya abaki ameshika mdomo wake huku damu zikivuja mdomoni mwake, kujiokoa aliamua atoke nduki akikimbia kama kuku aliekatwa shingo hapo hapo na wale wenzie ndipo wakajitokeza wakanishika wakiwa kama watu saba huku kati nikiwa mtu mmoja. Nilikusanya nguvu za kutosha kisha niliinama kidogo niliponyanyuka idadi yao kubwa walipepesukia huko huku baadhi yao wakikanyagana vibaya kabisa mimi sikujali niliruka juu na kumuachia kila mmoja wao zawadi ya mateke ya uso huku nikitulia pembeni kidogo hapo ndipo niliwafanya kama mpira kila aliyekuwa akinisogelea nilipo ilikuwa ni mteke wenye afya lazima aupokee ili akakae pembeni na kupumzika nao baada ya kuona shughuli imekuwa nzito kwao wakajikwamua na kukimbilia walikotoka mimi nikajisemea watu mdebwedo halafu mnajitia kujua shit mbwa nyie.nilirudi zangu ndani lakini kabla sijaingia niufunge mlango vizuri niliangaza macho yangu nje niliona kundi jingine la watu wakija pale niliingia ndani na kufunga mlango haraka nao kwa kimbelembele chao waliufikia ule mlango na kuanza kugonga kwa fujo sana nikamwambia merry anipe ile remot akasema kama ni hivo tuu ngoja niwape shoo watajua tuu aliichukua ile remot kilichofuata huko nje ni sauti za vilio ndio zilizosikika kwa wale watu mlangoni pale lakini akili yangu ilishatambua kuwa wale walikuwa ni baadhi yao tuu niliingia chumbani kwangu na kubadili yale mavazi sikutaka kutokea mlangoni pale nilipita katika emergency door ambayo ilikuwa katika dari kisha unavuta kidogo bati kisha unatokea nje kabisa, kwa kutumia ile njia ndio nilitoka hadi nje nilifika katika bati niliruka kavu mbili dabo na kutua moja kwa moja njee huku nikiwa na nguo za kininja na kila silaha ambayo ni ya muhimu kwa ninja zikiwemo nyota,golori,cheni,upanga n.k nikiwa na staili ya goti moja chini huku nikiwa nimeinama nikawaza hawa leo lazima wanijue tuu nilinyanyuka pale na kuruka ukuta ili wanifuate nje kule nao bila kukosea wakazungukia nje kwa haraka huku wakiwa na hamu ya kunikamata et wamkamate ninja kweli wanandoto za mchana hawa.
...wakiwa na visu,mapanga, na silaha nyingine walitoka nje huku wakijadiliana leo hata kumuua tumuue tuu hakuna namna ya kusimamisha huu usumbufu wa hapa kitaa.....walinifuata huku baadhi wakinionyeshea mapanga na visu, wengi walivirusha visy vyao lakini vyote nilivipangua kwa mateke na mikono yangu baada ya hapo nilichomoa upanga wangu ambao mda wote niliuhifadhi tuu ila nao wale hawakuonyesha woga wowote walinifuata kwa moyo mmoja, waliponifikia nilianza kuuchezea upanga wangu sasa baadhi yao niliwafyeka kwa kuwajeruhi ila akili yangu ikanambia kuua si vyema hata kama ni ninja basi nikaruka na kuwasukuma kwa mateke watu watatu kisha nikasogea pembeni na kuurudisha upanga wangu tena mgongoni hapo waliobaki walijipa moyo wa kunifuata hapo na mimi sikuzubaa nikatoka na kuanza kucheza nayo huku nikidank kwa stail mbalimbali huku nikiwa wasogelea hapo ndipo nilianza kutoa kichapo kitakatifu kwa kila mmoja mana cheni ilikuwa haiui ila inakuacha na maumivu ambayo ni lazima ukae chini kuugulia baada ya dakika chache watu tayari walikuwa wameshakaa zao chini kwa maumivu makali kwenye miili yao. Niliwaambia hku nikiwa nikiwa nimebadilisha sauti kama sio mimi vile """"ondokeni hapa fasta kabla sijatumia njia ambayo ni mBaya zaidi kwao"""" waliogopa kisha wakasimama na kuondoka zao bila hata kuangalia uelekeo wao ni wapi maana baadhi yao waliangukiana waliokuwa nyuma niliwasindikiza kwa mateke mazito ili wakome wasijejaribu huu mziki.
******baada ya hapo nilijivuta tena na kuruka kavu yenye ujazo wa namna yake na kurudi tena ndani kisha nikatoa kamba niliirusha kwenye paa na kukwea kuingia ndani,, nilibadilisha nguo na kutoka tena sebuleni kusha tukaendelea na story kama kawaida macho yangu yalikuwa yakimwangalia anna mda mwingi hii yote kwa sababu nilikuwa simfahamu na kibaya sijatambulishwa ni nani ila kwakuwa mimi mwenyewe nadandia tuu kukaa pale hata sikuhitaji kumjaji kiuwazi..tukiwa tumetulia cm yangu iliita nilipoangalia alikuwa ni baba akinipigia nilipokea na kumwamkia:_
,,,,ok marhaba ben hujambo mwanangu
..baba mimi ni mzima kabisa mungu anasaidia sijui hali yenu jee
,,,huku tupo salama hofu ilikuwa kwako
..ni kweli sijawapigia mda mrefu kwakeli tatizo salio
,,,,haya sa si ungesema tu tujue cha kufanya
..nilisahau tuu
,,,,ok kesho unaweza kuja au ngumu
..ah sio ngumu nitajitahidi tuu mana nimewamisi huko
,,,,sawa basi toa taarifa unapoondoka.....alimaliza baba kwa kusema vile.
Nililala na siku iliyofuata nikiwa kwa usafiri wa miguu niliianza safari yangu nilitembea hadi......itaendeleaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni