Gangstar noma
By: benchrys
34
..siku iliyofuata niliamka na kuanza rasmi safari yangu nilitembea hadi maeneo Fulani ambako palikuwa na mti mkubwa sana nikiwa sina hili wala lile gafla nikashangaa mtu kashanivaa na baiskel nilianguka chini ambapo na yeye alianguka chini alisimama na kuniambia dogo kama siku nyingine kuwa makini sana unapokuwa katika barabara za watu kama hizi duh nilimwangalia nikajisemea halafu sometime watu sijui wanakuwa na visa na watu kwa kila eneo, nae baada ya kuona nimemwangalia akanifuata tena na kusimama mbele yangu,,,,,dogo mbona unanitumbulia macho inamaana kukwambia kwa mdomo umeniona mimi zoba au. Baada ya kuuliza vile akanipiga bonge la kofi kidogo nianguke hadi chini lakini kwakuwa tayari nilijengwa kwa kuwa na stamina sikuweza kuanguka hadi chini,,,,, baada ya pale akanifuata na kutaka anirushie ngumi niliudaka mkono na kuubana kasha nikamwambia samahani sana usijione kama unajua sana sawa mzee,,, kasha nikamwachilia ule mkono huku nikiondoka ili niendelee na safari zangu lakini bado akajifanya kidume ambapo hatua hii alinifuata ili anipige na teke mgongoni lakini nilipogundua nilidank na kumfumua huku akiwa bado kule juu. Hapo ndipo nikazipanga kwa maana nilijua lazima ataamka na hasira zake za kutosha tu, na ndivo ambavo ilikuwa
Alinyanyuka toka pale chini na kuanza kurusha ngumi za ugomvi lakini hata moja haikuweza kunipata baada ya hapo nilidank juu na kutua katika kifua chache alianguka chini na kukohoa kwa shida sana,,,,, nilicheka kidogo kasha nikamwambia kama siku nyingine hiyo nifundisho acha kujitia kidume siyo kila tu ni boya hivo sasa kwakuwa umenichelewesha naondoka na hii baiskel utafuata mtaa wa ishirini sawa. Niliokota baiskel yake na kuanza kuondoka nayo alipiga kelele za kuita lakini hata sikutaka kusikia chochote mana nilishamwambia mtaa upi afuate
Nikiwa kama kilometa mbili hivi nishapita kutoka pale niliweza kuona kama kuna magari ambayo yalikuwa msururu sikuweza kujua yanaenda wapi,,,,na mimi nikaongeza mwendo ili niwahi kufika ambako nafika lakini cha ajabu nikiwa naweza kuendelea na safari yangu kuna mtu alijitokeza mbele yangu na kuniambia et anaomba nimwazimishe baiskel yangu hafiki mbali nimsubiri hapohapo sikukubali nikakataa baada ya mimi kukataa akasema lazima nimpe tuu nikamwambia mkubwa hizo ndoto hapa huchukui baiskel kasha nikashuka katika baiskel ile,,,,, alirudi nyuma kidogo na kutoa kisu fulani kidogo hapo ndio nikagundua kumbe sio mtu mwema nae. dah hii dunia kweli hakuna wa kumwamini,,nilijisemea maneno yale huku nikiwa nailaza baiskel yangu pale chini ili nijiandae na kitakacho tokea
Kwanza aliokota jiwe na kunitishia nalo kisha akarusha lakini nililidaka na kumrudishia ambapo liliweza kukita katika mkono wake uliokuwa umeshika kila kisu. Kisu kilianguka chini kisha nikakiokota na kuchukua baiskel ili niondoke nikiwa nataka kuondoka na ule msururu wa magari tayari ulikuwa umeshafika jirani na sisi,,, kilichonishitua ni baada ya kuona wakipunguza mwendo wa magari yao, basi sikulaza damu niligeuza baiskel yangu na kurudi nilipotoka ili nikatafute njia mbele kama ipo itakayo niwezesha kufika hadi mahali husika ambako ni nyumbani kwetu..
..wale wenye gari waliposimama walienda moja kwa moja hadi kwa yule ambae aliniomba baiskel kibabe na kumfunga pingu kisha wakampakia kwenye gari na kuondoka nae huku mmoja wao akisema kwa jazba sana
ndugu kazi itakamilika tuu hata kama unafanya hutaki haya huyo jamaa yako ulikuwa nae ni nani naihitaji kumfahamu nae pengine anaweza kuwa msaada
Hapana huyu mimi hata sifahamiani nae kwa namna yeyote ile alijibu hivo kwa woga lakini alipiga kofila uso na kuulizwa tena ni nani huyo usituletee uboya hapa kama unavonifahamu huwaga sioni kama ni hasara kutumia hasara nyingi sana kutumia pesa iliniweze kumpata mbaya wangu wewe nishakupata lakini kuwa huyu ben ni miezi mingi sasa namtafuta lakini hakuna mafanikio ila nna mpango mwingine kabambe subirini, hapo aliongea huku amewageulia walle wenzake
..kwa bahati nzuri niliweza kupata njia nyingine ambayo inaelekea kule ambako mimi naenda basi niliifuata kwa haraka na baadaya muda tayari nikawa barabara kuu nilitembea hadi karibia nafika mtaa wetu kufika hapo simu yangu ilianza kuita nilisimama kisha nikaitoa mfukoni ili nijue ni nani kapiga hiyo simu lakini niliona ni namba ngeni sikujali nikapokea huku nikiwana tahadhali kubwa sana
ya ben uko wapi mchizi wangu mana adimu kinyama
acha uboya namba ngeni halafu eti mchizi uko wap
we sema uko wapi ilituonane,, baada kuona vile kama anataka kulazimisha nikamwambia nipo nyumbani. Baada mimi kumjibu vile tuu akakata simu na mimi nilipalaza pedeli za baiskel haraka ili niwahi pale yumbani baada ya nusu saa tayari nikawa nimeshaingia nyumbani
;waoooh jamani ben dah tulikumisije bro wetu njoo ndani basi ukapate kwanza hatamsosi wa nguvu halafu mambo mengine yaendelee,,alikuwa ni Naomi ambae alionyesha kuwa na furaha sana alinipokea begi langu kisha tukaelekea ndani. Kiukwei njaa ilkuwa ikiniuma sana nilkaa kisha ukaletwa msosi..
Hivi ben sijui atakuwa kafika salama kweli huko(alikuwa ni merry huku akiongea na Anna)
Wewe hata usijali yule kamanda hakuna cha kumtisha ila mapema bado atakuwa njiani kwanza kwao ni jirai sana. Aliongea vile Anna,,, hata sijui sana
Hawakuendelea na wakaishia pale
******nilipokuwa tayari nimesha kula nilitoka nje na kuchungulia hali ya nje vizuri baadaya kuona hakuna jipya nilirudi ndani na kulala kidogo niliamka saa mbili jioni.. kisha nikaenda nje ili nipunge angalau hata upepo lakini nilipotoka nje niliona hali tofauti maana geti lilikuwa wazi, nilirudi ndani ilinijue kama wanaacha wazi vile ila nilipofika ndani nikasikia sauti yalile geti kubamizwa ushara ya kuwa linafungwa sikutaka kutoka nje niliingia ndani huku nikiwa na imani alienipigia ndio mda wake wa kuja hapa.baada ya mda nilitoka chumbani kwangu huku nikiwa ninja mwenye nguo zake nyeusi nilpita sebuleni huku nikielekea njeitaendeleaaaaaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni