Ijumaa, 23 Septemba 2016

De 31

Gangstar noma
By: benchrys
31

......niliamka mapema sana ile siku akili yangu ilinituma nikawashe tv niliweza kufanya hivo ikaja breaking newz asubuhi tu hadi nilishangaa habari ilikuwa ikisema kwamba
"polisi watatu walioweza kutumwa jana kufanya uchunguzi katika nyumba namba xxxxxx wamepotea na mpaka sasa hatuna mawasiliano yeyote kisha wakaziweka picha za wale polisi na kumalizia yeyote atakae weza kuwaona atoe taarifa kupitia namba...waliitaja hiyo namba.. nikacheka pekeyangu huku najisemea daaaaah ivi na polisi sikuhizi ni watoto wa chekechea hadi watafutwe kwa taarifa kama hivi shida sana kwakeli. Nilitoka na kwenda bafuni nilinawa kisha nikarudi ndani.....

..........wale polisi waliolala kwenye gari huku ikifahamika kwamba wamepotea ilipofika asubuhi tuu waliamka na kuweza kutafuta sehem ambayo wanaweza kupata msaada ili wazibe pancha kwenye lile tairi la gari yao, walitembetemba kwa umbali fulani ndipo waliweza kupata garage na kisha hapo ndipo wakaazima vijana wachache ili wawasaidie katika kusolve tatizo lao waliondoka had eneo la tukio ambapo ipo ile gari yao kwakweli ilikuwa ni mbali hadi wale mafundi walichukia sema hawakuweza kutoa hisia zao kutokana na woga wa kuwa wale ni polisi..baada ya kutembea sana ndio walifika hadi kwenye lile gari
...duu huu mbons msumari inamaana hii njia ni mbovu namna hii.yalikuwa ni maneno ya kijana mmoja wa garage huku akiwa ameshika spana zake na kuweka kwenye gurudumu lile tayari kuanza kazi,,,,,,,,,,baada ya nusu saa tayari wakawa wameshaziba ile pancha, walifunga kila kitu kisha wakamgeukia alieenda hadi kule garage kuwaita na kumwambia mzee hapa ni elf thelathin na tano tuu kama hamtojali kisha akatulia baada ya kuongea vile yule polisi akajisemea moyoni "inamaana huu tayari umekuwa msala wangu ila sio tatizo sana, aliingiza mkono mfukoni na kutoa wallet yake kisha akahesabu ile thelathini na tano na kumkabidhi ila yule kijana akaongezea "samahani mzee hii kazi sijafanyia ofisini kwahiyo hapa inatakiwa kupewa na hela ya nauli mana tumesafili. Duuuh yule polisi ndipo alichoka zaidi na kuvuta pumzi ndefu kisha akatulia kidogo na kuuliza tena sh ngapi na hiyo. Yule kijana alimwangalia kisha akamwonea huruma kisha akasema tupatia elf tano tuu kwa wote mana inaonekana we ni mchaga. Yule kijana alipokea ile elfu tano na kuondoka na wenzie

Wale polisi walipanda gari na kuanza safari yao polisi mmoja akawasha redio ya kwenye gari akashtuka baada ya kusikia kwamba eti wametoweka tangu jana
Duuh hili jau wakuu umesikia taarifa za hawa wapuuzi...aliongea polisi mmoja
Aaaah mi naona wapo sawa kututafuta we hujui tuliondoka hatujapatikana had saizi kwenye simu zetu kwanini isionekane tumepotea...baada ya huyu kuongea hivi mmoja tuu ndie hakuchangia alibaki akiwaangalia tuu wote walimgeukia na kumuuliza ivi wewe unamatatizo mbona kimya kama bundi,,,, duuh nahisi jamaa aliboreka sana mana hata kama ilikuwa kwenye gari alinyanyuka akang'aka kama anamapepo vile. Polisi mmoja akamwambia hizo hasira ungeleta jana usiku boga wewe mtu nyoronyoro halafu unapaniki tuu...walipeana machambo hatimae walifika kituoni kisha wakaeleza kilichowakuta, mkubwa wao baada ya kuwasikiliza na kuwaelewa akawajibu safari ijayo tuongeze kikosi....

*****huku kwa ben****
Ben kama nilishajua kuwa hawa lazima watajipanga tena sikupoteza hata dakika asubuhi ilr nilienda katika nilitega mitego ya kutosha huku nikiendelea kufanya mazoezi hadi ilipofika saa saba mchana ndipo nilirudi nyumbani nilipofika nyumbani merry sikumkuta ila nikamwona dada mmoja ambae alikuwa mrefu wastan alijionyesha kuwa ni mwenye busara sana, nilimwangalia ila sikutaka kumjaji sana nilimsalimu kisha nikaingia ndani nae alifuata na kuingia sebulen huku akikaa kwenye sofa mle ndani, mimi baada ya kupepesa macho ndipo nikaona chakula kilishaandaliwa kwakuwa sikuonja kitu tangu asubuhi nilichukua jagi lililokuwa tupu nikiwa na lengo nikachote maji ninawe mikono lakini aliweza kuniwahi na kuniambia kakaangu usijisumbue acha nikusaidie tuu nikawa mbishi kwa maana ilikuwa sura ngeni machoni mwangu.
'''' samahani hata hujajitambulisha halafu unisaidie kiurahisi tuu nitakuaminije mimi wewe....nilimuuliza hivo, nae baada ya hapo akajitambulisha jina kwamba anaitwa Anna ubini sikuhitaji sana kuujua alieleza mengi ndipo nikaamua nimwachie tuu lile jagi ili akachote maji kama alivohitaji
Alichukua jagi na kutoa na mimi nilikuwa nikimwangalia tuu alifika hadi kwenye bomba na kuanza kukinga maji mimi nilipotupa macho yangu njee nikaita #anna njoo ndani haraka nilimwita hivo kisa kwa Mbali niliweza kuona kundi likija lenye watu kama hamsini hivi baada ya anna kuingia ndani kwa haraka niliamua kwa haraka ku....itaendeleaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni