Jumatano, 5 Oktoba 2016

Whi am i

Who am i(mimi ni nani)
Benchrys
03

------nilishtuka baada ya kuona picha ya mtu tofauti ambae hata sikuwahi kumwona katika maisha yangu pia nilijawa na maswali mengi sana kichwani mwangu hadi nikahisi kuchanganyikiwa kabisa,,,,, usoni mwake alikuwa kavaa ngozi ambayo inasura halisi ya baba yangu lengo nadhani ilikuwa ni kurahisisha kazi yake ya kunipata waondoke na mimi.

*****gari ilitembea kwa spidi sana hadi maeneo fulani ambapo palikuwa na magorofa mazuri sana na magari mengi zaidi. Lakini katika kichwa changu hata kama nilikuwa nikiviona hivyo vyote mawazo yangu hayakuwa kabisa katika maeneo yale, ila tuu nilikuwa nikiwaza kwa kujiuliza hawa ni akina nani na kwanini waniteke kwa namna kama hii isitoshe huku ni wapi hata sifahamu(ni baadhi ya mawazo ambayo nilikuwa nayo kichwani) baada ya hapo niliteremsha mkono wangu na kuuingiza katika mfuko wangu ili niipate simu lakini nilishangaa kuona simu yangu haipo tena hapo ndipo nikasema kweli kama ni uchawi upo mana tangu nakaa humu kwenye gari hakuna aliyeweza kunigusa katika nguo zangu ama mwili wangu, lakini basi ikanibidi nitulie huku nikiwaza kama baba inatakiwa ajue wapi nipo sasa nitapataje mawasiliano nae----nikiwa bado naendelea kufikiria vile aliingia mzee mmoja hivi ambae uso wake ulionekana kuwa kama alishawahi kuungua na moto, mana alikuwa anatisha sio kidogo kisha akanambia kijana kaa tu chini kuwa huru jisikie upo kwenu sawa, wala usijekuwa na woga wowote kiti hicho hapo special for you kitumie tuu,, kisha akakivutia kile kiti jirani na mimi ili nikae

     Samahani kwanza naombakujua hapa ni wapi na nimeletwa kwa sababu gani tena kwa misingi ipi mana hadi sasa siwaelewi////nilimuuliza hivo yule mzee licha ya kuwa nilimwogopa lakini nilijikaza tuu kuuliza lakini baada ya kuuliza vile cha ajabu yule mzee alianza kucheka     hahahahahahahaaaaa tehteheteh kisha akaongea kwa sauti kubwa sana kijana hayo maswali utayajua huko mbeleni majibu yake yote cha msingi wewe saizi fuata tuu kila unachoambiwa tena kuwa mpole. Baada ya kuongea maneno yale akatoka na kuelekea katika sehemu fulani ambayo ilionekana kuwa inamlango, nikakumbuka kuwa naitaji mawasiliano na baba nilifuata hadi pale alipopotelea lakini nilipofika pale nilichokiona ni korido ndefu sana lakini sikumwona mtu yeyote pale. Hii too much sasa nitawasilianaje na baba mimi dah(ni maneno ambayo nilijikuta nikiyasema pekeyangu pale ndani muda ulienda sana huku nikiwa pale sebuleni nilipopepesa macho niliiona saa ya ukutani ambapo ilisema kuwa ni saa moja na robo usiku. Kwakweli hii siku kama ni kujiona ni mdogo kuliko kirikuu hii siku ndo ilieleza wazi kabisa kuwa kweli mm ni mdogo mana sijawahi kushindishwa ndani kama hivi nikiwa sina mawasiliano na mtu yeyote yule

////nikiwa nimekaa aliingia baba mmoja na kuleta chakula kwenye meza pale huku akiniambia ni cha kwako hiki kwahiyo inatakiwa nikile, lakini nikamjibu tafadhari sina njaa hapa nilipo kwahiyo hicho chakula kirudishe tuu hukohuko, alijitahidi kunilazimisha lakini nilikuwa ni mbishi sana hadi akaona sasa hakuna njia ni bora nikampe tuu majibu aliyenituma kuwa umekataa kula chakula ila na mimi sikuchelewa nikamjibu ni kweli nimeshiba sana hapa nilipo kwahiyo sina haja ya kula muda kama huu. Alinyanyua kile vyombo vyake na kurudi navyo kule ambako ametoka navyo;;;;;;hii nyumba tangu nafika hadi masaa yameenda hivi sijafanikiwa kukujua hata chumba kimoja huku nikiwa sina mawasiliano na mtu yeyote

-------huku nyumbani baba alikuwa akihangaika sana kupiga namba yangu lakini haipatkani .hivi huyu leo kaenda wapi hadi saivi harudi tuu au kuna jambo limempata huko shuleni (yalikuwa ni maswali ambayo baba alijiuliza kule nyumbani na baada ya hapo akaamua kuondoka na kwenda mtaani ili kuulizia kama kuna mtu aliyeweza kumwona bon sehemu yoyote sehemu ya kwanza ilkuwa ni joel ambae nilikuwa ninaurafiki nae wa jirani sana
---jamani wenye nyumba hodiiii
-karibu haa baba bon kulikoni leo mda kama huu,, ilikuwa ni sauti ya baba ake na joel baada ya kumpokea baba aliuliza hivo kwakuwa haikuwa kawaida ya baba kuonekana mtaani au kwa jirani mda kama ule
---najua utakuwa unashangaa kuniona mda kama huu kwako samahani eti naweza kumwona joel au tayari kalala (aliuliza hivo baba)
- kalala lakini naweza kumwamsha tuu hakuna tatizo ila kuna tatizo limetokea au maana ni bora tukashirikishana mapema(aliongea baba joel)
---ndugu yangu kwakweli hapa hata sielewi kabisa bon tangu asubuhi aondoke bado sijaweza kuiona sura yake kabisa na sielewi ni wapi atakuwa yupo na ndio maana naomba kuongea na joel

\\\\baba ake na joel alisimama na kwenda moja kwa moja hadi chumbani kwa joel huku akimwacha baba kwenye sofa pale sebuleni

++++++++HUNA HAJA YA KUHANGAIKA KUMTAFUTA KIJANA WAKO YUPO MAHALI SALAMA KABISA TENA USIJARIBU KUMSHIRIKISHA MTU YEYOTE KWA MAANA ITAKUWA NI HATARI KWA MAISHA YA WOTE WATAKAO WEZA KUFAHAMU KUHUSIANA NA HILI ANAEJUA HADI SASA KUHUSU KUTOKUWEPO KWA BON NI WEWE NA BABA JOEL SASA NAKUAMBIA ONDOKA HARAKA ILI HATA AKIJA AJUE ULIMTANIA TUU+++++++ Hii sauti aliisikia baba akiwa amekaa pale sebuleni muda ule baba joel yupo kumwamsha joel lakini joel nae hakuamka kabisa alionyesha kuwa anausingizi mzito sana hii siku jambo ambalo hata baba ake alilishangaa na kuondoka kule chumbani lakini alipofika sebuleni hakuweza kumwona tena baba na yale mawazo ya kuwa kulikuwa na kuulizia kuhusu bon yalishapotea akendelea kufanya yake,,,*

****usiku nikiwa katika hili jumba ambalo hata silijui vizuri alikuja baba mmoja na kushika mkono kishakanambia njoo nikuonyeshe chumba chako cha kulala namimi nilisimama na kuongozana nae had kule kwenye chumba baada ya kukabidhiwa kile chumba nilipokea funguo kisha yeye akaondoka. Niliegama kidogo tu kwenye lile godoro hata dakika haikuisha nilishikwa na usingizi usiku nikiwa nimelala

__________ben mwanangu hiyo kamba uliyopewa na bibi yako naomba uifanyie marekebisho maana imekufunga baadhi ya mambo kuyafahamu ila utajua kama ukifuata ninachokuambia hapa muda huu hebu nizingatie mama yeko
     Kuna hizo gorori tatu nyekundu, kijani na nyeusi hiyo nyeusi fanya uwezavyo uichomoe kisha tupia katika dirisha la chumba chako na hiyo nyekundu itengenezee kamba nyingine kisha hiyo ya kijani iache iache humo humo katika hicho kidan naomba uanze hiyo kazi nikiwa nakuona hata mimi. Nilifuata maelekezo  yote kadiri nilivoambiwa lakini kamba ya kutengenezea kingine ndio sikuweza kupata akatoa kamba fulani nyekundu na kunipatia niliipokea na kuvalisha kile kigorori. Kisha mama akaniambia nitakuja wakati mwingine______hiyo ilikuwa ni ndoto!!!!! Nilishtuka pale nilipoegama huku mwili ukijawa na jasho sana hadi nilijishangaa, baada ya hapo niliamka------itaendeleaaaaa

benchrys.blospot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni