WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 4
-------niliamka na kuangalia mahali ambapo naweza kwenda kupata angalau hata maji ya baridi ili nipooze huu mwili, huku nikijiuliza hivi hii ndoto inamaana au la mbona siielewi. Lakini nilipojipapasa shingoni ni kweli nilihisi kuna kamba mbili zenye vigorori tofauti hapo ndipo niliweza kugundua kwamba ile hata haikuwa ni ndoto bali ni kitu cha ukweli.
Kiukweli hapo nadhani nilihis hadi kichwa kuniuma maana mawazo niliyoanza kuyapata hata stress za maisha nilihisi nindogo but zangu ni too much
//////inamaana mama yupo huku, kaletwa na nani,)))))nilikuwa nikiongea hayo hukunimeshikiia zile kamba huku nikiwa hata siamin kama ni kweli kamba zimeongezeka shingoni mwangu_____
Baad ya hapo niliondoka na kuingia bafuni, ambapo bafu ilikuwa mlemle ndani ya kile chumba cha kulala mmezoea kuita master,
Nilianza kuoga maji ya baridi yale lakini baada ya dakika chache maji yalianza kutoka ya moto hadi nikayaloki tena kwa kunyonga ile koki ya lile bomba la bafu. Kisha baada ya kutulia sekunde kadhaa niliifungulia tena, ambapo mda huu yalitoka maji ya baridi,. Nilioga na baada ya hapo nikarudi tena kitandani ili kuutafuta usingizi.
Masaa yalipita lakini sipati usingizi kwasababu macho yalikuwa ni makavu sana hali ambayo sikuielewa. Nilikosa raha kabisa kisha nikaamka na kuanza kuzunguka zunguka tu mle chumbani nikiwa hata sielewi chochote kuhusiana na lile jumba.
Nikiwa naendelea kuzunguka mle ndani uliingia upepo fulani mwanana ambao ulinifanya nikakae tena kwenye kitanda ndipo macho yalianza tena kulegea ili kuuita usingizi. Taratibu nilijilaza pale kitandani huku nikifurahia ule upepo na macho yangu yakianza kujifumba. Laikini gafla nikasikia sauti ikiniambia *****BON MWANANGU USILALE USILALE USILALEEEEEEEEEE NASEMA UKILALA UTATIMIZA NDOTO ZAO KIULAHISI SANA NISIKILIZE MAMA YAKO*** na mimi baadaya kuisikia ile sauti niliamka tena kwa kushtuka kama nilikalia mwiba kwa bahati mbaya.
-------nyumbani kwa baba nae hali ilikuwa sio shwari kabisa
Akiwa amekaa sebulei huku akiwa na mawazo mengi sana juu ya upoteaji wa familia yake mara akasikia kama mtu anagonga mlangoni
Ngongongo!!!!!
-nani,
Ngongongo
-nauliza nani wewe(aliuliza hivo baba) lakini hakuna jibu alilopokea lakini ilikuwa ni mwendo wa kugonga tuu, hakutaka kufungua mlango wakati mtu hajitambulishi ndipo akabaki amekaa tuu huku akiwaza mambo mengi sana, na baada ya mda akaondoka na kuelekea chumbani kwake akalale maana mda ulikuwa tayari umeshaenda sana, ilikuwa ni saa sita kasoro robo na kwakuwa iltakiwa kesho aende kazini mapema nab ado alikuwa na ratiba za kwenda kituo cha matangazo ili akaombe tangazo la kupotelewa mwanae bon, ilimpasa alale mapema tu.
Usisngizi ulimchukua mapema kabisa akalala fofofo*****
WEWE KAMA MZAZI UNAEMPENDA SANA MWANAO NAKUSHAURI USIFANYE HILO UNALOLIWAZA NILISHAKWAMBIA HATA KULE OLE WAKO UTANGAZE KUHUSU KUPOTELEWA NA MWANAO. NA KWAMBIA MTAPOTEA WOTE NIELEWE HIVO*****
Yalikuwa ni maneno ambayo baba aliyakumbuka wakati ule akiwa amelala alishtuka kutoka usingizini na kukaa lakini akashangaa kuona chumba kizima ni giza totoro, akaanza kupapasa simu yake ili awashe tochi ya simu alipoiona akawasha nakuenda kuangalia pengine unit ziliisha kumbe umeme ulikata usiku ule.
Usiku huu baba hata hakulala alikesha hadi asubuhi na asubuhi aliamka na kwenda kazini kama kawaida.
_____upande wa bon kule katika jumba la watu
Nikiwa nimekaa nilihisi nashikwa mkono lakini nilipogeuka kuangalia katika chumba nilkuwa mimi pekeyangu, lakini cha ajabu hata sikushituka kuonyesha hali ya kuogopa. Baada ya hapo nikaweza kuiona sura ya mama akiwa kashika upanga katika mkono wake huku akiunyanyua juu kisha akaukitisha hewani tuu, ndivyo ambavo mimi nilikuwa nikiona na baada ya hapo akapiga magoti huku akiwa kashika ule upanga huku akifanya kama anajutia alichokifanya kwa wakati ule.
Baada ya hapo alisimama toka pale alipopiga magoti na kunifuata huku akinikabidhi ule upanga. Mwanzo nilitaka kukataa lakini akaniambia bon usipokubali kupokea huu upanga inamaana utakuwa umethibitisha na baba ako kule nyumbani aweze kupotea kama mimi nilivopotea, huu upanga utakulinda wewe pamoja na baba ako au wanandugu wengine.
Sasa ndio nitaupokea huu upanga na kuutumia hata sujui kutakuwa na maana yoyote hapo(nilimuuliza vile mama) ndipo akaendelea kusema kwamba nitakupa ujuzi kwa njia ya ndoto ili asiwezekufahamu mtu yeyote lakini nitakuomba uzingatie mambo nitakayo kwambia yawe ya muhimu sana maisha yako maana mimi hapa sio binadamu kama binadamu wengine kwa hiyo siwezi kurudi kwenye ile hali yangu ya zamani na sijapenda na nyie mpotee kama mimi. Baba yangu na mama yangu ndio visababishi wakuu wa hili jambo, shida yao ni watu wa kuwatumia katika kazi zao ili wafanikiwe katika kazi zao, baada ya kukupa mafunzo ya kuutumia huu upanga nitakutoa hapa ndani. Usiulize ntakutoeje/alimaliza mama kwa kuongea yale lakini bado nilikuwa na shauku ya kujua nilipotaka kuuliza swali jingine sikumwona tena mama tayari alikuwa ameshapotea machoni pangu huku akiniachia ule upanga.
Nikiwa pale kitandani nimeshika ule upanga mlango wangu ulifunguliwa kisha akaingia mzee fulani mwenye ndevu nyeupe, nywele nyeupe hadi kope zake zilikuwa ni nyeupe, nilibaki natetemeka pale ndani huku nimeushika ule upanga maana nilijua tayari amesha uona tayari kwa hiyo itakuwa shida ikiwezekana watanishtukia kwamba naongeaga na mama.
Yule mzee alinisogelea jirani kabisa kisha akakaa kitandani pale na kuanza kuongea, mbona ni usiku lakini hulali tuu? Nikiwa nataka kumjibu simu yake ilianza kuita akatulia kidogo na kutoa simu mfukoni kisha akaipokea
Ndio bwana mkubwa, aaah ndio, eheeee tayari kabisa hata usipate shida,, aaaah no so hivyo ndio, ndio ehee, ok sawa,. Nilimsikia tuu akiongea hayo maneno katika simu yake aliyo ipokea, sikuelewa mazungumzo yao yalikuwa yakihusu nini au yakimhusu nani.
Alivo maliza kuongea akatoa simu tena sikioni na kuishusha hadi kwenye kitanda kwa wakati huu hakuiweka mfukoni, alipoiweka kitandani akanigeukia mimi huku akiwa ametoamacho hata yalikuwa na ya kizee lakini yalionekana yakiwa yametoka
Duuh nahisi atakuwa tayari ashauona huu upanga sijui ntafanyaje hapa (nilisema pekeyangu hayo maneno moyoni ambapo sikjua hata cha kuamua kwa wakati ule lakini nilijikaza na kubaki nimekaa vilevile nione atasema kitu gani. Nae alinyanyuka na kukaa upande nilioweka lile panga kisha-----itaendeleaaaaaaa
benchrys.blogspot.com
#panga_ameliona_au_hajaliona_mimi_na_wewe_hatujui_kabisa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni