WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 05
------kwa jinsi alivokuwa akiniangalia nilijua kwamba dhahiri inawezekana tayari ameshaniona na ule upanga ambao nilipewa na mama, lakini cha kushangaza alianza kuongea habari nyingine kabisa licha ya kuwa zilinishtua lakini ilikuwa ni tofauti na ule upanga .
Kijana wangu nimekufata huku mimi kama mimi na hakuna anaejua kuwa mimi mda huu nipo huku nisikilize tena kwa umakini,
Najua nyumbani kwenu mama yako alipotea katika mazingira ambayo hakuna aliyeweza kuelewa ni wapi mahali ambako ameenda, ila itatakiwa utambue kwamba babu yako na bibi yako kipindi kile wamekuja kule kuwasalimia lengo lao haikuwa ni kuwasalimia ila ilikuwa ni kumpoteza mama yako, samahani kwa kukwambia hili( alivuta pumzi kidogo kisha akaendelea) mama yako hadi saizi sio binadamu kama binadamu wengine, unaweza ukabahatika kuonana nae na akakupa chochote cha kujilinda hebu pokea hata usikatae,
Kwa maana, walipogundua kwamba anampenda sana mwanae ambae ndie wewe, walichukua uamuzi wa kukuteka na wewe huku wakitumia uso wa baba yako ambao ulifanya kutengenezwa kama aina fulani ya kofia, nimekuja kukwambia haya kwamaana wewe bado ni mdogo na mambo watakayo taka kukukabidhi sio mema kwa kuishi na wenzio(alisimama na kuanza kuondoka huku akisema) naomba uyashike sana haya maneno kijana wangu.
*****nilishtuka sana pia nikabaki nikijiuliza inamaana huu upanga hauonekani au/////lakini sikukazia sana kuhusu hilo swala
Baada ya dakika chache usingizi ulinipitia
****usiku nikiwa nimelala nilianza kuota*****
+++++++++ hebu nyanyuka acha uzembe wewe utakuja kufa kizembe wewe, sa a awa naanya nyuka, (nilinyanyuka huku nikiwa nimechoka sana lakini huyu hakuwa na huruma kabisa++++haya ruka hizo kamba moja baada ya nyingine tena kwa sekunde ishirini tu ole wako ufeli mana kule chini kuna joka linalokula nyama za watu wazembe, kusikia hivo nilifanya kadiri nilivyoambiwa sijui hata nguvu zilitokea wapi niliruka kambamoja hadi nyingine hadi nikawa tayari nimeshafaulu lile zoezi na kujikuta nipo upande wa pili chini nilipoangalia niliweza kuuona ule upanga ambao nimepewa na mama kule chumbani. Roho ya kuokota sijui hata ilikotokea niliuokota ule upanga na kusimama toka pale chini nikiwa sifahamu lolote.. alitokea kiumbe fulani wa kutisha sana mwenye miguu minne na mkia mrefu mrefu wenye kushiba sana, hapohapo nilianza kuogopa nikasahau kuwa nilishika upanga, kile kiumbe kilianza kunisogelea huku macho yake yakiwa na rangi kama taa inayotoa mwanga mwekundu,
Nilianza kurudi nyuma kwa uoga sana(BON TUMIA HUO UPANGA KUPAMBANA NA HICHO KIUMBE KITAKUTEKETEZA) hii sauti hata sikuelewa ilikotoka lakini ndio ilinikumbusha kuwa nina upanga mkononi
Kile kiumbe kiligeuka kwa kasi ya ajabu na kuuzungusha mkia wake, niljitahidi kuukwepa usinipate lakini jitihada zangu hazikufanikiwa haa kidogo,
Ule mkia ulikita vyema katika mgongo wangu nikajikuta nikirushwa kule huku nikibaki na maumivu makali sana katika mgongo wangu,. Nikiwa bado pale chini nikasikia sauti nyingine tena ikisema UKIFANYA UZEMBE UMEKUFA BEN
Nilinyanyuka tena kwa spidi huku nikiangalia huku na kule kama yule kiumbe anakuja tena lakini niliweza kusikia tua sauti kubwa ya kutisha ukitoka katika pori la upande pili
\\\aghrrrrrrrrrrrrrrrr aghrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr aghrrrrrrrrrrrrrrr
Kwa kusikia hivo nilifahamu dhahiri ni yule kiumbe anataka kuja kwa mara nyingine, na kweli baada ya mda mfupi kilisikika kishindo kikubwa hadi tetemeko kisha yule kiumbe akaokea tena huku anafuka moshi kwenye matundu ya pua lake ambayo usingeweza kutofautisha na shimo la toilet(choo) kwa wakati huu uoga wote niliutupia kule na kujipanga ili nipambanane na huyu kiumbe.
Hili likiumbe lilitoka kasi sana huku likinyoosha kwangu, na mimi kwa ustadi mkubwa niliruka juu kama mita kadhaa huku nikiwa na upanga wangu kisha nikakadiria kwenye jicho moja la yule kiumbe,
Ule upanga ulipoingia tuu katika lile jicho kiumbe hiki kilianguka chini PUUUUU ambako tetemeko lililotokea msitu mzima ilikuwa ni vumbi tuu na baadhi ya miti ilianguka. Nikajua nieshamaliza kazi ya kumuungamiza huyu kiumbe, niliyanyua upanga wangu na kuanza kuondoka,
Lakini kabla sijarusha hata hatua kumi ardhi ilianza kutetemeka upya hadi nikahisi kizunguzungu, nilipogeuka nyuma kile kiumbe kiliamka tena huku macho yakiwaka moto halafu kinanifuata, nilijikuta nikipiga magoti kumwomba mungu anisaidie, kisha nikasimama tena kujiandaa kupambana tena, safari hii ikikuwa kila nikiruka najikuta navutwa chini kinachonivuta hata sielewi,
Lakini nikapata akili nyingine, niliporuka tena nikavutwa chini, nilitanguliza ule upanga nikashangaa kuona upanga hauja fika chini na mimi nikiwa juujuu, hapo nilidank na kutua kwenye mti nikaudaka kama nyani vile kisha nikajirusha hadi mgongoni mwa yule kiumbe, nilivuta pumzi ya kutosha kisha nikauchomeka ule panga mgongoni.
Fuuuuuuuu ni sauti ambayo ilisikika huku vitu kama maji yakitoka mule mgongoni kwa yule kuimbe. Kumbe aliendelea kufumuka mana yale maji yalukuwa ni mengi nikiwa sijakaa vizuri nilirushwa juu******
Nikazinduka kutoka usingizini huku nikiwa nimechoka kuangalia mkono wangu ulikuwa umeshonwa ikionyesha kwamba kuna kitu kiliuchana, kiukkweli nilikuwa na maumivu makali sana katika mwili wote. Nilitaka kuingia bafuni lakini mwili hata kutembea ulipata uvivu maana ulikuwa na maumivu sio mfano yani
Nililala hadi akaja kuniamsha yule baba ambae anatumwa alitumwa mara kwanza aniletee chakula.
Kijana chakula chako hicho(aliongea huku akiwa anasogeza kimeza fulani cha kusukuma jiran na mimi, ilikuwa ni breakfast.
Baada ya kuweka yeye aliondoka nikasikia sauti ikisema hebu kula hakina madhara hicho, mpaka sasa nilishatambua kwamba hii ni sauti ya mama ndie ambae mara zote ananipa taarifa kwa njia ya sauti.
Basi na mimi kwa fujo nilikunywa ile chai kwa haraka sana kwa maana nilikuwa na njaa isitoshe jana nimekataa kula kwa sababu ya mawazo. Dakika tano zilitosha kabisa kumaliza vitafuno vyote mikate mitano na chupa nzima ya chai.
Nilimaliza kula kisha nilianza kujishangaa nawezaje kumaliza chakula chote hiki mimi tuu ila basi nikapotezea na kurudi tena kitandani.
Yule baba alikuja na kutoa vyombo kisha akaondoka alipoondoka tuu mama alitokea, kisha kaniambia pole kwa kazi uliyofanya
Mama kazi gani tena mi nililala mbona
- ulilala angalia huo mkono umeumia kwa sababu gani
Mmmmh mbona hata sielewi halafu nimechoka kweli yani
- ok najua wewe umeona ni kama ndoto lakini hadi sasa uwezo wako wa kupambana ni mkubwa sana, kwahiyo utakaa humu ndani kwa wiki moja ambapo nitakuwa nikifanya mpango wa kukutorosha. Chukua hiki kitabu kina list ya watu wabaya wote wanaohusika na kuupoteza ukoo wetu utaanza na mmoja baada ya mwingine iweke iwe siri yako tuu. Najua nikigundulika nitatolewa kabisa hata katika hii hali ambayo nipo nayo kwaheli(mama alipotea huku akiwa kaniachia kidaftari fulani kidogo) lakini mara ghafla nikasikia sauti USIMWOGOPE MTU WA HUMU NDANI---itaendeleaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni