WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 06
-------baada ya kusikia lile neno la usimwogope mtu wa humu ndani, nikauliza wewe ni nani unaesema hayo maneno?
Sikujibiwa tena kitu chochote zaidi ya sauti ya ndege ndio zilianza kusikika mle ndani, nilijaribu kunyanyuka ili niweze angalau hata kwenda msalani lakini mwili ulichoka sana, sikuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea kulala lakini nikiwa bado pale kitandani nimejifunika ndani ya blanket nilihisi kitu cha baridi kina tembea. Hapo hata nguvu sijui zilikotoka,
Niliruka juu kama nimepata zawadi katika shindano hiyo yote ni baada ya kugundua kuwa alikuw ni nyoka yupo pale kitandani, nilisimama pembeni huku nikiwa najiuliza huyu nyoka kaingiaje niienda hadi mlangoni ili niweze kupata msaada hata wa kutoka nje lakini baada ya kufika mlangoni mlango ulikuwa umelokiwa kwa nje, mama yangu na huyu nyoka itakuwaje sasa mungu nisaidie (niliongea maneno hayo huku nikiwa nasukuma mlango ule lakini sikuweza kufanikiwa kwa lolote) lakini akili yangu ikanituma kwamba tafuta hata chochote cha kuweza kujihami
Nikageuka tena nyuma ili nipepese hata macho mle ndani pengine naweza ona chochote, baada ya kugeuka nyuma macho yalitua moja kwa moja kwenye kona ya nyumba ambapo niliweza kuona ufagio fulani mrefu kwaajili usafi wa chumba nilinyoosha moja kwa moja ili niuchukue nikafaulu kuuchukua hapo ndipo nikarudi tena kwenye lile blanket ili nimtafute nyoka yule.
Nilivuta lile blanket kwa nguvu huku nikiandaa fimbo yangu lakini cha ajabu sikuweza kumwona nyoka tena pale kwenye kitanda sijui aliondokaje ili eneo basi nikaahirisha na kurudisha ile fimbo tena kuwa ufagio nakuenda kuurudisha mahali ambapo ulikuwepo nikiwa nipo pale kwenye kona nikawa nasikia sauti kwa mbali
Ya ndio hili swala sio gumu sana isipokuwa tu sisi tuwe makini na akili ya na huyu dogo ni lazima tuu afanye kadiri sisi tunavohitaji
Sawa tutakutuma wewe hapo ili ukaandae mahali pa kumteketezea ili liwe ni swala la kimya kimya sana tuelewane hivyo\\\\\////// wakiwa wanaendelea kuongea khohooo!!!!
Waliposikia sauti hii kila mtu alishtuka. Mmoja akasimama na kuja hadi mlangoni kwangu baada ya mm kugundua kuwa kuna mtu aanakauja jirani na mahali ambapo mimi ndio nilikuwepo niliondoka kwa mwendo wa kunyata tena haraka sana na kuelekea bafuni
Alifungua mlango kisha kaingia ndani, nikiwa bafuni kule niliona nae akija katika mlango wa bafu, nilijibana ili nisionekane lakini alizidi kuingia hadi ndani. Nilipata hasira sana nikamuuliza ndugu ulinzisaizi hadi mtu akiwa bafuni inatakiwa alindwe tu. Hakuongea chochote na kuchomoa kisu fulani katika mfuko wake huku akiendelea kunisogelea, nikajua hapa bila kujitetea naweza kupoteza uhai huku nikiwa najiona.
Baada ya yeye kunisogelea hadi jirani kabisa nilipo, nilijikuta naanguka chini kwa kupigwa ngumi nzito ya taya wakati huo aliye nipiga namuona kama wapo wawiliwawili hivi na kizunguzungu dah nilipata hasira sana. Lakini nae bado alikuwa akinifuata tuu nilipo nami nikaanda ngumi nzito huku mkono wangu ukiwa nyuma ya mgongo, akiwa anaendelea kunifuata kwa mwendo wa taratibu alishitukia akipokea ngumi kama jiwe na kuanguka chini huku akiwa hajielewi kabisa kule bafuni ilikuwa ni damu tuu kwa wakati huo. Baada ya kitendo hicho nilitoka nje huku nikiwa nawaza kama amezirai itakuwaje hapa ndani si pata bana lakini basi nikawa natoka nje ya ile bafu kurudi tena mahali pa kulala mara nikaweza kuiona tena sura ya mama huku akipiga makofi na kusema +++safi sana hivyo ndivyo ambavo nilikuwa nataka kuwa sio watu mnaonelewa na watu kama nyinyi hii dunia ya wote bhana.////alionyesha mwenye furaha sana hadi nikashangaa inamaaana anafahamu kilichotokea nilipotaka kuongea nae gafla tuu akapotea
______kwa baba______________
Baba akiwa kazini kule alipigiwa simu ya kwamba mwanae bon amepatikana katika jumba moja hivi ambalo zamani sana katika historia walikuwa wakiishi watu wan chi nyingine ambao wamekimbia kutokana na matatizo mbalimbali(wakimbizi)
Baba alifurahi sana kupata hizi taarifa akaomba ruhusa pale ofisi kwa wenzake
- jaman naenda mara moja mahala nimepigiwa simu sasa hivi tuu nitakuwa hapa akija mtu mwambie aningoje kisha akaondoka na kupotelea
****alipoondoka tuu kuna mtu akaingia pale
samahani nilikuwa na shida ya kumwona mpl sijui nimemwona
Hapana halafu katoka sasa hivi ila amesema yoyote atakae fika amsubiri hapahapa kwa maana anarudi sasa hivi tuu unaweza ukakaa tuu hapo (alimwambia huku akimwonesha kiti ili akae) lakini yule mgeni akauliza unaeza niambia ameelekea wapi?
Hapana kiufupi hajasema ni wapi ameenda ila wewe msubiri tuu labda kama shidayako sio ya mhimu sana(secretari alijibu tena vile)
Ninaharaka sana basi ningeomba unisaidie hata namba yake ya simu tuu (aliongea yule mgeni)
------hapo sekretari alishituka huyu mgeni kwa nini ni kingang;anizi namna hii hapa kuna kitu sio bure
Kiukweli mimi hapa sina ruhusa ya kutoa namba yake labda angenipa ruhusa ndio ningetoa. Baada ya sekretari kusema vile yule mgeni aliondoka ikiwa inaonyesha kabisa kwamba hajafurahishwa hata kidogona majibu ya sekretari,
Lakini kibaya zaidi yale mazungumzo yao yote kuna sehem maalum ambayo waliiset mnapoongea mkianza na salamu yenyewe inaanza kurekodi, kwahiyo yale mazungumzo yote yalirekodiwa na kile kifaa
****************
Baada ya baba kufika lile eneo ambalo alipigiwa simu kwamba yupo bon alifika pale na kuita lakini palikuwa kimya kama hapaja wahi kukaliwa na kitu chochote chenye kutoa kelele yoyote ile
Bon bon bon
Bon aliita mara kadhaa lakini hakuweza kuitikiwa akaamua arudi tuu kazini lakini alipogeuka nyuma mara moja akakutwa ameshazingirwa na kundi fulani la watu. Baba alibaki ameduwaa asijue ni nini atafanya mara kila mmoja wao akaanza kumsogelea baba hadi pale alipo huku wengine wakiongea lugha isiyo eleweka, na mmoja ndio aliongea Kiswahili
(((((((mzee tuna busara sana lakini kwa kitendo ambacho mwanao amekifanya kwa mwenzetu kwakweli hatuwezi kufumbia macho hata kidogo
(huku akitoa kama sauti ya kulia) amuue ndugu yetu sisi ivi mnajua sisi ni akina nani katika huu ulimwengu nianuwezo wa kukugeuza kitoeo tena kwa kukumaliza m bichi kabisa lakini sitaki
,wakati huo wote baba alikuwa hawaelewi ni nini wanaongea mana kama ni mwanae bon anajua kabisa alipotea katika mazingira ya kutatanisha halafu wao tena wanaongea kuhusu tena.
Yule aliyekuwa akiongea kwa uchungu sana akatoa kisu na kusema hapa naona tunapoteza tuu mda utalipa dhambi za mwanao mzee sawa kisha aka-------itaendeleaaaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni