Jumatano, 5 Oktoba 2016

Who am i

Who am i(mimi ni nani)
Benchrys
No 1

Katika kijiwe fulani kulikuwa na vijana sita wamekaa huku wakipiga stori zao kama kawaida jion baada ya shughuli za mchana. Lakini katika wale vijana sita kuna mwenzao mara nyingi alikuwa kimya pia ni mnyonge sana kitendo ambacho kiliwakwaza wenzie na hata kuanza kumwongelea yeye nae akiona wanamwongelea alikuwa akisimama na kurudi zake nyumbani bila hata sappota ya wenzie. Lakini wao bado hawakujua ni kwanini hapendi sana story na watu au hajisikii kwanini kuongea ovyo mda mwingi......

________songa nayo________

Nafahamika kwa jina la bon ni jina ambalo kila mmoja analifaham hata mtaan wengi huniita jina hilo lakini katika hali ambayo kila siku najiuliza na kukosa majibu ni pale nikitembelewa na babu au bibi huniita ben mara nyingi kipindi cha mwanzo sikuwa naitika kwasababu sikujua ni nani huyo ben lakini baada ya kuzoweshwa na babu hilo jina nikawa naitika tuu endapo amekuja yeye kutoka kijijini.

*****Ilikuwa siku moja bibi na babu walikaa sebuleni ghafla tu mama akaanza kujisikia kizunguzungu hali ambayo ilimtoa hadi nje ya nyumba na hakuna ambae aliweza kutambua ni wapi kaenda upande wangu nilikuwa bado mdogo sana hata akili ya kusema nifuate sikuwa nayo, baada ya mama kutoka nje kwangu mimi nilitegemea atarudi baada ya mda mfupi tuu ila hayo yalikuwa ni mawazo yangu tuu na ukweli hata haukuwa hivo ilifika hadi jion baba anatoka kazini lakini mama bado hajarudi ndipo tukaulizwa swali na baba
,,,,Mama bon kaenda wapi mbona simwoni humu ndani. Na majibu yakawa kama hivi
Babu..alitoka nje mara moja nadhani atarudi sasa hivi
Bibi..wew unawasiwasi gani yule sio mtoto hapa anapafahamu kwahiyo atarudi.

Lakini baba aliendelea kuuliza mbona siyo kawaida kuchelewa kurudi namna hii, aliwaaga anaenda wapi alipoondoka.. hapo babu na bibi wote hawakutoa majibu baba aliponigeukiwa mimi akakuta machozi yakinitoka tuu kama mfiwa.
Tulikaa masaa yalienda na kukata lakini mama harudi baba akijaribu kupiga simu inaita tuu humu humu ndani lakini wakiitafuta haionekani mahali ilipo... Baba akiwa chumbani alichanganyikiwa huku akisema kwanini aondoke bila kuaga na simu ameiacha tuu hapa ndani. Baada ya kuongea hivyo alitoka na kwenda kuwapa taarifa majirani kwamba anamtafuta mama kama alionekana sehemu yoyote, lakini hakufanikiwa kupata jibu lenye faraja mana kuna wengine walisema walimwona asubuhi akiwa anaelekea kama sokoni lakini hawajamwona tena. Baba akasafiri hadi kituo kimoja cha matangazo na kuomba tangazo la kumtafuta mtu. Tangazo la kwanza liliunganishwa na taarifa ya habari ya asubuhi kabisa ambapo walisikia wachache lakini walijitahidi kwa uwezo wao kuzisambaza, wengi hawakuweza kuamini lakini ilikuwa ndio hivo kilicho tangazwa ni ukweli mtupu

......tulikaa wiki nzima bila kumwona mama machoni petu tukawa wakiwa kwa kuondokewa na mwenzetu kiutata zaidi na redio ziliendelea kutangaza kila baada ya dakika kadhaa kwa yeyote atakae weza kumwona atoe taarifa lakini hakukuwa na mafanikio hadi mwezi mmoja uliisha babu na bibi waliaga kuwa wanaondoka ili warudi tena kijijini lakini akawaambia ni bora wabaki wanakaa hapa hapa. Babu na bibi walikataa kabisa wakidai kwamba mazao yataharibika na hakuna wa kusimamia huko kijijini kisha walipanga vitu vyao na kuondoka baba aliwapa baadhi ya vitu vya kuwasaidia waendako lakini walikataa kupokea, mimi walinipa kitu kama kamba fulani ambayo walisema niwe naivaa shingoni, bila kinyongo niliipokea kisha nikaivaa shingoni baada ya mda tuliagana kisha wao wakaondoka

....nilikaa na baba hadi inafika usiku shughuli zote alikuwa akizifanya baba pale nyumbani mana tulikuwa wawili tuu. Tukiwa tumesha maliza kula baba aliita bon mwanangu niliitika kisha nikawa makini kusikiliza lakini akiwa anaanza kuongea simu ilianza kuita akaipokea na kutulia kimya huku akionyesha mshangao wa ajabu hadi nikamuuliza baba mbona hivo kuna nini lakini alitoa ishara ya kwamba nitulie kimya kwa kutumia kidole chake baada ya mda alishusha simu toka sikioni na kuelekea chumbani lakini alipofika chumbani alisimama kidogo akatafakari kisha akarudi kukaa pale akasema mwanangu bon niliitika naam baba....itaendelea

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni