WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 07
------utalipa dhambi za mwanao kisha akatoa kisu na kutaka amchinje baba lakini kabla hajatimiza lile lengo lake alishitukia mkono wake ukivunjwa asijue ni nani aliye mvunja ule mkono
Kisu kilianguka chini ambapo wale wenzake baada ya kuona vile wakabaki wanashangaa tuu.
Oya tuacheni uboya ivi mwenzetu imemtokea vile halafu nyie bado tu mnashangaa hebu twende. Mmoja wao aliongea yale maneno kisha wote wakaondoka na kufuata pale aliposimama baba lakini kabla hawajafika ulitokea mwanga fulani mkali sana ambapo kila mmoja akajikuta akiziba macho yake ili yasiumie zaidi.
Walipofungua tena macho yao hawakuweza kuona tena kitu machoni pao, kila mmoja wao alibaki na swali ni nini hiki sasa huyu mzee kaenda wapi
-------Tukirudi upande wa pili baba yupo ofisini anacheka tuu na wafanyakazi wenzake hata hana shida yoyote
;;tumeongea mengi ivi nlisahau kusema. Mda ule umeondoka kuna mzee fulani alikuja na kukuulizia wewe(alikuwa akisema sekretari kwa baba kama bosi wake)
---kwahiyo yuko wapi mbona sijamwona
-kiukweli baada ya kumwambia kuwa haupo na umesema yeyote akifika amngoje, yeye alikuwa mbishi sana hadi akataka nimpe namba yako ya simu ila nimekataa
---huyo mtu yupoje labda
- yeye ni____akiwa anataka aendelee kuongea simu yake ilianza kuita akaangalia aliona ni namba ngeni lakini aliipokea vile vile na kuiweka sikioni
Halo,,, hallo,, haloo mbona huongei
Shit labda niweke loud kwanza,. Baadaya kuongea vile akaiweka simu yake iwe loud kisha kaendelea kisikiliza. Hapo ndio ikasikika sauti
++++NASHUKURU SANA DADA KWA MSIMAMO WAKO LAKINI TAMBUA HAPA DUNIANI HAKUNA JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI, NAMBA NITAIPATA TUU TENA KWA NAMNA YOYOTE ILE. PIA USISHANGAE HII NAMBA NIMETOA WAPI(kisha akavuta pumzi kidogo lakini iliyokuwa ni ndefu na kuendelea) KAMA UPO NAE HAPO SAIZI NAKUOMBA TUU UMPE SIMU ILI NIONGEE NAE KUHUSU MWANAE AMBAE ANAMTAFUTA++++
Maneno hayo yote baba aliyasikia kisha kaanza kwa kusema ndugu yangu najua ndio lengo uniteke mimi kwa jinsi unavoweza wewe lakini sidhani hilo swala kama litakuwa rahisi kama vile unavodhani jipange kwa jinsi unavoweza sawa kwaheli
(mda wote huo kitufe cha kurekodia kilikuwa kimeshikiliwa tena kiufasaha sana kwahiyo yale maongezi yalihifadhiwa)
Baada ya baba kuongea vile kwenye simu kilisikika kicheko
HAHAHAHAHAHAHAHAHAAAAA, HAHAAAAAA YAANI UNAJITIA MJANJA LEO HUKU HAKUNA UNALOWEZA KULIFANYA. HAYABASI UMESEMA SITAWEZA NI KWELI ILA KESHO UKIFIKA KAZINI HAPO NENDA KATOA SADAKA YOTE BILA KUBAKISHA HATA CHENJI KWAHELI MKUBWA.
Alisema kwaheli lakini simu haikukatwa zaidi zilianza kusikia sauti za kilio. Hadi pale walibaki wanajiuliza kisha ikarudi sauti tena kwenye simu BABA MIMI BIN USIWE NA WASIWASI NA MIMI SASA HUYU NDIO HATA BAADAE HAIONI PUMBAVU ZAKE. Alimaliza hivo kisha ilisikika sauti ya upanga kama umekata kamba na hapo simu ilikatwa.
Pale ofisini ile siku hata kazi hazikuenda kabisa waliamua kujipa off ya wiki moja wawe nyumbani. Basi waliagana kila mtu na kuelekea kwake yule sekretari akiwa njiani alikuwa akiwaza mambo mengi sana inamaana amekufa au, ila isiwe shida sana sikaya taka yeye mwenyewe.
Akiwa anaendelea kwenda ulisikika mlio wa honi ya gari ambayo ilikuwa tayari ipo miguuni kwake kisha zikafuata sauti za jazba sana kutoka kwa dereva wa lile gari
////ivi wewe dada hii barabara ya baba yako,
Jaman samahani sikuwa naona
///hukuwa unaona. Inamaana kuna ukuta hapa si ndio au
Kakaangu samahani kwakweli mawazo yalikuwa mbali sana na hapa naomba nisamehe tu
/// ivi hii dunia sikuhizi sijui imeingiliwa na pepo gani>>>> oya chogo acha uboya mwache tuu bovu huyo tuna chelewa tu hapa au ushamnoki halafu unafanya kumpandishia acha uboya bhana (yalisikika maneno maneno hayo kutoka kwa mmoja ambaye alikuwa ndani ya gari lile)
Haya maneno inaonekena yalimuudhi sana chogo maana aligeuka na kumtupia jicho yule wa kwenye gari kisha akarudi na kuendelea na safari yao sijui walikuwa wakienda wapi.
______kwa bon au ben_______
Nikiwa nimetulia chumbani kule ambako nilipangiwa kukaa siku zote mara wakaingia watu kama wanne ivi wote wakiwa wameshika magongo na kamba. Wakasogea hadi pale nilipokaa huku wakiangalia huku na kule mwingine akaingia hadi bafuni kisha akatoka na kusema ---oya mbona hakuna mtu humu ndani sijui kaenda wapi---
Hichi kitu nilikishangaa sana hadi nikajiuliza inamaana hawanioni au wanaigiza ili waone nitafanya nini. Wakiwa wanaendelea kujadiliana nilienda hadi mlangoni na kufunga mlango kisha nikarudi kukaa kitandani
Wao baada ya kuangalia zaidi wakawa wanaondoka lakini walipofika kwenye mlango walishangaa kuona umefungwa na wasijue ni nani kaufunga huu mlango wakajikusanya wote ili wauvunje
*****nikiwa nimekaa pale mama alikuja na kunipa mavazi fulani ambayo aliniamrisha nivae kwa haraka yeye anaharaka sana nikafanya hivo, kisha akanipa ule upanga na kuupachika nyuma ya mgongo na kunikabidhi kitu kingine kama koti linalofanana na mavazi yale. Vyote nilivipokea kisha akaniambia ben fuata niliyokuambia yote usiache hata mmoja kati yao sawa. Kisha akanikabidhi kitu kama karatasi na kuniambia leo ndio siku yako ambayo ndio unatakiwa uondoke.
Alipoongea vile nilisimama na kujitazama kwenye kioo nikajiona ni ninja. Alinishika na kusema usishituke chukua na hii uivae kichwani ili kuzuia uso wako usionekane, nilipokea na kuvaa kile kikofia ambacho kiliziba hadi uso mzima kasoro macho tuu. Baada ya hapo mama alipotea nilipotazama niliona dirisha lipo wazi nikasogea na kutaka kuruka====huu ujasiri sijui hata ulitoka wapi
Nilifika kwenye dirisha na kuchumpa sekunde chache nikawa tayari nipo nje kwenye bustani za ile nyumba. Nikiwa nipo chini kabisa kuna walinzi walikuwa wakizunguka katika lile jengo mlinzi mmoja akamshitua mwenzie na kumwambia angalia kule. Yule mwenzie alipogeuka hakuona kitu akampiga mwenzie kofi.
Pumbavu kabisa ushaanza utoto wa kutishiana haya nimeangalia kuna nini ambacho ulikuwa unanionyesha kwenye huko tupo kazini hapa jinga
----hichi kitendo kilimshangaza sana yule mwenzie maana amemwona ninja mda si mrefu kwenye bustani lakini tayari hakuna kitu
Waliachana nayo na kuendelea na kazi yao
Kule chumbani wale wakiwa bado wanahangaika kufungua hatimae wakawa wameweza kuufungua ule mlango na wote wakatoka njee huku wakijua aliye watuma hii kazi ndie amewafungia mlango. Baadaya kutoka hatua ya kwanza walienda jumla hadi kwa boss wao ambapo walimkuta amekaa tuu anakunywa kahawa ule mda kati ya wale mmoja alienda na kumnasa kubao yule boss wake. Boss wake aligeuka kwa hasira na kuchomoa pipe akamtandika nayo kwenye ubongo. Kisha akawaambia na wengine huu mfano na mwingine atafuata nani amewatuma huu ujinga. Wote walibaki wanashangaa tuu alinyanyua tena pipe na kuwatandika wote pale kisha akaita walinzi ili watoa yale maiti-----itaendeleaaaaaaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni