Jumatano, 5 Oktoba 2016

Who am i

WHO AM I(mimi ni nani)
Benchrys
No. 08

-------baada ya kuita walinzi kwa mda mrefu kashangaa hata mmoja haji kuitika ule wito ndipo akachukua uamuzi wa kusimama ili akawaone mweyewe kule nje. Alishituka baada ya kutoka kule nje aliwakuta walinzi wote wakiwa wamewasha wimbo kwenye simu na kuanza kucheza
Yule boss wao baada ya kuwaangalia akajisemea ivi mkiwaachisha kazi itaonekana mnaroho mbaya sana kama mabos sijui niwamwage ubongo nao????
Lakini baadaya kufikiria sana akasema hapa sio bure lazima kuna kitu nyuma ya pazia himaya yangu imesha ingiliwa tayari.
Alisogea hadi pale walipo na kumshika mlinzi mmoja na kumwambia nenda kauzime mziki huo ili tuongee yule mlinz kwa kuwa ni boss aliongea aliamua kufanya hivyo
Aaaaaa bamboo mambo gani sasa hayo hebu washa mziki
Bamboo aligeuka na kuwaambia angalieni au hamumuoni boss baada ya bamboo kuongea yale walinzi wote walishtuka na kusimama kisawasawa ili wamsikilize boss wao maana walijua kabisa hapa tayari tumesha haribu
;;;;;jaman ivi ni mambo gani mnayoyafanya saizi hapa, mmekuja hapa kufanya kazi au kucheza hizo nyimbo zenu za kibongo mnazoita bongo freva sijui(baada ya boss kuongea yale alivuta pumzi akatulia kisha kaendelea) ok sio mbaya naomba kujua kwa hivi mnavofanya mwishoni mnanidai ujira wenu au na mimi niwachezee hivohivo. Mlinzi mmoja aliropoka kwakusema
Boss mziki ulikuwa mzuri sana
Wenzie walimgeukia na kumwangalia sana yule aliyekuwa jirani nae alimuwasha bonge la kofi ikifuatiwa na ngumi ya tumbo hadi yule aliyeropoka akakaa chini kwa maumivu(((maana kati ya ngumi ambazo ukishitukizwa unaweza kuzirai ni pamoja na ngumi ya tumbo)))
Boss aliendelea kuongea
Cheki kama huyu mwenzenu yaani ameahau kabisa nini kimemleta hapa ili aje kukifanya eti mziki ulikuwa mtamu. Ok nimewaita tokea mda mrefu sana lakini hakuna aliyeweza kusikia wakati huo nawaita sasa sijaelewa ni kwa sababu ya huo mziki au ni kitu gani sijui lakini nili taka mje sebuleni mkawatoe wenzenu na kuwapeleka mahali ambako mimi nitawaonyesha..
Baada ya kuongea yale alianza kuondoka akiwa na maana inatakiwa wamfuate ambako yeye anaenda ambako ni kule sebuleni

Baada ya kufika sebuleni kila mlinzi alibaki ametumbua tuu macho yake kuwaangalia wale ambao kwa mda ule walikuwa wamelala chini huku wakiwa na damu kwenye vichwa vyao maana walipigwa risasi za kichwa kilamtu. Walinzi hawa hata kama wamelinda kwa mda mrefu sana lakini hakuna hata mmoja ambae amewahi kupoteza uhai wa kwa namna yoyote ile kwa hiyo wote waliona kama ni tukio la ajabu sana ambalo boss wao amelifanya.,
Walipomaliza kuwakusanya wale maiti waliwapeleka moja kwa mojahadi kwenye gari moja ambalo lilikuwa limezibwa upande wote na ndani ya hilo gari ni giza totoro ambalo tungefanaisha na gari la kubebea maiti lakini kwa hili lilikuwa likimilikiwana mtu binafsi.

Boss aliita bamboo hebu njoo ili nikupe maelekezo mahali ambako inatakiwa kupeleka hiyo mizoga. Bamboo bila kuchelewa alimfata boss na kupewa maelekezo mahali kwa kupeleka ule mzigo ambao ni watu, baada ya hapo safari ilianza na yule boss wao akawa anarudi sebuleni lakini katika hali ya sinto fahamu akashangaa mlango ambao inatakiwa aingie unafungwa kwa ndani. Alikimbia ili penginepo aweze kuuzuia lakini jitihada zake hata hazikufanikisha jambo lolote lile na badala yake aliuacha ufungwe tuu
Kwa wakati huu boss hapa nyumbani alibaki yeye pekeyake bila hata mlinzi yoyote yule kwahiyo kwakuwa mlango  wa upande mwingine nao aliufunga kwa ndani na kibaya hakuchukua funguo hata moja ikambidi akae tuu pale nje huku akifikilia ni jambo gani atalifanya ili aweze kuingia tena ndani
Alikaa sana masaa yalienda hadi inaaanza kuingia giza hapo ndipo akaona mlango unafunguliwa tena lakini mtu anaefungua hakuweza kumwona. Kwakuwa ni nyumba ya kwake alijisemea hata nikifia kwenye nyuma yangu sio mbaya kuliko nikafia nje huko. Hayo yote alikuwa akiongea huku anaingia ndani ya nyumba ile ambapo ndan ilikuwa giza sana. Alipojaribu kuwasha taa hata moja hakuna taa iliyokubali kuwaka, alijitahidi kubonyeza swichi mara kadhaa lakini hakuna kilicho badilika akaanza kutafutiza simu yake alipoiweka ili ampigie fundi umeme aje arekebishe hadi kuipata simu yake ilichukua nusu saa kwa kuwa ilikuwa ni giza mle ndani hapo ndipo akatafuta jina la fundi umeme ili apige

-/-/-/-/ mteja unaempigia hapatikani kwa sasa tafadhali jabu tena baadae. Thank you for_____hakutaka kusikiliza zaidi. Alikata simu na kutafuta jina jingine la fundi umeme lakini nae majibu yakawa
Mteja unaempigia anaongea na simu nyingine tafadhali jaribu tena baadae alijitahidi kungoja na hatimae simu ikakatwa

_______________________________
Tukiwa katika maeneo fulani ambao ni giza totoro tunamwona ninja fulani akiwa kashika kileo na kukata waya wa nguzo ambayo ilikuwa jirani na mnara kisha akaruka beki tatu mfululizo ambazo zinamfikisha hadi chini na baada ya hapo anaondoka na kuendelea na safari
********************

Wale walinzi baadaya kuondoka walitembea hadi lile eneo ambalo waliambiwa wakatupe zile maiti walifika hadi lile eneo na kutupa zile maiti na kuanza safari ya kurudi ambapo saa zao zilikuwa zikionyesha kwamba ni saa tatu na dakika kumi na tano
Baada ya hapo walianza safari ya kurudi nyumbani ambako ndio kwa yule boss, walifika hadi maeneo fulani gari lilzima na kugoma kabisa kuondoka walipojaribu kuangalia wakagundua kuwa mafuta yamewaishia na hawakuwa na akiba ya dumu hata la lita tano tuu, kwahiyo walichokipanga ni kuomba kama gari likipita waombe msaada wa kufika hadi kituo cha mafuta ili wanunue

______kwa boN________
Baadaya mambo yote niliyoyafanya mchana ambayo ni yale mauzauza ambayo yalikuwa yanatokea kwa boss pale nyumbani kwake nilitafuta hadi sehemu ambayo yeye anatumia kwaajili ya kuweka hela zake na kuchota kiasi fulani cha pesa ambacho kiliniwezesha kupata chumba cha kupanga kilichokuwa mbali kidgo na pale kwa boss.
Usiku niliingia katika kile chumba ili nilale lakini nikagundua kuwa ninanjaa sana kwakuwa hapa palikuwa na watu wengine niligonga mlango mmoja na kumkuta bro mmoja ambae alikuwa na mke wake. Aliponikaribisha niliingia na kuuliza mahali ambapo naweza kupata mgahawa ili nipate angalau hata chakula mana mimi ni mgeni katika mazingira haya.
Yule bro akasema ungeenda kuuliza kwa balozi mana yeye ndiye anaejua mitaa yake yote.,., duuh hili jibu liliniudhi sana nikamwambia poa kaka angu nashukuru kwa jibu lako kwaheli nikawa natoka.
Mke wake ambae alikuwa nae kwa mda huo akasema nenda mtaa wa nyuma huo pana ukuta mmoja unataa kubwa hili mlango wa tatu ndio kuna mgahawa. Nilimshukuru kisha nikawa naondoka huko nyuma
Kwahiyo wewe ndio unajifanya unajua sana kusaidia hawa mafara wanaoingilia mitaa ya watu na kutusumbua.
- hata wewe unaweza ukawa fara kinacho kufanya ushobokee nyumba ya watu ni nini  siujenge ya kwako mi mwanaume mingine bhana sijui ipoje((huku msonyo ukisikika)) yaani wewe kabisa una-___---itaendeleaaaaa

Whi am i

WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 07

------utalipa dhambi za mwanao kisha akatoa kisu na kutaka amchinje baba lakini kabla hajatimiza lile lengo lake alishitukia mkono wake ukivunjwa asijue ni nani aliye mvunja ule mkono
Kisu kilianguka chini ambapo wale wenzake baada ya kuona vile wakabaki wanashangaa tuu.
Oya tuacheni uboya ivi mwenzetu imemtokea vile halafu nyie bado tu mnashangaa hebu twende. Mmoja wao aliongea yale maneno kisha wote wakaondoka na kufuata pale aliposimama baba lakini kabla hawajafika ulitokea mwanga fulani mkali sana ambapo kila mmoja akajikuta akiziba macho yake ili yasiumie zaidi.
Walipofungua tena macho yao hawakuweza kuona tena kitu machoni pao, kila mmoja wao alibaki na swali ni nini hiki sasa huyu mzee kaenda wapi

-------Tukirudi upande wa pili baba yupo ofisini anacheka tuu na wafanyakazi wenzake hata hana shida yoyote
;;tumeongea mengi ivi nlisahau kusema. Mda ule umeondoka kuna mzee fulani alikuja na kukuulizia wewe(alikuwa akisema sekretari kwa baba kama bosi wake)
---kwahiyo yuko wapi mbona sijamwona
-kiukweli baada ya kumwambia kuwa haupo na umesema yeyote akifika amngoje, yeye alikuwa mbishi sana hadi akataka nimpe namba yako ya simu ila nimekataa
---huyo mtu yupoje labda
- yeye ni____akiwa anataka aendelee kuongea simu yake ilianza kuita akaangalia aliona ni namba ngeni lakini aliipokea vile vile na kuiweka sikioni
Halo,,, hallo,, haloo mbona huongei
Shit labda niweke loud kwanza,. Baadaya kuongea vile akaiweka simu yake iwe loud kisha kaendelea kisikiliza. Hapo ndio ikasikika sauti
++++NASHUKURU SANA DADA KWA MSIMAMO WAKO LAKINI TAMBUA HAPA DUNIANI HAKUNA JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI, NAMBA NITAIPATA TUU TENA KWA NAMNA YOYOTE ILE. PIA USISHANGAE HII NAMBA NIMETOA WAPI(kisha akavuta pumzi kidogo lakini iliyokuwa ni ndefu na kuendelea) KAMA UPO NAE HAPO SAIZI NAKUOMBA TUU UMPE SIMU ILI NIONGEE NAE KUHUSU MWANAE AMBAE ANAMTAFUTA++++
Maneno hayo yote baba aliyasikia kisha kaanza kwa kusema ndugu yangu najua ndio lengo uniteke mimi kwa jinsi unavoweza wewe lakini sidhani hilo swala kama litakuwa rahisi kama vile unavodhani jipange kwa jinsi unavoweza sawa kwaheli
(mda wote huo kitufe cha kurekodia kilikuwa kimeshikiliwa tena kiufasaha sana kwahiyo yale maongezi yalihifadhiwa)
Baada ya baba kuongea vile kwenye simu kilisikika kicheko

HAHAHAHAHAHAHAHAHAAAAA, HAHAAAAAA YAANI UNAJITIA MJANJA LEO HUKU HAKUNA UNALOWEZA KULIFANYA. HAYABASI UMESEMA SITAWEZA NI KWELI ILA KESHO UKIFIKA KAZINI HAPO NENDA KATOA SADAKA YOTE BILA KUBAKISHA HATA CHENJI KWAHELI  MKUBWA.

Alisema kwaheli lakini simu haikukatwa zaidi zilianza kusikia sauti za kilio. Hadi pale walibaki wanajiuliza kisha ikarudi sauti tena kwenye simu BABA MIMI BIN USIWE NA WASIWASI NA MIMI SASA HUYU NDIO HATA BAADAE HAIONI PUMBAVU ZAKE. Alimaliza hivo kisha ilisikika sauti ya upanga kama umekata kamba na hapo simu ilikatwa.
Pale ofisini ile siku hata kazi hazikuenda kabisa waliamua kujipa off ya wiki moja wawe nyumbani. Basi waliagana kila mtu na kuelekea kwake yule sekretari akiwa njiani alikuwa akiwaza mambo mengi sana inamaana amekufa au, ila isiwe shida sana sikaya taka yeye mwenyewe.
Akiwa anaendelea kwenda ulisikika mlio wa honi ya gari ambayo ilikuwa tayari ipo miguuni kwake kisha zikafuata sauti za jazba sana kutoka kwa dereva wa lile gari
////ivi wewe dada hii barabara ya baba yako,
Jaman samahani sikuwa naona
///hukuwa unaona. Inamaana kuna ukuta hapa si ndio au
Kakaangu samahani kwakweli mawazo yalikuwa mbali sana na hapa naomba nisamehe tu
/// ivi hii dunia sikuhizi sijui imeingiliwa na pepo gani>>>> oya chogo acha uboya mwache tuu bovu huyo tuna chelewa tu hapa au ushamnoki halafu unafanya kumpandishia acha uboya bhana (yalisikika maneno maneno hayo kutoka kwa mmoja ambaye alikuwa ndani ya gari lile)
Haya maneno inaonekena yalimuudhi sana chogo maana aligeuka na kumtupia jicho yule wa kwenye gari kisha akarudi na kuendelea na safari yao sijui walikuwa wakienda wapi.

______kwa bon au ben_______

Nikiwa nimetulia chumbani kule ambako nilipangiwa kukaa siku zote mara wakaingia watu kama wanne ivi wote wakiwa wameshika magongo na kamba. Wakasogea hadi pale nilipokaa huku wakiangalia huku na kule mwingine akaingia hadi bafuni kisha akatoka na kusema ---oya mbona hakuna mtu humu ndani sijui kaenda wapi---
Hichi kitu nilikishangaa sana hadi nikajiuliza inamaana hawanioni au wanaigiza ili waone nitafanya nini. Wakiwa wanaendelea kujadiliana nilienda hadi mlangoni na kufunga mlango kisha nikarudi kukaa kitandani
Wao baada ya kuangalia zaidi wakawa wanaondoka lakini walipofika kwenye mlango walishangaa kuona umefungwa na wasijue ni nani kaufunga huu mlango wakajikusanya wote ili wauvunje
*****nikiwa nimekaa pale mama alikuja na kunipa mavazi fulani ambayo aliniamrisha nivae kwa haraka yeye anaharaka sana nikafanya hivo, kisha akanipa ule upanga na kuupachika nyuma ya mgongo na kunikabidhi kitu kingine kama koti linalofanana na mavazi yale. Vyote nilivipokea kisha akaniambia ben fuata niliyokuambia yote usiache hata mmoja kati yao sawa. Kisha akanikabidhi kitu kama karatasi na kuniambia leo ndio siku yako ambayo ndio unatakiwa uondoke.
Alipoongea vile nilisimama na kujitazama kwenye kioo nikajiona ni ninja. Alinishika na kusema usishituke chukua na hii uivae kichwani ili kuzuia uso wako usionekane, nilipokea na kuvaa kile kikofia ambacho kiliziba hadi uso mzima kasoro macho tuu. Baada ya hapo mama alipotea nilipotazama niliona dirisha lipo wazi nikasogea na kutaka kuruka====huu ujasiri sijui hata ulitoka wapi

Nilifika kwenye dirisha na kuchumpa sekunde chache nikawa tayari nipo nje kwenye bustani za ile nyumba. Nikiwa nipo chini kabisa kuna walinzi walikuwa wakizunguka katika lile jengo mlinzi mmoja akamshitua mwenzie na kumwambia angalia kule. Yule mwenzie alipogeuka hakuona kitu akampiga mwenzie kofi.
Pumbavu kabisa ushaanza utoto wa kutishiana haya nimeangalia kuna nini ambacho ulikuwa unanionyesha kwenye huko tupo kazini hapa jinga
----hichi kitendo kilimshangaza sana yule mwenzie maana amemwona ninja mda si mrefu kwenye bustani lakini tayari hakuna kitu
Waliachana nayo na kuendelea na kazi yao

Kule chumbani wale wakiwa bado wanahangaika kufungua hatimae wakawa wameweza kuufungua ule mlango na wote wakatoka njee huku wakijua aliye watuma hii kazi ndie amewafungia mlango. Baadaya kutoka hatua ya kwanza walienda jumla hadi kwa boss wao ambapo walimkuta amekaa tuu anakunywa kahawa ule mda kati ya wale mmoja alienda na kumnasa kubao yule boss wake. Boss wake aligeuka kwa hasira na kuchomoa pipe akamtandika nayo kwenye ubongo. Kisha akawaambia na wengine huu mfano na mwingine atafuata nani amewatuma huu ujinga. Wote walibaki wanashangaa tuu alinyanyua tena pipe na kuwatandika wote pale kisha akaita walinzi ili watoa yale maiti-----itaendeleaaaaaaa

Who am i


WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 06

-------baada ya kusikia lile neno la usimwogope mtu wa humu ndani, nikauliza wewe ni nani unaesema hayo maneno?
Sikujibiwa tena kitu chochote zaidi ya sauti ya ndege ndio zilianza kusikika mle ndani, nilijaribu  kunyanyuka ili niweze angalau hata kwenda msalani lakini mwili ulichoka sana, sikuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea kulala lakini nikiwa bado pale kitandani nimejifunika ndani ya blanket nilihisi kitu cha baridi kina tembea. Hapo hata nguvu sijui zilikotoka,
Niliruka juu kama nimepata zawadi katika shindano hiyo yote ni baada ya kugundua kuwa alikuw ni nyoka yupo pale kitandani, nilisimama pembeni huku nikiwa najiuliza huyu nyoka kaingiaje niienda hadi mlangoni ili niweze kupata msaada hata wa kutoka nje lakini baada ya kufika mlangoni mlango ulikuwa umelokiwa kwa nje, mama yangu na huyu nyoka itakuwaje sasa mungu nisaidie (niliongea maneno hayo huku nikiwa nasukuma mlango ule lakini sikuweza kufanikiwa kwa lolote) lakini akili yangu ikanituma kwamba tafuta hata chochote cha kuweza kujihami
Nikageuka tena nyuma ili nipepese hata macho mle ndani pengine naweza ona chochote, baada ya kugeuka nyuma macho yalitua moja kwa moja kwenye kona ya nyumba ambapo niliweza kuona ufagio fulani mrefu kwaajili usafi wa chumba nilinyoosha moja kwa moja ili niuchukue nikafaulu kuuchukua hapo ndipo nikarudi tena kwenye lile blanket ili nimtafute nyoka yule.
Nilivuta lile blanket kwa nguvu huku nikiandaa fimbo yangu lakini cha ajabu sikuweza kumwona nyoka tena pale kwenye kitanda sijui aliondokaje ili eneo basi nikaahirisha na kurudisha ile fimbo tena kuwa ufagio nakuenda kuurudisha mahali ambapo ulikuwepo nikiwa nipo pale kwenye kona nikawa nasikia sauti kwa mbali

Ya ndio hili swala sio gumu sana isipokuwa tu sisi tuwe  makini na akili ya na huyu dogo ni lazima tuu afanye kadiri sisi tunavohitaji
Sawa tutakutuma wewe hapo ili ukaandae mahali pa kumteketezea ili liwe ni swala la kimya kimya sana tuelewane hivyo\\\\\////// wakiwa wanaendelea kuongea khohooo!!!!

Waliposikia sauti hii kila mtu alishtuka. Mmoja akasimama na kuja hadi mlangoni kwangu baada ya mm kugundua kuwa kuna mtu aanakauja jirani na mahali ambapo mimi ndio nilikuwepo niliondoka kwa mwendo wa kunyata tena haraka sana na kuelekea bafuni

Alifungua mlango kisha kaingia ndani, nikiwa bafuni kule niliona nae akija katika mlango wa bafu, nilijibana ili nisionekane lakini alizidi kuingia hadi ndani. Nilipata hasira sana nikamuuliza ndugu ulinzisaizi hadi mtu akiwa bafuni inatakiwa alindwe tu. Hakuongea chochote na kuchomoa kisu fulani katika mfuko wake huku akiendelea kunisogelea, nikajua hapa bila kujitetea naweza kupoteza uhai huku nikiwa najiona.

Baada ya yeye kunisogelea hadi jirani kabisa nilipo, nilijikuta naanguka chini kwa kupigwa ngumi nzito ya taya wakati huo aliye nipiga namuona kama wapo wawiliwawili hivi na kizunguzungu dah nilipata hasira sana. Lakini nae bado alikuwa akinifuata tuu nilipo nami nikaanda ngumi nzito huku mkono wangu ukiwa nyuma ya mgongo, akiwa anaendelea kunifuata kwa mwendo wa taratibu alishitukia akipokea ngumi kama jiwe na kuanguka chini huku akiwa hajielewi kabisa kule bafuni ilikuwa ni damu tuu kwa wakati huo. Baada ya kitendo hicho nilitoka nje huku nikiwa nawaza kama amezirai itakuwaje hapa ndani si pata bana lakini basi nikawa natoka nje ya ile bafu kurudi tena mahali pa kulala mara nikaweza kuiona tena sura ya mama huku akipiga makofi na kusema +++safi sana hivyo ndivyo ambavo nilikuwa nataka kuwa sio watu mnaonelewa na watu kama nyinyi hii dunia ya wote bhana.////alionyesha mwenye furaha sana hadi nikashangaa inamaaana anafahamu kilichotokea nilipotaka kuongea nae gafla tuu akapotea

______kwa baba______________

Baba akiwa kazini kule alipigiwa simu ya kwamba mwanae bon amepatikana katika jumba moja hivi ambalo zamani sana katika historia walikuwa wakiishi watu wan chi nyingine ambao wamekimbia kutokana na matatizo mbalimbali(wakimbizi)

Baba alifurahi sana kupata hizi taarifa akaomba ruhusa pale ofisi kwa wenzake

- jaman naenda mara moja mahala nimepigiwa simu sasa hivi tuu nitakuwa hapa akija mtu mwambie aningoje kisha akaondoka na kupotelea
****alipoondoka tuu kuna mtu akaingia pale

samahani nilikuwa na shida ya kumwona mpl sijui nimemwona
Hapana halafu katoka sasa hivi ila amesema yoyote atakae fika amsubiri hapahapa kwa maana anarudi sasa hivi tuu unaweza ukakaa tuu hapo (alimwambia huku akimwonesha kiti ili akae) lakini yule mgeni akauliza unaeza niambia ameelekea wapi?
Hapana kiufupi hajasema ni wapi ameenda ila wewe msubiri tuu labda kama shidayako sio ya mhimu sana(secretari alijibu tena vile)
Ninaharaka sana basi ningeomba unisaidie hata namba yake ya simu tuu (aliongea yule mgeni)

------hapo sekretari alishituka huyu mgeni kwa nini ni kingang;anizi namna hii hapa kuna kitu sio bure

Kiukweli mimi hapa sina ruhusa ya kutoa namba yake labda angenipa ruhusa ndio ningetoa. Baada ya sekretari kusema vile yule mgeni aliondoka ikiwa inaonyesha kabisa kwamba hajafurahishwa hata kidogona majibu ya sekretari,
Lakini kibaya zaidi yale mazungumzo yao yote kuna sehem maalum ambayo waliiset mnapoongea mkianza na salamu yenyewe inaanza kurekodi, kwahiyo yale mazungumzo yote yalirekodiwa na kile kifaa

****************
Baada ya baba kufika lile eneo ambalo alipigiwa simu kwamba yupo bon alifika pale na kuita lakini palikuwa kimya kama hapaja wahi kukaliwa na kitu chochote chenye kutoa kelele yoyote ile
Bon bon bon
Bon aliita mara kadhaa lakini hakuweza kuitikiwa akaamua arudi tuu kazini lakini alipogeuka nyuma mara moja akakutwa ameshazingirwa na kundi fulani la watu. Baba alibaki ameduwaa asijue ni nini atafanya mara kila mmoja wao akaanza kumsogelea baba hadi pale alipo huku wengine wakiongea lugha isiyo eleweka, na mmoja ndio aliongea Kiswahili
(((((((mzee tuna busara sana lakini kwa kitendo ambacho mwanao amekifanya kwa mwenzetu kwakweli hatuwezi kufumbia macho hata kidogo
(huku akitoa kama sauti ya kulia) amuue ndugu yetu sisi ivi mnajua sisi ni akina nani katika huu ulimwengu nianuwezo wa kukugeuza kitoeo tena kwa kukumaliza m bichi kabisa lakini sitaki
,wakati huo wote baba alikuwa hawaelewi ni nini wanaongea mana kama ni mwanae bon anajua kabisa alipotea katika mazingira ya kutatanisha halafu wao tena wanaongea kuhusu tena.
Yule aliyekuwa akiongea kwa uchungu sana akatoa kisu na kusema hapa naona tunapoteza tuu mda utalipa dhambi za mwanao mzee sawa kisha aka-------itaendeleaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Who am i

WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 05

------kwa jinsi alivokuwa akiniangalia nilijua kwamba dhahiri inawezekana tayari ameshaniona na ule upanga ambao nilipewa na mama, lakini cha kushangaza alianza kuongea habari nyingine kabisa licha ya kuwa zilinishtua lakini ilikuwa ni tofauti na ule upanga .

Kijana wangu nimekufata huku mimi kama mimi na hakuna anaejua kuwa mimi mda huu nipo huku nisikilize tena kwa umakini,
Najua nyumbani kwenu mama yako alipotea katika mazingira ambayo hakuna aliyeweza kuelewa ni wapi mahali ambako ameenda, ila itatakiwa utambue kwamba babu yako na bibi yako kipindi kile wamekuja kule kuwasalimia lengo lao haikuwa ni kuwasalimia ila ilikuwa ni kumpoteza mama yako, samahani kwa kukwambia hili( alivuta pumzi kidogo kisha akaendelea) mama yako hadi saizi sio binadamu kama binadamu wengine, unaweza ukabahatika kuonana nae na akakupa chochote cha kujilinda hebu pokea hata usikatae,
Kwa maana, walipogundua kwamba anampenda sana mwanae ambae ndie wewe, walichukua uamuzi wa kukuteka na wewe huku wakitumia uso wa baba yako ambao ulifanya kutengenezwa kama aina fulani ya kofia, nimekuja kukwambia haya kwamaana wewe bado ni mdogo na mambo watakayo taka kukukabidhi sio mema kwa kuishi na wenzio(alisimama na kuanza kuondoka huku akisema) naomba uyashike sana haya maneno kijana wangu.

*****nilishtuka sana pia nikabaki nikijiuliza inamaana huu upanga hauonekani au/////lakini sikukazia sana kuhusu hilo swala
Baada ya dakika chache usingizi ulinipitia

****usiku nikiwa nimelala nilianza kuota*****
+++++++++ hebu nyanyuka acha uzembe wewe utakuja kufa kizembe wewe, sa a awa naanya nyuka, (nilinyanyuka huku nikiwa nimechoka sana lakini huyu hakuwa na huruma kabisa++++haya ruka hizo kamba moja baada ya nyingine tena kwa sekunde ishirini tu ole wako ufeli mana kule chini kuna joka linalokula nyama za watu wazembe, kusikia hivo nilifanya kadiri nilivyoambiwa sijui hata nguvu zilitokea wapi niliruka kambamoja hadi nyingine hadi nikawa tayari nimeshafaulu lile zoezi na kujikuta nipo upande wa pili chini nilipoangalia niliweza kuuona ule upanga ambao nimepewa na mama kule chumbani. Roho ya kuokota sijui hata ilikotokea niliuokota ule upanga na kusimama toka pale chini nikiwa sifahamu lolote.. alitokea kiumbe fulani wa kutisha sana mwenye miguu minne na mkia mrefu mrefu wenye kushiba sana, hapohapo nilianza kuogopa nikasahau kuwa nilishika upanga, kile kiumbe kilianza kunisogelea huku macho yake yakiwa na rangi kama taa inayotoa mwanga mwekundu,
Nilianza kurudi nyuma kwa uoga sana(BON TUMIA HUO UPANGA KUPAMBANA NA HICHO KIUMBE KITAKUTEKETEZA) hii sauti hata sikuelewa ilikotoka lakini ndio ilinikumbusha kuwa nina upanga mkononi

Kile kiumbe kiligeuka kwa kasi ya ajabu na kuuzungusha mkia wake, niljitahidi kuukwepa usinipate lakini jitihada zangu hazikufanikiwa haa kidogo,
Ule mkia ulikita vyema katika mgongo wangu nikajikuta nikirushwa kule huku nikibaki na maumivu makali sana katika mgongo wangu,. Nikiwa bado pale chini nikasikia sauti nyingine tena ikisema UKIFANYA UZEMBE UMEKUFA BEN
Nilinyanyuka tena kwa spidi huku nikiangalia huku na kule kama yule kiumbe anakuja tena lakini niliweza kusikia tua sauti kubwa ya kutisha ukitoka katika pori la upande pili
\\\aghrrrrrrrrrrrrrrrr aghrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr aghrrrrrrrrrrrrrrr
Kwa kusikia hivo nilifahamu dhahiri ni yule kiumbe anataka kuja kwa mara nyingine, na kweli baada ya mda mfupi kilisikika kishindo kikubwa hadi tetemeko kisha yule kiumbe akaokea tena huku anafuka moshi kwenye matundu ya pua lake ambayo usingeweza kutofautisha na shimo la toilet(choo) kwa wakati huu uoga wote niliutupia kule na kujipanga ili nipambanane na huyu kiumbe.
Hili likiumbe lilitoka kasi sana huku likinyoosha kwangu, na mimi kwa ustadi mkubwa niliruka juu kama mita kadhaa huku nikiwa na upanga wangu kisha nikakadiria kwenye jicho moja la yule kiumbe,
Ule upanga ulipoingia tuu katika lile jicho kiumbe hiki kilianguka chini PUUUUU ambako tetemeko lililotokea msitu mzima ilikuwa ni vumbi tuu na baadhi ya miti ilianguka. Nikajua nieshamaliza kazi ya kumuungamiza huyu kiumbe, niliyanyua upanga wangu na kuanza kuondoka,
Lakini kabla sijarusha hata hatua kumi ardhi ilianza kutetemeka upya hadi nikahisi kizunguzungu, nilipogeuka nyuma kile kiumbe kiliamka tena huku macho yakiwaka moto halafu kinanifuata, nilijikuta nikipiga magoti kumwomba mungu anisaidie, kisha nikasimama tena kujiandaa kupambana tena, safari hii ikikuwa kila nikiruka najikuta navutwa chini kinachonivuta hata sielewi,
Lakini nikapata akili nyingine, niliporuka tena nikavutwa chini, nilitanguliza ule upanga nikashangaa kuona upanga hauja fika chini na mimi nikiwa juujuu, hapo nilidank na kutua kwenye mti nikaudaka kama nyani vile kisha nikajirusha hadi mgongoni mwa yule kiumbe, nilivuta pumzi ya kutosha kisha nikauchomeka ule panga mgongoni.
Fuuuuuuuu ni sauti ambayo ilisikika huku vitu kama maji yakitoka mule mgongoni kwa yule kuimbe. Kumbe aliendelea kufumuka mana yale maji yalukuwa ni mengi nikiwa sijakaa vizuri nilirushwa juu******

Nikazinduka kutoka usingizini huku nikiwa nimechoka kuangalia mkono wangu ulikuwa umeshonwa ikionyesha kwamba kuna kitu kiliuchana, kiukkweli nilikuwa na maumivu makali sana katika mwili wote. Nilitaka kuingia bafuni lakini mwili hata kutembea ulipata uvivu maana ulikuwa na maumivu sio mfano yani

Nililala hadi akaja kuniamsha yule baba ambae anatumwa alitumwa mara kwanza aniletee chakula.
Kijana chakula chako hicho(aliongea huku akiwa anasogeza kimeza fulani cha kusukuma jiran na mimi, ilikuwa ni breakfast.
Baada ya kuweka yeye aliondoka nikasikia sauti ikisema hebu kula hakina madhara hicho, mpaka sasa nilishatambua kwamba hii ni sauti ya mama ndie ambae mara zote ananipa taarifa kwa njia ya sauti.
Basi na mimi kwa fujo nilikunywa ile chai kwa haraka sana kwa maana nilikuwa na njaa isitoshe jana nimekataa kula kwa sababu ya mawazo. Dakika tano zilitosha kabisa kumaliza vitafuno vyote mikate mitano na chupa nzima ya chai.
Nilimaliza kula kisha nilianza kujishangaa nawezaje kumaliza chakula chote hiki mimi tuu ila basi nikapotezea na kurudi tena kitandani.
Yule baba alikuja na kutoa vyombo kisha akaondoka alipoondoka tuu mama alitokea, kisha kaniambia pole kwa kazi uliyofanya
Mama kazi gani tena mi nililala mbona
- ulilala angalia huo mkono umeumia kwa sababu gani
Mmmmh mbona hata sielewi halafu nimechoka kweli yani
- ok najua wewe umeona ni kama ndoto lakini hadi sasa uwezo wako wa kupambana ni mkubwa sana, kwahiyo utakaa humu ndani kwa wiki moja ambapo nitakuwa nikifanya mpango wa kukutorosha. Chukua hiki kitabu kina list ya watu wabaya wote wanaohusika na kuupoteza ukoo wetu utaanza na mmoja  baada ya mwingine iweke iwe siri yako tuu. Najua nikigundulika nitatolewa kabisa hata katika hii hali ambayo nipo nayo kwaheli(mama alipotea huku akiwa kaniachia kidaftari fulani kidogo) lakini mara ghafla nikasikia sauti USIMWOGOPE MTU WA HUMU NDANI---itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Who am i

WHO AM I (mimi ni nani)
Benchrys
No. 4

-------niliamka na kuangalia mahali ambapo naweza kwenda kupata angalau hata maji ya baridi ili nipooze huu mwili, huku nikijiuliza hivi hii ndoto inamaana au la mbona siielewi. Lakini nilipojipapasa shingoni ni kweli nilihisi kuna kamba mbili zenye vigorori tofauti hapo ndipo niliweza kugundua kwamba ile hata haikuwa ni ndoto bali ni kitu cha ukweli.
Kiukweli hapo nadhani nilihis hadi kichwa kuniuma maana mawazo niliyoanza kuyapata hata stress za maisha nilihisi nindogo but zangu ni too much
//////inamaana mama yupo huku, kaletwa na nani,)))))nilikuwa nikiongea hayo hukunimeshikiia zile kamba huku nikiwa hata siamin kama ni kweli kamba zimeongezeka shingoni mwangu_____

Baad ya hapo niliondoka na kuingia bafuni, ambapo bafu ilikuwa mlemle ndani ya kile chumba cha kulala mmezoea kuita master,
Nilianza kuoga maji ya baridi yale lakini baada ya dakika chache maji yalianza kutoka ya moto hadi nikayaloki tena kwa kunyonga ile koki ya lile bomba la bafu. Kisha baada ya kutulia sekunde kadhaa niliifungulia tena, ambapo mda huu yalitoka maji ya baridi,. Nilioga na baada ya hapo nikarudi tena kitandani ili kuutafuta usingizi.
Masaa yalipita lakini sipati usingizi kwasababu macho yalikuwa ni makavu sana hali ambayo sikuielewa. Nilikosa raha kabisa kisha nikaamka na kuanza kuzunguka zunguka tu mle chumbani nikiwa hata sielewi chochote kuhusiana na lile jumba.

Nikiwa naendelea kuzunguka mle ndani uliingia upepo fulani mwanana ambao ulinifanya nikakae tena kwenye kitanda ndipo macho yalianza tena kulegea ili kuuita usingizi. Taratibu nilijilaza pale kitandani huku nikifurahia ule upepo na macho yangu yakianza kujifumba. Laikini gafla nikasikia sauti ikiniambia *****BON MWANANGU USILALE USILALE USILALEEEEEEEEEE NASEMA UKILALA UTATIMIZA NDOTO ZAO KIULAHISI SANA NISIKILIZE MAMA YAKO*** na mimi baadaya kuisikia ile sauti niliamka tena kwa kushtuka kama nilikalia mwiba kwa bahati mbaya.

-------nyumbani kwa baba nae hali ilikuwa sio shwari kabisa

Akiwa amekaa sebulei huku akiwa na mawazo mengi sana juu ya upoteaji wa familia yake mara akasikia kama mtu anagonga mlangoni
Ngongongo!!!!!
-nani,
Ngongongo
-nauliza nani wewe(aliuliza hivo baba) lakini hakuna jibu alilopokea lakini ilikuwa ni mwendo wa kugonga tuu, hakutaka kufungua mlango wakati mtu hajitambulishi ndipo akabaki amekaa tuu huku akiwaza mambo mengi sana, na baada ya mda akaondoka na kuelekea chumbani kwake akalale maana mda ulikuwa tayari umeshaenda sana, ilikuwa ni saa sita kasoro robo na kwakuwa iltakiwa kesho aende kazini mapema nab ado alikuwa na ratiba za kwenda kituo cha matangazo ili akaombe tangazo la kupotelewa mwanae bon, ilimpasa alale mapema tu.
      Usisngizi ulimchukua mapema kabisa akalala fofofo*****
WEWE KAMA MZAZI UNAEMPENDA SANA MWANAO NAKUSHAURI USIFANYE HILO UNALOLIWAZA NILISHAKWAMBIA HATA KULE OLE WAKO UTANGAZE KUHUSU KUPOTELEWA NA MWANAO. NA KWAMBIA MTAPOTEA WOTE NIELEWE HIVO*****
Yalikuwa ni maneno ambayo baba aliyakumbuka wakati ule akiwa amelala alishtuka kutoka usingizini na kukaa lakini akashangaa kuona chumba kizima ni giza totoro, akaanza kupapasa simu yake ili awashe tochi ya simu alipoiona akawasha nakuenda kuangalia pengine unit ziliisha kumbe umeme ulikata usiku ule.
Usiku huu baba hata hakulala alikesha hadi asubuhi na asubuhi aliamka na kwenda kazini kama kawaida.

_____upande wa bon kule katika jumba la watu
Nikiwa nimekaa nilihisi nashikwa mkono lakini nilipogeuka kuangalia katika chumba nilkuwa mimi pekeyangu, lakini cha ajabu hata sikushituka kuonyesha hali ya kuogopa. Baada ya hapo nikaweza kuiona sura ya mama akiwa kashika upanga katika mkono wake huku akiunyanyua juu kisha akaukitisha hewani tuu, ndivyo ambavo mimi nilikuwa nikiona na baada ya hapo akapiga magoti huku akiwa kashika ule upanga huku akifanya kama anajutia alichokifanya kwa wakati ule.
Baada ya hapo alisimama toka pale alipopiga magoti na kunifuata huku akinikabidhi ule upanga. Mwanzo nilitaka kukataa lakini akaniambia bon usipokubali kupokea huu upanga inamaana utakuwa umethibitisha na baba ako kule nyumbani aweze kupotea kama mimi nilivopotea, huu upanga utakulinda wewe pamoja na baba ako au wanandugu wengine.

Sasa ndio nitaupokea huu upanga na kuutumia hata sujui kutakuwa na maana yoyote hapo(nilimuuliza vile mama) ndipo akaendelea kusema kwamba nitakupa ujuzi kwa njia ya ndoto ili asiwezekufahamu mtu yeyote lakini nitakuomba uzingatie mambo nitakayo kwambia yawe ya muhimu sana maisha yako maana mimi hapa sio binadamu kama binadamu wengine kwa hiyo siwezi kurudi kwenye ile hali yangu ya zamani na sijapenda na nyie mpotee kama mimi. Baba yangu na mama yangu ndio visababishi wakuu wa hili jambo, shida yao ni watu wa kuwatumia katika kazi zao ili wafanikiwe katika kazi zao, baada ya kukupa mafunzo ya kuutumia huu upanga nitakutoa hapa ndani. Usiulize ntakutoeje/alimaliza mama kwa kuongea yale lakini bado nilikuwa na shauku ya kujua nilipotaka kuuliza swali jingine sikumwona tena mama tayari alikuwa ameshapotea machoni pangu huku akiniachia ule upanga.
Nikiwa pale kitandani nimeshika ule upanga mlango wangu ulifunguliwa kisha akaingia mzee fulani mwenye ndevu nyeupe, nywele nyeupe hadi kope zake zilikuwa ni nyeupe, nilibaki natetemeka pale ndani huku nimeushika ule upanga maana nilijua tayari amesha uona tayari kwa hiyo itakuwa shida ikiwezekana watanishtukia kwamba naongeaga na mama.

Yule mzee alinisogelea jirani kabisa kisha akakaa kitandani pale na kuanza kuongea, mbona ni usiku lakini hulali tuu? Nikiwa nataka kumjibu simu yake ilianza kuita akatulia kidogo na kutoa simu mfukoni kisha akaipokea
Ndio bwana mkubwa, aaah ndio, eheeee tayari kabisa hata usipate shida,, aaaah no so hivyo ndio, ndio ehee, ok sawa,. Nilimsikia tuu akiongea hayo maneno katika simu yake aliyo ipokea, sikuelewa mazungumzo yao yalikuwa yakihusu nini au yakimhusu nani.

Alivo maliza kuongea akatoa simu tena sikioni na kuishusha hadi kwenye kitanda kwa wakati huu hakuiweka mfukoni, alipoiweka kitandani akanigeukia mimi huku akiwa ametoamacho hata yalikuwa na ya kizee lakini yalionekana yakiwa yametoka

Duuh nahisi atakuwa tayari ashauona huu upanga sijui ntafanyaje hapa (nilisema pekeyangu hayo maneno moyoni ambapo sikjua hata cha kuamua kwa wakati ule lakini nilijikaza na kubaki nimekaa vilevile nione atasema kitu gani. Nae alinyanyuka na kukaa upande nilioweka lile panga kisha-----itaendeleaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

#panga_ameliona_au_hajaliona_mimi_na_wewe_hatujui_kabisa

Whi am i

Who am i(mimi ni nani)
Benchrys
03

------nilishtuka baada ya kuona picha ya mtu tofauti ambae hata sikuwahi kumwona katika maisha yangu pia nilijawa na maswali mengi sana kichwani mwangu hadi nikahisi kuchanganyikiwa kabisa,,,,, usoni mwake alikuwa kavaa ngozi ambayo inasura halisi ya baba yangu lengo nadhani ilikuwa ni kurahisisha kazi yake ya kunipata waondoke na mimi.

*****gari ilitembea kwa spidi sana hadi maeneo fulani ambapo palikuwa na magorofa mazuri sana na magari mengi zaidi. Lakini katika kichwa changu hata kama nilikuwa nikiviona hivyo vyote mawazo yangu hayakuwa kabisa katika maeneo yale, ila tuu nilikuwa nikiwaza kwa kujiuliza hawa ni akina nani na kwanini waniteke kwa namna kama hii isitoshe huku ni wapi hata sifahamu(ni baadhi ya mawazo ambayo nilikuwa nayo kichwani) baada ya hapo niliteremsha mkono wangu na kuuingiza katika mfuko wangu ili niipate simu lakini nilishangaa kuona simu yangu haipo tena hapo ndipo nikasema kweli kama ni uchawi upo mana tangu nakaa humu kwenye gari hakuna aliyeweza kunigusa katika nguo zangu ama mwili wangu, lakini basi ikanibidi nitulie huku nikiwaza kama baba inatakiwa ajue wapi nipo sasa nitapataje mawasiliano nae----nikiwa bado naendelea kufikiria vile aliingia mzee mmoja hivi ambae uso wake ulionekana kuwa kama alishawahi kuungua na moto, mana alikuwa anatisha sio kidogo kisha akanambia kijana kaa tu chini kuwa huru jisikie upo kwenu sawa, wala usijekuwa na woga wowote kiti hicho hapo special for you kitumie tuu,, kisha akakivutia kile kiti jirani na mimi ili nikae

     Samahani kwanza naombakujua hapa ni wapi na nimeletwa kwa sababu gani tena kwa misingi ipi mana hadi sasa siwaelewi////nilimuuliza hivo yule mzee licha ya kuwa nilimwogopa lakini nilijikaza tuu kuuliza lakini baada ya kuuliza vile cha ajabu yule mzee alianza kucheka     hahahahahahahaaaaa tehteheteh kisha akaongea kwa sauti kubwa sana kijana hayo maswali utayajua huko mbeleni majibu yake yote cha msingi wewe saizi fuata tuu kila unachoambiwa tena kuwa mpole. Baada ya kuongea maneno yale akatoka na kuelekea katika sehemu fulani ambayo ilionekana kuwa inamlango, nikakumbuka kuwa naitaji mawasiliano na baba nilifuata hadi pale alipopotelea lakini nilipofika pale nilichokiona ni korido ndefu sana lakini sikumwona mtu yeyote pale. Hii too much sasa nitawasilianaje na baba mimi dah(ni maneno ambayo nilijikuta nikiyasema pekeyangu pale ndani muda ulienda sana huku nikiwa pale sebuleni nilipopepesa macho niliiona saa ya ukutani ambapo ilisema kuwa ni saa moja na robo usiku. Kwakweli hii siku kama ni kujiona ni mdogo kuliko kirikuu hii siku ndo ilieleza wazi kabisa kuwa kweli mm ni mdogo mana sijawahi kushindishwa ndani kama hivi nikiwa sina mawasiliano na mtu yeyote yule

////nikiwa nimekaa aliingia baba mmoja na kuleta chakula kwenye meza pale huku akiniambia ni cha kwako hiki kwahiyo inatakiwa nikile, lakini nikamjibu tafadhari sina njaa hapa nilipo kwahiyo hicho chakula kirudishe tuu hukohuko, alijitahidi kunilazimisha lakini nilikuwa ni mbishi sana hadi akaona sasa hakuna njia ni bora nikampe tuu majibu aliyenituma kuwa umekataa kula chakula ila na mimi sikuchelewa nikamjibu ni kweli nimeshiba sana hapa nilipo kwahiyo sina haja ya kula muda kama huu. Alinyanyua kile vyombo vyake na kurudi navyo kule ambako ametoka navyo;;;;;;hii nyumba tangu nafika hadi masaa yameenda hivi sijafanikiwa kukujua hata chumba kimoja huku nikiwa sina mawasiliano na mtu yeyote

-------huku nyumbani baba alikuwa akihangaika sana kupiga namba yangu lakini haipatkani .hivi huyu leo kaenda wapi hadi saivi harudi tuu au kuna jambo limempata huko shuleni (yalikuwa ni maswali ambayo baba alijiuliza kule nyumbani na baada ya hapo akaamua kuondoka na kwenda mtaani ili kuulizia kama kuna mtu aliyeweza kumwona bon sehemu yoyote sehemu ya kwanza ilkuwa ni joel ambae nilikuwa ninaurafiki nae wa jirani sana
---jamani wenye nyumba hodiiii
-karibu haa baba bon kulikoni leo mda kama huu,, ilikuwa ni sauti ya baba ake na joel baada ya kumpokea baba aliuliza hivo kwakuwa haikuwa kawaida ya baba kuonekana mtaani au kwa jirani mda kama ule
---najua utakuwa unashangaa kuniona mda kama huu kwako samahani eti naweza kumwona joel au tayari kalala (aliuliza hivo baba)
- kalala lakini naweza kumwamsha tuu hakuna tatizo ila kuna tatizo limetokea au maana ni bora tukashirikishana mapema(aliongea baba joel)
---ndugu yangu kwakweli hapa hata sielewi kabisa bon tangu asubuhi aondoke bado sijaweza kuiona sura yake kabisa na sielewi ni wapi atakuwa yupo na ndio maana naomba kuongea na joel

\\\\baba ake na joel alisimama na kwenda moja kwa moja hadi chumbani kwa joel huku akimwacha baba kwenye sofa pale sebuleni

++++++++HUNA HAJA YA KUHANGAIKA KUMTAFUTA KIJANA WAKO YUPO MAHALI SALAMA KABISA TENA USIJARIBU KUMSHIRIKISHA MTU YEYOTE KWA MAANA ITAKUWA NI HATARI KWA MAISHA YA WOTE WATAKAO WEZA KUFAHAMU KUHUSIANA NA HILI ANAEJUA HADI SASA KUHUSU KUTOKUWEPO KWA BON NI WEWE NA BABA JOEL SASA NAKUAMBIA ONDOKA HARAKA ILI HATA AKIJA AJUE ULIMTANIA TUU+++++++ Hii sauti aliisikia baba akiwa amekaa pale sebuleni muda ule baba joel yupo kumwamsha joel lakini joel nae hakuamka kabisa alionyesha kuwa anausingizi mzito sana hii siku jambo ambalo hata baba ake alilishangaa na kuondoka kule chumbani lakini alipofika sebuleni hakuweza kumwona tena baba na yale mawazo ya kuwa kulikuwa na kuulizia kuhusu bon yalishapotea akendelea kufanya yake,,,*

****usiku nikiwa katika hili jumba ambalo hata silijui vizuri alikuja baba mmoja na kushika mkono kishakanambia njoo nikuonyeshe chumba chako cha kulala namimi nilisimama na kuongozana nae had kule kwenye chumba baada ya kukabidhiwa kile chumba nilipokea funguo kisha yeye akaondoka. Niliegama kidogo tu kwenye lile godoro hata dakika haikuisha nilishikwa na usingizi usiku nikiwa nimelala

__________ben mwanangu hiyo kamba uliyopewa na bibi yako naomba uifanyie marekebisho maana imekufunga baadhi ya mambo kuyafahamu ila utajua kama ukifuata ninachokuambia hapa muda huu hebu nizingatie mama yeko
     Kuna hizo gorori tatu nyekundu, kijani na nyeusi hiyo nyeusi fanya uwezavyo uichomoe kisha tupia katika dirisha la chumba chako na hiyo nyekundu itengenezee kamba nyingine kisha hiyo ya kijani iache iache humo humo katika hicho kidan naomba uanze hiyo kazi nikiwa nakuona hata mimi. Nilifuata maelekezo  yote kadiri nilivoambiwa lakini kamba ya kutengenezea kingine ndio sikuweza kupata akatoa kamba fulani nyekundu na kunipatia niliipokea na kuvalisha kile kigorori. Kisha mama akaniambia nitakuja wakati mwingine______hiyo ilikuwa ni ndoto!!!!! Nilishtuka pale nilipoegama huku mwili ukijawa na jasho sana hadi nilijishangaa, baada ya hapo niliamka------itaendeleaaaaa

benchrys.blospot.com

Who am i

Who am i(mimi ni nani)
Benchrys
No 2

.niliitika naam ilikumsikiliza ambacho anataka kunambia kwa mda ule lakini bado hakuweza kusema chochote nikahisi hapa baba kuna kitu lazima ananificha hataki kuniambia na ni kwanini hatakama nilikuwa mdogo sana lakini niliweza kugundua hicho kitu ila sikutaka kumuuliza kwanini ananificha baada ya hapo baba akaondoka na kuingia kule ndani bila hata kusimama ishara ya kusita na kisha akakaa mda kidogo na kutoka tena nje, baada ya hapo tulifanya kinachotupasa hadi inaingia giza utaratibu kwa mda huo ukazoeleka licha ilikuwa ni ngumu sana baba anapoenda kazini lazima na mimi niwe nyuma hadi nilipoanza kukuakua ndipo niliachwa nyumbani pekeyangu kisha nilipelekwa shuleni kuanza awali miaka ilienda hadi nilihitimu shule ya msingi na kuchaguliwa katika shule ya kata yetu.
Siku moja mwalimu wakiswahili alitoa kazi ya kuandika historia ya maisha kiufupi ila alikazia kusema kwamba iwe inahusu sana wazazi wako vingine hata havitaki viwepo katika historia hiyo, kati ya siku ambazo niliona mwalimu ametoa mtihani mgumu ilikuwa ndio ile siku maana kazi ilikuwa na masharti ya kutosha kwamba tumiakaratasi zaidi ya nne kwa upande wangu nikijiangalia mwandiko wangu ni mdogo kana kwamba katika historia yangu naweza nikaandika tuu mistari hata kumi isifike kiufupi cha kuandika sikujua sana lakini sikuwa na namna niliandika kinacho takiwa nikiandike. Ulifika mda wa mwalimu kuja ili azipitie zile kazi ambazo alitupatia ili tuweze kuzifanya watu walijaza karatasi nne upande na upande lakini mimi niliandika hata nusu ya karatasi moja haikufika kitendo ambacho wanafunzi wengi waliokuwa jirani na mimi pale darasani walianza kushangaa na kuniuliza kuwa ninautani na mwalimu..

****ok nadhani huu ndio mda wa kila mwanafunzi kuja hapa mbele tutaenda upande kwa upande, haya tuanze na upande upi,,aliongea vile mwalimu na kuwaachia wanafunzi waanze makelele ya kuchagua upande wa kuanza zilikuwa kelele kama dakika mbili kisha uamuzi ukatolewa kwamba upande wa mlangoni ndio unaoanza na upande huo ni upande ambao hata mimi nilikuwa nikikaa alitoka msichana mmoja kwa jina la Katherine ambapo wengi tulizoea kumwita cath akaenda mbele kwa mbwembwe za kutosha na kuanza kutoa historia yao huko nyumbani wengi walipiga makofi baada ya yeye kumaliza kutoa ile historia yake kisha akarudi kukaa kwenye dawati lake la kwanza huku akifuatiwa na mwenzake jully ambapo nae alitoa hisoria yake nae wakampigia makofi zamu iliyofuata ilikuwa ni zamu yangu bon kama nilivyo sajiliwa huko shuleni karatasi ile niliyoiandika historia yangu sikuichukua nikaiacha palepale kwenye meza yangu na kuenda mbele hukunikiwa mikono mitupu mwalimu alingaka na kusema bon utani na wanafunzi kama wewe hata sihitaji niligawa karatasi za kutosha ili kila mmoja aandike historia yake,,aliongea hivyo yule mwalimu na kumalizia kuwa rudi kwenye meza yako na uichukue hiyo karatasi
Sikuwa na namna nikarudi kwenye meza yangu na kuchukua ile karatasi kisha nikaenda nayo mbele ilikuwasomea wanafunzi historia yangu
//historia yangu hakuna ambae ilimpa furaha zaidi ya masikitiko na maswali kibao ambayo hata mimi mwenyewe majibu yake siyaelewi laiti wangeamua kuniuliza
Nilipokuwa nikianza kusoma historia mwalimu alikuwa kasimama lakini nilipomaliza ile historia mwalimu alikuwa kakaa kwenye meza yangu kama mwanafunzi huku akionyesha ananifuatilia kwa umakini sana baada kumaliza alisimama na kuvuta pumzi ndefu kisha akasema ok inatosha njoo kwenye meza yako na ndio maana ya kwenda mbele bila karatasi

_______miaka ilikatika  nilhitimu kidato cha nne lakini sikufanikiwa kuendelea----
Baada ya hapo baba alinishauri kurudia kufanya mtihani lakini roho yangu iligoma kabisa nikamjibu kwamba labda niende veta hakupinga kisha nikaanza kusoma
,,,,,miaka mitatu ilikatika karibia kumalima yale mafunzo ya vet course ya umeme wiki moja likiwa limebaki baba alinifuata na kuniambia nafahamu nini kuhusiana na mama yangu nikamjibu kwamba sijui lolote maana tangu aondoke nikiwana miaka mitatu sikuweza kumwona lakini nilikuwa tuu na kumbukumbu kuwa aliondoka baba akasema ukihitimu nitakupa maelezo yote, kwakuwa aliniahidi yeye mwenyewe sikuwa na la zaidi nilikubaliana nae na kuondoka

siku ya kukaribia na mahafari yetu pale shuleni kila mtu alikuwa bize na yake ambapo mimi nilienda mjini kwa aajili ya kutafuta baadhi ya mahitaji, nikiwa sina hili wala lile kuna gari ilikuja na kusimama mbele yangu huku mle ndani kukiwa na sura ya baba yangu naiona akaniita niingie mle ndani ya gari. Sikuleta ubishi nikaingia ndani na kukaa kwenye nafasi niliyoonyeshwa kisha gari ilianza kuondoka,, tulitembea umbali fulani kisha nikaona yule mwenye sura ya baba yangu mzazi kama anavuta nywele zake baada ya mda alitoa zile nywele na kuweka pembeni nilipomuangalia haikuwa sura ya baba tena.....itaendeleaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Who am i

Who am i(mimi ni nani)
Benchrys
No 1

Katika kijiwe fulani kulikuwa na vijana sita wamekaa huku wakipiga stori zao kama kawaida jion baada ya shughuli za mchana. Lakini katika wale vijana sita kuna mwenzao mara nyingi alikuwa kimya pia ni mnyonge sana kitendo ambacho kiliwakwaza wenzie na hata kuanza kumwongelea yeye nae akiona wanamwongelea alikuwa akisimama na kurudi zake nyumbani bila hata sappota ya wenzie. Lakini wao bado hawakujua ni kwanini hapendi sana story na watu au hajisikii kwanini kuongea ovyo mda mwingi......

________songa nayo________

Nafahamika kwa jina la bon ni jina ambalo kila mmoja analifaham hata mtaan wengi huniita jina hilo lakini katika hali ambayo kila siku najiuliza na kukosa majibu ni pale nikitembelewa na babu au bibi huniita ben mara nyingi kipindi cha mwanzo sikuwa naitika kwasababu sikujua ni nani huyo ben lakini baada ya kuzoweshwa na babu hilo jina nikawa naitika tuu endapo amekuja yeye kutoka kijijini.

*****Ilikuwa siku moja bibi na babu walikaa sebuleni ghafla tu mama akaanza kujisikia kizunguzungu hali ambayo ilimtoa hadi nje ya nyumba na hakuna ambae aliweza kutambua ni wapi kaenda upande wangu nilikuwa bado mdogo sana hata akili ya kusema nifuate sikuwa nayo, baada ya mama kutoka nje kwangu mimi nilitegemea atarudi baada ya mda mfupi tuu ila hayo yalikuwa ni mawazo yangu tuu na ukweli hata haukuwa hivo ilifika hadi jion baba anatoka kazini lakini mama bado hajarudi ndipo tukaulizwa swali na baba
,,,,Mama bon kaenda wapi mbona simwoni humu ndani. Na majibu yakawa kama hivi
Babu..alitoka nje mara moja nadhani atarudi sasa hivi
Bibi..wew unawasiwasi gani yule sio mtoto hapa anapafahamu kwahiyo atarudi.

Lakini baba aliendelea kuuliza mbona siyo kawaida kuchelewa kurudi namna hii, aliwaaga anaenda wapi alipoondoka.. hapo babu na bibi wote hawakutoa majibu baba aliponigeukiwa mimi akakuta machozi yakinitoka tuu kama mfiwa.
Tulikaa masaa yalienda na kukata lakini mama harudi baba akijaribu kupiga simu inaita tuu humu humu ndani lakini wakiitafuta haionekani mahali ilipo... Baba akiwa chumbani alichanganyikiwa huku akisema kwanini aondoke bila kuaga na simu ameiacha tuu hapa ndani. Baada ya kuongea hivyo alitoka na kwenda kuwapa taarifa majirani kwamba anamtafuta mama kama alionekana sehemu yoyote, lakini hakufanikiwa kupata jibu lenye faraja mana kuna wengine walisema walimwona asubuhi akiwa anaelekea kama sokoni lakini hawajamwona tena. Baba akasafiri hadi kituo kimoja cha matangazo na kuomba tangazo la kumtafuta mtu. Tangazo la kwanza liliunganishwa na taarifa ya habari ya asubuhi kabisa ambapo walisikia wachache lakini walijitahidi kwa uwezo wao kuzisambaza, wengi hawakuweza kuamini lakini ilikuwa ndio hivo kilicho tangazwa ni ukweli mtupu

......tulikaa wiki nzima bila kumwona mama machoni petu tukawa wakiwa kwa kuondokewa na mwenzetu kiutata zaidi na redio ziliendelea kutangaza kila baada ya dakika kadhaa kwa yeyote atakae weza kumwona atoe taarifa lakini hakukuwa na mafanikio hadi mwezi mmoja uliisha babu na bibi waliaga kuwa wanaondoka ili warudi tena kijijini lakini akawaambia ni bora wabaki wanakaa hapa hapa. Babu na bibi walikataa kabisa wakidai kwamba mazao yataharibika na hakuna wa kusimamia huko kijijini kisha walipanga vitu vyao na kuondoka baba aliwapa baadhi ya vitu vya kuwasaidia waendako lakini walikataa kupokea, mimi walinipa kitu kama kamba fulani ambayo walisema niwe naivaa shingoni, bila kinyongo niliipokea kisha nikaivaa shingoni baada ya mda tuliagana kisha wao wakaondoka

....nilikaa na baba hadi inafika usiku shughuli zote alikuwa akizifanya baba pale nyumbani mana tulikuwa wawili tuu. Tukiwa tumesha maliza kula baba aliita bon mwanangu niliitika kisha nikawa makini kusikiliza lakini akiwa anaanza kuongea simu ilianza kuita akaipokea na kutulia kimya huku akionyesha mshangao wa ajabu hadi nikamuuliza baba mbona hivo kuna nini lakini alitoa ishara ya kwamba nitulie kimya kwa kutumia kidole chake baada ya mda alishusha simu toka sikioni na kuelekea chumbani lakini alipofika chumbani alisimama kidogo akatafakari kisha akarudi kukaa pale akasema mwanangu bon niliitika naam baba....itaendelea

De 37 (end)

Gangster noma
By: benchrys
37(mwisho)

--------nilitoka hadi nje ndipo nilisikia vingora vikilia huku na taa za mwanga mkali vikinimulika
Sikupoteza mda kabisa niliruka beki juu sana na kutua tena chini waliokuwa wamezunguka lile eneo walibaki tuu kushangaa mana pale hapakuonekana kitu tena
Mtu kapotea kimiujiza hapohapo wote walitawanyika nakusambaratika kila upande ili kama nikionekana tuu nidakwe ( duuuh kwakweli hawa polisi sijui waliahidiwa zawadi gani endapo wakinishika)

Tukiwa maeneo fulani kuna watu walikuwa wakipiga stor zao za kawaida

Duh ivi na nyinyi mmesikia kuhusu ninja ambae anaharibu mapolisi na baadhi ya watu wanaojifanya kujipendekeza kifarafara
Aaaah acha ndoto hizo wewe ivi hii Tanzania kabisa iwe na ninja badae utasema spider man nae ameonekana tanzania acha kutushika maskio wewe
Sio kwamba nawashikamskio ila ndio ukweli, duuuh kweli hata redio  hamsikilizagi majumbani kwenu
Acha hizo sasa mi redio nisikilize inanifaidisha nini sikuizi ni mwendo music kene flash basi hizo habari za redio achana nazo ushamba huo

Ndo maana hakuna unalo fahamu jinga wewe

Aaaah mi siwezi kubishana na wewe mtoto wa mama vipi wewe kalale huko

Dadeki powa mimi mtoto wa mama we siulinyonya kon ya babaako(alijibu hivi bada ya kuona ameambiwa mtoto wa mama)

Gafla tuu pakawa hapakaliki tena ngumi za mavumbini zilianza. Wakati huo wote mimi nilikuwa nimekaa pembeni nawasikiliza tuu jinsi wanavobishana hadi saizi wanabishana lakini kwa kutotaka kuwa shahidi nikasimama na kuondoka hata kama haya maeneo sikuwa mwenyeji baada ya mimi kuondoka bila kuaga hata kwa mtu mmoja. Gafla watu wakakuta wakipigwa virungu na maafande fulani watatu
Vijana kazi za kufanya ni nyingi nyie mchana huu mnapigana kama kuku mnaakili nzuri kweli nyinyi nawauliza mnaakili
Maneno hayo yalikuwa yameambatana na virungu 

Ben nikiwa nyuma ya ukuta  fulani hivi niliweza kusikia sauti ya vilio vya watu wakilia sana nilirukia hadi juu na kuchungulia ni nini kinaendelea upande mwingine ndipo nikaona wau wakipokea kipigo. Hapohapo nilichange na kuwa ninja nikiwa na lengo nikawa tishe tuu

Maafande wakiwa wanatoa ile dozi hevi wakashangaa ninja anakuja mbele yao waliondoka mbio na kusahau vile virungu vyao nilibaki nikicheka tuu lakini gafla nikakuta tunazingirwa na watu waliovalia nguo za kijeshi huku wakiwa wanaonyesha dhahiri kwamba hawapo kimzaha na mtu mana kuna jamaa alijipitisha alipokea teke moja na kwenda kuanguka mbali sana na mimi nikajisemea kama kudakwa hadakwi mtu naondoka na roho za watu leo
Wakati huo nimechuchumaa mguu mmoja chini nikabadilisha style na kukaa kama muislam akiwa kuswali (wanaohusika wanajua) na kuweka ishara fulan katika vidole vyangu kishanikanyanyuka kwa kasi ya ajabu
Wale wanajeshi wakajipanga alisogea mmoja nikampiga ngumi ya uso ambapo alipepesuka na kwenda kuangukia kwa mwenzake wakaja wawili niliruka beki mbili mfululizo juu huku nikizunguka kama gurudumu nikaduna chini na kutua katika vifua vyao wote walianguka chini huku wakikohoa mmoja nilishuhudia akitokwa na damu mdomoni lakini sikujali kuliko nikamatwe

Baada ya hapo nikaona wote wakija nilichomoa upanga wangu na kuanza kuwafuata lakini hawa wote walikuwa na roho za nini sijui mana woga kwao walishatupaga na ulikopotelea wamesahau
Nilianza kuuzungusha ule upanga lakini kwa uwezo wao waliweza kukwepa nilipoona hii njia kama ni mbaya niliruka beki juu na kupita kwenye vichwa vyao ili nipate nafasi ndoto tuu baada ya kuwapita wote nilitoa cheni iliyokuwa imefungwa na gorori nzito za vyuma na kuanza kuwatandikia zoezi lilitembea kwa mda wa dakika kama ishirini baada ya hapo wote walikuwa chini tena wapo hoi kabisa

Niliondoka humu nikiwa na furaha ya kuwa sijakamatwa lakini kufika mbele nilikutana mwanajeshi mmoja ambae alikuwa kasimama katika ya barabara aliponiona akaanza kupiga makofi akinishangilia ninapo kuja ila sikujali nikaendelea kumfata tuu

Baadaya hapo akanisimamisha kwa alama ya vidole nikasimama
Wewe ndie unajifanya mwanaume sana sasa leo nataka tuone mimi na wewe nani zaidi
Baada ya kuongea yale alidank juu na kunipiga teke zito la kifua, teke lile lilinipeleka moja kwa moja hadi chini hadi sikuamin sijakaa vizuri ngumi ya uso lakini alikosea kunipa upenyo wa kusimama niliposimama
Alidank tena ili arudie ile style ya mwanzo lakini alifeli nilimuwahi kwa kupiga kwa nguvu sana katika kiuno chake akatua chini kama gogo nilimgoja asimame aliposimama nikaona asinipotezee mda hapo nikawa namchanganyia mateke ngumi huku vyote vikiwa ni vizito hadi baadae akawa hawezi kusimama ndipo akaaanza kuropoka
NIMEJITAHIDI KUKUTAFUTA KWA KILA NAMNA LENGO NIKUDAKE LAKINI NAONA KAMA NI UJANJA UMENISHINDA UMENIVUNJA MGUU NA MKONO TAFADHALI USIENDELEE UTANIUA BURE WEWE NI ZAIDI YANGU
HATA MLIOKUWA MKISOMA NAO BAADHI NILIWAUA NA WENGINE NILISHA WATEKA KITAMBO baadaya kuona ameongea hivo nikamuuliza moja ya watu uliowaua akataja jane nilipata hasira sana nilitoa upanga na kufyeka shingo yake kama nyasi
Pumbavu umeniulia msichana ambae nilishampenda na dada ake nitamueleza ni nini niliposema hivo niliondoka na kupotelea nikiwa katika nyumba ya merry siku ya tatu taarifa ikatangaza
Aliyekuwa akionekana kama ni ninja ameweza kumteketeza jambazi sugu na gaidi ambae alikuwa anaisumbua serikali kwa kipindi chote na kwakuwa ninja tumeshamfahamu tutamfata kwa wakati wetu na kumpa pongezi yake
Siku iliyofuata nilipigiwa simu na kuitwa katika ofisi fulani nikakabidhiwa pesa na cheki ya benk ambayo ilisoma hela nyingi sana, niliwashukuru na kuondoka kisha maisha yakaanza upya ndani nyumba yangu mpya na magari kadhaa niliyonunua na moja la kupewa****
XxxxxxxxxxxxxxxxxxTHE ENDxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
benchrys.blogspot.com