Jumapili, 28 Agosti 2016

De 17

Gangstar noma
By: benchrys
17

.........niliipokea line ile ya merry ambayo haitumii kisha nikajaza zile namba ambazo wamezitaja kwenye lile tangazo niliziandika kwenye simu baada ya hapo maongezi yakawa hivi
..hallow habari za sasa bila kukosea nadhani hii ndiyo namba ambayo mmeitaja kwenye tangazo kwamba atakae mwona ben atoe taarifa kupitia hii namba si ndiyo.. Baada ya kuongea hivo nilijibiwa ndio hii ni namba ya kutolea taarifa za kuhusu kupotea kwa ben mana tumemtafuta sasa linakaribia wiki moja Kuisha,, baada ya yeye kusema vile nilimjibu ok huyo ben ni nan yako wewe mpaka uwe na bidii ya kumtafuta hivi....yule niliyekuwa nikijibizana nae akajibu acha uboya ben ni mwanangu halaf wewe unipe maswali kama hayo pu****vu kweli wewe baada ya kuongea hayo alikata Simu kwa hasira hapa pembeni merry alikuwa akicheka tuu.. Baada ya yeye kukata simu nikatuma meseji kwenye ile namba inayo someka

****pole kwa mpango wako wa kitoto mimi hapa ndio benchrys mwenyewe sasa subiria kidogo utapata majibu yako*****

Baada ya ule ujumbe kupokelewa kwenye simu yake alipiga simu tena kwenye ile namba lakini sikuhitahi kupokea akatuma na meseji tena akidai kwamba tafadhali pokea simu hiyo kisha akapiga tena simu lakini sikupokea.....

Baada ya hapo niliwatumia ujumbe nyumbani wa kwamba naomba namba za polisi za jirani,,, baada yamda mfupi nilipokea ujumbe kwenye simu yangu sikuchelewa nilizinakili zile namba kisha nikapiga....

***ya kituo cha polisi moja kwa moja nani anaongea tukusaidie.. Na mimi ili wasishituke niliwaambia kwamba jina langu naitwa bon akanijibu ndiyo bon naweza kukusaidia nipe shida yako. Baada ya yeye kusema hayo akawa tayari ashanipa uhuru wa kujieleza.... Nilimwambia lengo bila kupoteza wakati na kukata simu haikupita dadika hata tano simu yangu ilianza kuita nilisita kupokea kwa kuhofia naweza jikologa mwenyewe nilipoangalia kwenye simu niliona ni namba ngeni ilikuwa ikipiga simu sikuipokea ile simu baada ya kuita kwa mda mrefu ilikata kisha ikaingia meseji nayo hata sikutaka kuisoma mana nilishahisi lazima atakuwa huyuhuyu tu si mwingine siku hii ilipita kwa staili hii siku iliyofuatia ile namba ilipiga tena kwakuwa ile line ngeni nilishatoa niliipokea na kuweka sikioni lakini nilibaki kimya kama kawaida mpaka yeye aanze kuongea nikiridhia ndipo na mimi naitikia
"oya ben nhaje mkuu
"full nan wewe
"wewe acha kuzingua inamaana hii namba huna zarau
"kudadeki kama hujielezi nakata simu sawa
"kama kila nijieleze fwesh joh langu
"ok hamna noma tufanye nna zarau,,,, nilijibu hivo na kukata simu lakini baada ya muda nikaja kuikumbuka ile sauti maana ilikuwa ikifanana na sauti ya god aliyekuwa m mbea wa darasa ila kwanini atumie namba ngeni au nae kasetiwa boya kweli huyu yupo simpo kama yebo hivi shit.....nilijikuta nikijisemea hayo pekeyangu......

       Siku iliyofuata asubuhi mida kama ya saa tano na nusu hivi nikiwa ndani nikasikia sauti za watu kulia nje nkajiuliza kuna nini huko lakini kwakuwa sikuwa mhusika sikufanikiwa kujua chochote mana nilikuwa nipo ndani bado kwa haraka nikataka nitoke ili nikafahamu nini kimewasibu hawa watu mpka wanaliliana hadi mikelele kwa sisi wengine nikakumbuka kwamba kuna ile remoti inayohusika kwaajili ya alarm na shot kwenye hii nyumba nilitafuta ilipo kisha nikabonyeza kitufe kilichokuwa kina alama kama ya kengele hivi hapo zilitokea kelele nyumba nzima hadi mimi mwenyewe nilianza kuogopa maana ilikuwa kila kona ya ile nyumba ni kelele tuu yani...
Nilikuja kushtuka baadae baada ya kuangalia nje na kutowaona tena wale waliokuwa wanalia hapo nikajua vyema kwamba hapa nishaharibu tayari hayakupita hata masaa nilianza kuyaona magari yale ambayo yaliisogelea shule ile siku yakiwa na watu waliotinga nguo za jeshi nilishuhudia hayo yote kupitia kile kioo ambacho kipo ukutani baada ya kuona vile niliianda tena remoti kwaajili ya shoti endapo wataleta fujo zao niweze kufanya yangu akashuka baba mmoja kwenye gari ambalo lilikuwa mbele kabisa akiwa amevaa suti nyeupe huku yupo na walinzi wanne nyuma yake baada ya hapo walishuka wengine waliokuwa kwenye magari mengine huku wakiwa ns sare maalum nilipoangalia vizuri niligundua ni wengi kana kwamba hata idadi yao sikuweza kuijua kiurahisi,,,,, lakini kwa wakati nilikuwa sijifikirii mimi nilichokuwa nawaza ni kwamba merry ataingia vipi humu ndani lakini nikiwa naendelea kuwaza nilihisi kushikwa bega kabla ya kugeuka nikavuta pumzi maana mawazo yangu yalijua kwamba baadhi yao tayari washaingia hadi ndani ila nilipogeuka sikuamini kumkuta merry akiwa mule nilitamani kuuliza ameingiaje lakini sikuwa na wakati kabisa wa kuuliza baada ya hapo alipokea ile remoti kisha akasema funua pale kuna mlango kachukue mabegi yale yote kusha tumbukiza hapo wewe kajifiche kwa siku zile..... Aliposema niliona kama ashakuwa mdogo kiakili ndipo nikamuuliza kwa kumwambia merry kama ni utani huu wa leo to much mi ntafunuaje malumalu hizo si utani huu ila yeye alisisitiza kwa kusema chelewa ile kwako cjui mwenyewe we nenda kajaribu kama hapafunguki niliondoka na kwenda kufunua nilipofika pale nilitumia nguvu nyingi kuvuta kumbe hata hapahitaji nguvu "duuhh nyumba za wenyewe hizi jaman" baada ya kufungua kutokana na nilivyoviona kule chini nilijisemea hivo_basi nilifanya kadiri alivonambia kisha nilienda kujificha nilikoambiwa nijifiche

.........baada ya mimi kujificha merry alitoka nje na....... Lakini kabla hajafungua mlango hadi mwisho zilipigwa risasi za hewani mfululizo kutoka kwa wale watu. Walikuwa na maana gani hakuna aliyeweza kufahamu ila merry hakuwa mwoga alifungua mlango akawasalimia kisha akawauliza naweza kuwasaidia mnahitaji nini
"tunahitaji sisi ni kajana mmoja kwa jina ben inasemekana yupo hapa na sura yake ni hii hapa akachomoka mmoja wao akiwa ameshika karatasi kubwa yenye picha ya ben akimuonyesha merry kisha wakamuuliza jee unaweza kutusaidia kwa hilo.....
"hapana siwezi mana hii sura hata kwangu ni ngeni. Baada ya merry kujibu vile yule kiongozi wao akasema kamtazameni ndani. Wale watu wake nao wakajitia ni vipele kutaka kuingia kwa nguvu mle ndani kabla hawajafanikiwa kuingia merry akawambia nyumba yangu nyie mnajifanya kuijua ok nendeni huko ndani tuone. Walicheka dharau kisha wakasema mtu mzima hatishiwi nyau ngoja tuingie sasa, walimsukuma pale aliposimama ili waingie ndani lakini walipofika kati ya mlango na mlango walisimama kusha mmoja baada ya mwingine alianza kugeuza na kurudi nje hadi wote baadhi yao walitoka huku macho yanamachozi kiumbali,,,,
   Vipi mmeshamaliza kukagua au bado mana mmetoka mapema mno nipeni mrejesho. Hakuna aliyemjibu kila mmoja alielekea kwenye gari lake na kuweka standby kwa kuondoka, yule mkubwa wao alimwangalia merry kwa hasira akarudisha mkono wake mmoja nyuma baada ya mda kidogo ulisikika mlio "paa" hadi ben alikokuwa kajificha alistuka na wale wote walioingia kwenye magari wote walishuka baada ya kuona......itaendeleaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni