Gangstar noma
By: benchrys
22
........ivi ni wewe uliyekuwa unapigana ni wewe au kuna kivuli chako mbona kama siamini hivi ni kweli au maigizo haya kama ni edit zimefika hadi hizi level basi mi najiuzuru kabisa aliongea maneno hayo merry akiwa haamini kama ni ben kweli ambaye alikuwa akiongelewa katika taarifa ya habari kuwa kapiga watu hadi baadhi yao wanazirai kabisa na baadhi yao inasemekana ni watu wanoogopwa sana katika mitaa.... Samahani kama nitakukwaza merry ila ukweli ndio huo maana nikiwa naenda nyumbani kama nilivokuaga kuna mtu akaniletea mambo ya ajabu sikumwacha nilimpa adhabu yake tena nilikuja nae hadi hapa nyumbani ili anipe ukweli juu ya kwanini walikuwa wananitafuta nilipata ukweli niliweza kumwachilia na kwenda uwanjani lakini nikiwa narudi kuna watu wakawa wananifuatilia nikaon upuuzi mana baada ya kumvuruga huyo mmoja ndipo nikaona bastola kwenye mfuko wake. Nilipomaliza kutoa hayo maelezo kwa merry nikamtolea ile bastola ilibaiweke ndani
Merry hata hakuamini alivoona na kusikia yale maneno kutoka kwangu, alipokea ile bastola akaiweka ndani kisha akarudi na kuniuliza ben kwa hiyo umejifunza wapi hayo mambo ya kupigana " daah merry ni mda mfupi sana ila ni stori ndefu sitaweza kukusimulia sahizi labda kesho... Nikiwa naendelea kuongea simu yangu iliita niliipokea bila kuangalia mpigaji ni nani
;;;;;jaman mi sitakiiiiiiiii nakufa mimiiiii niachebi huko mi sitaki jaman. Msadaa jamaniiiiiiiii.. Ilikuwa ni sauti ambayo ilisikika katika simu yangu pindi tuu nilipoipokea na kuweka sikioni nilibaki nimeduwaa baada ya kusikia mtu analia mda kama ule tena kwenye simu baadhi ya maswali niliyojiuliza ni kwanini nipigiwe mimi na ni namba ngeni iliyopiga ila akili yangu ilinituma nitoke nje, na mimi bila kuchelewa nilifungua mlango na kutoka nje pengine hili tukio lipo jirani hapahapa nilipotoka nje nilisikia kama mtu akilia vilevile mbali kidogo na pale ambapo mimi nilikuwepo nilijaribu kufuata ile sauti na baada ya mda mfupi nikawa nimeshafika pale kabla ya kuongea neno niliruka na kumpiga na teke la kichwa jamaa mmoha ambaye alikuwa amembananisha msichana fulani ambae sikumtambua ukutani baada ya hapo nilimfuata yule bint na kumwambia kimbia nae hakuzubaa hata sekunde aliondoka spidi hadi nikashangaa. Nikiwa naendelea kumshangaa yule dada nilipigwa ngumi ya kifua akataka kuongeza na ya pili nilidaka mkono nikauvunja kisha nikaondoka
Nilifika nyumbani merry bado amekaa anangoja kinachojili niliingia ndani nikafunga mlango
"wasichana wenzenu muda mwingine sijui wana matatizo gani usikuu huu mtu unatembea pekeyako vichochoroni... nilikuwa nikiongea pekeyangu maneno kisha merry nae akadakia kwani ni nani huyo
;;ahaa hata simjui na namba yangu sijui kapata wapi
;;huyo anakufahamu vizuri kabisa nawe utakuwa unamjua..... Nikiwa naendelea kuongea ikaingia meseji kwenye simu yangu nilipofungua nilikutana na ujumbe "asante ben kwa msaada wako nakushukuru ntakutafuta kesho mimi ni jane mdgo na naomi usiku mwema" nilijikuta nikicheka pekeyangu huku nikijiuliza maswali kama ni jen huku kaja kufanya pia kafahamu vipi kama mimi nipo huu mtaa maswali mengi yalinijia kichwani bila ya majibu. Nikiwa naendelea kujiuliza maswali simu yangu iliita tena kuangalia niliiona ni namba ya madam linda
;;hallo ben mambo
;;powa tuu nambie madam
;;hakuna jipya ila nataka kukuuliza huo mtaa unao kaa saivi hauna mauzauza yoyote maana naona kama kila siku habari za ajabu tuu niambie tuu maana huku kumetulia saizi unaweza kurudi tuu
;;unaniambia ukweli au na wewe umesetiwa kama akina jen walivosetiwa zile siku za mwanzo..
;;hapana ben niamini tuu yaana nakuomba
;;haya basi kesho au kesho kutwa nakuja huko nitatoa taarifa nikiwa karibu
;; haya powa usiku mwema.... Yalikuwa ni maongezi yangu baada ya kupigiwa simu na madam linda, baada ya mfupi macho yangu yalianza kuwa mazito ishara ya usingizi nilisimama nikamuaga merry kisha nikaingia kulala
*******
Jaman ivi ni upumbavu gani tunaufanya ivi tayari mmekuwa watu wajinga namna hiyo ivi nawalisha mbwa au nalisha watu ambai nao inatakiwa wajue namna ya kula wao kama wao haya kamewapiga kamtu kama kale ambako kwanza ni kadogo kwenu,mwezi uliopita mliniambia hata haonekani saizi anaonekana anawapiga watu kama nyinyi kuna maana ya mimi kuwalipa si bora nikanywee bia tuu hizi hela kama mtu nnae mtaka mimi hamuwezi kumshika kadiri nnavotaka mimi na kitu kibaya mnathubutu kumwachia hata silaha ambazo nimewapatia mnajua kesi ambayo mnajitengenezea kama akiamua kuzipeleka mahali husika..
Samahani mkuu haya ni makosa madogo tu hata hupaswi kutoa lawama kama hizo maana hata sisi wenyewe tunashangaa kama kweli kamtu kama kale kanaweza hata kupigana ila kesho ntajitahidi kumwonesha adabu na ni lazima nimkamate katoto kadogo hakawezi kutusumbua akili watu wazima kama sisi. Sio kwamba hakawezi mbona kamewasumbua sasa inamaana mlikuwa mnacheza hadi akawashika akili zenu. .dah boss mbona inaonekana kama ni makosa ya kila siku tumekosea mara ngapi ivi hii si ndio mara ya kwanza tuu mbona umefura hivi boss hata sisi ni binadam boss naomba ufahamu hivyo.. Ok nawasubiri hiyo kesho ili nijue mwisho itakuwaje ila tambueni kwamba mnavoendelea kuzubaa tunazidi kujiharibia kumbukeni hatumtafuti sisi tuu na ndio maana yule aliyeweka tangazo kwenye tv siku chache zilizopita nasikia kafungwa sasa kwetu umakini ni swala la muhimu sana katika hii kazi. .sawa mkuu umesomeka kwa hiyo kesho mkuu.ok tuonane kesho*******
Yalikuwa ni majibizano boss akilaumu kwa wafanyakazi wake kwanini wanashindwa kumshik ben ila wakajifariji na kuachana****
Jaman mbona nimemmiss sana mwanangu ben sijui yupo salama kweli maana nina muda sijasikia hata sauti yake aliongea hivo mama huko nyumbani kisha akanyanyua simu na kuchagua namba ya ben ili ampigie simu lakini akajibiwa mteja unaempigia hapatikani kwa sasa jaribu tena baadae alitoa simu sikioni na kuitupa kwenye kochi kisha akaondoka na kwenda kulala
........................
Siku iliyofuata asubuhi simu yangu ilikuwa ikiita baada ya kuiwasha saa 10 za usiku nilinyanyuka kiuvivu maana nilikuwa bado ninausingizi "aaa nani tena tunasumbuana asubuhi yote hii shit,,,,,,,,, nilionfea maneno hayo baada ya simu kunishitua huku bado ninausingizi.. Niliipokea simu hiyo ambayo ilionyesha jina la naomi
Hallo naomi vipi za huko
.safi tuu mbona umetususa hivo
..amna sijawasusa sema watu mnanifanya nisiwaamini maana....
.kwanini usituamini tena
.ntasema tukuonana sawa
.sawa kwakuwa maneno unayo wewe ntasubiri tuu
.nnapokuja ntakwambia ila sitaki umwambie mtu yeyote yule
.powa usijali simwambii mtu ila ufike hadi hapa nyumbani maana tumekukumbuka ile mbaya
.usijali naa
Baada ya kuongea na naomi sikupata tena usingizi niliamka na kufanya taratibu zote nikachukua begi moja na lile karatasi alilonipa babu kisha nikaanza safari ya kwenda nyumbani baada ya kumuaga merry nilitembea sana nikafika sehemu fulani niliweza kuona watu wakiwa wamejazana wakiwa kama wanashangaa kitu fulani. Macho yangu na ubongi viliungana na kuweka mpango wa lazima ushuhudie pana kitu gani pale. Nililifuata lile kundi la watu nikajifanya naangalia ila sifikii juu nikawa najipenyeza katikati ya watu hadi nilifanikiwa kufika mbele kabisa ambako ndiko kuna jambo maalumu lililowajaza watu wengi pale baada ya kuweza kuona kinachofanyika nilipata hasira sana kisha nikajikuta na mimi nikiingia pale katikati hiyo yote ilikuwa ni baada ya kumwona rafiki yangu wa shuleni akipigwa na jamaa mmoja hivi ambaye anasura kama machete hivi nitaka nilivue begi langu ila nilikumbuka maneni ya babu juu ya utunzaji wa lile karatasi ambalo linastaili nyingi juu ya upiganaji nikiwa nimevaa begi langu niliruka juu na kutua juu ya kifua cha huyu jamaa alianguka kama boga kisha nikawa nimesimama nikimngoja aamke, alinitazama kwa hasira kisha akataka aamke haraka ili anisogelee lakini alijikuta hana nguvu tena za kunyanyuka. Akatoa amri kwa wenzake mkanateni huyo mbweha asiondoke hata hatua moja,___ nilimshika mkono joel kisha nikaondoka nae kuendelea na safari lakini kabla sijaondoka kuna watu wawili nilihisi wanakuja nyuma sikutaka kujisumbua sana kwakuwa chini kulikuwa na vumbi nilitumia mguu wangu kuchapua lile vumbi na kuwarushia usoni walipoanza kujifutafuta ikawa nafasi ya sisi kuondoka lakini kabla hatujafika mbali niligeuka nyuma nikaona kuna mtu anakuja anakimbia huku akiwa na mti sijali nilimwacha aje tuu alipotaka kurusha mti niligeuka haraka na kuudaka ule mti na kumfumua teke la uso mda mfupi akawa yupo chini hajielewi mimi na joel tuliendelea kusonga mbele wakati huo wote joel aliona kama mauzauza tu huku njiani mambo ninayoyafanya tulitembea hadi nafika mtaani kwetu jirani na nyumbani nikaanza kumuaga joel lakini nikiwa naendelea kumuaga nilimwona god yule m mbeya wa darasa kule shuleni aliniona tuu alinyanyua simu yake akawa anatafuta baadhi ya namba lakini kabla hajapiga nilikimbia na kumuwahi asije akawa walewale na yeye. Baada ya kumfikia nilinyang'anya ile simu kisha nikaangalia ni nani anataka kumpigia
Ivi na wewe kumbe ni mmoja wao mnaotaka kunisaka mimi huku uwezo hamna baada ya mimi kuongea vile god alitoa pipe na kuniwekea kichwani kisha akasema ben upo chini ya ulinzi lakini akiwa kazubaa akajikuta pipe ipo kichwani kwake.. Kisha nikamuuliza nani yupo chini ya ulinzi baada ya kuona vile akanyoosha mikono juu kukubali. Nilimnasa tu kofi zito kisha nikatoa risasi zote na kumtupia pipe tupu bila risasi alipoona nimemtupia vile akaikota haraka kisha akaanza kuvuta triger kwa lengo anipige na risasi zile, baada ya mimi kusikia ule mlio wa pipe isiyo na nligeuka na kumwambia kama umetumwa ntawanyonga wote nikaendelea na safari yangu hadi nyumbani nilipoingia tuu ndani......itaendeleaaaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni