Gangstar noma
By: benchrys
23
..........waoh ben umerudiiiiiii mamaaaaaaa ben huyu hapa amerudi mama njoo, ben karibu ndani tulikumiss wenzio huku hadi karibia kuumwa yaan jaman...alikuwa ni naomi ambaye alinipokea kwa shangwe hadi mi mwenyewe nilijiogopa nilizubaa kama sekunde mama nae akatoka akiwa na furaha ya hali ya juu.. Basi tuliingia ndani duuh chakula sijui kimeandaliwa mda gani hata sielewi maana nilipoingia tuu ndani haikupotea hata sekunde nilinawishwa mikono tayari kwa kuanza kula baada ya dakika chache tulishamaliza kukusanya kila chombo kilichokuwapo pale
Jaman mbona baba simwoni yuko wapi maana nlisahau kuuliza hilo jambo
..baba yupo kazini bado hajarudi
,nilijibiwa hivo baada ya kuuliza hilo swali ok kama yupo kazini powa. Nikiwa nimekaa pale na naomi. Naomi simu yake ilianza kuita aliipokea simu ile kwa furaha huku akiniangalia, nilipoona kile kitendo nilishituka kisha nikamuuliza..
We vipi mbona mimacho kwangu vipi kwani au nimekula sumu.... Aliiweka simu pembeni kisha akaniambia kwa sauti ndogo huyu ni jane alikuwa anakusalimia. Baada ya yeye kusema vile nikatulia kwa amani maana nilijua tayari nimeuzwa
.............
Oya kale kajamaa mbona hakaonekani tena toka ile juzi sikaoni sijui kapo wapi ila ntakapata tuu hata kasijali na jinsi nilivo na hasira nako sijui itakuwaje... Aah unazingua wewe ivi kama mtu humwoni inatakiwa ujiulize yupo wapi sio unamtafuta kwa hasira kuwa mpole mambo yako yatakuwa fresh nautamnyaka tuu hata usijali jomba punguza presha huyu yupo na ni wetu wala hana kwakwenda na atakuwa amejificha
.........hayo yalikuwa ni mazungumzo ya vijana wawili wakiwa wanavuta mibangi yao sijui hata ni akina nani na ni nani wanamwongelea
Basi kwa akina ben mda ulikwenda hadi baba alikuwa tayari amesharudi ilipofika kama saa moja hivi...
Jamani natoka mara moja ntarudi sasa hata geti msirudishie.. Niliongea hivo kwa maana nlihitaji kufika kwa joel maana nilimmisi jamaa yangu lakini nlipoongea vile mama akauliza "ivi wewe umefika unamasaa tu ila unatoka kwanini huko unakoenda usiende kesho tafadhali. Basi kwakuwa aliongea mama tena kwa msisitizo nilibadili mawazo ila sikupenda kwa maana lengo sikuwa nalo moja tuu. Nilirudi ndani ila kichwani nilishapanga wakiuliza nilikokuwa naishi nitadanganya...tulikaa sebuleni masaa mengi huku tukiwa na stori nyingi kilichonishangaza hadi naenda kulala sikuulizwa swali la wapi nilikuwa naishi ilipofika saa nne na nusu niliwaaga naenda naenda kulala wote wakaridhia basi niliondoka baada ya muda kila mmoja alitawanyika kwenda chumbani kwake. Nikiwa naendelea kuutafuta usingizi kwenye simu yangu iliingia meseji nilinyanyuka kwenye kitanda nilipoegama kisha nikaifungua, kumbe alikuwa ni merry
Ben mbona kimya umefika salama kweli nijibu niwe na amani ..baada ya kusoma hiyo meseji nikafuata sehemu ya replay kisha nikarudisha,
Nimefika salama tuu nilisahau kukwambia nipo nyumbani saizi kwaheli usiku mwema nikutakie, nikaituma sio mda mrefu akarudisha na kwako pia nilidelete kisha nikaanza kutafuta usingizi tena ila usingizi haukuja
Nikakumbuka ivi kumbe kuna wasap kwenye simu yangu basi nikafungua data kama kawaida nilipowasha data ziliingia meseji ishiri na zaidi idadi kubwa zilikuwa ni za madam linda. Nilianza kufuatilia meseji moja baada ya nyingine ila nilishangaa kuona nimetumiwa picha za watu wengi kweli kisha mwishoni kukawa na ujumbe kuwa makini na hizo sura popote unapopita
Niliposoma ule ujumbe nilimakinika ndipo niliweza kumuona hadi yule niliyempiga kule mtaani kwa akina merry basi nilisoma meseji zote nikawa tayari nimemaliza kuzisoma hapo nikawaza cha kufanya kingine....nikiwa nipo bado pale nilihisi kama nje kuna mtu vile nilinyata hadi sebuleni kisha nikaka dirishani ili nijue anataka kufanya nini, mara nikaona anafuata mlango akasogea kisha akachomoa kitu kama chuma hivi sikuweza kuona vizuri anachokifanya baada ya muda mfupi mlango ulifunguka baada ya kuona vile nilirudi nyuma kidogo kisha nikaruka juu na kumtulia kifuani alianguka chini nilimsogelea na kushika pembeni mwa shingo hapo ndipo akatulia kama roba la mahindi nilimfunga kamba na kumweka stoo ambayo haina kitu chochote nililock mlango kisha nikarudi kulala kabla sijapata usingizi tena nilisikia mlio wa simu kuita kule stoo nilijua wazi ni simu huyu jambazi nilinyanyuka na kwenda kuinyakua nilipofika ikawa ndio inakata ila nikaichukua na kurudi chumbani kwangu nikiwa chumbani simu iliita tena niliipokea na kusema hebu ngoja kwanza ambapo nina liliseviwa boss baada ya kusema vile nilikata simu na kuizima kabisa kisha nikalala
*****\
Baba naomba uwapigie polisi waje hapa saizi
Baba alinipuuzia ila baada ya muda si mwingi alibadilisha mawazo na kuwapigia hayakupita hata masaa polisi walifika nikawaonyesha mtuhumiwa ni nani kisha wakamfunga pingu na kuondoka nae wamashukuru kwa kuwasaidia
......ila binadamu bhana sijui wanamatatizo gani mtu unakazi ila bado unataka na kazi ya wizi ivi kwanini hawaridhiki binadamu hawa duuh hii shida sana.. Alikuwa akiongea baba hayo maneno baada ya kumwona yule mwizi kumbe walikuwa wakifanya kazi kampuni moja......
****mama mmoja anatangaza kupotelewa na mme wake anadai aliondoka usiku bila kumuaga mahali anapoenda lakini cha kushangaza hadi wakati huu hajamwona mme wake kwa atakae mwona atoe taarifa kwa kupitia namba au atoe taarifa kituo cha polisi kilicho karibu tunaomba ushirikiano wenu ahsante*****ilikuwa ni breaking newz katika tv baada ya kuona zile picha za anaetafutwa nilicheka sana na kijisemea wewe pomole kweli unatafuta mwizi.....baada ya muda simu yangu iliita kwa namba ngeni
;;hallow
;;ya nambie ben vipi
;;powa we nan
;;mi mchizi wako bhana vipi wewe uko wapi now
;;ahaa kama ni mchizi wangu powa mi nipo tanzania jee wewe uko wapi
;;unazingua mwanangu tz kubwa bhana vipi
;;usiniendeshe sikujui halafu nikwambie nipo wapi unaumwa au.... Hallo, hallo, hallo we ben hallo,,,,, baada ya kujibu vile nilikata simu akaendelea kuita baada ya kugundua simu haipo hewani akajaribu kupiga tena nilipokea kisha nikamwambia tuonane sehemu fulani hivi hawakuchelewa wakachukua pikipiki huku wakiwa watatu na mabegi yao kuwahi lile eneo lakini mimi nilienda lile eneo kwa kupitia njia nyingine...
Duuh mbona hatokei au katuenjoy huyu mpuuzi dadeki zake tuweke haya mabegi chini maana yanachosha tu migongo. Walikubaliana na kuvua yale mabegi kisha wakaweka kwenye pikipiki zao juu ya kiti....wakati huo wote mimi nilikuwa kwenye kona moja nikiwasoma tu nilipoona wameenda mbali kidogo na zile pikipiki nilisogelea yale mabegi na kufungua ndipo nilipoweza kujua kuwa nao ni wapuuzi kumbe, ndani ya mabegi yale kulikuwa visu fulani vidogo sana ila vinauzito fulani. Nilivichukua visu vyote na kutia kwenye begi moja kisha lile begi nikalivaa mimi na kuanza kuondoka, nikiwa naondoka nyuma yangu nilisikia kelele oya kijamaa kile pale, baada ya kusikia vile nilijua wazi kuwa ni wenyewe tu nilijifanya nakimbia nai hawakuchelewa nilipopita katika nyumba moja geti lilikuwa wazi nilirusha lile begi kisha nikaendelea kukimbia hadi maeneo fulani ambapo palikuwa na uwanja wa mpira
Walifika jirani kukaribia kunikuta. Daah niliangua kicheko baada ya kuona wanaonikimbiza et hadi hichi kijamaa kinanitafuta dah sa si kinaweza kikaishia huku huku tuu aisee ila sio mbaya njooni,, nilisogea jilani na mwamba mmoja nao walinifuata kisha.....itaendeleaaaaaaaaaaaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni